Suala la madini Tanzania; Kanuni ya 'Wagawanye ili uwatawale' inafanya kazi

Kweli wazungu wana akili!.Wametuibia miaka mingi kwa kudanganya kuwa wanapeleka mchanga wa dhahabu kuchenjua huko Japan pengine na kwingineko.

Mtu mmoja mdadisi Siku zote alikuwa anatilia shaka.Anaamua aunde tume kuchunguza.

Anagundua wizi mkubwa.Wale wa upande wake waliohusika na wizi huo,anawachukulia hatua kali na kuanza kutafakari achukue hatua gani dhidi ya alioingia nao mkataba.

Cha ajabu,badala ya watz kuungana pamoja kumkemea mwizi,baadhi ya wataz,kwa mgongo wa demokrasia tuliyoletewa na wazungu,wanamtetea mwizi na kumlaani aliyegundua wizi.Anatishwa kuwa tutashitakiwa na mwizi na hivyo kulipa pesa nyingi.

Wengine wanasema chanzo ni mikataba mibovu hivyo ubovu wa mikataba hiyo anabebeshwa rais mwenye mwaka mmoja na nusu madarakani.Huyu hajawahi kuwa Waziri wa wizara hiyo.

Hata kama kuna uzembe upande wa serikali,kwa akili ya kawaida,nilitegemea walioibiwa waungane wamshughulikie mwizi.Wakishamaliza kumshughulikia mwizi,basi warejee na kusutana kwa uzembe!.Hapa ni kinyume chake!.

Ni sawa na kumfumania mtu akizini na mkeo,halafu badala ya jamaa zako kuungana nawe japo kumlaani mgoni wako,wao wanakubeza na kukuambia mgoni wako atakushitaki,na hivyo utamfidia fedha nyingi!.Woga huu unatoka wapi?.Ni heri nishitakiwe lakini mwizi wangu nimemjua.

Wengine wanapima uwezo wa Acacia dhidi ya TZ na kutetemeka.Kama watz ni waoga hivi bora kuishi Korea Kaskazini..Wengine wanasema tutafukuza wawekezaji.

Unaibiwa hivyo halafu bado unyamaze eti mwekezaji atakwenda!.Heri kukosa wawekezaji.Lakini kikubwa kinachotufikisha ktk mgawanyiko huu ni siasa.

Upinzani wanajua wakisifia hatua ya Rais itampa nguvu kisiasa na hivyo itakuwa vigumu kumshinda ktk chaguzi zijazo.

Kwa hiyo heri kumuunga mkono mwizi wetu wa madini kuliko rais aliyewagundua kuwa wanatuibia.Sikujua kuwa demokrasia ya vyama vingi ilikuja ili kutugawanya na kututawala!.

Moja ya vigezo Nyerere alivyotumia kuondoa mfumo wa vyama vingi ni kwa sababu unaondoa umoja.WATZ TUUNGANENI DHIDI YA WANYONYAJI WETU.
wacha porojo CCM miaka 55 wanaibia nchi hukuona lolote maana zaidi ya wizi
 
Anachotakiwa kufanya huyo Rais asiye taka kusjauriwa ni kufuata ushauri wa wanasheria na siyo kukurupuka kama anaenda chooni.

Issue ni Umoja na ushirikiano lakini Umoja si wa upande mmoja tukiongea kuhusu umoja Nina maana ya Watanzania maana JPM Watanzania kwake ni wanaccm tu ndipo shida ilipo.
Kwani rais kafanya nini mkuu naomba msaada maana sijaelewa watu wanafoka foka wakati kamati ya wataalamu wa uchumi na wanasheria haitoa ripoti yao na Rais kawachukulia adhabu watumishi aliyewachagua lakini makelele mengi sana.
 
Kwani rais kafanya nini mkuu naomba msaada maana sijaelewa watu wanafoka foka wakati kamati ya wataalamu wa uchumi na wanasheria haitoa ripoti yao na Rais kawachukulia adhabu watumishi aliyewachagua lakini makelele mengi sana.

Hakuna anayefoka kukiwa na HAKI kunakuwa na amani na umoja na mshikamano.Kukiwa na ubaguzi kunakuwa na chuki visasi na utengano
 
Back
Top Bottom