Suala la Magufuli ni VITA YA URAIS 2015!

Kama kuna mtu wanaiva na Magufuli amshauri awaombe radhi wanakigamboni kwa kupotoka lakini nauli mpya iendelee.
Akifanya hivyo itamjenga kupita maelezo badala ya kulaumu kwamba anapigwa vita!
 
WEWE SIO POLITICAL ANALYST UNAJIKWEZA TU.kwanza hakuna mtu anayeitwa AHMED SALIM AHMED hapa tanzania,bali kuna salim Ahmed Salim.

Pili,suala la kupandisha nauli ya kivuko haliingiliani na urais hata kidogo,ni suala la utendaji na hali halisi ya maisha kwa sasa.kile kivuko ni sawa na daraja hivyo wananchi walitakiwa wapite bure.kwa kuwa nchi yetu ni maskini serikali ikaona angalau basi wananchi wachangie kidogo.
kilichotakiwa ni mh.magufuli,jembe la kazi awashirikishe wananchi wanaotumia kivuko hicho hususan wana kigamboni klupitia kwa wabunge wao au kwa kufanya mikutano ya hadhara kutoa elimu hiyo na kupokea mawazo/maoni ya wadau angepata ushirikiano mkubwa sana.sasa na wewe unajifanya mchambuzi wa masuala ya kisiasa kumbe unapotosha kabisa ukweli kwa kutokutambua baadhi ya mambo yanayoendelea.pamoja na utendaji mzuri wa magufuli lakini naye ni binadamu,anakosea na anapaswa kupokea maoni ya wanaompinga.

Ktk hili suala la Dr.Magufuli naona KATIKATI wewe ndiye unastahili kupewa elimu tena si ndogo bali ya muda na zana za mazoezi ya vitendo,Kama unafikia sehemu unakiita kivuko ni sawa na daraja pole sana ila si bure una lako jambo.Kama si maslahi kutoka meza za mafisadi basi ni chuki binafsi na msongo wa mawazo utokanao na siasa chafu za nchi yako tanzania.Pole..........
 
Wakuu heshima kwenu,

unatakiwa kutumia akili kidogo kubaini suala la Dr Magufuli linakuzwa na kutumiwa na wapinzani wake wakubwa kisiasa kummaliza kabla ya mwaka 2015.Wabunge wa Dar wameshadadia utadhani ni jambo la maana nauli haijapanda kwa zaidi ya miaka kumi na nne hawalioni.Nauli za daladala zimepanda,nauli za mabasi yaendayo mikoani zimepanda,bei za bidhaa mbali mbali zinapanda kila kukicha ongezeko la tsh 100 inakuwa nongwa.Mbona hamkuandamana mlipoambiwa ndege ya Rais lazima inunuliwe ikibidi mtakula majani ?.

Wewe ulitaka wabunge wakae kimya? nani angewaelewa ! hao ndio WANA DAR ES SALAAM! wazawa wa Dar wenye uchungu na watu wao!

Mbona mnataja Tsh 200 tu ? mbona hamtaji tozo nyingine,

Guta ni usafiri unaomuwezesha mwanajamii wa kipato cha chini kabisa kuweza kuvusha mizigo yake kutoka dar kwenda Kigamboni kutoka tsh 300 mpaka 1,800 mbona mmekazania tsh 200 tu ?
GAri ndogo kutoka tsh 800 mpaka 1,500
Gari station wagon , pickup na nyingine kubwa kutoka tsh 1,000 mpaka tsh 2,000
Kilichonishangaza jamani ! looh nahema ! ETI MZIGO WA KILO 50 nao ulipiwe TSH 500 hii mmeona wapi jamani! nyie msidhani watu wa Kigamboni wanalalama na hako kanauli ka tsh 200 kuna mengi yanayowaumiza ! na hapo hapo msidhani yeye anatoka tu nyumbani moja kwa moja anapanda kivuko! mfikirie mtu anaetokea Mbutu , Mwasonga ! Pona Gezaulole na Kwengineko! anakuja pale na Basi kwa nauli mpaka afike pale ni tsh 800 apande kivuko tsh 200 tayari 1,000 jamani msiseme tu kwa sababu nyie hayawagusi!
NA kumbukeni wana kigamboni hawapingi nauli kupanda , ila washirikishwe na zipande kuendeana na kipato cha mtu ! sio kupandishwa kiholela tu mradi tu mwendawazimu fulani amelala usiku akaamka akaamua kupandisha ! kama serikali yetu itakuwa na akili hizi nadhani tutarajie mengi kipindi kijacho!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
quote_icon.png
By katikati WEWE SIO POLITICAL ANALYST UNAJIKWEZA TU.kwanza hakuna mtu anayeitwa AHMED SALIM AHMED hapa tanzania,bali kuna salim Ahmed Salim.

Pili,suala la kupandisha nauli ya kivuko haliingiliani na urais hata kidogo,ni suala la utendaji na hali halisi ya maisha kwa sasa.kile kivuko ni sawa na daraja hivyo wananchi walitakiwa wapite bure.kwa kuwa nchi yetu ni maskini serikali ikaona angalau basi wananchi wachangie kidogo.
kilichotakiwa ni mh.magufuli,jembe la kazi awashirikishe wananchi wanaotumia kivuko hicho hususan wana kigamboni klupitia kwa wabunge wao au kwa kufanya mikutano ya hadhara kutoa elimu hiyo na kupokea mawazo/maoni ya wadau angepata ushirikiano mkubwa sana.sasa na wewe unajifanya mchambuzi wa masuala ya kisiasa kumbe unapotosha kabisa ukweli kwa kutokutambua baadhi ya mambo yanayoendelea.pamoja na utendaji mzuri wa magufuli lakini naye ni binadamu,anakosea na anapaswa kupokea maoni ya wanaompinga.

Ktk hili suala la Dr.Magufuli naona KATIKATI wewe ndiye unastahili kupewa elimu tena si ndogo bali ya muda na zana za mazoezi ya vitendo,Kama unafikia sehemu unakiita kivuko ni sawa na daraja pole sana ila si bure una lako jambo.Kama si maslahi kutoka meza za mafisadi basi ni chuki binafsi na msongo wa mawazo utokanao na siasa chafu za nchi yako tanzania.Pole..........

Sioni baya lolote aloliandika huyo katikati, yeye ameonesha hisia na ameandika sahihi kabisa , anatakiwa awashirikishe wananchi! nadhani mmepitiliza!
 
Naamini kuwa ni kukosa uwezo wa kuchambua mambo kwa watu ku-link hili la kupandisha nauli za vivuko na ugombea urais wa 2015. Ikiwa kama kila anachofanya waziri [yeyote yule ambaye ni potential 2015 preseidential candidate] utahusishwa na kampeini hizo za urais kupitia chama cha CCM basi Rais wa sasa kati ya 2012 mpaka 2015 ameshafanywa kama wanavyosema wazungu Lame Duck [au bata kiwete].
 
Duh yaani Tanzania sasa kila kitu kinahusishwa na Urais! Mtu akizomewa ni Urais 2015, mtu akienda kusali kanisani ni Urais 2015, mtu akiwambia watu wapige mbizi kuvuka bahari ni Urais 2015, mtu akiugua ni Urais 2015! Urais 2015, Urais 2015!!

Jiulize kwa nini Uraisi 2015 wakati kwa sasa kuna Raisi!!! au wananchi wameshamdelete ila yeye yupo tu?
 
uraisi vs uwajibikaji.
Kumbe JF imekuwa kisiasa. mmepoteza dira. kwani magufuli ameonyesha nia na uraisi??
uzushi mtupu
 
Tatizo Magufuli alitegwa naye akategeka, lawama juu yake mpaka pale atakapoomba radhi kwa kauli ya kukera aliyoitoa. Kama ishu ni urais, bado anayo nafasi ya kujijenga na kujirekebisha kasoro ndogo ndogo alizonazo..!
 
Ktk hili suala la Dr.Magufuli naona KATIKATI wewe ndiye unastahili kupewa elimu tena si ndogo bali ya muda na zana za mazoezi ya vitendo,Kama unafikia sehemu unakiita kivuko ni sawa na daraja pole sana ila si bure una lako jambo.Kama si maslahi kutoka meza za mafisadi basi ni chuki binafsi na msongo wa mawazo utokanao na siasa chafu za nchi yako tanzania.Pole..........

Mkuu kwa watu wa mabarabara kivuko is a moving Bridge (kwa tafsiri yangu sijui ya kwako: Daraja linalotembea). kwa maana hiyo naona Katikati hakukosea.
 
tatizo naliona kwa tanzanianist kushindwa kuelewa sababu ya magufuli kuzomewa ni tabia yake ya ubabe a kejeli. anapenda dana kujiona yeye ndio sahihi sana na mwerevu sana na wengine wote wajinga. amrshindwa kuwalipamakandarasi lakini bado anawakrjeli na kuwatulkana. huyu hafai hatakuwa waziri amebomoa nyumba za watu kwa kisingizio cha sheria lakini bila kujali utu wala. huruma. mtu kajenga nyumba for a lifetime leo unbomolea unadhani ni mchezo halafu unamtukana na kumkejeli.binafsi ananichefua sana
 
Aisee Jamani inaelekea hizo posho za EL ni nono sana...,Haya kijana Kasign Posho yako ya Leo

Jibu hoja' ni haki guta kulipishwa 1500 huku VX ikilipia 2000? Ilishindikana vyp Magufuli kuwashirikisha wadau? Mambo ya Top-down yanakwisha sasa hv!
 
quote_icon.png
By Tanzaniaist
Aisee Jamani inaelekea hizo posho za EL ni nono sana...,Haya kijana Kasign Posho yako ya Leo

Jibu hoja' ni haki guta kulipishwa 1500 huku VX ikilipia 2000? Ilishindikana vyp Magufuli kuwashirikisha wadau? Mambo ya Top-down yanakwisha sasa hv!

Mkuu naomba nikusahihishe ni tsh 1,800 sio 1,500 umeacha tsh 300 katikatik, naomba niongeze ... Mzigo wa Kg 50 unalipiwa tsh 500 ! maana umeubeba mgongoni kama mtoto au umeuweka chini ni kwamba unaulipia tsh 500 na huku wewe mwenyewe umeshalipa tsh 200 so ukiwa na zigo lako la kilo 50 , unalipa tsh 200 ukijumlisha na tsh 500 jumla tsh 700 .... upo hapo? je mwanakigamboni asilalame? akilalama eti amewekwa kumzomea rais mtarajiwa ! maweee! huyu ndio awe rais ! mimi si shabiki sana lakini nitaingia katika kumfanyia fitna huyu ili muradi tu akose huo urais ! HAFAI HUYU JAMANI!

siku alotaka kuvunja nyumba za watu na kusema hawatalipwa fidia JE INGEKUWA NYUMBA YA MAMA YAKE MZAZI IMEPITA PALE ANGEVUNJA ??? au ASINGELIPA FIDIA ??? wewe usipandishe hasira zetu hapa!
 
kila kitu MBIO ZA URAIS , wengi wanafanya mazoezi jinsi ya kuongoza nchi, mawaziri wote wako likizo kisha MBIO Za URAIS, wote hawa si waanzishe vyama kwa kuwa unaruhusiwa kugombea hata kama ni mia tano. KAULI za kimasaburi hatutaki sie. Mmeacha mambo muhimu mnakimbilia mawazo ya mika mitatu ijayo!!
 
00.jpg

Na hii je alienda kwa babu wa Loliondo kwa ajili ya urais?

Teh teh teh !! yaani nilisikia watu wanataka kumshikati babu kwa udanganyifu na uuwaji! nadhani na huyu rias wao mtarajiwa anafaa kufunguliwa mashitaka pia! yaani ni maoni yangu tu ! ndio rais huyo ! loh! kweli Tanzania tuna kazi !
 
Back
Top Bottom