Suala la kubariki ndoa katika dhehebu la waadventista Wasabato

shibela

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
687
2,274
Habari wana JF,naomba msaada kwa Wanaofahamu,mfano mwanamke na mwanamume wameanza kuishi pamoja kwa ndoa ya bomani,je kwa taratibu za kisabato wanaruhusiwa kwenda kubariki ile ndoa kanisani na ikafungishwa bila shida yoyote mbele ya kanisa na mashahidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF,naomba msaada kwa Wanaofahamu,mfano mwanamke na mwanamume wameanza kuishi pamoja kwa ndoa ya bomani,je kwa taratibu za kisabato wanaruhusiwa kwenda kubariki ile ndoa kanisani na ikafungishwa bila shida yoyote mbele ya kanisa na mashahidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inakuwaje kuwa wewe ni msabato alafu hujui sheria zenu?? Kwa swali lako ni hapana, ni mpk uhudhurie darasa la ubatizo kwa mda flan, then baada ya hpo ndio unabatizwa, then tangazo la ndoa linatolewa kanisan kama hakuna pingamizi lolote ndoa inafungwa, so kama ilishafungwa bomani hilo halitambuliki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ninavyofaham.
Ndoa ya bomani inatambulika ila kama wewe siyo Msabato unapaswa kujihudhulisha kanisani then utapelekwa kwa darasa la kujifunza Biblia kwa muda flani, ukishaelewa Biblia na Imani ya wasabato ndipo unazamishwa kwa maji a.k.a UBATIZO hapo ni bega kwa bega na mkwe wangu.


Zoezi hilo likiisha unakaa na mchungaji wa kanisa utakalokuwepo anakupa mashauri/nasaha kisha mnabarikiwa na kusepa zenu kuijenga familiar.

NB. Kanisa halina cheti kingine cha Ndoa zaidi ya kile kinachotolewa na serikali.
 
Ndoa ya bomani inatambuliwa na kanisa LA waadventista wasabato. Kwa sababu hata wachungaji wanaofungisha ndoa wanafanya hivyo kwa mamlaka waliopewa na serikali. Na Vyeti wanavyotoa hutolewaga na serikali. Hivyo kama wewe siyo mwadventista ukiamini kuwa mwadventista kama ndoa yako ni halali itatambulika kanisani. Ila ukishabatizwa unaweza kuomba kubariki ndoa ingawa hutapewa cheti kipya cha ndoa maana umeishapewa. Lakini kama ulikuwa msabato ukatenda dhambi kisha kuamua kwenda kufunga bomani itabidi ufutwe ushirika ubatizwe upya lakini ndoa hiyo itatambuliwa ikiwa ni ya mke mmoja.
 
umesahau walipiga kambi airport wakisema wametumwa kwenda Ulaya na Arabuni kueneza injili, na hawakuwa na passport, hela wala visa, wamesema wameambiwa lazima wafike huko.

SASA huo si uwendawazimu , mpaka wakatimuliwa na polisi
Wale walikua wanajiita wasabato masalia sasa usijumlishe mambo kienyeji.kila dhehebu au dini kuna watu wenye matatizo yao sasa haimaanishi baadhi ya watu kukengeuka nakuanzisha taratibu zao ndo hiyo taasisi au jumuia nzima iko ivyo.
 
Hapana lakini nataka kuwa msabato

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wewe siyo Mwaadventista Wasabato utabatizwa na kubarikiwq ndoa yako.
Utabatizwa kwa sababu hujakiri matakwa ya Kikanuni.
Kanisa la Waadventista Wasabato wanatambua aina tatu ya Ufungaji ndoa.
1.Ndoa iliyofungwa kanisani
2. Ndoa serikali maarufu ndoa ya Bomani
3. Ndoa ya Kimila.
Kama wewe ulioa kabla hujawa muumini baada ya kubatizwa unaendelea na ndoa yako kama kawaida.
Kama wewe ni muumini lakini pia ukaoa Kimila au Bomani pia unaruhusiwa kubarikiwa ndoa yako bila kubatizwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom