Suala la ardhi halimo kwenye Muungano, Zanzibar wapo makini kulinda ardhi yao lakini wametuzidi akili kuimiliki ardhi ya bara

Mtambwe

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
759
1,000
Kwenye katiba ya Tanzania hakuna sehemu iliyohusisha ardhi kwenye muungano, Ardhi ya Tanzania bara ni kwajili ya raia wake na ardhi ya Zanzibar ni ya raia wake.

Hatuna budi kuwapongeza wazanzibari maana hawana mchezo kwenye kulitekeleza hili kwa kulinda ardhi yao iwe kwajili yao, Lakini sasa huku bara ni kama vile tuna upofu katika kusimamia haki yetu kwasababu katiba imeshaweka wazi hii ardhi ni ya raia wa bara pekee lakini cha ajabu wazanzibari wanapewa umiliki wa ardhi, ndugu zangu hivi hatuna uchungu na ardhi yetu kama ilivyo kwa wazanzibari wenye uchungu na ardhi yao ?

Mtu wa bara ukienda huko Zanzibar hata uwe na pesa vipi utapigwa stop, ukiona unamilikishwa kirahisbi rahisi jua ya kwamba umekutana na wajanja wa kipemba, watakufojia hadi hati za ardhi feki ilimradi uingie kingi, utatapeliwa pesa zako mchana kweupe, siku unaanza shughuli zako ndipo unakuja kugundua umetapeliwa.

Ajabu ni kwamba Kigamboni karibu yote, Temeke, Buguruni, Wazanzibar wanamiliki ardhi bila bugudha. Msingi wa hoja yangu ni kwanini Wazanzibari wanamiliki ardhi Bara licha ya kwamba katiba hata ya sasa ipo wazi haiwaruhusu ?

Kimsingi Tanganyika imekuwa kama shamba la bibi au yatima, haina mwenyewe wala mtetezi.

Kuna kila sababu ya kuona kwamba Zanzibar "wametuzidi akili", Sizungumzii akili za kukariri darasani what is physics, ni akili ya kawaida kabisa ambayo mtu inabidi awe nayo, kwa kiingereza huitwa "common sense"

Tatizo liko Palepale, nyinyi kuiuwa Tanganyika yene kiujanja na nyinyi kujifanya ndio Tanzania, Kutokana na katiba ya Tanzania , Mzanzibari anayo haki ya kumiliki ardhi Tanzania Bara, kwani na yeye ni Mtanzania. Lakini mtanzania Bara (mTanganyika) yeye hawezi kumiliki Zanzibar kwani yeye sio Mzanzibari . Kwanza ifufueni hi Tanganyika ionekane, ndio itakaa pamoja na Zanzibar itetee maslahi ya Tanganyika kwenye Tanzania.
 
Bepari2020

JF-Expert Member
Nov 7, 2020
974
1,000
Wewe utakuwa umevimbirwa na maurojo.
Nchi kimsingi ni kipande cha ardhi majina yanaweza kubadilika ila wananchi wake bado wapo.
Mwaka 1964 territory ya tanganyika inajulikana ilikuwaje
Tanganyika ilianzishwa rasmi na Mwingereza chini ya League of Nations mandate mwaka 1922 lakini ilikufa mwaka 1964. Siyo ilibadilika jina, ilikufa kabisa. Nyerere aliiuwa. Hakuna wananchi wa Tanganyika, wapo wananchi wa Tanzania. Ukiitaka Tanganyika tena itabidi uanze upya na hamuwezi. Wala usijidanganye. Ni Nyerere peke yake aliyeweza kuyaunganisha hayo makabila zaidi ya 120 yaishi kama nchi moja. Hakuna atakayeweza tena. Mtagawanyika kikabila, kikanda siyo Tanganyika tena.
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
6,046
2,000
Hao Wazanzibari wenyewe hawamiliki ardhi wanapewa hati ya matumizi ya ardhi tu. Serikali ikiitaka hiyo ardhi inaichukuwa tu bali unalipwa fidia ya mazao na majengo ikiwa hujaiendeleza inachukuliwa bila yakulipwa hata senti.

wameshawaumiza watu sana kwa style kam hiyo, hata ukiwa na nyumba unalipwa thamani ya jengo tu bila ya kujumlisha thamani ya kiwanja. Africa uonevu ndio msingi mkuu wa watawala
 
Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,463
2,000

Weka namba yako hapa ili nikupigie kabisa, haiwrzekani ukashindwa kuwafikiria wajukuu wa wajukuu wako Kama watakuwa na ardhi, unawaza wewe TU kwamba Tanganyika tupo wachache...weweeeee!!!
Pointi yangu ni kwamba tunaweza kujadili mambo bila kutukanana kama ambavyo umejaribu kutishia hapo juu.

Carrying capacity ya Zanzibar ni ndogo kuliko ya Tanzania bara. Ndio maana naelewa wale walio wachache "kuruhusiwa" kwenda kumiliki ardhi sehemu kubwa, na "kukataza" walio wengi kwenda sehemu ndogo.

Zanzibar ina eneo la mraba lipatalo Km² 2,400 wakati Tanzania bara ina km² 950,000.

Sidhani kwa eneo hilo kuna haja ya "sisi" wabara kuwafurusha "wenzetu" katika muungano.

Hoja ya vitukuu vyetu wataishi wapi, jibu lake halipatikani katika kuwazuia wazenji mkuu.
Maana hata ukiwazuia wazenji, ardhi ya Tanganyika haiongezeki wakati watu watazidi kuongezeka kwa kadri ya miaka inavyosogea.
Je, utataka kuiteka Kenya ili hao vitukuu walioongezeka kwenye ardhi ile ile wapate sehemu ya kuishi ?

Lakini pia, kibailojia ni kwamba "nature" ina tabia ya kuji "balance" yenyewe.

Nature haiwezi kuki host kitu chochote kisichohitajika au kilichozidi.
Litatokea "punguzo" la viumbe ili kuweza kuendana na mahitaji na uwezo wa eneo husika bila kujali anayepungua ni "kitukuu chetu" au ni mzenji.
 
Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,463
2,000
We we ndio unataka kupotosha kuna kitu kinaitwa certificate of occupancy ambayo inampa mtu rght of occupancy kwenye eneo fulani kwa muda wa kuanzia miaka 33,66,au 99.
Mgeni hapati hiyo, mzanzibar anapata certificate of occupancy huku bar a ila mbara hapatiwi certificate of occupancy kule Zanzibar anakuwa anakodishiwa kama mgeni mwingine yeyote tuu,
Kuna tofauti kubwa na nyingi kati ya mtu anayemiliki ardhi kwa kutumia certificate of occupancy na mtu anayekodishiwa th
Mfano mdogo ukiwa na certificate of occupancy unaweza kuitumia kupata mkopo au hata kumdhamini mtu mahakamani ila document ya kukodishiwa haikubaliki
Mkuu, kuna kitu kinaitwa "Upendeleo wenye kuleta usawa"

Unaposhughulika na pande mbili ambazo haziko sawa ki-hadhi kama vile;

kubwa vs ndogo,
imara vs dhaifu,
kinyonge vs chenye nguvu,

tajiri vs maskini, n.k,

kuna wakati unatakiwa kumpendelea "mnyonge" ili kuleta mazingira ya "usawa."

Nitatoa mifano kadhaa...
1. Zifikirie privileges ambazo huwa wana enjoy watu ambao ni ma last born kwenye familia. Udogo au utoto wao huwafanya waupate usawa katika upendeleo.

2. Ukikuta mtoto wa miaka kumi na mwingine ana miaka mitatu wanagombania "andazi", kesi hii inakua best solved kwa kumpa yule mdogo andazi lote au kipande kikubwa zaidi kuliko huyu mkubwa.
Unatumia upendeleo kuleta usawa.

3. Haki za wanawake na usawa wa kijinsia, unapatikana katika kufanya "upendeleo wa makusudi" kwa wanawake ili kuleta "usawa" na wanaume. Mfano suala la wabunge wa viti maalum, n.k

Katika mazingira ya namna hii, Zanzibar ambaye ni mdogo anapata "upendeleo" katika mambo kadha wa kadha dhidi ya Bara ambaye ni mkubwa ili kuleta "usawa".

Na miongoni mwa hizo pendeleo ni hili suala la ardhi, ajira na nafasi za uongozi.

Mimi sioni tatizo katika hili.
 
Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,336
2,000
Zanzibar kisiwa
Ardhi yao ndogo
Wangeruhusu wabara wamiliki ardhi
Mpaka sasa kungekwisha

Basi tupige marufuku Wazaramo na Wakurya kununua ardhi Kilimanjaro na Kagera ili ardhi ya Wachagga na Wahaya isimalizwe!

kuna ubaya gani kama "Zanzibar kungekwisha" kwa kujazwa michanganyiko ya Watanganyika na Wazanzibari ?????

Julius Nyerere's most historically wrongheaded decision was force feeding Tanganyikan's with the Zanzibar union.
 
UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
6,208
2,000
Ajabu ni kwamba Kigamboni karibu yote, Temeke, Buguruni, Wazanzibar wanamiliki ardhi bila bugudha. Msingi wa hoja yangu ni kwanini Wazanzibari wanamiliki ardhi Bara licha ya kwamba katiba hata ya sasa ipo wazi haiwaruhusu ?
Kama ardhi siyo issue ya Muungano, basi ni wazi hao wazanzibari wanamiliki ardhi kinyume cha sheria mama, katiba. Ipo siku wabara wakiamka toka usingizini watadai ardhi yao kikatiba na itabidi wazanzibari waiachie kikatiba (kisheria).
 
Averoes

JF-Expert Member
Jan 30, 2014
984
1,000
Kama ardhi siyo jambo la muungano kwa Znz, je kwa Tanganyika ardhi ni issue ya muungano? Kama siyo, kwa nini wanajimilikishwa ardhi Bara?
As far as sheria za Uraia Uhamiaji, Mambo ya ndani, Ulinzi na Sarafu ni Muungano Wazanzibari na hata wazungu na Wahindi watamiliki Ardhi Bara.
Tatizo kubwa mlofanya ni kuipokonya Zanzibar Sovereignity yake, si hivyo isingalikuwa issue.
Kuna mali na rasilmali nyingi za Zanzibar mumezipora ndani ya Tanganyika na ndani ya Zanzibar in the name of Muungano hicho kilobaki bado mnataka kukimaliza? Na wazanzibar watakuwa kama viroboto nguoni mwenu au chura ndani ya mkonga wa tembo.
 
Ibumalo

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
379
500
Kwenye katiba ya Tanzania hakuna sehemu iliyohusisha ardhi kwenye muungano, Ardhi ya Tanzania bara ni kwajili ya raia wake na ardhi ya Zanzibar ni ya raia wake.

Hatuna budi kuwapongeza wazanzibari maana hawana mchezo kwenye kulitekeleza hili kwa kulinda ardhi yao iwe kwajili yao, Lakini sasa huku bara ni kama vile tuna upofu katika kusimamia haki yetu kwasababu katiba imeshaweka wazi hii ardhi ni ya raia wa bara pekee lakini cha ajabu wazanzibari wanapewa umiliki wa ardhi, ndugu zangu hivi hatuna uchungu na ardhi yetu kama ilivyo kwa wazanzibari wenye uchungu na ardhi yao ?

Mtu wa bara ukienda huko Zanzibar hata uwe na pesa vipi utapigwa stop, ukiona unamilikishwa kirahisbi rahisi jua ya kwamba umekutana na wajanja wa kipemba, watakufojia hadi hati za ardhi feki ilimradi uingie kingi, utatapeliwa pesa zako mchana kweupe, siku unaanza shughuli zako ndipo unakuja kugundua umetapeliwa.

Ajabu ni kwamba Kigamboni karibu yote, Temeke, Buguruni, Wazanzibar wanamiliki ardhi bila bugudha. Msingi wa hoja yangu ni kwanini Wazanzibari wanamiliki ardhi Bara licha ya kwamba katiba hata ya sasa ipo wazi haiwaruhusu ?

Kimsingi Tanganyika imekuwa kama shamba la bibi au yatima, haina mwenyewe wala mtetezi.

Kuna kila sababu ya kuona kwamba Zanzibar "wametuzidi akili", Sizungumzii akili za kukariri darasani what is physics, ni akili ya kawaida kabisa ambayo mtu inabidi awe nayo, kwa kiingereza huitwa "common sense"

Bara mkiamua kuwapa ardhi wazanzibari ni hiari yenu kulingana na sheria na sera zenu. Zanzibar kulingana na sera na sheria zao wameamua hivyo msiwalaumu.

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
16,846
2,000
Pointi yangu ni kwamba tunaweza kujadili mambo bila kutukanana kama ambavyo umejaribu kutishia hapo juu.

Carrying capacity ya Zanzibar ni ndogo kuliko ya Tanzania bara. Ndio maana naelewa wale walio wachache "kuruhusiwa" kwenda kumiliki ardhi sehemu kubwa, na "kukataza" walio wengi kwenda sehemu ndogo.

Zanzibar ina eneo la mraba lipatalo Km² 2,400 wakati Tanzania bara ina km² 950,000.

Sidhani kwa eneo hilo kuna haja ya "sisi" wabara kuwafurusha "wenzetu" katika muungano.

Hoja ya vitukuu vyetu wataishi wapi, jibu lake halipatikani katika kuwazuia wazenji mkuu.
Maana hata ukiwazuia wazenji, ardhi ya Tanganyika haiongezeki wakati watu watazidi kuongezeka kwa kadri ya miaka inavyosogea.
Je, utataka kuiteka Kenya ili hao vitukuu walioongezeka kwenye ardhi ile ile wapate sehemu ya kuishi ?

Lakini pia, kibailojia ni kwamba "nature" ina tabia ya kuji "balance" yenyewe.

Nature haiwezi kuki host kitu chochote kisichohitajika au kilichozidi.
Litatokea "punguzo" la viumbe ili kuweza kuendana na mahitaji na uwezo wa eneo husika bila kujali anayepungua ni "kitukuu chetu" au ni mzenji.
Hizo nyuzi za uzanzibari ni nyingi kipindi hiki rais SSH akiwa ni mzenji, wengi ni wale wanaoitwa Sukuma Gang wanajaribu kuisagia kunguni serikali ya sasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom