Suala la kurekebisha katiba halihitaji dharura hii inayoonyeshwa na serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suala la kurekebisha katiba halihitaji dharura hii inayoonyeshwa na serikali

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Ntemi Kazwile, Apr 7, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa mara nyingine tena tunashuhudia jinsi serikali yetu isivyo na vipaumbele, suala la katiba ni suala la haraka lakini siyo kwa namna ya dharura ya serikali.

  Muswada ambao tunatakiwa tuujadili tarehe 7 & 8 April ndio utatufikisha kwenye katiba mpya ajabu ni kwamba ni Dodoma na Dar es Salaam tu ndio wamepewa fursa ya kutoa maoni yao, na kibaya zaidi kwa kipindi kifupi sana (leo kuna taarifa kuwa Dodoma kuna vurugu kwa sababu watu ni wengi kuliko ukumbi uliotengwa).

  Kwa nini maeneo mengine hayajasikilizwa? Kila eneo lina changamoto za aina yake na kwa muswada wenye uzito wa aina hii ulipaswa usiwe wa dharura kiasi hiki na wadau wote angalau wapate muda wa angalau mwezi mmoja kuujadili na kutoa mapendekezo yao, siyo siku moja.. ina maana watanzania wanaoishi Kigoma, Musoma, Lindi, Wete, Namanga, kwa mfano hawana haki ya kusikilizwa. Au watanzania wanaoishi vijijini (zaidi ya 80% ya watanzania) hawana umuhimu kwenye huu mchakato wa katiba?

  Napendekeza wabunge wakatae dharura ya aina hii ili wadau wapewe angalau mwezi mmoja kuchangia mawazo yao.....
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka waziri kombani aliwahi kusema kuwa,wafadhali wanataka kuona serikali inasikiliza kilio cha wananchi kuhusu katiba labda ndio sababu wanataka wasije wakaktwa panga kwenye budget ijayo,kwa sababu siwezi kuamini kwamba wameshindwa kuwatuliza wanachi mpaka wawalipulie mabomu kwa nini hakuahirisha na kutafuta eneo linalo faa,hii ndio serikali na bunge wasiojali wananchi wake wakati wenyewe waliwaita
   
 3. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Kwa mimi hapa nailaumu sana chadema, they are coz of all these, how? they do believe that katiba ikibadilishwa haraka kabla ya uchaguzi ujao kuwa watashinda, which is never.

  Nawalaum CDM kwa sababu suala la katiba wanataka kulipeleka kisiasa zaidi. Na kwa sababu hiyo ccm na chadema wanacheza na akili za watanzania walio wengi ambao hawajawashitukia interest zao za kisiasa kuwa ndio ziko juu kuliko uhalisia. Mie nilitarajia jopo la wanaharaki toka taasisi na dini zote wateuwe wawakilishi watao simamia kazi ya kukusanya maoni ya wananchi nchi nzima kwa kupita mijini na vijijini, kisha wacompile na kuchambua maoni yote kisha watoe pre katiba igawiwe kwa wananchi waisome kisha wapite tena kusikiliza wananchi wamekosoa wapi kisha kufanyiwa marekebisho na kamati.

  Kwahiyo itachukua muda na siyo kama chadema wanavyotaka, wanakosea sana.
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  lakini walipanga mda wa kusikiliza hayo maoni sio chadema,na walie andaa mswada pia sio chadema ni serikali iliyopo madarakani ikiongozwa na chama kilichoshinda nafasi ya Uraisi

  kwa hiyo wakulaumu hapo ni waziri husika na wabunge kwa ujumla waliokubaliana na ratiba nzima ya ukusanyaji maoni
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  "Wadanganyika " wenzangu...CCM will never ever make the process fair, neither will they dig their own grave....

  Hii katiba ijayo ndiyo itakayoleta nchi moja, serikali moja chini ya CCM.

  Siku nyingi sana tumesema lakini watu wao wameamini CDM makini, wakasahau CCM ni master wa kumanipulate kila kitu.

  If still people believe there will be a peoples Katiba, we may well wake up now!
  If people believe we will get independent Electoral commission, I am not one of those.
  If people belive CCM led gvt will do anything to lay fair ground for political parties to operate....then that person should go to "kupata kikombe" kwa Babu.

  Tulisema CCM wameshateka nyara mjadala wa katiba and the end product even if they promise a new katiba ,will be a newly fashioned to favor CCM Katiba.
  Now you start seeing and understand.

  Yet some people were saying, CCM will soon be gone!!! Do we realise how difficult it is now to get rid of CCM?
  Yet opposition prefer to be / stay divided.
   
 6. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kinachofanyika sasa ni usanii mtupu; muswanda huu kama ulivyokaa haupashwi kujadiliwa na wananchi. Kama tungelikuwa na bunge makini ungelikataliwa na kurejeshwa serikalini katika ngazi ya kamati ya sheria.
   
Loading...