Suala la Job Ndugai kujiuzulu na hatma ya muhimili wa Bunge

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,873
Kikatiba na kisiasa muhimili wa Bunge ndio muhimili mkubwa (Supreme or Principal Organ ) kuliko mihilimili yote. Jukumu kubwa la Bunge ni kuisimamia Serikali na kuishauri kwa mujibu wa ibara ya 63(2) ya Katiba yetu ya JMT .

Kauli ya Ndugai kuhusu Madeni na Mikopo aliyoitoa, ilitafsiriwa na watu katika mitazamo tofauti.

1.Wapo waliotafsiri kwamba Ndugai ni mwana CCM na Mjumbe wa Kamati kuu ya chama hivyo hakupaswa kusema yale dhidi ya Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM . Wanaona alipaswa kusemea katika vikao vya chama .

2.Wapo waliotafsiri kwamba Ndugai alikuwa na Agenda zake tuu kwani sio kweli kwamba alichukizwa na mikopo na madeni kwani wakati wa utawala wa Magufuli alikuwa Kimya ikiwa Magufuli alikopo kwa miaka 5 trilion 29 ,mikopo ya muda mfupi miaka 5 hadi 6 ambayo pia ni mikopo ya Riba kubwa kwanini Ndugai hakuongea ?

Wana hoji iweje Ndugai aongee leo katika utawala wa Rais Samia ambaye amekopa tril.
1.3 kutoka IMF mkopo wa muda mrefu miaka 15 hadi 20 kuulipa na usio kuwa na Riba,kwanini Ndagai aoneshe kukasirishwa leo na sio kipindi cha utawala wa Magufuli?.Hivyo watu wanaamini Ndugai alikuwa na Agenda yake.

Hawa pia wanapinga hoja zake za nchi kuto kopa bali itoze kodi ndani ili kujenga miradi ili kuepuka madeni ,hawa wanapinga kwa hoja kwamba huwezi Jenga miradi mikubwa kwa kodi za wananchi wasio na shughuli za kiuchumi , utawaumiza wananchi na miradi itachukua muda mrefu.

3.Wapo walioamini kwamba Ndugai alikuwa na hoja za msingi ila Muktadha,Hadhira na kauli zake katika uwasilishaji wa maneno ilitengeneza ukakasi.

Hawa wanaamini pia Ndugai kabla ya kuzungumza alikuwa na nafasi ya kuihoji Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango au Waziri Mkuu ili apate majibu ikiwa walipitisha Tozo kwanini tena walienda kukopa ?

Ila inaonekana wazi Spika hakuhoji wala kutaka kujua kwani hadi anakwenda kuongea alikuwa hana taarifa kama Fedha za Tozo zimejenga Madarasa 560 na fedha za IMF (za Uviko) zinapaswa jenga Madarasa 15,000 . Hivyo watu wana hitimisha kwamba Ndugai alikuwa na Agenda zake ukizingatia Hoja yake ya kugusia 2025 kuwaondoa viongozi.

4.Wapo walioamini kwamba Ndugai alikuwa na hoja na hoja zake zilipaswa kujibiwa bila kuangalia Historia yake,nafasi yake ndani ya chama, Muktadha wala namna alivyowasilisha.Yaani hoja zake zingejibiwa tuu . Hawa wanaamini Ndugai alikuwa sahihi kuhoji vile.

Makundi haya kuanzia la kwanza hadi la 3 ,walimkalia kooni Ndugai kwa kumkosoa vikali kutoka kila upande hadi serikali , mawaziri na hata Rais Samia pia alionesha kukasirishwa na kauli za Ndugai.

NDUGAI KUOMBA RADHI.

Baadaye Mh.Ndugai alijitokeza kuomba radhi na msamaha juu ya kauli zake na kufanya utetezi wake alipokutana na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Bunge Dodoma.

Katika hili la Ndugai kuomba radhi kulikuwa na Makundi matatu yaliyotofautiana kimtazamo.

1.Kuna kundi ambalo liliona Ndugai ametumia Busara na Hekma kuomba radhi kutokana na kauli zake .

2.Kuna Kundi ambalo waliona Ndugai hakupaswa kuomba radhi sababu hakukosea chochote katika kauli zake .

3.Kuna Kundi ambalo wanaamini kwamba Ndugai amefanya makosa makubwa kuomba radhi kama Spika ,kwani kitendo chake hicho kinatafsiriwa kulishushia hadhi Bunge kama muhimili mkubwa wa kuisimamia Serikali.

Hawa wao hawajali kama Spika alikosea au hakukosea ila kitendo tuu cha kuomba radhi wao wanatafsiri kitendo hiki kama kushusha hadhi na kudogodesha muhimili wa Bunge,kwani wanatafsiri kwamba Spika ndio kiongozi wa muhimili wa Bunge ambao ndio muhimili mkubwa kushinda yote(Supreme or Principal Organ) katika kuisimamia na kuishauri serikali hivyo kitendo hiki kama kimeshusha hadhi ya Bunge kwa watu wengi.

Hawa wanaamini kwamba bila kujali kama Spika alikosea au hakukosea alipaswa kufumba macho na masikio bila kuomba radhi yeyote ili kulinda hadi ya muhimili wa Bunge.

Hawa wanaamini kwa Ndugai kuomba radhi kama Spika wa Muhimili.Kuna dhana (Conception,Precedents au narratives) zimejengeka kwa watu wengi.

1.Chama kina Nguvu zaidi ya Muhimili wa Bunge .(Party Supremacy is above legislature).

2.Sasa inaonekana kinyume chake kwamba Muhimili wa Serikali (Executive) una nguvu zaidi kuliko muhimili wa Bunge (Executive is a Supreme or Principal Organ while The legislature /Parliament is now an agent organ.

Ikiwa kisheria na kisiasa Muhimili wa Bunge ndio Mkubwa na wenye nguvu yaani Supreme and principal organ.

NDUGAI KUJIUZULU.

Pia katika hili la Ndugai kujiuzulu kuna makundi matatu ambayo yana mitazamo tofauti.

1.Kundi linaloamini kwamba Ndugai amefanya vyema kujiuzulu , sababu asingeweza kufanya kazi vyema kutokana na mazingira.

Hawa wanaamini ya kwamba mbali na Bunge kuwa na jukumu la kuisimamia serikali ila katika mgawanyo wa madaraka (Functional Separation of power) mihimili hii inahitaji kuwa na mahusiano ambayo hayata athiri utendaji na majukumu yao .

Na Kiongozi anayeunganisha mahusiano ya kimajukumu kati ya Muhimili wa Bunge na Serikali (Executive) ni Spika , kwa hali ilivyokuwa Spika asingeweza tena kuwa na uwezo kutekeleza majukumu yake katika kuisimamia serikali kikamilifu na kulinda mahusiano ya kimajukumu yanayopaswa kuwepo katika mihimili hii.

Kama angeliongoza Bunge kuisimamia serikali kikamilifu ingeonekana ni Agenda zake za 2025 dhidi ya Serikali ya Rais Samia, kama angejifanya kusifu serikali ingeonekana ni mnafiki na muhimili wa Bunge ungezidi kupoteza maana kabisa na kuzidi kuwa tawi la serikali.

Hivyo hawa wanaamini bora aje Spika mwingine ambaye atakuwa huru katika kutekeleza majukumu yake bila kudhaniwa au kuangaliwa tofauti kama ambavyo Ndugai alikuwa akidhaniwa kuwa na Agenda zake dhidi ya Serikali ya Rais Samia.

2.Kuna Kundi ambalo linaamini kwamba Ndugai hakupaswa kujiuzulu , hata kama alikosea au hakukosea ila hakupaswa kujiuzulu sababu imetengeneza dhana kwamba ,

(a).Chama kina Nguvu zaidi ya Muhimili wa Bunge kufanya hadi Spika kujiuzulu.

(b).Kwamba Muhimili wa Serikali (Executive) una Nguvu zaidi ya muhimili wa Bunge ,kufanya Spika kujiuzulu.

(c).Itatengeneza dhana kwamba Spika ajae akiwa tofauti na mawazo ya chama chake au Serikali atakuwa "Ndugailized " yaani yatamkuta kama yaliyomkuta Ndugai , hadi kujiuzulu hivyo kuna hatari ya kumpata Spika ambaye atakuwa muoga kukosoa,kusema ukweli na kuliongoza Bunge katika kuisimamia serikali kikamilifu sababu tuu ya hofu yaliyotokea kwa Ndugai.

