Suala la kuwa na imani tofauti linapotatiza taasisi ya ndoa

Sipati picha mwislam anayeshika dini kutoka moyoni anawezaje ishi na mkristo kama mume/mke.

Mwanaume wa kislam anapokubali kufunga ndoa na mkristo sharti kwanza abatizwe, na anapokuwa anabatiwza anabatiwza kwa kukiri imani ya utatu mtakatifu wa Mungu. Mwislam akikubali hilo anakuwa amekufuru. Shughuri na maisha yote ya mwislam sharti ya ambatane na uwepo wa Allah na Mohamed kama mtume wake tofauti na hapo ni kufuru tupu.

Mwanaume wa kislama sharti watoto wake wazaliwe katika ndoa ya kiislam tofauti na hapo dini haito watambua hao watoto hivyo baba atakuwa hana uhalali nao katika maswala ya kulithi au kulithisha mali zake, hana pia uhalali wa kuozesha.

Mwanaume wa kiislam ni dhambi kubwa kufanya ngono nje ya ndoa ya kiislam.

Kwa minajili hii, uhalali wa mwanaume wa kiislam kuishi na mwanamke wa dini nyingine haupo. Hata hao waliozaa na wanawake wa kikristo alafu wakaanza kung'ang'ania watoto kwa kuwapa majina ya kiislama dini bado haiwatambui hao watoto na tena inawatambua hao watoto kuwa ni mali ya mama yao.

Tusidanganyane! Yoyote anayefanya haya anakuwa anafanya kinyume na dini ya kiislam na huesabiwa kama kafiri tu japo hafukuzwi msikitini kwa maana ya kuzidi kupewa muda wa kurekebisha makosa yake kabla hajafa.

Mwanamke wa kiislam naye pia haruhusiwi kabisa kufanya ngono nje ya ndoa ya kiislam lakini dini bado inatambua uhalali wa watoto wake katika maswala yote ikiwa ni pamoja na kulithi mali na kulithisha watoto ili mladi watoto ni waislam hatakama baba yao ni mkristo

Kwamaana hiyo ni bora mwanamke wa kiislam azae na mwanaume wa kikristo ili aendelee kuwa na uhalali na watoto kuliko mwanaume wa kiislam kuzaa na mwanamke wa kikristo na kupoteza uhalali wa watoto.

Nyinyi wanaume wa kiislam vichwa ngumu, siku mtakapo kufa mali mtakazo acha zitagawiwa (mirathi) kwa kufuata matakwa ya korani. Mtu asiyehusika hatapata hata kijiko labda uache umeshampa kabisa kama vile umetoa tu zawadi lakini ukiacha eti umeandika sijui eti wosia hiyo karatasi itachomwa moto, hayo hayatasikilizwa katika ugawaji wa mali.
Hivyohivyo zaa na mwanamke wa kikristo alafu mtoto aje afe aache mali nyingi wewe baba jina huto ambulia hata kijiko, mali zote atarithi mama mtu, wewe ponapona yako ukimbilie mahakama ya serikali isiyotambua dini ndio utapewa mgao.

Katika ukristo hakuna ndoa nje ya ukristo inayokubalika japo hakuna masharti sana kama kwenye uwislam, watoto waliozaliwa na wazazi wenye dini 2 tofauti bado huesabiwa kuwa ni mali ya wazazi wote wawili.

Hitimisho kama unataka kuitendea haki dini yako owa/olewa na mtu wa dini yako.
 
Watu wanapoteza muda na dini walizozikuta na watakazoziacha wakifa.

Binadamu ni kiumbe pekee anayejipa presha za bure kwa kuangaika na vitu visivyo na mantiki
 
muslim-family-at-eid.jpg

Kujadili dini ni mojawapo ya mijadala inayokwepwa na baadhi ya wanajamii ili kuepusha shari na kudumisha amani. Lakini linapokuja swala mahusiano hususan pale watu wawili wenye imani tofauti za kidini wanapotaka kuoana, unaweza kuzuka mjadala mzito miongoni mwa ndugu na jamaa wa wapenzi hao na wakati mwingine hata marafiki hutokea kupinga muunganiko huo.

Ninao mfano unaonihusu. Mdogo wangu anayenifuatia kuzaliwa alipata mchumba (mume) mwenye imani tofauti na imani yetu, jambo hilo lilizusha mtafaruku katika familia yetu kila mmoja akisema lake. Ilitokea tu mimi na baadhi ya ndugu zangu akiwemo baba tuliafiki ule muunganiko wao na ndoa ikafungwa na sasa ndoa yao ni imara na imetimiza miaka tisa mwaka huu wakiwa na watoto watatu.

Ukweli ni kwamba jambo hili limekuwa likileta mtafaruku katika baadhi ya familia na wakati mwingine familia hujikuta ikisambaratika hasa pale ambapo familia moja inashindwa kukubali utashi wa mtoto wao kuolewa au kuoa mtu mwenye imani tofauti na mara nyingi hii hutokea katika familia zenye msimamo mkali wa kidini. Kama inavyofahamika mapenzi ni kitu cha ajabu sana. Pale ambapo penzi linapochipua hufunika imani zetu kiasi cha kujikuta wakati mwingine tunazisaliti imani hizo ambazo hata hivyo baadhi yetu hazikuwa utashi wetu bali tu tumejikuta tukiwa humo kwa sababu ni imani ambazo tumezaliwa na kukuta wazazi wetu wakiwa ni wafuasi wa imani hizo.

family-praying.jpg

Huu ni mtihani mgumu sana kwetu na mara nyingi waathirika wa mtihani huu wengi wao ni wanawake na watoto ukilinganisha na wanaume. Wakati mwingine huwa najiuliza inakuwaje mtu anampata mpenzi anayempeda sana na mwenye sifa azitakazo lakini anashindwa kufunga naye ndoa kwa sababu ya kuwa na imani tofauti? Lakini pia wapo ambao wanalazimika kufunga ndoa na wapenzi wao sio kwa sababu wamependana, bali ni kwa sababu tu imani zao zinafanana…………!

Kuna wanawake wengi sana wa kiasi cha kutosha wanalazimika kuishi katika ndoa ngumu kwa sababu ya imani zao, kilichowavuta kuingia katika muunganiko huo ni imani zao lakini sio upendo. Lazima tukubali kwamba mapenzi ni kitu kingine na imani ni kitu kingine. Kuingia katika ndoa kwa kigezo cha imani kunakuwa na changamoto zake ambazo mara nyingi hazina matokeao mazuri.

Naamini hata humu JF wapo ambao wamewahi kukabiliana na mtihani huu au wako katika hati hati ya kukabiliana na mtihani huu. Hebu tupeane uzoefu juu ya jambo hili linalowatatiza wengi.

Swali: Iwapo wewe ni single, Je uko tayari kufunga ndoa na mtu mwenye imani tofauti na imani yako? Je umejiandaaje kukabiliana na changamoto za wazazi, ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla watakapopinga muunganiko wenu ?

Nisingependa mjadala huu uwe ni wa kidini.

Nadhani mmenielewa.........
watoto wa kike siku zote wanyenyekevu ukiweza kuishi nao vzr,mke wangu muislam mimi mkristo,hakuwa na shida wakati nataka kumuoa ila baba mkwe ndiye alikuwa anakazana nibadili dini lasivyo mke simpati,tumesumbuanaaaa mwishowe nikamwambia hapo mwanao alipo anamimba yangu miezi minne sasahivi......hapo ndio nilimkata maini kabisa,mkwe wangu ninaye ndani saivi na tunaishi vizuri bila tatizo lolote,na tumempatia wajukuu wawili,
 
Wote ni makafiri, hakuna mwenye dini hapo. Ndoa ilifungwa msikitini au kanisani? Najua haikufungwa popote pengine ni ya kiserikali. Wanapohitaji msaada au ushauri wa kiroho wanaenda wapi?
Hata wangefunga kanisani bado ni maqafir!
 
Dini haina nafasi kwa wapendanao
Nakubaliana na wewe, kwa wawili wapendanao dini inaweza isiwe na nafasi lakini inaweza kuwa na nafasi tena kubwa kwenye issue ya uimara wa familia husika - mfano, watoto watafuata imani ya baba au mama? nani atahamua ikiwa kila mmoja atataka wafuate imani yake?
 
Wote ni makafiri, hakuna mwenye dini hapo. Ndoa ilifungwa msikitini au kanisani? Najua haikufungwa popote pengine ni ya kiserikali. Wanapohitaji msaada au ushauri wa kiroho wanaenda wapi?

Kafiri ndo mtu wa aina gani mkuu??!!!!,binafsi mimi pia ni zao la ndoa baina ya mamaangu mkristo na babaangu muislam na ndoa ilifungwa kanisani,nilichokishuhudia kwa kipindi chote cha maisha yao ni Upendo wa dhati, utofauti wa dini haukuwa chochote katika maisha yao na mpaka kwetu watoto (tulichagua kusali kanisani) it never occured hata kufikiria utofauti wa dini ya wazazi wetu
 
udini utatuua

nilikuwa na mahusiano na mdada wa dini tofauti, mipango ya kujitambulisha imeanza dingi yake kupenyezewa habari akatoa msimamo wake.

"sitakuchagulia mume, kabila ila dini lazima awe........" nami si dini iyo.

tukashauriana na binti nimtie mimba jamaa yangu akanishauri yaweza tokea matatizo katika mimba, uzazi nao wamemtenga binti nitaweza yamudu. daaah tuliachana hivi hivi

aliye leta dini alituweza
 
Kafiri ndo mtu wa aina gani mkuu??!!!!,binafsi mimi pia ni zao la ndoa baina ya mamaangu mkristo na babaangu muislam na ndoa ilifungwa kanisani,nilichokishuhudia kwa kipindi chote cha maisha yao ni Upendo wa dhati, utofauti wa dini haukuwa chochote katika maisha yao na mpaka kwetu watoto (tulichagua kusali kanisani) it never occured hata kufikiria utofauti wa dini ya wazazi wetu
Ninamaanisha hawakiamini na kuishi kadri dini zao zinavyoelekeza. Ukristo unafundisha "..msifungiwe nira na wasioamini..." Najua hakuna kiongozi wa kikristo atakayefungisha ndoa ya watu wa dini tofauti kanisani kwa kuzingatia hilo. Hivyo ndoa kati yao ni uasi kwa agizo hilo. Naamini kwa upande wa pili ndivyo ilivyo pia. Swala la amani kati yao halimaanishi kuwa ni matokeo ya ucha Mungu.
 
muslim-family-at-eid.jpg

Kujadili dini ni mojawapo ya mijadala inayokwepwa na baadhi ya wanajamii ili kuepusha shari na kudumisha amani. Lakini linapokuja swala mahusiano hususan pale watu wawili wenye imani tofauti za kidini wanapotaka kuoana, unaweza kuzuka mjadala mzito miongoni mwa ndugu na jamaa wa wapenzi hao na wakati mwingine hata marafiki hutokea kupinga muunganiko huo.

Ninao mfano unaonihusu. Mdogo wangu anayenifuatia kuzaliwa alipata mchumba (mume) mwenye imani tofauti na imani yetu, jambo hilo lilizusha mtafaruku katika familia yetu kila mmoja akisema lake. Ilitokea tu mimi na baadhi ya ndugu zangu akiwemo baba tuliafiki ule muunganiko wao na ndoa ikafungwa na sasa ndoa yao ni imara na imetimiza miaka tisa mwaka huu wakiwa na watoto watatu.

Ukweli ni kwamba jambo hili limekuwa likileta mtafaruku katika baadhi ya familia na wakati mwingine familia hujikuta ikisambaratika hasa pale ambapo familia moja inashindwa kukubali utashi wa mtoto wao kuolewa au kuoa mtu mwenye imani tofauti na mara nyingi hii hutokea katika familia zenye msimamo mkali wa kidini. Kama inavyofahamika mapenzi ni kitu cha ajabu sana. Pale ambapo penzi linapochipua hufunika imani zetu kiasi cha kujikuta wakati mwingine tunazisaliti imani hizo ambazo hata hivyo baadhi yetu hazikuwa utashi wetu bali tu tumejikuta tukiwa humo kwa sababu ni imani ambazo tumezaliwa na kukuta wazazi wetu wakiwa ni wafuasi wa imani hizo.
family-praying.jpg

Huu ni mtihani mgumu sana kwetu na mara nyingi waathirika wa mtihani huu wengi wao ni wanawake na watoto ukilinganisha na wanaume. Wakati mwingine huwa najiuliza inakuwaje mtu anampata mpenzi anayempeda sana na mwenye sifa azitakazo lakini anashindwa kufunga naye ndoa kwa sababu ya kuwa na imani tofauti? Lakini pia wapo ambao wanalazimika kufunga ndoa na wapenzi wao sio kwa sababu wamependana, bali ni kwa sababu tu imani zao zinafanana…………!

Kuna wanawake wengi sana wa kiasi cha kutosha wanalazimika kuishi katika ndoa ngumu kwa sababu ya imani zao, kilichowavuta kuingia katika muunganiko huo ni imani zao lakini sio upendo. Lazima tukubali kwamba mapenzi ni kitu kingine na imani ni kitu kingine. Kuingia katika ndoa kwa kigezo cha imani kunakuwa na changamoto zake ambazo mara nyingi hazina matokeao mazuri.

Naamini hata humu JF wapo ambao wamewahi kukabiliana na mtihani huu au wako katika hati hati ya kukabiliana na mtihani huu. Hebu tupeane uzoefu juu ya jambo hili linalowatatiza wengi.

Swali: Iwapo wewe ni single, Je uko tayari kufunga ndoa na mtu mwenye imani tofauti na imani yako? Je umejiandaaje kukabiliana na changamoto za wazazi, ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla watakapopinga muunganiko wenu ?

Nisingependa mjadala huu uwe ni wa kidini.

Nadhani mmenielewa.........
Mkuu nakubaliana na wewe kwamba suala hili ni nyeti,na ni kweli pia kwamba limeleta maumivu mengi kwenye familia nyingi na hata wakati mwingine utengano kati ya watoto na wazazi.

Niseme hata hivyo jambo moja la msingi.Ni kwamba wote tungekuwa "wacha Mungu wa kweli na kufuata maaagizo yake kama yeye Mwenyewe alivyotaka," matatizo yote tunayoyapata yasingekuwepo.Mambo haya yameletwa na imani zetu za kijinga tulizojitungia, ambazo ziko kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu wa kweli.

Nisisitize bila woga kwamba mbinguni sio sawa na sokoni,ambapo unaweza kupitia kichochoro chochote na ukafika .Ipo njia moja tu ya kuingia mbinguni,ambayo ni kupitia kwa Bwana Yesu.Kama wote tungekuwa tunamwamini Kristo Yesu,matatizo yote haya na mengine mengi yanayoikumba dunia leo yasingekuwepo.The world is in chaos because we have chosen the wrong path in our journey to haeven.We as humanity have only two choices,we either go on with our chaotic world or choose Christ Jesus for an orderly world.The choice is ours,there is no shortcut.

Kwa wale ambao wamemchagua Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao,my strongest advice to them is this, do not marry outside your faith,because by doing so you will be inviting Satan into your life and household.
 
muslim-family-at-eid.jpg

Kujadili dini ni mojawapo ya mijadala inayokwepwa na baadhi ya wanajamii ili kuepusha shari na kudumisha amani. Lakini linapokuja swala mahusiano hususan pale watu wawili wenye imani tofauti za kidini wanapotaka kuoana, unaweza kuzuka mjadala mzito miongoni mwa ndugu na jamaa wa wapenzi hao na wakati mwingine hata marafiki hutokea kupinga muunganiko huo.

Ninao mfano unaonihusu. Mdogo wangu anayenifuatia kuzaliwa alipata mchumba (mume) mwenye imani tofauti na imani yetu, jambo hilo lilizusha mtafaruku katika familia yetu kila mmoja akisema lake. Ilitokea tu mimi na baadhi ya ndugu zangu akiwemo baba tuliafiki ule muunganiko wao na ndoa ikafungwa na sasa ndoa yao ni imara na imetimiza miaka tisa mwaka huu wakiwa na watoto watatu.

Ukweli ni kwamba jambo hili limekuwa likileta mtafaruku katika baadhi ya familia na wakati mwingine familia hujikuta ikisambaratika hasa pale ambapo familia moja inashindwa kukubali utashi wa mtoto wao kuolewa au kuoa mtu mwenye imani tofauti na mara nyingi hii hutokea katika familia zenye msimamo mkali wa kidini. Kama inavyofahamika mapenzi ni kitu cha ajabu sana. Pale ambapo penzi linapochipua hufunika imani zetu kiasi cha kujikuta wakati mwingine tunazisaliti imani hizo ambazo hata hivyo baadhi yetu hazikuwa utashi wetu bali tu tumejikuta tukiwa humo kwa sababu ni imani ambazo tumezaliwa na kukuta wazazi wetu wakiwa ni wafuasi wa imani hizo.
family-praying.jpg

Huu ni mtihani mgumu sana kwetu na mara nyingi waathirika wa mtihani huu wengi wao ni wanawake na watoto ukilinganisha na wanaume. Wakati mwingine huwa najiuliza inakuwaje mtu anampata mpenzi anayempeda sana na mwenye sifa azitakazo lakini anashindwa kufunga naye ndoa kwa sababu ya kuwa na imani tofauti? Lakini pia wapo ambao wanalazimika kufunga ndoa na wapenzi wao sio kwa sababu wamependana, bali ni kwa sababu tu imani zao zinafanana…………!

Kuna wanawake wengi sana wa kiasi cha kutosha wanalazimika kuishi katika ndoa ngumu kwa sababu ya imani zao, kilichowavuta kuingia katika muunganiko huo ni imani zao lakini sio upendo. Lazima tukubali kwamba mapenzi ni kitu kingine na imani ni kitu kingine. Kuingia katika ndoa kwa kigezo cha imani kunakuwa na changamoto zake ambazo mara nyingi hazina matokeao mazuri.

Naamini hata humu JF wapo ambao wamewahi kukabiliana na mtihani huu au wako katika hati hati ya kukabiliana na mtihani huu. Hebu tupeane uzoefu juu ya jambo hili linalowatatiza wengi.

Swali: Iwapo wewe ni single, Je uko tayari kufunga ndoa na mtu mwenye imani tofauti na imani yako? Je umejiandaaje kukabiliana na changamoto za wazazi, ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla watakapopinga muunganiko wenu ?

Nisingependa mjadala huu uwe ni wa kidini.

Nadhani mmenielewa.........
Kiukweli zamani watu hawakuwa na imani kali kama kipindi hichi. Kwa sasa imani zetu zimekuwa kama siasa. Si ajabu kukuta watu wa dini tofauti wakitoana povu kisa kuangalia weakness za dini nyingine, kulinganisha vitabu vitakatifu na kwa kuwa kila mtu kwa sasa hasa upande fulani kusoma sana biblia, hujikuta wakiona kuwa dini yao ndo ya kweli na yao kuonekana kuwa ni mkusanyiko wa vitabu na imeandikwa na watu tu huku yao ikionekana kuwa imeshushwa na mungu na hivyo haina maandiko toka kwa mzungu.

Ila ni ukweli usiopingika ukisoma kitabu chao tukufu, inakataza mtu mwenye imani hiyo kuoa, kummilikisha chochote kile na hata uzao wa watoto hao wote ni haramu unless kabla ya ndoa wote wawe ni dini moja. Tofauti na hapo utasikia kuwa unaitwa hawala na hakuna ndoa.

Yapo mengi ambayo kama wewe si mfuasi wa itikadi hyo basi wewe ni kafiri na km humuamini huyo mtume, unapaswa kuuawa.

Kutokea kwa matabaka ya vita ambayo wanaotekeleza hayo hupaswa kuuliza kwanza dini yako ndo uuawe, ni mfumo huo pia
 
Katika mahusiano, asilimia kubwa ya watu, kwao dini ni kipengele cha kutazama sana. Mimi binafsi ninapinga mtazamo huo. Dini hazikupaswa kutenganisha watu wenye mahusiano kutofunga ndoa. Kuna watu wanaweza kuwa na dini tofauti na wakaishi vyema pamoja.

Dini zinalazimisha watu kuwa kwenye dini moja ili kuhakikisha zinapata wafuasi. Lakini kiuhalisia, ndoa haiitaji dini moja ili kufungwa. Mungu hana dini, na unaweza kuwa na dini tofauti lakini bado ukawa unajiheshimu, muaminifu na ukawa na mapenzi ya dhati kwa mwenza wako.
Mkuu Siku hizi una amini uwepo wa Mungu?
 
mi sikubaliani na wewe hata kidogo,hizo ni hadithi tu za kufikirika,mi baba yangu ni muislam na mama yangu ni mkristo na ni mdini kweli kweli na wapo kwenye ndoa yao zaidi ya miaka 40....kwa ushahidi huu wa wazazi wangu unafikiri mi ntakuunga mkono?
Wewe umechagua kumfata baba au mama? hii haijaleta shida?
Kwa mfano majina yenu, kwenda kanisani au msikitini, sherehe zenu za kidini?
Naona giza...
 
Back
Top Bottom