Suala la kufuta wakuu wa wilaya.... Je? linaubaya wowote,

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,338
Mambo ambayo Chadema wangeyafanya ni pamoja na kufuta hiki cheo cha wakuu wa wilaya ili kubana matumizi.

Hata wale ambao hawapendi Chadema (Ushabiki Pembeni), Jambo hili naona lina manufaa na more positives than negatives. Hata wale wanaounga mkono kazi hii ya wakuu wa wilaya naomba mnifahamishe ni nini kazi ya hawa watu na Je? kazi hii haiwezi kufanywa na mtu mwingine?

Na Hivi vyeo vya Acting District Commissioner whats it all about? Dont even start me kwenye kuongeza wilaya na Mikoa inayoongezwa kila siku..Why?
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,676
2,189
Kuna mzee nilikuwa naongea nae jana alikuwaga MKUU WA IDARA apo DSM akasema DC hana kazi yoyote zaidi ya kutengeneza majungu ya apa na pale
 

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,338
Kuna mzee nilikuwa naongea nae jana alikuwaga MKUU WA IDARA apo DSM akasema DC hana kazi yoyote zaidi ya kutengeneza majungu ya apa na pale

Its about time tuanze kuelewa kazi za hawa watu, mimi hata DC wangu simjui..... Na sioni ningepungukiwa nini kama angekuwa hayupo
 

Mtemakuni

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
258
22
Me nadhani katika sehemu ambapo serikali inapoteza bilions of money for nathing ni kwenye hiki cheo...!
kwenye wilaya kuna watu wanaitwa ma DED(wakurugenzi) hawa ndo watendaji wakuu humu wilayani, na ndo wanaosimamia na kuidhinisha kila kitu sa me nashangaa mkuu wa wilaya wa nini tena???????
Achilia mbali maadimistrator kibao walioko huku ie DAS hawa wanatosha jamani hizi hela nyingine zingetumika katika kuleta maendeleo kama kujenga shule, kuchimba visima badala ya kuajiri watu wasiona kazi za kufanya zaidi ya kusaini saini tu na kusafiri..!

kwa maoni yangu hiki cheo hakipaswi kabisa kuwepo unless otherwise kimewekwa kwa aji ya kuwapooza wahanga wa siasa i.e nape na pia as a present kwa makada wazuri wa sisiem....!:whoo:
 

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,338
Jamani kwa anayejua hawa watu wanakazi gani... na je hawa pia wanalipwa maposho makubwa.... isije ikawa ninalalamika bure kumbe mshahara wao ni kama wa waalimu
 

Questt

JF-Expert Member
Oct 8, 2009
3,010
422
Hawana Kazi??? unafikiri CCM inashinda kupitia watu gani???? Hata Masha leo kang'oa vitasa vya Ofisi ya Mbunge wa Nyamagana na alipoulizwa akasema Muulizeni Mkuu wa Wilaya......bado hujajua wana Kazi gani???? Waulize wagombea wa Upinzani watakuambia kazi ya mkuu wa wilaya....kifupi ndo CCM inashinda kupitia watu Hao......
 

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,338
I know practically hawana kazi..... ila je wakati hiki cheo wanakijustify walidanganya kwamba hawa watu wanafanya nini... Honestly i think balozi wa nyumba kumi used to have more work than hawa watu
 

fikramakini

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
247
60
mi nakumbuka enzi nikiwa mdogo nilikua namwona mkuu wa wilaya kwenye mbio za mwenge tuu, tehe tehe tehe
 

Double X

Senior Member
Nov 4, 2010
184
3
Hiki cheo cha ukuu wa wilaya hakifai kabisa, hawana kazi yoyote, kazi zote zinafanywa na wakurugenzi wa halmashauri,kifutiliwe mbali.
 

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,338
Hivi na hawa wanapewa mashangingi au? Naomba kama kuna mkuu wa wilaya humu jamvini aje atwambie mwaka jana alifanya mambo mangapi am sure all that could have been done in a day ukitoa kuhudhuria sherehe na ufunguzi wa vitu
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom