BUBERWA D.
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 2,293
- 1,170
Sasa ni dhahiri kuwa swala la chama gani chaweza kutoa rais wa JMT limezikwa rasmi na uhakika ni kuwa, CCM peke yake ndicho kitaendelea kutoa rais.
Ukifuatilia mijadala inayoendelea hasa ndani ya vyama vya upinzani na wapambe wao (wanaharakati) ni dhahiri kuwa wamebadili mashambulizi yao dhidi ya CCM na kuhamishia kwa mtu binafsi (JPM).
Tulizoea mara zote, kutokana na uasili na chimbuko la vyama pinzani na vyama vya kiharakati huwa ni kushambulia serikali na chama kilicho madrakani ili kuonesha kile wanachoita "ukosoaji."
Kwa Tanzania mambo yamebadilika; si wapinzani, wanaharakati, wala wale wanaowatuma na kuwafadhili wanashambulia CCM kama ilivyo, bali wamejikita katika kutafuta namna ya kushirikiana na makundi (kama yapo)ndani ya CCM ili kujaribu kutikisa utawala uliopo na hata ikiwezekana kuuondoa na kuingiza mtu ambaye ataendeleza utamaduni waliozoea wa kufyonza taifa. Hekaheka hizi zinasukumwa na mambo kadha wa kadha.
Kutokana na Tanzania tulipokuwa tumefikia, wanasiasa bila kujali vyama vyao, wanaharakati, wanahabari, viongozi wa serikali n.k kwa wingi wao japo si wote walitegemea kujinufaisha kwa kupora fedha za umma, kufyonza rasilimali za taifa n.k Wachache sana walikosa pesa za wizi, miradi ilikwama huku deni la taifa likikua, misafara isiyokoma kwenda ugaibuni wakilipana masurufu makubwa, n.k.
Hili kundi bila ya kujali itikadi ya vyama vyao, lilitengeneza kabila lao jipya la walaji. Kabila hili sasa limeungana kuhakikisha serikali iliyo madarakani, iliyojikita kuhakikisha inakata mirija ya minyoo ambayo imelifyonza taifa hili kwa miaka mingi inaondoshwa.
Kwa bahati mbaya, na mara zote ilivyo, huwa kuna kundi ambalo hutumika kufanikisha mipango ya kabila la walaji. Kundi hili lina sifa zifuatazo:-
Aidha, kabila hili la walaji linaendesha vikao vya siri kila usiku kwa kushirikiana na baadhi ya watu waovu wa mataifa ya nje yenye uchu pia na mali za taifa letu kuhakikisha serikali hii inayowazibia inaondoka bila kujali ni chama gani ilimradi anayeingia atokane na kabila lao la walaji.
Kwahiyo, uchaguzi ujao ni kati ya kundi la wale wanaolitakia mema taifa hili liondokane na ufisadi na ubadhirifu uliokithiri na kufuata njia njema ya kimaendeleo na uadilifu dhidi ya kabila la walaji waliokatwa mirija yao iliyo lifyonza taifa hili. Uwanja wa mapambano waliochagua ni CCM. Hivyo ni kazi kwa kundi adilifu kucheza karata yake na kuwaondosha waovu (walaji) ndani ya chama kwa weledi mkubwa basi hapo itakuwa "..kazi iendelee.."
Tupo tayari kutokuchezewa na kabila ovu, uwezo tunao, sababu tunayo na nia tunayo.
Dunstan Buberwa Ntamilyango,
Mwananchi wa kawaida.
Biharamulo.
0759829015.

- Kuendeshwa na mihemko
- Halina utamaduni wa kufikiri kwa udhati (critical thinking)
- Huwa na tabia ya matumaini ya maisha mazuri bila kufuata njia sahihi
- Ni kundi mara nyingi la umri wa kati