Suala la Halima Mdee na wenzake linafanana sana na lile la mbunge Kihiyo wa Temeke 1995, hatimaye Kihiyo alipoteza ubunge

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,042
2,000
Sisi wahenga tukiliangalia tukio la wabunge wa viti maalumu wa Chadema akina Halima Mdee tunaweza kulifananisha na lile la mbunge wa Temeke 1995 mh Kihiyo.

Kihiyo siyo kwamba hakusoma shule, No alisoma isipokuwa alicheza na makaratasi ili aonekane almaarufu wakati sifa ya mbunge ni kujua Kusoma na Kuandika tu.

Hali hii ilipelekea yeye kupoteza ubunge na kurithiwa na Augustino Mrema aliyemgaragaza mtoto wa mjini Abdul Cisco.

Halima Mdee na wenzake hawajateuliwa na kamati kuu ya CHADEMA hilo liko wazi kabisa lakini wanaowakumbatia wanasahau kuwa walimwingiza kwenye orodha Nusrat Henje na hapo ndipo Kihiyo anapoingia.

Kumpa Nusrat ubunge katika mazingira " yale" ni sawa kabisa na kumpa Uinjinia yule fundi mchundo wa FTC ya DIT.

Upuuzi wa siasani ulianza kitambo.

Kazi Iendelee.
 

Bhikalamba

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
1,068
2,000
Jamaa yako anadai viambatanishi vya katiba na muhtasari wa kikao cha kuwafukuza uanachama hao covid-19, lakini kwenye kuwaapisha hakudai vitu kama hivyo very pathetic huyo mic & loudspeaker.
 

Ryaro ryaro

JF-Expert Member
Feb 10, 2021
328
1,000
Kihiyo sio wale COVID- 19 bali Speaker wa Bunge la JMT ndio Kihiyo. Alishirikiana Kufanya hii Utopolo Hayupo Sijui anashindwa nini Kuchukua hatua japo tayari ni Aibu Kubwa Kwake.

Kwa urguments zake kuhusu wao watu wake 19, nadhani Kuna shida kwenye shule zake alizojielimisha. Hili swala liko wazi wao 19 sio wabunge, you don't need even to involves hao anaosema unao wanasheria wabobezi. Swala hili kuwahusisha wanasheria inaonyesha ubovu wa kiuongozi bungeni.
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,951
2,000
Jamaa yako anadai viambatanishi vya katiba na muhtasari wa kikao cha kuwafukuza uanachama hao covid-19, lakini kwenye kuwaapisha hakudai vitu kama hivyo very pathetic huyo mic & loudspeaker
Ndugai anasahau kuwa mmoja wa wale covid 19 alikuwa Mahabusu,sijui sahihi yake waliipataje?
 

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
1,761
2,000
Halima Mdee alishitukia dili Mbowe na akina Mnyika vile viti walitaka wawape wake zao

Scheni rohombaya zenu wale wadada wote ndio icon ya Chadema kuna shida gani wakikalia vile viti

Au mlitaka mviuze kama mlivyo uza kiti cha Dk Slaa
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,979
2,000
Huoni mfano sahihi ungekuwa ni wa Zitto Kabwe ambae alipoteza ubunge baada ya kutimuliwa CHADEMA?

Au Lazaro Nyalandu ambae alipoteza ubunge baada ya kuhama CCM?

Au mimi ndo nakosea hizo kumbukumbu?!
 

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
5,137
2,000
Wanasheria na wanaharakati wa haki za banadamu waende Mahakamani wakafungue order ya ceteorari and mandamus dhidi ya maamuzi ya Spika Ndugai.

Hizi za kuongea tu hazisaidii kitu.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,830
2,000
Halima Mdee alishitukia dili Mbowe na akina Mnyika vile viti walitaka wawape wake zao

Scheni rohombaya zenu wale wadada wote ndio icon ya Chadema kuna shida gani wakikalia vile viti

Au mlitaka mviuze kama mlivyo uza kiti cha Dk Slaa
Peleka upumbaf wako huko! Mtu mzima unaandika ujinga? Unao ushahidi wa huu upuuzi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom