Suala la Kibu Dennis na Fifa ranking, tutakoswa adhabu kweli?

Hiz comments sijuh watu wanafikiria Kabla ya kuandika naona utopolo tu ongeen Kama great thinker think higher
 
Baada ya kusajiliwa simba imeibuka fitna kwamba Kibu ni mburundi ,ndiyo maana hachezi hadi sasa na kocha wa stars analalmika anasema anamuhitaji sana, simba imepaniwa kila kona soon utasikia wachezaji wetu wanapigwa visu mitaani
Tuhuma zinazomkabili ni kuwa na uraia wa nchi mbili ambayo kwa FIFA siyo kosa
 
Kuna Shuti Moja Kali Sana Lilitoka Sentimita Chache Saaaaana lilipigwa Na huyu Dogo mechi na TP Mazembe....Nadhani ndilo Ndilo Kosa alilolifanya Dogo Kupelekea Hizi Figisu.
 
Ana kitambilisho cha kupigia kura.

Ana Kitambulisho cha Taifa.

Ana Passport ya Tanzania.

Hao ni Nyuma Mwiko
 
Wasomali ni magaidi mjue
Hivi unadhani natania kama mchezaji ambaye tayari keshacheza top level for 3 years na team ya taifa leo anaambiwa siyo raia kisa simba unadhani hawa jamaa wanatania? FOR HOOKS OR CROOKS watafanya lolote lile wameumia sana miaka 4 they are confused.
 
Mbona rahisi sana. Simba iombe uchunguzi wa kina ufanyike haraka na kwa uwazi ili haki itendeke. Hii ndio kazi mojawapo ya viongozi wa Simba waliochaguliwa kuifanya.

Ikibainika ni raia aruhusiwe acheze. Ikibainika sio raia basi aombewe uraia mapema acheze mpira kwa kigezo kuwa ana kitu "special" cha kulisaidia taifa hili.

Ndivyo yanavyofanya mataifa mengi duniani siku hizi Na mataifa mengine yanaenda mbali zaidi mpaka yanafika kuwarubuni wachezaji au wanataaluma wenye vipaji visivyo vya kawaida na kuwapa uraia.

Leo ukiangalia mashindano mbali mbali kwenye TV si ajabu kuona wanariadha wa Kenya lakini wana uaraia wa Bahrain, UAE, n.k.

Na hii mbinu Marekani ndio mwasisi wake. Na jambo zuri kwa Kibu ameshaonyesha uzalendo kwa kulitumikia taifa kwenye mechi na Malawi.
 
Ana kitambilisho cha kupigia kura.

Ana Kitambulisho cha Taifa.

Ana Passport ya Tanzania.

Hao ni Nyuma Mwiko

Wakati anachezea Taifa Stars hayo yote hawakuyajua? Kweli hawa Nyuma mwiko safari hii wamedhamiria,mpira ndani ya uwanja umewashinda wamebakia na huu upuuzi wa figisu za kipuuzi
 
Kote Geita gold, mbeya city, taifa stars kacheza kama Mtanzania, Utanzania wake ulikoma baada aya kusajiliwa simba, kila siku nasema mafanikio ya simba ya miaka 4 ni kosa kubwa sana waliowahi kulifanya mwaka huu vita viko kila upande bado kulipua tu kambi pale wachezaji wafe wote
Wala sio mafanikio ya simba,mafanikio gani hayo ya kutisha? tatizo la nchi hii ni kuwa na mfumo mbovu wa kujua raia wake, kwa ufupi huyu jamaa ni mrundi na aliingia Tz, kama mkimbizi akaishi kwenye kambi za wakimbizi, chini ya UNHCR, na jina lake limeonekana huko, hapo uyanga na usimba unatoka wapi?mwenye jukumu la kudhibitisha uraia wake, ni yeye mwenyewe, na idara husika ikiridhika suala limekwisha, au aombe tu uraia c basi?
 
Back
Top Bottom