Suala la kisera: Utashi wa kisiasa na mawazo ya umma vinapokutana, tatizo kubwa linalotukabili linaweza kupata ufumbuzi

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Kuna baadhi ya changamoto kubwa zinazotukabili ambazo, ili zipate ufumbuzi; inabidi ifike mahali maoni ya umma yakutane na utashi wa kisiasa na hapo jambo linaweza kutokea na kuleta mabadiliko makubwa. Moja ya changamoto tunayoweza kuizungumzia kwa leo ni;

Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana ni swala tete sana na linaendelea kukuwa siku hadi siku na mwisho wake itakuwa ni balaa.

Mwanzoni hoja ilikuwa kuwa vijana hawapati ajira maana hawajasoma. Sasa hivi wengi wamesoma, kuna hoja kuwa hawaajiriki maana hawana maarifa ‘Skills’ jambo ambalo ni kweli. Lakini hayo yote madogo, kubwa ni kwamba nafasi za kazi ni chache kuliko idadi ya wahitimu, kwa hiyo hata hao wahitimu wawe competent kiasi gani, hawawezi kupata nafasi za kuajiriwa kwenye ajira rasmi.

Sasa kuna hoja kwamba vijana wanaosoma kwenye vyuo mbalimbali wafikirie kujiajiri wakimaliza badala ya kuajiriwa lakini kuna masuala matatu yanajitokeza. Kwanza, elimu wanazosoma vyuoni ni ‘Academics’ ambazo hazifanyi kazi mtaani. Mfano mtu ana shahada ya Historia ambapo amejikita kwenye masomo ya jinsi ‘Wazungu walivyotunyonya’.

Cngangamoto ya pili, ni wahitimu kutokuwa na maarifa ya biashara na maisha ‘ Business and life skills’ Kwa hiyo wanapoambiwa wajiajiri wanakuwa hawaoni pakuanzia. Na

Tatu, wahitimu hao wanakuwa hawana mitaji. Fikiria kama watu walioajiriwa miaka na miaka hawana mitaji na hivyo hawana mradi wowote, vipi mhitimu toka chuo aliyesomeshwa kwa mkopo?

Sasa nini cha kufanya?

Ushauri huu wa cha kufanya ni kama kuchokoza mjadala tu, lakini naamini wadau wataongezea ushauri wa msingi ili wazo likae vizuri na liwasaidie wenye uhitaji.

Tunaweza kushauri kuwa badala ya wanafunzi wengi kupewa mikopo kisha wasome ‘Degree’ baada ya hapo hawazifanyii kazi, ajira hawapati, kujiajiri hawawezi, mikopo hawawezi kurudisha na kujitegemea hawawezi; mikopo hiyo igawanywe mafungu mawili.

Fungu moja wakopeshwe vijana kadhaa ambao wana ‘strong commitment’ na ‘academics’ na fungu jingine wakopeshwe vijana ambao wako ‘committed’ na biashara, uzalishaji na ujasiriamali.

kwa kufanya hivi tutakuwa hatujaweka mayai yote kwa kapu moja. Tutakuwa tumefanya ‘diversification’ na kutengeneza mazingira ya mambo kwenda vizuri zaidi.

Kwa kufanya hivyo, kama nchi tutakuwa tunajenga mazingira ya watu kutawanyika kwenye shughuli za kiuchumi na hivyo kuchochea uchumi kukua, tutakuwa tumepunguza changamoto ya ukosefu wa ajira, tutakuwa tumeongeza uzalishaji na hivyo kuchochea kuongezeka kwa pato la taifa na kuweka mazingira ambayo angalau wahusika wataweza kulipa mikopo na kuweza kujitegemea kiuchumi.

Ndugu yangu nakuomba sana usaidie kufikisha wazo hili kwa wahusika na waone kama inafaa kuliboresha na kulifanyia kazi kwani litakuwa ni jambo jema kwa Watanzania wote.Nakushukuru sana .

kutokana na kusoma trend mbali mbali, sasa naweza kutoa hoja kwamba; ukosefu Wa ajira kwa vijana huenda likawa janga kubwa zaidi nchini, kuliko majanga mengine katika miaka michache tu ijayo.

Ikumbukwe kila mmoja wetu anahitaji kuishi maisha ya heshima na kuweza kujitegemea. Ni jambo gani la kizalendo zaidi ya hili ambalo tutakuwa tumelifanya kama tukifanikisha baadhi ya wenzetu wenye uhitaji wakaweza kuishi maisha yenye heshima na mafanikio?

Inawezekana wewe jambo hili lisiwe linakugusa moja kwa moja, ila ungetaka kulielewa vizuri, jiweke kwenye nafasi ya muhanga halafu fikiria sulubu ambayo ingekuwa inakukabili.

Uzuri wa jambo wazo hili, ni ‘Win Win’ hakuna atakayepoteza na wala hailazimiki kuwekeza fedha nyingi zaidi ambazo pengone hazipo.

Ili kulifanikisha hili, vinahitajika vitu vitatu vikubwa, Kwanza wazo ambalo limekaa vizuri na linatekelezeka, Pili uungwaji mkono wa wadau na tatu utashi wa kisiasa

Ni muhimu wadau wakaliboresha zaidi wazo hili ili kama likionekana linafaa, linaweza kuwasaidia wengi.
 
Nusu saa iliyopita ulisema tujipe likizo ya discussions zooote tudiscuss issue ya ajira, then wewe huyohuyo unakuja na uzi mpya usiohusu ajira tena?

Unforgetable
Unahusu ajira mkuu, ule haupo tena. Nadhani aliyeondoa kaondoa bila kusoma maudhui.
Nadhani tuendelee na hoja
 
Back
Top Bottom