Suala la kuajiri kwa kutaka mtu awe kapitia JKT liangaliwe upya, JKT huwa hawachukui wote wanaomaliza kidato cha sita mafunzoni

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
30,438
2,000
Ni kawaida Kila mwaka JKT kuchukua wanafunzi wa kidato Cha sita na kuwapangia kambi za mafunzo ya JKT wanakotakiwa kuripoti.Lakini huwa hawachukui wote waliomaliza form six huchukua wachache na wengine kuachwa

Sasa linapokuja suala la ajira mtu hutakiwa awe na cheti Cha JKT Sasa huyo ambaye hakupewa hiyo nafasi inakuwaje ? Sababu si kuwa aligoma kwenda Bali hakupata nafasi .
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,612
2,000
Ni suala la uvunjifu mkubwa wa haki za kikatiba. Nilitegemea angalau CSOs zikemee hili na hata kulifikisha mahakamani. Halikubaliki.
 
cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
20,782
2,000
Hicho kigezo Cha jkt ni Cha kufutwa na uonevu mtupu hafu pia Kuna watu walioanzia certificate mpaka bachelor kwahyo wakose nafasi kisa jkt, na vigezo vingine wanavyo plus uzoefu na ubunifu wa kazi?

Vyombo vya ulinzi wafikirie hili na watafte watu competent based on talents kupitia jkt pekee hakiwezi kuwa kigezo kikuu huo ni uonevu flani
 
cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
20,782
2,000
In fact ni ubaguzi. Kuna wengine kwa sababu za hali zao kiafya na kimaumbile (wenye ulemavu kwa mfano) hawawezi kwenda JKT, ina maana hawatapata ajira hizo husika?
Hata kazi nyingine za serikali kipindi cha Magu ilikuwa lazima mtu apitie jkt huo ni ubaguzi hivi competency ya mtu inapimwaje na kuwa judged eti mtu kuwa na cheti Cha jkt pekee na kuacha wenye degree. Serikali iache huu ubaguzi
 
Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
3,819
2,000
In fact ni ubaguzi. Kuna wengine kwa sababu za hali zao kiafya na kimaumbile (wenye ulemavu kwa mfano) hawawezi kwenda JKT, ina maana hawatapata ajira hizo husika?
Una taarifa na ulichochangia, au umekurupuka?

Ajira zinazohitaji kupita JKT ni hizo za vyombo vya ulinzi na usalama, ambazo kiuhalisia nyingi (ukiacha IT) zinahitaji usiwe na ulemavu wowote.

Siku nyingine tafuta taarifa kabla ya kuchangia. Siyo kila mada lazima uchangie.
 
Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
4,996
2,000
Ni mtu kwenda mahakamani kufungua maombi kutaka mahakama imuamuru mtoa tangazo kufuta ama kurekebisha tangazo kwa kuondoa hicho kigezo.

"Ila sasa ndio hivyo wanyonge sisi" (kwa sauti ya Nyerere)
 
Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
6,037
2,000
Hicho kigezo Cha jkt ni Cha kufutwa na uonevu mtupu hafu pia Kuna watu walioanzia certificate mpaka bachelor kwahyo wakose nafasi kisa jkt, na vigezo vingine wanavyo plus uzoefu na ubunifu wa kazi?..
Wameandika ktk documents zao za ajira, hadi wenye vyeti vya udereva basic, fundi wa veta hizo sio degree wqlq masters, nk hivyo na wenyewe wameangaliwa muhimu ni jkt

Polisi waliajiri watu walio pitia JKT na wenye taalma ambao hawa kupita JKT kama sikosei usaili wamefanyia DSM, wajkt wamefanyia ktk makambi na mikoani

Serikali ipo makini ina tambuq wimbi la wasio na ajira

Tukumbuke vijana wengi walio JKT walirejeshwa makwao na jamii ilipaza sauti, serikali ikawasikia na kuwarejesha makambini na sasa wana waajiri lakini naona ni kama jamii ile ile haitak mfumo huo
 
Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
6,037
2,000
Mkuu samahani mimi naona kuna 'Kupunguza' na 'kubagua' hivi ni vitu viwili tofauti kabisa. Huu utaratibu ni kubagua sio kupunguza, yaani tokea mwanzo mtu hawamuitaji kivipi watakuwa wamempunguza?.
Hivi ni vigezo, kila ajira ina vigezo, itakuwa tuna baguliwa kama Mimi niliesoma architect kutaka kufanya kazi ya uhasibu au udaktari??

Vigezo, sifa ktk ajira husika, kila kazi zina ambatana na sifa na Sera pia ktk utekelezaji wake, kama jambo ni la kisera pia
 
Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
3,819
2,000
Mkuu samahani mimi naona kuna 'Kupunguza' na 'kubagua' hivi ni vitu viwili tofauti kabisa. Huu utaratibu ni kubagua sio kupunguza, yaani tokea mwanzo mtu hawamuitaji kivipi watakuwa wamempunguza?.
JKT wanaenda hata ambao hawajachaguliwa na wote hupokelewa.

Kutokwenda JKT kwa sababu yoyote ile ni uamuzi binafsi na mhusika anawajibika moja kwa moja.

Hawabaguliwi kwa kuwa hawana vigezo vinavyohitajika, kimojawapo ni kutoshiriki mafunzo ya JKT.
 
Kohelethi

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,638
2,000
In fact ni ubaguzi. Kuna wengine kwa sababu za hali zao kiafya na kimaumbile (wenye ulemavu kwa mfano) hawawezi kwenda JKT, ina maana hawatapata ajira hizo husika?
Acha tu yaani tuna watu hawana uwezo wa kufikili kabisa Na ni viongozi
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
30,438
2,000
JKT wanaenda hata ambao hawajachaguliwa na wote hupokelewa.

Kutokwenda JKT kwa sababu yoyote ile ni uamuzi binafsi na mhusika anawajibika moja kwa moja.

Hawabaguliwi kwa kuwa hawana vigezo vinavyohitajika, kimojawapo ni kutoshiriki mafunzo ya JKT.
Hii ni mpya ndio naisikia leo ina maana yale yote JKT hutangaza huwa hayana maana basi si wangesema tu wote waliomaliza kidato Cha sita wakaripoti JKT kutangaza lengo lake huwa Nini Kama Kuna wengine hunyemelea gizani kwenda kujiunga bila kupangiwa Wala kuitwa?
 
Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
3,819
2,000
Hii ni mpya ndio naisikia leo ina maana yale yote JKT hutangaza huwa hayana maana basi si wangesema tu wote waliomaliza kidato Cha sita wakaripoti JKT kutangaza lengo lake huwa Nini Kama Kuna wengine hunyemelea gizani kwenda kujiunga bila kupangiwa Wala kuitwa?
Kama hukujua now you know.
 
Kimpyempye

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
595
1,000
Hii ni mpya ndio naisikia leo ina maana yale yote JKT hutangaza huwa hayana maana basi si wangesema tu wote waliomaliza kidato Cha sita wakaripoti JKT kutangaza lengo lake huwa Nini Kama Kuna wengine hunyemelea gizani kwenda kujiunga bila kupangiwa Wala kuitwa?
Hujaona jina lako kwenye orodha ya wanaotakiwa kwenda JKT na unahisi unatamani kwenda we nenda karipoti kambi yeyote uone kama hawatakupokea. Pale utapigwa biti la maana getini na kichurachura cha hapa na pale halafu unapokelewa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom