Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,090
Nataka niongee kwa hasira kali na leo Mod naomba mnivumilie lugha yangu. Hapa bongo kuna mambo ya kikhanithi yanaendelea sana na matokeo yake wananchi tunapata shida kwa sababu ya ukhanithi wa watu wachache.
Leo Nipashe wametoa taarifa kuwa kuna mchina amekamatwa anachepusha maji ya mto ruvu lita milioni moja kwa saa kumwagilia mbogamboga zake tu. Huu kama siyo ukhanithi ni kitu gani?
Huyu mtu haiwezekani anaingia nchini, anapewa vibali vyote halafu eti serikali isijue, Haiwezekani labda kama ni serikali ya mazuzu.
Leo kwa sababu kimenuka, maji hakuna wanajifanya kuja mbelembele kukamata bangusilo ili wammwagie lawama.
Tumeshasema mara kibao kuwa huu uhusiano wa kifala kati ya serikali yetu na wachina unatugharimu sana. Wachina wamekata miti sana nchi hii, Wao ndo wanconsume magogo ya miti kwa rate ya kutisha, halafu juzi serikali inajifanya kujikosha kwa kuzuia biashara ya magogo. Ilikuwa wapi siku zote?
Leo nilikuwa namsikiliza waziri wa zamani katika mtandao w clubhouse anaeleza kipindi alivyokuwa waziri wa mazingira alipojaribu kuwadhibiti wachina wasimalize misitu yetu. akapigiwa simu na wakubwa awaachie tu wachina waendelee!. Huu kama siyo uhujumu uchumi kwa nchi yetu ni nini?. Huu kama siyo Ukhanithi ni kitu gani?
Tunataka serikali yetu iache kuwaabudu Wachina, Tunataka serikali ilinde rasilimali za nchi hii. Hii tabia ya ubinafsi uliokithiri, upumbavu na kuuza nchi kukomeshwe mara moja.
Na wale wakubwa wanaouza nchi kwa vizawadi vidogo vya kufanyiwa massage huko Beijing waache mara moja tabia hizi za Kikhanithi