Suala la ATCL kupata hasara ya Tzs bilioni 60 na kuendeshwa kihasara kwa miaka 5

Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
161
364
Mwishoni mwa mwezi Machi Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan alipokea ripoti mbili za CAG na TAKUKURU na moja ya mambo yaliyoibuka na kuchukua mjadala mpana na mkubwa sana ni hatua ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Bwana Charles Kichere kusema kwenye ukaguzi wao wa mwaka 2019/20 waligundua Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) kupata hasara ya Bilioni 60 huku likiendeshwa kihasara kwa takriban miaka 5.

Suala hili limeibua mjadala mkubwa na mpana sana maeneo mbalimbali na kila mmoja akitoa maoni yake kuhusu ripoti hiyo hasa kwenye eneo la Shirika letu la ndege (ATCL).

Mimi nitazungumzia jambo hili kwenye maeneo makubwa mawili aliyoyagusia CAG. Kwanza, hasara ya Bilioni 60 iliyopata ATCL kwa mwaka wa fedha uliopita. Pili, Shirika hilo kuendeshwa kihasara kwa miaka 5.

Kuhusu hasara ya Bilioni 60 ya ATCL kwa mwaka 2019/20.

Kimsingi mwaka 2019/20 haukuwa mzuri sana kwenye biashara na sekta ya anga tena kwa Shirika linalochipukia na lililofanya uwekezaji mkubwa karibuni kama ATCL. Mwaka 2019/20 ulikuwa mbaya mno kwenye sekta ya anga hasa baada ya mripuko wa ugonjwa wa Corona. Wakati kwanza ATCL inapambana kutanua wigo wake wa kutoa huduma na kufika maeneo mengi zaidi, Corona iliingia na anga la dunia nzima lilifungwa ili kuzuia kasi ya kuenea kwa Corona.

Safari zote za nje za ATCL kwenda Kenya, Ethiopia, Uganda, Zimbabwe na kote zilifungwa na hata safari nyingi za ndani ziliathirika kwa kupungua kwa wasafiri kwa kiwango kikubwa sana.

Kama kuna sekta iliathirika moja kwa moja na mripuko wa Corona basi sekta ya anga iliongoza na mwaka uliopita halipo Shirika lolote duniani lililopata faida zaidi ya hasara ya matrilioni mpaka mengine yakaelekea kuanguka kabisa kama Ethiopia Airlines na UAE.

Ukienda Kenya Airways walipata hasara ya zaidi ya Billioni 700, Ethiopia kama Shirika mama na kubwa zaidi kote Afrika wao walitangaza hasara ya Trilioni 1.1, Rwanda zaidi ya Billioni 200, Uganda na kote ulimwenguni mashirika makubwa yote ya ndege yalitangaza hasara ya zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 100.

Licha ya uchanga na mwanzo mzuri wa uwekezaji wa ATCL lakini bado Shirika letu limepata hasara kiduchu sana ukilinganisha na mashirika mengine ya majirani zetu na kote ulimwenguni kwahiyo kabla ya Watanzania kuhoji hasara hii ya ATCL kwa mwaka wa fedha uliopita ni lazima tuangalie mazingira ya biashara yenyewe ya anga hapa nchini na ulimwenguni kwa msimu uliopita. Hapo hujaweka changamoto zingine za uwekezaji na uzoefu hasa tukizingatia ndiyo kwanza Shirika hili linaendelea kukua kutoka kuwa hoi bin taabani.

Kuhusu Shirika lenyewe kuendeshwa kihasara kwa miaka 5 iliyopita.

Kwanza lazima tukubaliane, miaka mitano ya ATCL iliyotajwa kwenye ripoti ya CAG kuendeshwa kihasara ndiyo miaka ambayo Shirika hili lilifanyiwa uwekezaji mkubwa sana. Tukumbuke, wakati Hayati Rais Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015, Shirika hili lilikuwa na ndege moja tu tena mbovu. ATCL ilikuwa hoi ikikodi ndege zake na ilikuwa inaelekea kufa kabisa. Rais Magufuli aliamua kulifufua Shirika hili kwa kuamua kununua ndege zake mpya 11 ambazo 9 zimeshaingia tayali, kuboresha miundombinu ya viwanja karibu vyote vya ndege na kununua rada zake zenyewe za kuendeshea ndege.

Kimsingi Serikali ilikuwa inalifufua Shirika hili lililokuwa linaelekea kufa kabisa na kulirudisha kwenye utoaji wa huduma na ushindani. Sasa kwa kanuni za uchumi, ni ngumu kufanya uwekezaji mkubwa kama huu uliofanywa pale ATCL halafu ghafla na haraka tu utegemee kupata faida sana tena kwa Shirika lililofufuliwa kama ATCL.

Kwa namna ATCL ilivyokuwa huko nyuma na kwa jinsi ilivyofanyiwa uwekezaji mkubwa kwa hii miaka mitano, ni mapema mno kuanza kupata faida tena kwa ukanda wetu ambao bado yako mashirika mengine makongwe na makubwa tu kama la Ethiopia, Kenya Airlines na Rwanda Airlines yenye uzoefu mkubwa kwenye biashara hii kwa muda mrefu ukiachana na sisi ambao ndiyo kwanza tunapambana kulirudisha kwenye mstari Shirika letu.

Mabilioni yaliyowekwa kwenye ununuzi wa ndege zetu mpya 11, upanuzi na uboreshaji wa viwanja vyetu vya ndege nchi nzima na ununuzi wa rada, bado tunahitaji muda kuanza kuhesabu faida na kunufaika moja kwa moja kiuchumi na uwekezaji huu.

Kwahiyo suala la Shirika letu kuendeshwa kihasara kwa miaka 5 ni hatua ya awali ya uwekezaji wetu mkubwa tulioufanya kwa ATCL ambao utakuwa na faida huko mbeleni wakati huu tukiendelea kuliboresha Shirika letu, kushughulikia changamoto zinazojitokeza na kujitanua zaidi kibiashara.

Tujiulize ni lini ukaanza kuwekeza na ukatengeneza faida papo hapo? Kwenye uwekezaji ni lazima uweke mtaji (inputs) halafu baadae utengeneze faida (outputs). Watu wa uchumi wanaelewa vyema kabisa ninachokieleza hapa. Leo hii ukinunua basi la milioni 300 la kusafirishia abiria, tegemea kupata faida (outputs) baada ya mwaka mmoja mpaka miwili, sasa sisi tuliowekeza zaidi ya Trilioni 1 kwenye sekta hii ya anga bado tunahitaji muda, nidhamu na uzoefu kutengeneza faida zaidi huko mbele lakini kwasasa bado hatuwezi kuona au kuhesabu moja kwa moja faida ya uwekezaji huu mkubwa tulioufanya kwasababu bado ni mapema sana. Miaka mitano pekee haitoshi kupima faida au hasara ya uwekezaji wa Mabilioni kwa Mabilioni ya pesa tulizoweka pale ATCL.

Kwahiyo kilichosemwa kwenye ripoti ya CAG kwa ATCL kuendeshwa kwa miaka 5 kwa hasara ni cha kawaida sana kiuwekezaji hasa kwa hatua ya sasa tuliyochukua kufanya uwekezaji mkubwa pale ATCL. Hii ndiyo kusema tuendelee kula taratibu na nyama tutazikuta chini.
 
Sasa kwann magu alisema atcl inapata faida na kupeleka gawio kwa serikali? Au na nyie mmekua wanasiasa?View attachment 1749484


Hiyo faida ndio imepunguza hasara mwaka hata mwaka. Hapa kinachotafutwa ni ndege zilizoko ATCL ziuzwa kama mitumba kwa farm price yashamba la bibi. Zilizoko kiwandani ziuzwe kama chuma chakavu.

Hamna anayetaka kuzungumzia faida zisizo za moja kwa moja, kama kushamirisha utalii. Na kuponya ndoa za familia za wahanga wa kuhamia Dodoma nk.

Hamna anayezungumzia hasara kwa mfano wa ile ndege ATC ya kukodishwa kutoka Costarica ambayo iliokotwa kutoka jalalani ikapigwa rangi kwa brush ya mkono na ikaipotezea ATC mabilioni ya toxi ta kukodishwa kwake. Kwa saa ni junk hapo airport. Mambo haya ni made in Tanzania tu.
 
Shida hapa sii uchanga wa shirika shida ni kuficha hata hizo taarifa ya kupata hasara kiduchu.Nakudanganya mabilioni ya faida.
 
Whether kuna sababu za kupata hiyo hasara au hakuna sisi haituhusu bali the fact that tuliambiwa shirika linatengeneza faida na kugawa gawio la zaidi ya bilioni 27 kwa serikali kuu hiyo ilitufanya tuamini tupo salama.

Hakuna asiyejua matatizo yaliyotokea globally na kuikumba sekta ya anga, kwanza tulikuwa tunamshangaa yaani katikati ya global pandemic jamaa hajali hata kuweka akiba anaenda kununua mandege mengine tu.

He was crazy man, hasira yetu sio hizo sababu za kupata loss, Ila alituona sisi ni mafala sana na kundi lake la wahuni wanahakikisha wanabrainwash watu.

Hii ndio tunakataa, kwa hiyo hayo maelezo yako kawaite watu wa Chato pale airport ya Chato waelezee hayo halafu mkimaliza nenda ziwani mkaogelee na samaki.
 
Back
Top Bottom