Suala la LOLIONDO linaonyesha udhaifu wa Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suala la LOLIONDO linaonyesha udhaifu wa Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kashaijabutege, Mar 16, 2011.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Habari za Babu wa Loliondo nazipata kupitia vyombo vya habari. Sijawahi kuzungumza ana kwa ana na mtu aliyetoka "kwa Babu". Mrema na Chatanda wametoa ushuhuda wao kwenye TV; na wengine wengi wamefanya hivyo.

  Sikatai kwamba Babu anatibu kwa walio na imani. Wala sikatai kwamba Mrema, Chatanda na wengine wamepona. Aidha sikatai kuwa dawa ya Babu (Mthemanini-kama alivyoiita Lipumba) ameteshwa na Mungu. Yote nayakubali.

  Hata hivyo, mimi sifurahii kabisa hali inayoendelea Loliondo. Nilionalo ni kwamba Mungu ameamua kuiumbua serikali ya CCM. Kama viongozi walio na uwezo wa kwenda kutibiwa nje ya nchi wanapigana kupata KIKOMBE kwa Babu, sie wanyonge tusio na uwezo wa kununua hata dozi ya malaria itakuwaje?

  Nasikia viongozi "WAKUBWA KABISA" walishatangulia na wake zao.

  Watanzania wamekata tamaa.
   
 2. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Sio siri mi nashangazwa na kauli za muundo huu. Suala la babu la kutibu au kutotibu ni la kiimani zaidi wala tusiliongelee kisiasa au wanasiasa. Hapa hakuna maneno ya Lipumba eti wananchi wamekata tamaa ndo maana wamekimbilia kwa babu. Ni ufinyu wa kufikiri ktk imani,ugonjwa unaowapata akina prof.Lipumba,RA et all. Kama watu wametoka south africa,somalia,kenya ,rwanda na burundi iweje tukae na kusema eti ni kwa sababu ya uzembe ktk serikali? Madktari wa Muhimbili, kcmc n.k wameenda huko iweje sie tukae muhimbili ktk foleni! Hapana. Tusijadili imani na maono tukiunganisha wanasiasa!
   
 3. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tukubali kuna mvuto wa kimungu katika uponyaji huu!! Wanachokifanya akina lipumba, RA, mwingira, na wengineo i kuendeleza ile dhana kuwa "mtu hatukuzwi nyumbani kwake....ingawa thamani yake yaweza kuwa kubwa kusiko kwake...". Jambo hili ni la ki imani; lakini hata hivyo lina ukweli maana huweze kuendelea kuvuta maelefu ya watu kama wajao huko hawaponi au kupata "positive effect". Mungu abariki huduma hii kwani yaweza weka tanzania katika historia mpya duniani.
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280

  Hope so, kama hatutakuwa kichekesho dunianai!!
   
Loading...