Suala la ajira kwa vijana limekosa ubunifu katika kutengeneza fursa za kipekee

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
Na Peter Mwaihola

Sio ajabu kwa sasa kupita mtaa mmoja na kukuta Video Library zaidi ya 20 ambapo kila baada ya nyumba 3 unakuta library.

Hali hii inadhihirisha ni namna gani suala la ajira kwa Vijana limekosa ubunifu katika kutengeneza fursa za kipekee.

Kumekuwa na ombwe la Vijana wabunifu katika kutengeneza fursa hivyo kupelekea Vijana wengi kurundikana katika fursa moja au mbili zinazoonekana kuwa rahisi katika eneo husika.

Kwa sasa fursa Kama uendeshaji wa bodaboda na kufungua maktaba za Kanda za video yaani, video library ndizo zinaonekana kuwa na mrundikano wa wa Vijana wengi hususani waliohitimu elimu ya juu katika taaluma mbalimbali nchini.

Ubora wa elimu inayotolewa na vyuo nchini nayo inatiliwa mashaka kwakua imeshindwa kutoa Vijana wenye uwezo wa kubuni fursa mpya badala yake wanaishia kuzitumia tu zile zilizopo.

Aidha inaonekana Kuna kasumba ya wahitimu na Vijana wengi kuwa na kasumba ya kuchagua kazi fulani hususani za ofisini hivyo kushindwa kubuni kazi nyingine zikiwemo za kilimo.

Venance Makirika ambae ni mhadhiri wa uchumi kutoka chuo kikuu Cha kikatoliki Mbeya, CUCoM anasema kuwa vyuo vingi nchini haviwapiki Vijana kwenye ubora unaotakiwa ili wawe wabunifu pindi wanapohitimu elimu zao.

Pia Makirika anashauri kuwe na utaratibu wa kila chuo kufundisha masomo ya ziada yanayohusu ujasiriamali na ubunifu ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa ajira kwa Vijana.

Makirika anawaasa Vijana kuondoa kasumba ya kusubiri kuajiriwa pamoja na kuchagua kazi Jambo ambalo Ni kikwazo Cha Vijana wengi kufikiri namna ya kujikwamua.
 
Hizi fursa mbili ndizo zinachangamkiwa na vijana wengi kwakua ndizo nyepesi zisizohitaji mtaji au mtaji mkubwa na zinatoa faida ya angalau usife njaa.

Mfano library kompyuta yenye speed ya kukutosha kufungua library unaipata kwa kuanzia 200K mpaka 300K. Hard drive 1TB unaweza ipata kwa 60K mpaka 130K kutegemea kama ni external na kama ni dukani au mkononi.

Pia muvi haziozi. Ukinunua season leo ukaicopy kwenye mashine utaiburn na kuwauzia wateja for months to come. Wakati wewe ile muvi umeinunua KKoo 1K, na kuburn unaburn kwa 1K mpaka 2K kutegemea na location.

Kopo la empty linakaa empty cd 50. Tuassume 10 zimeharibika so ukiburn cd 40 per day wewe una 40K. Wakati kopo la empty umenunua kwa 10K mpaka 13K.

So ni biashara fulani ambayo ilinifanya niishi bila kuhofia kabla watu hawajazagaa kama unavyosema. Na sababu ni hiyo, ina easy access na ina faida.

Kwenye bodaboda tulipata sana pesa kabla ya ujio wa taxify na uber, safari ya kutoka Masaki mpaka Ubungo ilikua mtu anakulipa 7K baada ya taxify na uber kuja hiyo safari imekua 2500.

Sasa mtaji wa bodaboda ni nini?

Ni muda wako tu kujitolea kujifunza, ndani ya saa moja unakua ushajua kuendesha, ndani ya siku moja unakua ushajua kupishana na magari. Kesho kutwa unaenda kijiweni kupiga deiwaka.

Hayo yote na hauna leseni. Na maisha yanasonga.

Wewe mwenyewe mleta uzi kama unaweza kutaja fursa unayoamini ina urahisi kuiexploit itaje watu turuke nayo.
 
Mkuu nakubaliana na wewe.

Hao watu wanaofundisha biashara kwa nadharia ni wa kupuuzwa tu utakuta mtu anafundisha watu biashara na hajawahi hata kuuza karanga.

Biashara kwa nadharia na kwa vitendo ni vitu viwili tofauti na huwezi kufanya biashara bila kujua jamii yako iliyokuzunguka inataka nini.

