johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,904
- 141,855
Sisi wahenga tukiliangalia tukio la wabunge wa viti maalumu wa Chadema akina Halima Mdee tunaweza kulifananisha na lile la mbunge wa Temeke 1995 mh Kihiyo.
Kihiyo siyo kwamba hakusoma shule, No alisoma isipokuwa alicheza na makaratasi ili aonekane almaarufu wakati sifa ya mbunge ni kujua Kusoma na Kuandika tu.
Hali hii ilipelekea yeye kupoteza ubunge na kurithiwa na Augustino Mrema aliyemgaragaza mtoto wa mjini Abdul Cisco.
Halima Mdee na wenzake hawajateuliwa na kamati kuu ya CHADEMA hilo liko wazi kabisa lakini wanaowakumbatia wanasahau kuwa walimwingiza kwenye orodha Nusrat Henje na hapo ndipo Kihiyo anapoingia.
Kumpa Nusrat ubunge katika mazingira " yale" ni sawa kabisa na kumpa Uinjinia yule fundi mchundo wa FTC ya DIT.
Upuuzi wa siasani ulianza kitambo.
Kazi Iendelee.