Suala la Magufuli ni VITA YA URAIS 2015! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suala la Magufuli ni VITA YA URAIS 2015!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tanzaniaist, Jan 3, 2012.

 1. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wana JF!
  Naona mwaka umeanza na tukio likimhusisha Mh.John Magufuli...! mimi kama Political exepert naweza kusema hizi ndizo mbinu za kisasa za kummaliza mtu kisiasa kwa kumchonganisha na wananchi au kumjengea chuki ndani ya jamii....!

  Ikumbukwe Magufuli ni tishio kubwa kwenye vita ya uraisi 2015 ndani ya chama chake CCM! kutokana na msimamo na uchpa kazi wake...na ninaona wapinzani wake washaanza fitna na mbinu za kummaliza mapema!

  Mfano mzuri...tulishuhudia kwa Dk.Ahmed Salim Ahmed alivyohusishwa na kifo cha karume na pia Hata Sumaye Kuhusishwa na Kashfa mbalimbali....

  Tukija Suala la Kigamboni...,Tukiongea kiukweli Mh.John Magufuli alizalilishwa kwa kutukanwa na kuzomewa na wananchi...,ambao ni kama kikundi cha watu fulani hivi kilipangwa kumchefua...naye akawajibu kwa jazba akijua ni kikundi mahususi kilichowekwa kuchochea fitna dhidi yake! Magufuli tumemjua tangia 2000 alivyokuwa waziri wa wizara hiyo hiyo lakini mbona matukio kama hayo yalikuwa hayatokei au magufuli amebadilika! tujiulize?

  Naomba Mh.Magufuli Aamke! ajue hizi zote ni mbinu za kisiasa kumdidimisha huku vyombo vya havari vikitumika kuhakikisha ndani ya mwaka 2015...hakubaliki ndani ya chama na ndani ya CCM!
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mimi nilijua hilo mapema
  wabunge wamenunuliwa ili kuchochea....
  eti nauli isipande kwa miaka 14 waandamane
  mbona daladala kila mwaka zinapanda hawaandamani???????
   
 3. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hata kama ukimfariji, Magufuli naye hupo katika kapu hilo lenye maembe yaliyooza hivyo hatuna imani kama yeye yupo salama.
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  WEWE SIO POLITICAL ANALYST UNAJIKWEZA TU.kwanza hakuna mtu anayeitwa AHMED SALIM AHMED hapa tanzania,bali kuna salim Ahmed Salim.

  Pili,suala la kupandisha nauli ya kivuko haliingiliani na urais hata kidogo,ni suala la utendaji na hali halisi ya maisha kwa sasa.kile kivuko ni sawa na daraja hivyo wananchi walitakiwa wapite bure.kwa kuwa nchi yetu ni maskini serikali ikaona angalau basi wananchi wachangie kidogo.
  kilichotakiwa ni mh.magufuli,jembe la kazi awashirikishe wananchi wanaotumia kivuko hicho hususan wana kigamboni klupitia kwa wabunge wao au kwa kufanya mikutano ya hadhara kutoa elimu hiyo na kupokea mawazo/maoni ya wadau angepata ushirikiano mkubwa sana.sasa na wewe unajifanya mchambuzi wa masuala ya kisiasa kumbe unapotosha kabisa ukweli kwa kutokutambua baadhi ya mambo yanayoendelea.pamoja na utendaji mzuri wa magufuli lakini naye ni binadamu,anakosea na anapaswa kupokea maoni ya wanaompinga.
   
 5. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya kaka safi sana....kasign posho yako kwa EL
   
 6. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  FAizaFoxy huwa anasema unanchekesha ,

  NAomba niibe usemi wake , kwa kweli "unanchekesha" na unanshangaza ! ! yaani dah! siwezi hata kuendelea kuandika bado nashangaaa!

  Yaani nani amuharibie magufuli ! ? ni yeye mwenyewe amelikoroga ! kwa maneno yake ya dharau na kejeli kila wakati ! yeye kama kiongozi linapotokea jambo kama hilo hususan linalohusu jamii HATAKIWI KUKURUPUKA ! Magufuli hupenda sana kukurupuka katika kujibu na hasa anapodeal na jamii.

  Mfano wakati wa kuuza nyumba za serikali nakumbuka kuna mfankazi wa serikali alikuwa anakaa katika nyumba yake nae alitaka auziwe kama wengine walivofanyiwa ! Philemon Sarungi aliitaka nyumba ya yule mfanyakazi sikumbuki jina lake ! Magufuli alimtoa kama kuku bwana yule na kumwambia angepata nyumba nyingine badili ya ile kwa sababau tu yeye alikuwa na nguvu na huo ubabe wake anaojitwika ! yule bwana alilalamika mpaka kwenye magazeti na sisi wengine kina kapuku ndio tukapata habari kutoka humo! mwisho yule bwana akasema naonewa kwa sababu hao ni mawaziri alipozidi kulalama alipoendewa na waandishi wa habari Magufuli akajibu kwa kusema " Analalamika nini ? kama anaona kaonewa kwa sababau sisi mawaziri na yeye si autafute tu huo uwaziri?"

