Suala la Mdee na wenzake: Tusitoke kwenye msingi wa hoja ya CHADEMA kuwashughulikia

May 21, 2020
69
125
Habari wakuu,

Nimefuatilia hoja za watu mbalimbali humu na katika sehemu nyingine mtaani na media, nimefuatilia wengi wanaotoa hoja ya hawa ndugu 19 kutoshughulikiwa, msingi wao ni chama kupata ruzuku ili kiweze kuwa na nguvu ya fedha kujiendesha, wengine wanasema chama kiendelee kuonekana kupitia bunge, wengine wanadai uzalendo na maslahi ya taifa kwanza, wengine wanadai mbona chaguzi zilizopita hawakukubali matokeo ila walienda bungeni, wengine wanadai wanawake ni haki yao na mengine mengi sana.

Kwanza najua hoja hizi zinatolewa na watu huru ambao ni maoni yao binafsi tu, lakini pia yanatolewa na watu ambao ni strategically planted (wamewekwa) ili kutengeneza hoja hizo na kuinfluence mijadala iwe namna wanavyotaka waliowatuma na hili lipo wazi, ndio maana ni muhimu kujadili hoja kwa mtazamo wako huru kuliko kudandia hoja, kitu kitakachokufanya uwe unatimiza malengo ya watu flani.

Sasa, hoja ambayo ni ya msingi naona watu wanajaribu kuikwepa isiwe na mashiko ni hoja ya hawa watu 19 au zaidi, kukiuka taratibu rasmi za chama chao, napenda kusema kuwa CHADEMA ni Chama cha kidemokrasia ambacho kama vyama vingine, kinaongozwa na katiba, kanuni, taratibu, na miongozo mbalimbali. Kwa utaratibu wa chama au taasisi nyingine mambo hujadiliwa rasmi kwa vikao na kutolewa maamuzi ambapo hoja za wengi katka kikao ndizo hupita, hata kama ulikuwa na hoja nzuri kiasi gani, maadam umeshindwa kushawishi iungwe mkono basi unaungana na wenzako na huo unakuwa ndio msimamo wa pamoja.

Akina Mdee hata kama wana hoja nzuri kiasi gani, wanafeli kwenye kigezo cha kutoheshimu taratibu rasmi za chama, hata kama wanaungwa mkono na nani ubatili unakuja kwa kufanya uamuzi huo kwa kutofuata taratibu na hapo ndipo panapohitajika kushughulikiwa maana kama kila mtu akijichukulia maamuzi yake basi kunakuwa hakuna chama wala hakuna taasisi

Hoja yangu ni wanawajibika kwa kutofuata taratibu rasmi za chama.

NB: Chama kikubwa kama CHADEMA lazima kina vyanzo vya taarifa za ndani pia kina intelligence yake najua wanapoketi wanazo taarifa zaidi za kujiridhisha kuwa ni taratibu pekee zilivunjwa au kuna usaliti, hongo nzito, hujuma n.k

Nawatakia kila la heri katika maamuzi yao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom