Suala la kushirikishwa upandaji bei ya umeme, Profesa Muhongo mkweli?

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
18,173
13,776
Gazeti la Mwananchi limelivalia njuga suala la kushirikishwa au la kwa Waziri wa Nishati, Prof Muhongo, na kuonyesha kuwa, wadau wanasema alishirikishwa kikamilifu.

Prof Muhongo katika barua yake ya kusitisha upandaji wa bei ya umeme, yeye alisema hakushirikishwa.
Leo 13/1/2017 Pg 5, gazeti la Mwananchi limewakariri wadau tofauti na kusema
"Wachambuzi wamesema hakuna uwezekano kwa waziri Nishati na Madini kutoarifiwa kuhusu kupanda kwa bei ya umeme"

Prof Muhongo aweza kuwa anasema kweli?
 
c37080a5199c6bbb4332642417794bd7.jpg
eb0ae08cb41b68a547d38165f43fc75a.jpg
 
Asante sana kwa ufafanuzi.
Utekelezaji wa items no 2 na no 3, ie kuongeza ufanisi ndani ya TANESCO na kupunguza deni la TANESCO unaendelea vipi?
 
Hayo magazeti yasulubiwe tu!
Halafu hawa National Media tumewakosea nini sisi Watanzania hadi kutopotosha mbona huko kwao Kenya hawafanyi hivyo?
Kama Mwananchi wanaandika hisia zao tu, kama mzee JPM alivyosema, watatumbuliwa tu.
 
Umeme haujapanda Muhongo alitoa tamko hautapanda. Pia Umeme sasa ni wa uhakika watanzania mnataka nini zaidi ya Waziri kama Muhongo.
 
Muhongo alishiriki vizuri kabisa na barua ya Tanesco ilifika ofisini kwake. Tatizo ni wananchi walipiga kelele wakaona aibu na kuamua kuwakana wengine kwa manufaa yao.
 
Alishiriki, alijua kila hatua, ila kaamua kukwepa aibu ya kujiuzulu na hafukuziki si kweli kuwa kila aneharibu hufukuzwa kama tunavyo imbiwa wengine ni maswahiba.
 
Haw wkenya mzee awadabishe ili ifundisho htutki uchochez ktk nch y2 hao wenyew vkiharibika wnakmbilia hk halfu wnatka na cc tuw km wao km vp wfungiwe maishat
 
Hayo magazeti yasulubiwe tu!
Halafu hawa National Media tumewakosea nini sisi Watanzania hadi kutupotosha mbona huko kwao Kenya hawafanyi hivyo?
Hilo gazeti ni la Agha khan sio la Kenya sema office kuu zao zipo Nairobi kwa kanda hii.
Hata hivyo kwa hili la muhongo cpat shida Sana coz nakumbuka enz za escrow Dr hamis kigwangala alitudhibitishia kwa maneno na documents kuwa hajawah kumuona prof muongo kama prof Muhongo.
 
Back
Top Bottom