Suala la mishahara linakuzwa mno, tuzungumzie maslahi ya watumishi kwa ujumla

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,457
1,440
Mjadala na propoganda ya mishahara kwa watumishi wa umma inakuzwa mno na Wapinzani kama mtaji wao kwenye kampeni hizi bila kuzingatia hatua zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano kuhusu uboreshaji wa maslahi kwa Watumishi wa Umma. Ieleweke kuwa mishahara ni sehemu tu ya maslahi katika utumishi wa umma.

Wapinzani wanasahau upandishwaji madaraja yanayoendana na mabadiliko ya mishahara, pia mabadiliko mapya ya posho mbalimbali zilizoongezeka, kupungua kwa Paye kutoka asilimia 11 hadi 9 na mengineyo mengi ambayo kimsingi yametumia fedha za umma na fedha za walipa kodi.

Tunapojadili mishahara tuzungumze kwa kujumuisha maslahi yote tutaeleweka tusibague manufaa mengine.
 
Wewe unazungumzia madaraja yapi yaliopandishwa? Kisheria ni baada ya 3 hadi 4 mtu anatakiwa apande daraja. Watu wa 2013 ndio wamepandishwa mwaka 2019. Na wa mwaka 2014 hawajui hatima yao. Wa mwaka 2015 kuja juu ndio hawapo kwenye mpango huu wa miaka mitano. Acha kuandika pumba hapa.
 
Hoja hapa ni kwamba maslahi ya watumishi ni mapana ukiwemo mshahara ni vizuri kuangalia kwa kina hatua zilizochukuliwa na serikali ikiwemo posho na marupurupu mengineyo,mazingira ya kazi, pensheni, mikataba ya kazi na upandishwaji vyeo nk.

Tatizo watu wamechukua eneo moja tu la mshahara kwa sababu za kisiasa zaidi na kulishadidia.Hata hivyo nani kafanya utafiti wa kina kuhusu suala hili atupe matokeo tujadili kwa takwimu na taarifa za kisayansi.
 
Hivi mleta bandiko unaona watu wajinga Sana eeh!

Kama una tetea chama we tetea tu, lakini watumishi Wana hasira Sana na mtaziina siku ya siku ikifika.

Au wewe, kila kitu kimepanda yangu 2015 na maslahi yao yako vile vile, acha kabisa kuhusu maslahi.

Watu Wana madeni Sana,binafsi namfahamu Kuna mwalimu kastaafu mwaka huu mwezi wa nne mpaka leo hajapata mafao wakati wabunge wamemaliza mwezi wa sita wameashalipwa mafao, unadhani Yule mwalimu atawachagua CCM?

Yangu mwezi wa tano yeye na familia wanakula nini?
 
Come on now dndagula , we as CHADEMA have survived the past 20+ years under extreme oppression under every single president of this country. We know Voting Meko out will not change our condition.

But again No President from the Green will change our condition to the better, therefore We must change the ruling system or suffer the consequences later.
 
Hoja hapa ni kwamba maslahi ya watumishi ni mapana ukiwemo mshahara ni vizuri kuangalia kwa kina hatua zilizochukuliwa na serikali ikiwemo posho na marupurupu mengineyo,mazingira ya kazi, pensheni, mikataba ya kazi na upandishwaji vyeo nk. Tatizo watu wamechukua eneo moja tu la mshahara kwa sababu za kisiasa zaidi na kulishadidia.Hata hivyo nani kafanya utafiti wa kina kuhusu suala hili atupe matokeo tujadili kwa takwimu na taarifa za kisayansi.
Mwalimu kwa mfano ana posho ipi na marupurupu yapi?

Mwalimu yeye anataka Annual Increment,Daraja kila miaka mitatu,kulipwa likizo,katika hayo yote Serikali imefeli.Tena Rais amekuwa akiongea wazi kuwa hawezi ongeza mshahara akaacha kufanya miradi mingine ya maendeleo
 
Hoja hapa ni kwamba maslahi ya watumishi ni mapana ukiwemo mshahara ni vizuri kuangalia kwa kina hatua zilizochukuliwa na serikali ikiwemo posho na marupurupu mengineyo,mazingira ya kazi, pensheni, mikataba ya kazi na upandishwaji vyeo nk. Tatizo watu wamechukua eneo moja tu la mshahara kwa sababu za kisiasa zaidi na kulishadidia.Hata hivyo nani kafanya utafiti wa kina kuhusu suala hili atupe matokeo tujadili kwa takwimu na taarifa za kisayansi.
Fuatilia mijadala hii sio Nawe unaangalia kitu kimoja. Wanaposema maslahi ya watumishi ni yote hayo uliyosema pamoja na ustaafu. Ndio maana Lissu kuna mahali alisema ataleta neema kwa yote yaliyopungua hapa kati.
 
Nimegundua kitu ,wengi wa wachangiaji hamjawahi kuwa watumishi bàli ni wanasiasa na mnaona hii ni kama hoja wakati ni hoka nyepesi mno.

CCM ni chama cha ujamaa na kujitegemea na yanayofanyika ni katika kuhakikisha nchi inajitegemea na jamii yetu inainuka kwa usawa kwenye vipato,matibabu na elimu.

Ahsante Dr John Pombe Magufuli tunaona mtazamo wako.
 
Unataka kusema ukichanganya Omo na Foma unapata povu!!! La hasha haizewezekani hata, ili mchanganyiko huo wa Omo na Foma ulete povu ni sharti kitu kingine kiongezeke ambacho ni maji.

Hivyo maslahi ya watumishi ni pamoja na mishahara iliyoboreshwa,punguzo la kodi, upandishwaji wa madaraja na mambo mengine mengi kadha wa kadha
 
Back
Top Bottom