(d) Itatengeneza dhana kwa Wabunge wengi wa CCM kwamba katika kutekeleza majukumu yao watakuwa salama siku zote kama watasifu na kupongeza zaidi serikali ,Rais Samia na chama chao cha CCM na wataona kukosoa serikali au Rais na kushauri sio salama kwani wanaweza kuwa "Ndugailized " kupatwa kama yaliyompata Ndugai .Hivyo muhimili wa Bunge unaweza kupoteza maaana kabisa na kuzidi kuwa tawi la Serikali.

3.Kuna kundi linaloamini kwamba Ndugai hakupaswa kujiuzulu,angeendelea kuwa Spika na angeamua kufumba macho na masikio akabadilika kutokuwa mnafiki na mamluki hivyo angeanza kulitengenezea Bunge heshima kwa kuliongoza vyema katika kuisimamia serikali kikamilifu bila woga wala hofu ya chama chake au serikali,bila kujali mashambulizi yeyote anayopata .

Hii ingefanya watu wamuone Ndugai amebadilika yaani amekuwa mpya au kuzaliwa upya, hii ingekuwa fursa yake ya kutengeneza heshima yake hata kama wangemuona kikwazo na kumuondoa ila angeondoka na Heshma kidogo tofauti na alivyoondoka sasa.

Hitimisho.

Spika ajae ana nafasi ya kulitengenezea Bunge heshima kwa kuisimamia serikali na kuihoji serikali bila woga ikiwa atatafsiri yaliyomkuta Ndugai ni kwasababu ya makosa yake Ndugai au Agenda zake mwenyewe na kutofuata sheria na taratibu hivyo yeye (Spika Mpya ) anuie kufuata taratibu, sheria na katiba katika kusimamia serikali kikamilifu bila hofu wala woga wa kuangalia yaliyotokea kwa Ndugai.

Lakini pia anaweza kulifanya Bunge kuwa tawi la Serikali au chama cha Mapinduzi hivyo kupoteza kabisa uwezo wa kuisimamia Serikali hata kidogo ikiwa atatafsiri yaliyomkuta Ndugai ni kwa sababu ya kuisimamia serikali au kwasababu ya kukosoa serikali . Akitafsiri namna hii kamwe ataona kuisimamia serikali au kuikosoa Serikali sio salama kwani atakuwa "Ndugailized".

Hivyo atakuwa Spika wa hovyo zaidi kuwahi kutokea na Bunge litakuwa zaidi tawi la Serikali (Executive).

Mwisho, kuna haja sasa suala hili la Ndugai tuliweke katika Mjadala wa namna gani sasa tunaweza kupata katiba mpya ambayo itafanya muhimili wa Bunge kuwa na Nguvu , na hii ni vyema sana Kama Taifa tuwaze kuwa na Spika ambaye hapaswi kuwa Mwanachama wa chama Chochote ili kuondoa hofu na wasiwasi wa yeye kufukuzwa uwanachama na chama chake pindi itakapotokea tofauti za kifikra na kimtazamo.

Lakini pia katiba yetu ya 1977 kuanzia ibara ya 84(3),84(5),84(7 e na g) inatengeneza dhana iliyowazi kwamba Rais ana nguvu zaidi ya Spika kwa kutamka kwamba Spika anatawasilisha tamko la Mali kwa Rais wa JMT, naweza kuondoka kuwa Spika akichelewa kuwasilisha . Hii inatengeneza dhana kwamba Spika Bosi wake ni Rais .

Kuna haja ya kuhimiza mabadiliko ya katiba ili kuwa Spika imara ambaye hataweza kuwa mnafiki, kigeugeu,muoga na mwenye hofu ya kuchukuliwa hatua zozote au ndani ya chama hivyo Spika vyema asiwe Mwanachama wa chama chochote cha Siasa .

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa.

07/Januari/2022.
Kigoma, Ujiji .
 
Nimesoma aya ya kwanza tu ndio nikabaini kwamba unalazimisha kuonekana unajua na ujuaji wako unasababisha tuanze kuhoji uwezo wako.

Aya ya kwanza umepotosha pakubwa sana, kitendo cha kusema bunge ni 'supreme organ' ni upotoshaji. Katiba haijaipa mhimili wowote ukuu kwa mwingine kulingana na principle ya balance and check baina ya mihimili.

