Suala la kuajiri kwa kutaka mtu awe kapitia JKT liangaliwe upya, JKT huwa hawachukui wote wanaomaliza kidato cha sita mafunzoni

Ni kawaida Kila mwaka JKT kuchukua wanafunzi wa kidato Cha sita na kuwapangia kambi za mafunzo ya JKT wanakotakiwa kuripoti.Lakini huwa hawachukui wote waliomaliza form six huchukua wachache na wengine kuachwa

Sasa linapokuja suala la ajira mtu hutakiwa awe na cheti Cha JKT Sasa huyo ambaye hakupewa hiyo nafasi inakuwaje ? Sababu si kuwa aligoma kwenda Bali hakupata nafasi .
Kwanza tujiulize vigezo vinavyotumika kuwachagua wa kwenda jkt. Kama ulivosema si wahitimu wote huenda, nafasi ni chache, japo pia ndani ya walio chaguliwa wengine hukwepa kwenda. Nafasi za kazi nazo ni chache, hata hao wanao kuwa wameitwa jkt si wote wanao chukuliwa. Kwa kazi serikalini naunga mkono hoja, kuwachukua waliopitia jkt ni sahihi.
 
In fact ni ubaguzi. Kuna wengine kwa sababu za hali zao kiafya na kimaumbile (wenye ulemavu kwa mfano) hawawezi kwenda JKT, ina maana hawatapata ajira hizo husika?
Wakati wa wito kwenda jkt, wenye ulemavu hutaarifiwa kambi ya kwenda, japo sikumbuki jina. Si kweli kwamba walemavu wote hawaendi jkt.
 
Ni mtu kwenda mahakamani kufungua maombi kutaka mahakama imuamuru mtoa tangazo kufuta ama kurekebisha tangazo kwa kuondoa hicho kigezo.

"Ila sasa ndio hivyo wanyonge sisi" (kwa sauti ya Nyerere)
Kila kazi huwa na vigezo vyake. Kuna siku walokole wataenda mahakamani kudai waruhusiwe kujiunga na jeshi lakini mahakama iamuru wasiende vitani.
 
Kama hukujua now you know.
Ni ujinga iwe inatangazwa wazi kuwa yeyote hata Kama hayuko kwenye list ya walioitwa JKT aende usiri wa Nini? Mnataka watoto wenu watukutu walioshindikana Kota za Jeshi na polisi na shule ndio waende au? Maana huko ndiko mitoto mitukutu inakopatikana
 
Hiyo inajulikana hata kama haipo rasmi. As a matter of fact, inatokea miaka yote tangu 2013, hasa baada ya kuwepo na tetesi kuwa usipopita JKT hauwezi kuajiriwa.
 
Kama hukujua now you know.
Mjiandae safari hi mkitoa List jiandaeni maelfu ambao hamkuwa list kujiunga na JKT kujaa kambi za JKT.Asante kutuonyesha kuwa Kuna mlango wa siri mlificha kuwa mtu hata Kama hayuko kwenye List ruksa kuripoti kambi yoyote
 
Hiyo inajulikana hata kama haipo rasmi. As a matter of fact, inatokea miaka yote tangu 2013, hasa baada ya kuwepo na tetesi kuwa usipopita JKT hauwezi kuajiriwa.
Uwazi kitu Cha muhimu Sasa ona watoto wa masikini kibao wasiokuwa informed wamesoma Hadi vyuo vikuu wanaachwa kwenye ajira wakati hawakuchaguliwa kwenda JKT na hawakujua kuwa waweza ingia kupitia mlango wa nyuma ili nao waajirike mbeleni .This is unfair.Mtoto Yuko kijijini kamaliza form six ana kabando ka Mia tano anacheki list anajiona hayumo si anajua basi Tena hatakiwi JKT? Waliojua haya watakuwa watoto wa mjini na wenye ndugu kwenye majeshi.Haiko sawa
 
Ni kawaida Kila mwaka JKT kuchukua wanafunzi wa kidato Cha sita na kuwapangia kambi za mafunzo ya JKT wanakotakiwa kuripoti.Lakini huwa hawachukui wote waliomaliza form six huchukua wachache na wengine kuachwa

Sasa linapokuja suala la ajira mtu hutakiwa awe na cheti Cha JKT Sasa huyo ambaye hakupewa hiyo nafasi inakuwaje ? Sababu si kuwa aligoma kwenda Bali hakupata nafasi .
Tatizo sheria nyingi zinatungwa bila kuangalia mazingira ya jamii kwa wakati husika
 
Una taarifa na ulichochangia, au umekurupuka?

Ajira zinazohitaji kupita JKT ni hizo za vyombo vya ulinzi na usalama, ambazo kiuhalisia nyingi (ukiacha IT) zinahitaji usiwe na ulemavu wowote.

Siku nyingine tafuta taarifa kabla ya kuchangia. Siyo kila mada lazima uchangie.
Sahihi mkuu
 
Mjiandae safari hi mkitoa List jiandaeni maelfu ambao hamkuwa list kujiunga na JKT kujaa kambi za JKT.Asante kutuonyesha kuwa Kuna mlango wa siri mlificha kuwa mtu hata Kama hayuko kwenye List ruksa kuripoti kambi yoyote
Huwa wana-report kila mwaka boss, hata kama hawajapangiwa.
 
Uwazi kitu Cha muhimu Sasa ona watoto wa masikini kibao wasiokuwa informed wamesoma Hadi vyuo vikuu wanaachwa kwenye ajira wakati hawakuchaguliwa kwenda JKT na hawakujua kuwa waweza ingia kupitia mlango wa nyuma ili nao waajirike mbeleni .This is unfair.Mtoto Yuko kijijini kamaliza form six ana kabando ka Mia tano anacheki list anajiona hayumo si anajua basi Tena hatakiwi JKT? Waliojua haya watakuwa watoto wa mjini na wenye ndugu kwenye majeshi.Haiko sawa
Nilijua hiki kitu nikiwa shuleni. Huko mashuleni tunaambizana sana, na kweli tulikuta ndiyo uhalisia.
 
Ni kawaida Kila mwaka JKT kuchukua wanafunzi wa kidato Cha sita na kuwapangia kambi za mafunzo ya JKT wanakotakiwa kuripoti.Lakini huwa hawachukui wote waliomaliza form six huchukua wachache na wengine kuachwa

Sasa linapokuja suala la ajira mtu hutakiwa awe na cheti Cha JKT Sasa huyo ambaye hakupewa hiyo nafasi inakuwaje ? Sababu si kuwa aligoma kwenda Bali hakupata nafasi .
Yehodaya na wewe unataka kazi? wakati juzi kati ulileta uzi hapa ukiwabeza vijana kwamba uliwafanyia interview ya kazi na kuwauliza noti ya shilingi elfu kumi ina mnyama gani wakashindwa kujibu.

Ni nini kilikukuta mkuu.
 
Kwani ajira zotee zinahitaji mtu awe amepita jkt? Kwa ambae hajapita jkt ataomba sehemu ambazo hazihitaji sifa za kupita jkt.Over! Ajira zipi zinahitaji mtu awe kapita jkt?
Sasa uhamiaji na kupitia JKT wapi na wapi kwa mfano??
 
Wameandika ktk documents zao za ajira, hadi wenye vyeti vya udereva basic, fundi wa veta hizo sio degree wqlq masters, nk hivyo na wenyewe wameangaliwa muhimu ni jkt

Polisi waliajiri watu walio pitia JKT na wenye taalma ambao hawa kupita JKT kama sikosei usaili wamefanyia DSM, wajkt wamefanyia ktk makambi na mikoani

Serikali ipo makini ina tambuq wimbi la wasio na ajira

Tukumbuke vijana wengi walio JKT walirejeshwa makwao na jamii ilipaza sauti, serikali ikawasikia na kuwarejesha makambini na sasa wana waajiri lakini naona ni kama jamii ile ile haitak mfumo huo
Bado haihalalishi kuchukua hao wa jkt ajira zitolewe atakayeshinda usahili achukuliwe tu Sasa bila jkt huitwi interview na una vigezo vingine vyote why wasikuchukue wamekazania jkt, hizo mambo ndio zinazouaga ubunifu maofisini maana watu waishi Kwa ku cremisha tu na sio competency
 
Yehodaya na wewe unataka kazi? wakati juzi kati ulileta uzi hapa ukiwabeza vijana kwamba uliwafanyia interview ya kazi na kuwauliza noti ya shilingi elfu kumi ina mnyama gani wakashindwa kujibu.

Ni nini kilikukuta mkuu.
Wapi nimesema nataka kazi? Umelewa au ? Nini? pombe sio chai acha pombe
 
Back
Top Bottom