Kuna biashara ambazo ukiziweka uswahilini hulali njaa lakini pia kuna biashara zingine ni kwa ajili ya uzunguni.

Watu wa uswahilini kutokana na ugumu wa maisha wanaopitia huwa wanapenda sana vitu vya kuwapa burudani ili kujifariji.

Mfano wa biashara za burudani ni kama hiyo video library,kukodisha mziki(maspika),Grocery(bia na soda),banda la chipsi ambalo linakaa pamoja na grocery,Play games station.

Hizi ndio biashara ambazo ukianzisha uswahilini hazitakuangusha,lakini wewe jifanye mwanateknolojia eti sijui umegundua gari ya utalii,au sijui unauza majiko ya solar watu hawakuelewi utahubiri hadi uchoke.
 
Nyie na maneno ya vijana wamekosa ubunifu siku mkifukuzwa kazi muwe jobless ndiyo huwa mnajinyonga kabisa au kufa kwa msongo wa mawazo sasa sijui huo ndiyo ubunifu wenu?

Hali ya mtaani siyo nyepesi kama inavyoongelewa vijana wanakomaa sana ila mambo ndiyo hivyo tena vice versa, tupeni ubunifu mliofanya nyie ambao ni mpya kabisa haujawahi kuwepo.
 
Mkuu nakubaliana na wewe.
Hao watu wanaofundisha biashara kwa nadharia ni wa kupuuzwa tu utakuta mtu anafundisha watu biashara na hajawahi hata kuuza karanga...
Mimi hua nasema ni asilimia ndogo ya watu/ vijana hawataki kufanya kazi. Ila asilimia kubwa kila mmoja anataka apate sehemu ya kumpa angalau pesa ya kula na kodi hata kama atakua na godoro tu ndani.

Shida inayokuja ni swala la mtaji. Sasa mhadhiri wa hiko chuo pengine anapata picha kwamba kujiajiri kwa kijana ni kua na ekari 10 za nyanya au matikiti.

Hapo kwenye majiko ya solar umenigusa ila niamini mimi bidhaa nyingi za solar zinauzika sana vijijini ila ujitoe kuzurura haswaaaa. Jana nilikua sehemu hiyo ndiyo nikajua kumbe kuna waTanzania wanamiliki ngamia, farasi na mbogo.
 
Mimi huwa nasema ni asilimia ndogo ya watu/ vijana hawataki kufanya kazi. Ila asilimia kubwa kila mmoja anataka apate sehemu ya kumpa angalau pesa ya kula na kodi hata kama atakua na godoro tu ndani...
Mikoani bidhaa za sola zinauzika japo kuna wadau wananiambia soko lake limeshuka baada ya umeme wa REA kusambazwa mikoani.
 
Mikoani bidhaa za sola zinauzika japo kuna wadau wananiambia soko lake limeshuka baada ya umeme wa REA kusambazwa mikoani.
Nafikiri huu umeme wa REA ukizidi kusambaa na kuendana na kasi ya mahitaji kwa kua na material na nguvu kazi itachukua muda kidogo. And yeah soko linashuka
 
Kufundisha Ubunifu ?

Ubunifu ni Process, Ubunifu ni utamaduni, Ubunifu ni Mazingira..., huwezi kupata watoto wabunifu kama watu wanakuwa indoctrinated, hawaruhusiwi kuhoji na kila kitu wanaaminishwa kinapatikana kwenye kitabu fulani na ni muumba ndio ameamua

Ubunifu utaongezeka iwapo tu tutakuwa na utamaduni wa kuhoji na kutokukubaliana na status quo..., ikiwa tutakiwa critical
 
Na Peter Mwaihola.

Sio ajabu kwa sasa kupita mtaa mmoja na kukuta Video Library zaidi ya 20 ambapo kila baada ya nyumba 3 unakuta library...
Sio wahitimu tu kuigana kwenye kufungua biashara zisizona ubunifu, hata wewe mtoa mada umekosa ubunifu kwa kuleta thread ambayo ni clone. Thread kama hizi zipo nyingi sana umu Jamiiforums.
 
siwezi walaumu sana vijana mtu anamaliza chuo hana hata akiba ya elfu kumi bado anapambana na njaaa atainvest vipi?

tatizo naliona kwa waliopata fursa ya kuajiliwa wakashidwa kuinvest na kuajiri wengine
 
Back
Top Bottom