  Juzi juzi alitaka kuvunja majengo kadhaa kwa ubabe wake mpaka rais na waziri mkuuwa wakaingilia kati

  Leo anawakejeli watu wa kigamboni ! halafu eti useme ANAHARIBIWA? unataka wabunge wa Dar es salaam wanyamaze kimya? basi itakuwa nini maana ya kuwa na mbunge ambae hana uwezo hata wa kupaza sauti kutetea watu wake hususan pale wanapooenewa!

  Nasema magufuli hafai kuwa rais , nilimuona mtu wa maana sana lakini sasa hivi nadiriki kusema kuwa hafai hafai tena hafai hata chembe kuwa rais, kwa sababu atatuendesha huyu na dharau namna hii sijui kama tutapona watu wa kipato cha chini! LooooH!!!!

  Eti anaharibiwa ! sidhani kam nyie ni great thinkers ! hebu fikirini kwa undani!

  Pia nashangazwa na watu wanaoteta nauli ya tsh 200, what about za magari ? ni haki kupandisha nauli kutoka tsh 800 mpaka 1,500 au kutoka 1,000 mpaka 2,000? guta kutooka 300 mpaka 1,800 jamani hebu kuweni makini kwanza !
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Haya mambo ya ushabiki wa kisiasa na kiitikadi yanatuharibu. Hayo unayoona wewe kama ni mbio za urais ni maoni yako binafsi ambayo huwezi kutufanya wengi tuwe na mtazamo wako.

  Kilichotokea katika uamuzi na matamko ya Magufuli hayana uhusiano wo wote na mbio za urasi, ila ni mambo ya utekelezaji na uwajibikaji wa wizara yake, ila kasoro iliyojitokeza ni kutotumia busara na taratibu katika utekelezaji wake, na pale alipoona wananchi wamekuja juu kwa kutoshirikishwa akaamua kutumia ubabe kama kinga ya kujitetea alivyozoeleka, kumbe wananchi wa Darisalama wamezoeshwa kushirikishwa yatokeapo mabadiliko na kwa vile kivuko hivyo ni muhimu si kwa raia tu ila kwa serikali pia, manufaa yake yasitazamwe individual bali kwa upana zaidi katika shughuli za umma mzima, elimu uchumi na usalama kwa taifa.

  Haya ndiyo mambo ambayo serikali inapsawa kuwa makini katika kutoa huduma za msingi badala ya kufikiria kiuchumi. Commuter transit serikali imeshindwa sasa hadi vivuko vianawashinda, jambo hili haliwezi kukubalika kihivyo.
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mimi sifikirii kwa kutumia meya wa jiji la dar,wala sina uhusiano na richmonduli,hakuna mtu aliye juu ya sheria wala hakuna mtu aliyekamilika.sote tuna mapungufu na tunapaswa kujadiliana kwa pamoja kuhusu mambo yanayohusu maisha yetu.any way,kabla hujani group km mpokea posho,wewe unaona guta kulipishwa 1800 zaidi hata ya gari ni sahihi? ina maana mwenye guta ana maisha mazuri kuliko mwenye gari ndogo?tuache kufikiria urais tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu hata kwenye masuala ya msingi kaka.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh yaani Tanzania sasa kila kitu kinahusishwa na Urais! Mtu akizomewa ni Urais 2015, mtu akienda kusali kanisani ni Urais 2015, mtu akiwambia watu wapige mbizi kuvuka bahari ni Urais 2015, mtu akiugua ni Urais 2015! Urais 2015, Urais 2015!!
   
 10. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aisee Jamani inaelekea hizo posho za EL ni nono sana...,Haya kijana Kasign Posho yako ya Leo
   
 11. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280

  Umesema "kuntu" kabisa,.

  Serikali wakati wote inapenda kuburuza watu kama mambumbumbu! jamani sasa hivi ule ujinga tulotiwa na nyerere unafifia! maana kila kitu NDIO ! kila kitu NDIO! sasa hivi watu wanaamka!