Vivo hivyo kazi ya bunge ni kusimamia tu serikali na sio kuiendesha serikali ,unapozungumzia ukuu wa bunge una maana kwamba bunge lina mamlaka ya kuiendesha serikali.

Sijamaliza kusoma chote ulichoandika lakini mpaka kufika hapo nimebaini mapungufu makubwa yenye lengo la upotoshaji
 
Umeandika vizuri sana bila ushabiki
Tatizo linatokana na Ndugai kujisahau kwamba yeye ni spika na anapaswa kuisimamia Serikali akiwa bungeni. Kitendo cha kutoa lawama kwa Serikali nje ya vikao vya bunge ndio alipokosea. Ila pia kosa lilikua pale alipotumia siasa kuelekeza au kutanabahisha kuhusu uchaguzi ujao na hivyo kujengeka kwa dhana kwamba anahusisha uchaguzi ujao ama akiwa na maslahi ya moja kwa moja au vinginevyo. Wabunge wanayo kinga ya kusema lolote wawapo bungeni tu na si mahala pengine wala si vingine.
 
Nimesoma aya ya kwanza tu ndio nikabaini kwamba unalazimisha kuonekana unajua na ujuaji wako unasababisha tuanze kuhoji uwezo wako.

Aya ya kwanza umepotosha pakubwa sana, kitendo cha kusema bunge ni 'supreme organ' ni upotoshaji. Katiba haijaipa mhimili wowote ukuu kwa mwingine kulingana na principle ya balance and check baina ya mihimili.

Vivo hivyo kazi ya bunge ni kusimamia tu serikali na sio kuiendesha serikali ,unapozungumzia ukuu wa bunge una maana kwamba bunge lina mamlaka ya kuiendesha serikali.

Sijamaliza kusoma chote ulichoandika lakini mpaka kufika hapo nimebaini mapungufu makubwa yenye lengo la upotoshaji
Nakubaliana nawe. Katiba yetu ni ya Presidential system na sio parliamentary. Kwa hivyo katika mifumo yote ya Presidential system executive ina nguvu kuliko mihimili yote ukiacha suala la check and balance ulilolizungumzia. Mfano wa presidential constitution ni marekani ambapo ikiwa bunge litakwamisha suala fulani kwa mfano budget rais ana veto power au suala lolote lile bunge likikataa rais anaweza kulazimisha.
Mfano wa parliamentary ni wa UK kule Parliament is supreme than excutive...wenyewe wanaita parliamentary supremacy.
Mwisho ukweli mwingine mchungu kwa presidential constitution ni kwamba rais ni mkuu wA state yaani mkuu WA mihimili yote mitatu. Exacutive, bunge na judiciary.
 
Actually Katiba ilivyokaa unaona kabisa executive ndio supreme over the other arms of the state. Huyu Abdu sijui Dulla anatuzingua.
 
Nimesoma aya ya kwanza tu ndio nikabaini kwamba unalazimisha kuonekana unajua na ujuaji wako unasababisha tuanze kuhoji uwezo wako.

Aya ya kwanza umepotosha pakubwa sana, kitendo cha kusema bunge ni 'supreme organ' ni upotoshaji. Katiba haijaipa mhimili wowote ukuu kwa mwingine kulingana na principle ya balance and check baina ya mihimili.

Vivo hivyo kazi ya bunge ni kusimamia tu serikali na sio kuiendesha serikali ,unapozungumzia ukuu wa bunge una maana kwamba bunge lina mamlaka ya kuiendesha serikali.

Sijamaliza kusoma chote ulichoandika lakini mpaka kufika hapo nimebaini mapungufu makubwa yenye lengo la upotoshaji
... amejenga hoja yake ya superiority ya Bunge dhidi ya Serikali kwa context ya kikatiba ya "Bunge Kuisimamia Serikali". Anayesimamia na anayesimamiwa nani (anapaswa kuwa) superior Chief?

And, in fact, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi - actually ndio wananchi wenyewe walioiweka serikali madarakani; nani (anapaswa kuwa) mkubwa hapo? Si hata mawaziri/serikali huenda "kujieleza" Bungeni? Tatizo Bunge la nchi hii halijitambui wala halijui mamlaka liliyo nayo even kwa Katiba hiyo hiyo mbovu!

Hongera Abdul Nondo umedadavua vizuri.
 
Ahsante sana, umeiweka vizuri sana !! Ahsante sana .

Watu waelewe kwamba , msingi wa Bunge kupaswa kuwa muhimili Mkubwa Supreme kuliko mihimili yote ni kutokana na na dhana ya Popular Sovereignty yaani ukubwa na mamlaka ya watu au wananchi kwa nchi yao kama inavyoelezwa ibara ya 8 (1) kwamba Sovereignty resides in the people (Citizens) .

Hivyo Bunge ni muhimili wa wananchi (watu ) ,ambao wapo Bungeni kupitia wawakilishi wao kuisimamia Serikali ili iweze kutekeleza ibara ya 8 1(b na c) .

Kwa mantiki hiyo Bunge ni Muhimili mkubwa kati ya mihimili yote na ndio unapaswa kuwa hivyo kisheria ,kikatiba na kisiasa hasa katika nchi yeyote ambayo ni ya kidemokrasia.
 
nilikuwa sio muumini wa katba mpya,lkn suala la ndugai limenifungua macho aise,kitendo Cha kumlqzimisha ndugai aombe msamaha ,hii inaonyesha muhimili wa bunge unamilikiwa na ccm,na serikali, na wao ndio controla wa huu mhimili wa bunge!! Mwal.nyerere aliwahi kusema ,namnukuu(kwa katiba hii tukipata rais wa hovyo tutajuta ). Dawa ni kupata katiba mpya !!
 
... watu (na Bunge lenyewe) wanatishwa na hofu za "mhimili uliojichimbia zaidi" wakajua kwa kuwa mfalme kasema basi ndio katiba na sheria; but in real sense it isn't. Hii nchi kuna mambo yanapelekeshwa kienyeji sana; unachosomea shule huko ukija kwenye political arena quietly different!
 
nilikuwa sio muumini wa katba mpya,lkn suala la ndugai limenifungua macho aise,kitendo Cha kumlqzimisha ndugai aombe msamaha ,hii inaonyesha muhimili wa bunge unamilikiwa na ccm,na serikali, na wao ndio controla wa huu mhimili wa bunge!! Mwal.nyerere aliwahi kusema ,namnukuu(kwa katiba hii tukipata rais wa hovyo tutajuta ). Dawa ni kupata katiba mpya !!
... stuka sasa! Tunapigwa sound za kisiasa kama wajinga fulani hivi! Eti, "katiba mpya italeta ugali mezani"? Wajingawajinga woyo woyo woyoooo! Wanatutimulia vumbi kali turbo VX-V8 latest model from Japan kodi zetu! Arrrg!
 
Endeleeni kupiga vyombo maza kesha maliza kazi kuwa ni 2025 fever wachambuzi uchwara na wa michongo endeleeni kupiga marktime huku mkilipwa kwa uchambuzi maza kesha maliza chambueni wee ila imeisha hiyo subirini mumchambue spika mpya naye.
Kikatiba na kisiasa muhimili wa Bunge ndio muhimili mkubwa (Supreme or Principal Organ ) kuliko mihilimili yote. Jukumu kubwa la Bunge ni kuisimamia Serikali na kuishauri kwa mujibu wa ibara ya 63(2) ya Katiba yetu ya JMT .

Kauli ya Ndugai kuhusu Madeni na Mikopo aliyoitoa, ilitafsiriwa na watu katika mitazamo tofauti.

1.Wapo waliotafsiri kwamba Ndugai ni mwana CCM na Mjumbe wa Kamati kuu ya chama hivyo hakupaswa kusema yale dhidi ya Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM . Wanaona alipaswa kusemea katika vikao vya chama .

2.Wapo waliotafsiri kwamba Ndugai alikuwa na Agenda zake tuu kwani sio kweli kwamba alichukizwa na mikopo na madeni kwani wakati wa utawala wa Magufuli alikuwa Kimya ikiwa Magufuli alikopo kwa miaka 5 trilion 29 ,mikopo ya muda mfupi miaka 5 hadi 6 ambayo pia ni mikopo ya Riba kubwa kwanini Ndugai hakuongea ?

