Suala la kuajiri kwa kutaka mtu awe kapitia JKT liangaliwe upya, JKT huwa hawachukui wote wanaomaliza kidato cha sita mafunzoni

TISS na Takukuru chukueni majina yote ya waliojiunga nje ya kuitwa JKT walioingia kinyemela mlango wa nyuma walioomba kazi serikalini I smell a rotten rat somewhere Kuna watu waweza kutaka kupenyezwa ndani ya system ya nchi kupitia dirishani badala ya mlangoni .TISS scrutize kila aliyepitia dirishani badala ya mlango official wa kuitwa ku report kambi za JKT .
What a paranoid soul! Ni kitu kinachojulikana, ninakushangaa haukujua muda wote huo. 😀
 
Hapo kujipeleka Ndio Kuna maneno

Form six umeacha kuwachukua kibao halafu watu hawajaripoti kwa Nini usiite wengine uingize watu wapya gizani? Kuna maneno TISS wote walioomba kazi serikalini ambao walioingia JKT kupitia gizani bila official wito wa JKT wapigeni chini
Sijakuelewa...nachojua Mimi jkt huwa wanatangaza second selection baada ya wiki3 wakiona namba haijatimia....halafu watu kibao Tu sio hata TISS huwa wanajipeleka...Mimi mwenyewe kambi nliloenda sikuchaguliwa huko nlichaguliwa kwingine lakini Wala hata sikuulizwa ,nilipofika wakatuandika majina Tu tukaanza mzigo...walkuja kuanza kufatilia majina ya Ambao hawakuchaguliwa Hilo kambi kipindi cha ugawaji wa posho mwisho wa mwezi Na wote tuliozamia tukaandikwa majina ili posho yetu iletwe Basi. Wala hawakuwahi kutuuliza kwanini tumekuja apo
 
Ni kawaida Kila mwaka JKT kuchukua wanafunzi wa kidato Cha sita na kuwapangia kambi za mafunzo ya JKT wanakotakiwa kuripoti.Lakini huwa hawachukui wote waliomaliza form six huchukua wachache na wengine kuachwa

Sasa linapokuja suala la ajira mtu hutakiwa awe na cheti Cha JKT Sasa huyo ambaye hakupewa hiyo nafasi inakuwaje ? Sababu si kuwa aligoma kwenda Bali hakupata nafasi .
Hivi,kuna watu walikaa mahali na kuja na hayo maelekezo kwenye tangazo au limetengenezwa sehemu fulani tu?
Kwamba watengeneza tangazo hawana ndugu ama watoto wao watakaoathirika kwa mtindo huu?
 
Mawazo ya kitumwa tumwa haya,
Wakenya huwa wanasema kuandikwa kazi
Wewe beba mikanda miwili, soksi jozi mbili,
Mifuko miwili, vikombe viwili hata vya plastiki, sahani mbili simama barabarani tayari unapiga pesa
 
In fact ni ubaguzi. Kuna wengine kwa sababu za hali zao kiafya na kimaumbile (wenye ulemavu kwa mfano) hawawezi kwenda JKT, ina maana hawatapata ajira hizo husika?
JKT ya mujibu wa sheria haijalishi una ulemavu wa viungo wote Wana hudhuria kozi,
 
Kwani ajira zotee zinahitaji mtu awe amepita jkt? Kwa ambae hajapita jkt ataomba sehemu ambazo hazihitaji sifa za kupita jkt.Over! Ajira zipi zinahitaji mtu awe kapita jkt?
JWTZ kwa recruit ambao hawana diploma kupanda juu huwa lazima awe amepita JKT na Hawa wa diploma, degree, masters nk huwa ni special intake ndio maana hawaweki ulazima wa kipengele Cha kupita JKT
 
Bado haihalalishi kuchukua hao wa jkt ajira zitolewe atakayeshinda usahili achukuliwe tu Sasa bila jkt huitwi interview na una vigezo vingine vyote why wasikuchukue wamekazania jkt, hizo mambo ndio zinazouaga ubunifu maofisini maana watu waishi Kwa ku cremisha tu na sio competency
Ni vigezo vimewekwa, tuna weza kubaliana hata ambaye hana cheti nae ashindane na wenye vyeti... Taifa letu sote hivyo kujenga au kubomoa ni juu yetu
 
Kwani ajira zotee zinahitaji mtu awe amepita jkt? Kwa ambae hajapita jkt ataomba sehemu ambazo hazihitaji sifa za kupita jkt.Over! Ajira zipi zinahitaji mtu awe kapita jkt?
Kama vile magereza,police,na uhamiaji sifa mojawapo uwe umepitia jkt na aliyemaliza mgambo yeye hapana wakati wote wanafundishwa na jesh la wananchi hii imekaaje Ina maana washauri wa mgambo mkoa na wilaya msisumbue vijana kucheza mgambo maana mmeshindwa hata kuwatetea serikali kupata ajira shame in you
 
Ni vigezo vimewekwa, tuna weza kubaliana hata ambaye hana cheti nae ashindane na wenye vyeti... Taifa letu sote hivyo kujenga au kubomoa ni juu yetu
Kikubwa inputs za mtu na ubunifu in problem solving tu basi
 
Back
Top Bottom