  Yeye kama waziri angeenda Kigamboni na kuongea na wananchi na kuwaelimisha jamani kuna a, b c, d na angesikia na angeorodhesha tozo zake na watu wangetoa na za kwao! lakini watu wanalalama yeye anatoa lugha ya kejeli eti asoweza "Apige MBIZI" au "AZUNGUKE KONGOWE" au ARUDI KIJIJINI ! hivi wewe ndugu yangu unaejiita political analyst umezianalyse
  hizi kejeli za magufuli halafu ndio uje na huo uzi wako! au unataka kujaza servers za wanajamii bure? ! think twice !
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Magufuli kuwakejeli wananchi inahusiana vipi na u-rais 2015?
   
 13. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Magufuli naye ni kimeo tu, hana jipya.
   
 14. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Inahusiana na nini?
   
 15. OPTIMISTIC

  OPTIMISTIC Senior Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa hili jf members naomba nitoe mawazo yangu.
  Tukitaka kuengelea maendeleo endelevu "sustainable development" suala la kuchangia huduma za jamii haliepukiki, na ukipata huduma yoyote bure ujue someone, somewhere amesweat ili wewe uenjoy free service.
  Kuhusu kivuko kina gharama kubwa tu katika uendeshaji kama vile mafuta ya kurun engines pamoja na generators, gharama za service na spares, gharama za mishahara kwa wafanyakazi, malipo ya insurance, malipo ya depreciation etc.
  Ili iwe reliable service lazima mapato yawe juu ya matumizi. Huu ndio ukweli tukiachana na siasa.
  Huyu Dr mbunge wa Kigamboni anajua huduma ya afya kwa Tanzania ni mbaya kwa sababu za kisiasa mwenye uwezo na asiyekuwa na uwezo, wakina wanawazito kutibiwa ni bure, watoto under 5 bure, wazee above 60 bure, wenye magonjwa sugu i.e HIV, Diabetis, pressure, tb bure,chakula bure kwa wagonjwa wote matokeo yake huduma ni mbovu.
  SUALA LA KUJIULIZA KWA UCHUMI TULIONAO SASA MCHANGO WA SH.100 UNA MSAADA GANI UNAFIKIRI WEWE BINAFSI kuvuka kwa sh.100 ni sahihi.
  HAPPY NEW YEAR
   
 16. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Katika mbinu za kisiasa, kuna tekniki ya kuchokoza hasira za mtu ili ufanikishe lengo la kumfarakanisha na jamii na kumfanya aonekane hafai kama kiongozi wa jamii. Mara nyingi agents hutumia mbinu ya kuuliza swali korofi, la kuudhi, kudhihaki ili mlengwa atoke katika mstari. Ni sawa na mtu ghafla anakuwa kama anakutisha kukupiga kofi halafu anaishia kujikuna kichwa! Lazima Wewe utashtuka na kutaka kujilinda au kukwepa. Baada ya hapo anakuwa amepata udhibitisho kukutangazia kuwa wewe ni mwoga.

  Maghufuli kaingia anga zao kama Nape anavyoingizwa kwenye mikenge na utitiri wa vyombo vya habari!


  Bonus Thread:


   
 17. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Wakuu heshima kwenu,

  unatakiwa kutumia akili kidogo kubaini suala la Dr Magufuli linakuzwa na kutumiwa na wapinzani wake wakubwa kisiasa kummaliza kabla ya mwaka 2015.Wabunge wa Dar wameshadadia utadhani ni jambo la maana nauli haijapanda kwa zaidi ya miaka kumi na nne hawalioni.Nauli za daladala zimepanda,nauli za mabasi yaendayo mikoani zimepanda,bei za bidhaa mbali mbali zinapanda kila kukicha ongezeko la tsh 100 inakuwa nongwa.Mbona hamkuandamana mlipoambiwa ndege ya Rais lazima inunuliwe ikibidi mtakula majani ?.
   
 18. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  magufuli arudishe nyumba za serikali alizoiba..
  anatembea ndani ya vx,kwake mia mbili ndogo lakini kwa wananchi ni kubwa
  magufuli rais??give me a break
   
 19. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  This is too low.....unataka kutuambia wewe unaenda ku-sign posho yako kwa Magufuli?

  Binafsi sioni suala hili kama linaingiliana na mbio za urais kwa sababu Magufuli hakushinikizwa kutoa kauli ya kejeli (hata kama angetukanwa na wananch!) na hao unaodhani ni wapinzani wake katika hizo mbio za urais 2015. Labda mbio hizo ni kwa yeye, katika kutaka kujionesha kuwa anawajibika, kwenda kivukoni kataka eti kuhakikisha nauli mpya zinaanza kutumika.....huku akiwa ame under estimate reaction ya wananchi/watumiaji wa kivuko.
   
 20. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nyie watu wa ajabu kweli. Yaani hamueleweki kabisa, mara Magufuli mara Lowassa. Hivi tuwaelewe vipi nyie watu?
   
Loading...