Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,653
Suala la kuwalipa tuzo dowans za mabillion ya shillingi linanipa mashaka mno na watu tuliowapa dhamana ya kuliongoza taifa hili, juu ya uzalendo wao na jinsi gani wanavyojitolea kwa manufaa ya taifa hili, linanipa mashaka na umakiini wao. Hivi hatuna wanasheria makini wenye uwezo wa juu katika masuala ya mikataba au ubinafsi na ufisadi umeshika hatamu miongoni mwetu? Wananchi wanabebeshwa mzigo wa kulipa hasara ambayo wao hawakuitenda, je ni hatua gani itachukuliwa kwa wote waliohusika? Nasikitishwa sana na taifa letu linakoelekea na watu wetu walivyokosa uzalendo kwa nchi yao wenyewe.