Suala la kuondoa wamachinga maeneo hatarishi

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Historia ya Wamachinga inaanza karne ya 20 ambapo kundi hili la wachuuzi lilitembeza bidhaa ndogondogo kama nguo,vyombo,na mitumba mitaani na majumbani kutafuta wateja ili kujipatia kipato cha kumudu maisha yao ya kila siku.Wamachinga wamekuwepo miaka mingi na wamekua wakifanya biashara zao katika mfumo huo.Mfumo wa ufanyaji huu wa biashara umebadilika kutokana na sababu nyingi.

1.Sababu za kisiasa-
Katika karne ya 21 kundi hili la vijana liliongzeka kutokea mikoa ya kusini na baadhi ya mikoa mingine na kuwa kubwa na lenye ushawishi wa kisiasa kutokana na maeneo yao ya biashara kuwa mijini.Kundi hili lilianza kushiriki katika siasa na kutoa ushawishi mkubwa kwa watu wa mijini.Wanasiasa katika nyakati tofauti wamekaua wakiwatumia wamachinga katika kampeni zao na kuwarejeshea fadhila ya kufanya biashara bure katika maeneo ya mijini.Kwa wale wanasiasa wasio na dola wamekua wakiwaahidi ahadi za kuwapa mitaji na kuwaruhusu kufanya biashara bure maeneo ya mijini.

2.Sababu za kibiashara-
Uwepo wa wamachinga kipindi cha nyuma ulikua kero kubwa kwa wafanyabiashara wale waaminifu na wanaolipa kodi na wale wasio waaminifu,baada ya muda kundi la wafanyabiashara wasio waaminifu walitumia wamachinga kama fursa badala ya tishio kwao kwa kuwatumia kukwepea kodi.Wafanya biashara wasi waaminifu walileta mali na kuzihifadhi kwenye magodown na kusambaza kwa wamachinga ambao waliuza mali zile bila kulipa kodi.Utaratibu huu upo maeneo mengi ya mijini na unafanywa na wafanyabiashara wakubwa wenye mitaji mikubwa.

3.Ukosefu wa ajira.
Wanaojiita wamachinga kwa sasa ni vijana wa kitanzania wanaojiajiri kupitia biashara za mitaji midogo na kukua katika mitaji mikubwa,wapo wanaoanza biashara hizi kwa mitaji ya milioni mpaka milioni ishirini.Niliwahi kufanya utafiti wa kupata meza katika mitaa ya kariakoo karibu na soko kuu.Meza yenye urefu na upana wa mita mbili kupata pakuweka ni kiasi cha milioni sita,hiyo unapata kadi ya machinga pamoja na haki zako zote.

Kutokana na sababu hizo na zingine ambazo sijaziweka ni wazi kuwa wengi wanajiita wamachinga sio kweli ni wamachinga bali ni wafanyabiashara wa kati ambao wanapitia kivuli cha umachinga kufanya biashara zao bila kulipa kodi. Uwepo wa wamachiga kwa sasa katika maeneo mengi ndio kichocheo kikubwa cha wizi wa mali za wafanyabiashara,wizi wa mifukoni kutokana na msongamno,na baiahara zingine za magendo katika maeneo mbalimbali ya mijini.Uwepo wa wamachinga unachangia kwa kiasi kikubwa foleni za barabarani na ajali nyingi katika maeneo ya mjini.Uwepo wa wamachinga unachangia uchafuzi wa mazingira na uholela katika kuweka maeneo safi.Yapo madhara mengi ya uwepo wa wamachinga katika maeneo mengi.

Mbinu wanazotumia viongozi wa serikali kuwaondoa wamachinga katika maeneo yasiyo rasmi bado sio mbinu zenye tija kwa mtizamo wangu.Niwape mbinu mbili za kuondosha biashara holela na ukwepaji wa kodi kwa wafanyabiashara.

1.Utumiaji wa Teknolojia
SErikali iweke mfumo maalumu wa kielekroniki wa kuwaweka watu katika maeneo yanayoruhusiwa kufanya biashara kwa wamachinga.Mapping of Machinga.Mfumo huu unakua na eneo na kitambulisho cha machinga kinachoonesha eneo analopaswa kufanyia kazi.Vitambulisho vya machinga viboreshwe

2.Kuhusisha Wananchi
Wananchi wahusishwe kwenye kuondoa wamachinga maeneo hatari ambayo yhayapaswi kufanya biashara.Wananchi walazimishwe kutokununua katika maeneo hayo na kama wakinunua kupigwa faini.Hli litawaondoa wamachinga maeneo hayo na kuwapeleka kule ambapo wanachi wanaruhusiwa kununua.

3.Yaanzishwe maeneo mengi ya kufanya bishara za wachuuzi na yasimamiwe

Ahsante
 
Back
Top Bottom