ISLETS
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 8,121
- 5,332
Igwee..
Kwanza samahani wa wanandoa(hasa wanaume) ulio kwenye huu upumbavu wa kutokutamba mipaka ya ndoa.
Imetokea zaidi ya mara moja nimeona wanaume(wanaojiita baba wa familia) wanashindwa kutoa maamuzi ya mwisho juu ya mambo ya kifamilia kwa madai apaka akamuulize baba mchungaji mara mzee wa kanisa sijui nani nani wa kanisa wakati sio swala la kidini, huo ni udhaifu mkubwa na haufai hata kuwa baba wa familia.
Mfano 1: Jamaa mke wake alikuwa mgonjwa, taarifa ya daktari ni kwamba mgonjwa anashida ya moyo na akimbizwe hospitali kubwa haraka sana. Jamaa alivyo jinga anapiga simu kumuita mzee wa kanisa ndio aende kusikiliza maelezo ya daktari, kama kwamba yeye hana mamlaka ya kuamua juu ya matibabu ya mke wake. Hivi hii ni akili au matope ! Bora hata angesema mzee wa kanisa akashushe maombi watu wangemuelewa.
Mfano 2: Jamaa ana mgogoro wa kifamilia na mkewe, inahusisha mambo ya michepuko na ushahidi anao. Ila anashindwa kuyajenga na mkewe wala kuongea naye chochote anaenda kuyaeleza kwa mchungaji, tena yuko ya mbele ya mchungaji na mama mchungaji akiwepo analialia mambo ya familia yake. Hivi mwanaume ukikosa kifua cha kuhimili jambo dogo kama hilo, si ni bora abaki single!!
Mifano hai ipo mingi, wala sio stori za kutunga. Lengo langu si kudharau umuhimu wa viongozi wa kidini, la, bali kuna vitu huwa sio kwa kulalamika kwao, wao wakomae na maswala ya dini na maombezi basi.
Mwanaume jitahidi kuwa msemaji wa mwisho ndani ya nyumba yako, mambo ya kulia lia kwa viongozi wa dini ni ya wanawake(wao kwao hili ni tatizo la kudumu na halina tiba).
Kuruhusu mchungaji kuwa na sauti zaidi yako kwenye nyumba yako ni kumkaribisha shetani, ndio shetani atatumia huo huo mwanya kuharibu ndio. Mwisho wa siku mtumishi wa bwana anaaza kujitetea oooh ule sio mkono wangu ni wa baunsa.
Hasta La Vista.