Wana hoji iweje Ndugai aongee leo katika utawala wa Rais Samia ambaye amekopa tril.
1.3 kutoka IMF mkopo wa muda mrefu miaka 15 hadi 20 kuulipa na usio kuwa na Riba,kwanini Ndagai aoneshe kukasirishwa leo na sio kipindi cha utawala wa Magufuli?.Hivyo watu wanaamini Ndugai alikuwa na Agenda yake.

Hawa pia wanapinga hoja zake za nchi kuto kopa bali itoze kodi ndani ili kujenga miradi ili kuepuka madeni ,hawa wanapinga kwa hoja kwamba huwezi Jenga miradi mikubwa kwa kodi za wananchi wasio na shughuli za kiuchumi , utawaumiza wananchi na miradi itachukua muda mrefu.

3.Wapo walioamini kwamba Ndugai alikuwa na hoja za msingi ila Muktadha,Hadhira na kauli zake katika uwasilishaji wa maneno ilitengeneza ukakasi.

Hawa wanaamini pia Ndugai kabla ya kuzungumza alikuwa na nafasi ya kuihoji Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango au Waziri Mkuu ili apate majibu ikiwa walipitisha Tozo kwanini tena walienda kukopa ?

Ila inaonekana wazi Spika hakuhoji wala kutaka kujua kwani hadi anakwenda kuongea alikuwa hana taarifa kama Fedha za Tozo zimejenga Madarasa 560 na fedha za IMF (za Uviko) zinapaswa jenga Madarasa 15,000 . Hivyo watu wana hitimisha kwamba Ndugai alikuwa na Agenda zake ukizingatia Hoja yake ya kugusia 2025 kuwaondoa viongozi.

4.Wapo walioamini kwamba Ndugai alikuwa na hoja na hoja zake zilipaswa kujibiwa bila kuangalia Historia yake,nafasi yake ndani ya chama, Muktadha wala namna alivyowasilisha.Yaani hoja zake zingejibiwa tuu . Hawa wanaamini Ndugai alikuwa sahihi kuhoji vile.

Makundi haya kuanzia la kwanza hadi la 3 ,walimkalia kooni Ndugai kwa kumkosoa vikali kutoka kila upande hadi serikali , mawaziri na hata Rais Samia pia alionesha kukasirishwa na kauli za Ndugai.

NDUGAI KUOMBA RADHI.

Baadaye Mh.Ndugai alijitokeza kuomba radhi na msamaha juu ya kauli zake na kufanya utetezi wake alipokutana na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Bunge Dodoma.

Katika hili la Ndugai kuomba radhi kulikuwa na Makundi matatu yaliyotofautiana kimtazamo.

1.Kuna kundi ambalo liliona Ndugai ametumia Busara na Hekma kuomba radhi kutokana na kauli zake .

2.Kuna Kundi ambalo waliona Ndugai hakupaswa kuomba radhi sababu hakukosea chochote katika kauli zake .

3.Kuna Kundi ambalo wanaamini kwamba Ndugai amefanya makosa makubwa kuomba radhi kama Spika ,kwani kitendo chake hicho kinatafsiriwa kulishushia hadhi Bunge kama muhimili mkubwa wa kuisimamia Serikali.

Hawa wao hawajali kama Spika alikosea au hakukosea ila kitendo tuu cha kuomba radhi wao wanatafsiri kitendo hiki kama kushusha hadhi na kudogodesha muhimili wa Bunge,kwani wanatafsiri kwamba Spika ndio kiongozi wa muhimili wa Bunge ambao ndio muhimili mkubwa kushinda yote(Supreme or Principal Organ) katika kuisimamia na kuishauri serikali hivyo kitendo hiki kama kimeshusha hadhi ya Bunge kwa watu wengi.

Hawa wanaamini kwamba bila kujali kama Spika alikosea au hakukosea alipaswa kufumba macho na masikio bila kuomba radhi yeyote ili kulinda hadi ya muhimili wa Bunge.

Hawa wanaamini kwa Ndugai kuomba radhi kama Spika wa Muhimili.Kuna dhana (Conception,Precedents au narratives) zimejengeka kwa watu wengi.

1.Chama kina Nguvu zaidi ya Muhimili wa Bunge .(Party Supremacy is above legislature).

2.Sasa inaonekana kinyume chake kwamba Muhimili wa Serikali (Executive) una nguvu zaidi kuliko muhimili wa Bunge (Executive is a Supreme or Principal Organ while The legislature /Parliament is now an agent organ.

