Suala la Academic International School kudai ada ya muhula wakati huu halikubaliki, Serikali tunaomba muingilie kati

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
May 8, 2013
9,548
24,159
Mh Waziri wa Elimu na Serikali tunaomba muingilie kati hili linaloendelea katika hii shule ya Academic International School ya hapo Dsm kwani wanawalazimisha Wazazi kulipa Ada ya term nzima wakati huu ambao tupo kwenye janga la Corona, shule zote zimefungwa na haijulikani ni lini hali itarudi kuwa ya kawaida pale shule zitakapofunguliwa rasmi.

Ipo hivi, mara baada ya Serikali kuzifunga shule zote kutokana na janga la corona, shule hii kama zilivyo nyingine nyingi, imekuwa ikiwatumia wanafunzi wake assignments/maswali mbalimbali kupitia walimu wa masomo kama sehemu ya kuwa keep watoto busy hasa kipindi hiki ambacho wapo nyumbani.

Hili ni jambo jema na Wazazi hawakatai kwamba kwenye hili kuna gharama za hapa na pale ambazo Shule na walimu wamekuwa wakiingia ili kulifanikisha hili la kuwasaidia watoto kipindi hiki wakiwa nyumbani. Lakini hili la kuwaambia Wazazi walipe ADA/TUITION FEES ya muhula mzima HALIKUBALIKI kwani watoto wapo nyumbani na hawapati zile class sessions za masomo yote kama wanapokuwa shuleni full time. Hakuna chochote kipya cha kwenye masomo ambacho wanakipata hivi sasa zaidi ya Walimu kuwatumia assignments/maswali ili kuwa keep busy kipindi hiki ambacho wapo nyumbani.

Shule walau ingesema Wazazi wanapaswa kulipa kiasi fulani cha Ada/percent fulani ya Ada ili kusaidia hili ambalo linafanywa na walimu hivi sasa la kuwasaidia wanafunzi wakiwa nyumbani lakini sio kulipa Ada kamili.

Tunaomba sana Serikali kupitia Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako kulimulika hili.Vyombo vya kiuchunguzi vya serikali viliangalie hili linalofanywa na hii Academic Internationl School la kudai Ada kwa Wazazi wenye watoto kwani hii sio HAKI kabisa.

20200416_071348.png

Screenshot_20200416-071311.png
Screenshot_20200416-071202.png
 
Mleta uzi ni mpumbavu sana

Shule za kata si zipo na ada ni elfu ishirini yaani bei ya bia 10 tu

Peleka mtoto huko shule ya kata

Unafahamu Capitalist economy wewe?

Tanzania uchumi hauodhiwi na serikali ndio maana kuna sekta binafsi upo?

Unajifanya tajiri kumbe maskini wa kutupwa, Peleka mtoto shule ya kata
 
Hapo ni kweli wanawaumiza lakini kwa upande wa pili pia na wao wanaumia maana wafanyakazi wao wana mikataba ambayo wanawalipa mishahara ambayo ni full hata kama wapo nyumbani kipindi hichi.

Na chanzo cha mapato ya shule ili iweze kuwalipa hao wafanyakazi ambao wana mikataba ni ada za wanafunzi.

Sema kinachotakiwa ni kupunguza hizo ada ili wao wasiumie sana na nyinyi msiumie sana.

Kwenye janga hili la corona kuna watu wengi wataumia.




Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hili janga likiiisha litaziacha baadhi ya shule hoi bin taaban na zipo zitakazofanya vizur sana kibiashara.
Kwasasa wazazi wengi hawapokei hata simu za shule, ukiwatisha sijui utawafukuza wasipolipa ada wanakucheki tu na siku shule zinafunguliwa watatafuta nyingine wawapeleke watoto wao huko, sasa kama shule nyingi zenye ada kubwa zitakurupuka basi zitajichimbia shimo zuri tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ni kweli wanawaumiza lakini kwa upande wa pili pia na wao wanaumia maana wafanyakazi wao wana mikataba ambayo wanawalipa mishahara ambayo ni full hata kama wapo nyumbani kipindi hichi.

Na chanzo cha mapato ya shule ili iweze kuwalipa hao wafanyakazi ambao wana mikataba ni ada za wanafunzi.

Sema kinachotakiwa ni kupunguza hizo ada ili wao wasiumie sana na nyinyi msiumie sana.

Kwenye janga hili la corona kuna watu wengi wataumia.




Sent from my iPhone using JamiiForums
Elimu mliyosomea shule ina msaada gani?

Uchumi wa nchi kama Tanzania sio wa kijamaa tena

Mwinyi aliporuhusu watu kumiliki mali binafsi ndio ilikuwa mwisho wa ujamaa

Sasa wewe unataka serikali iwapangie ada shule binafsi?

Kama huna pesa kuna shule za kata mpaka za watu kukaa kwenye mawe
 
Mtazamo wako si sahihi maana unataka kusema kwa kuwa shule zimefungwa walimu wasilipwe. Kwenye shule binafsi, walimu hulipwa kutokana na school fees, chukulia tuu kama watoto wako ile likizo ya Midterm (two weeks) na ile ya mwezi mzima (Juni) hivyo watakapofungua shule (mimi naamini mid May) watafidia huo muda kwa kusoma mpaka Desemba bila kufunga.

By the way, International school mnalipa ada kwa mwezi badala ya term? Ridiculous
 
Mleta uzi ni mpumbavu sana

Shule za kata si zipo na ada ni elfu ishirini yaani bei ya bia 10 tu

Peleka mtoto huko shule ya kata

Unafahamu Capitalist economy wewe?

Tanzania uchumi hauodhiwi na serikali ndio maana kuna sekta binafsi upo?

Unajifanya tajiri kumbe maskini wa kutupwa, Peleka mtoto shule ya kata
Kata Ni bureeeeeeee we Shona sare nunua daftari nenda shule
 
Naunga mkono hoja mkuu.

Maana hata mm najifikiria niwape kesho(shule jina kapuni) au nipotezee maana walileta mitihani ya watoto wafanyie nyumbani na karatasi ya msisitizo wa kulipia ada juu.
 
Mzazi lipa tu hiyo ada tafadhali maana ndiyo chanzo kikuu cha mishahara ya wale walimu wanaompa maarifa mtoto wako.

Usipolipa hiyo ada, walimu na wafanyakazi wengine wa shule kama walinzi, wapishi, nk. watakosa mishahara na fedha za kujikimu wakati huu wa hili janga la Corona.
 
Usilalamike lipa ada. Huo in wajibu wako, hivi shule zitakapoamua kuufidia muda huu, utatuandikia tena kulalamika? Jiongeze ndugu yangu hiyo shule inaendeshwa na binadamu, pamoja na korona wanatakiwa kuishi wathamini sana waalimu wa watoto wako acha kujidhalilisha humu.
 
Back
Top Bottom