Ikiwa kisheria na kisiasa Muhimili wa Bunge ndio Mkubwa na wenye nguvu yaani Supreme and principal organ.

NDUGAI KUJIUZULU.

Pia katika hili la Ndugai kujiuzulu kuna makundi matatu ambayo yana mitazamo tofauti.

1.Kundi linaloamini kwamba Ndugai amefanya vyema kujiuzulu , sababu asingeweza kufanya kazi vyema kutokana na mazingira.

Hawa wanaamini ya kwamba mbali na Bunge kuwa na jukumu la kuisimamia serikali ila katika mgawanyo wa madaraka (Functional Separation of power) mihimili hii inahitaji kuwa na mahusiano ambayo hayata athiri utendaji na majukumu yao .

Na Kiongozi anayeunganisha mahusiano ya kimajukumu kati ya Muhimili wa Bunge na Serikali (Executive) ni Spika , kwa hali ilivyokuwa Spika asingeweza tena kuwa na uwezo kutekeleza majukumu yake katika kuisimamia serikali kikamilifu na kulinda mahusiano ya kimajukumu yanayopaswa kuwepo katika mihimili hii.

Kama angeliongoza Bunge kuisimamia serikali kikamilifu ingeonekana ni Agenda zake za 2025 dhidi ya Serikali ya Rais Samia, kama angejifanya kusifu serikali ingeonekana ni mnafiki na muhimili wa Bunge ungezidi kupoteza maana kabisa na kuzidi kuwa tawi la serikali.

Hivyo hawa wanaamini bora aje Spika mwingine ambaye atakuwa huru katika kutekeleza majukumu yake bila kudhaniwa au kuangaliwa tofauti kama ambavyo Ndugai alikuwa akidhaniwa kuwa na Agenda zake dhidi ya Serikali ya Rais Samia.

2.Kuna Kundi ambalo linaamini kwamba Ndugai hakupaswa kujiuzulu , hata kama alikosea au hakukosea ila hakupaswa kujiuzulu sababu imetengeneza dhana kwamba ,

(a).Chama kina Nguvu zaidi ya Muhimili wa Bunge kufanya hadi Spika kujiuzulu.

(b).Kwamba Muhimili wa Serikali (Executive) una Nguvu zaidi ya muhimili wa Bunge ,kufanya Spika kujiuzulu.

(c).Itatengeneza dhana kwamba Spika ajae akiwa tofauti na mawazo ya chama chake au Serikali atakuwa "Ndugailized " yaani yatamkuta kama yaliyomkuta Ndugai , hadi kujiuzulu hivyo kuna hatari ya kumpata Spika ambaye atakuwa muoga kukosoa,kusema ukweli na kuliongoza Bunge katika kuisimamia serikali kikamilifu sababu tuu ya hofu yaliyotokea kwa Ndugai.

(d) Itatengeneza dhana kwa Wabunge wengi wa CCM kwamba katika kutekeleza majukumu yao watakuwa salama siku zote kama watasifu na kupongeza zaidi serikali ,Rais Samia na chama chao cha CCM na wataona kukosoa serikali au Rais na kushauri sio salama kwani wanaweza kuwa "Ndugailized " kupatwa kama yaliyompata Ndugai .Hivyo muhimili wa Bunge unaweza kupoteza maaana kabisa na kuzidi kuwa tawi la Serikali.

3.Kuna kundi linaloamini kwamba Ndugai hakupaswa kujiuzulu,angeendelea kuwa Spika na angeamua kufumba macho na masikio akabadilika kutokuwa mnafiki na mamluki hivyo angeanza kulitengenezea Bunge heshima kwa kuliongoza vyema katika kuisimamia serikali kikamilifu bila woga wala hofu ya chama chake au serikali,bila kujali mashambulizi yeyote anayopata .

Hii ingefanya watu wamuone Ndugai amebadilika yaani amekuwa mpya au kuzaliwa upya, hii ingekuwa fursa yake ya kutengeneza heshima yake hata kama wangemuona kikwazo na kumuondoa ila angeondoka na Heshma kidogo tofauti na alivyoondoka sasa.

Hitimisho.

Spika ajae ana nafasi ya kulitengenezea Bunge heshima kwa kuisimamia serikali na kuihoji serikali bila woga ikiwa atatafsiri yaliyomkuta Ndugai ni kwasababu ya makosa yake Ndugai au Agenda zake mwenyewe na kutofuata sheria na taratibu hivyo yeye (Spika Mpya ) anuie kufuata taratibu, sheria na katiba katika kusimamia serikali kikamilifu bila hofu wala woga wa kuangalia yaliyotokea kwa Ndugai.

Lakini pia anaweza kulifanya Bunge kuwa tawi la Serikali au chama cha Mapinduzi hivyo kupoteza kabisa uwezo wa kuisimamia Serikali hata kidogo ikiwa atatafsiri yaliyomkuta Ndugai ni kwa sababu ya kuisimamia serikali au kwasababu ya kukosoa serikali . Akitafsiri namna hii kamwe ataona kuisimamia serikali au kuikosoa Serikali sio salama kwani atakuwa "Ndugailized".

Hivyo atakuwa Spika wa hovyo zaidi kuwahi kutokea na Bunge litakuwa zaidi tawi la Serikali (Executive).

Mwisho, kuna haja sasa suala hili la Ndugai tuliweke katika Mjadala wa namna gani sasa tunaweza kupata katiba mpya ambayo itafanya muhimili wa Bunge kuwa na Nguvu , na hii ni vyema sana Kama Taifa tuwaze kuwa na Spika ambaye hapaswi kuwa Mwanachama wa chama Chochote ili kuondoa hofu na wasiwasi wa yeye kufukuzwa uwanachama na chama chake pindi itakapotokea tofauti za kifikra na kimtazamo.

Lakini pia katiba yetu ya 1977 kuanzia ibara ya 84(3),84(5),84(7 e na g) inatengeneza dhana iliyowazi kwamba Rais ana nguvu zaidi ya Spika kwa kutamka kwamba Spika anatawasilisha tamko la Mali kwa Rais wa JMT, naweza kuondoka kuwa Spika akichelewa kuwasilisha . Hii inatengeneza dhana kwamba Spika Bosi wake ni Rais .

Kuna haja ya kuhimiza mabadiliko ya katiba ili kuwa Spika imara ambaye hataweza kuwa mnafiki, kigeugeu,muoga na mwenye hofu ya kuchukuliwa hatua zozote au ndani ya chama hivyo Spika vyema asiwe Mwanachama wa chama chochote cha Siasa .

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa.

07/Januari/2022.
Kigoma, Ujiji .
 
Ahsante sana, umeiweka vizuri sana !! Ahsante sana .

Watu waelewe kwamba , msingi wa Bunge kupaswa kuwa muhimili Mkubwa Supreme kuliko mihimili yote ni kutokana na na dhana ya Popular Sovereignty yaani ukubwa na mamlaka ya watu au wananchi kwa nchi yao kama inavyoelezwa ibara ya 8 (1) kwamba Sovereignty resides in the people (Citizens) .

Hivyo Bunge ni muhimili wa wananchi (watu ) ,ambao wapo Bungeni kupitia wawakilishi wao kuisimamia Serikali ili iweze kutekeleza ibara ya 8 1(b na c) .

Kwa mantiki hiyo Bunge ni Muhimili mkubwa kati ya mihimili yote na ndio unapaswa kuwa hivyo kisheria ,kikatiba na kisiasa hasa katika nchi yeyote ambayo ni ya kidemokrasia.

..hivi kwanini ACT haipiganii uchunguzi ufanyike kuhusiana na kifo cha Aboubakar Khamis Bakari?

..kwanini hamdai hatua zichukuliwe dhidi ya waliohusika kuua na kujeruhi viongozi na wanachama wenu wakati wa uchaguzi?

..samahani kwa kutoka nje ya mada.
 
nilikuwa sio muumini wa katba mpya,lkn suala la ndugai limenifungua macho aise,kitendo Cha kumlqzimisha ndugai aombe msamaha ,hii inaonyesha muhimili wa bunge unamilikiwa na ccm,na serikali, na wao ndio controla wa huu mhimili wa bunge!! Mwal.nyerere aliwahi kusema ,namnukuu(kwa katiba hii tukipata rais wa hovyo tutajuta ). Dawa ni kupata katiba mpya !!
Mbona yeye Mwalimu hakuileta na alikuwa na nafasi?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom