Thadei Ole Mushi
R I P
- Oct 13, 2018
- 35
- 259
Na Thadei Ole Mushi.
SUA wamekuja na panya wa Kupima Corona... Mimi nshaanza kuchoka na hawa panya wa SUA.
Sayansi hii ya kufundisha wanyama kunusa (Sniffing) kwa wenzetu ilianza muda mrefu sana. Ni mojawapo ya Technolojia ya kizamani kabisa. Huko Cuba Panya wameanza kutumika toka 1954 kunusa maeneo yenye madini, mobomu nk. Kwa sasa haitumiki Sana kwa kuwa njia za kisasa zaidi zimeendelea kugundilika kila kukicha.
Ni wakati sasa wa kuwaambia SUA badala ya kutrain Panya zaidi ambao hatuwatumii popote wajikite kwenye kugundua mabomu ambayo tutayauza au wajikite kwenye kufanya tafiti tunawezaje kutumia uranium iliyopo kule Dodoma kuzalisha nguvu za Nyuklia. Au wajikite kutengeneza Chanjo ya Corona ambayo tutaiuza.
Waliwahi kuja na panya wa kutambua TB lakini hakuna Hospital hata Moja inayotumia Panya kunusa makohozi. Bado njia za kisasa za kupima TB ndizo zinazoendelea Kutumika mahospitalini.
Hata hii ya kutegua Mabomu kwa kunusa ni ya zamani Sana. Majeshi ya wenzetu hawatumii Tena sniffing technology Sana nadhani tunapaswa kuanza kufikiria kubadilika.
Sio kwamba wenzetu hawawezi ku train Panya kufanya sniffing. Wanaweza Sana Ila ni technolojia ya Zamani mno watu walishahama huko wanaitumia technolojia hii mara Chache Sana.
Yaani Maabara za Dunia zipo busy kutengeneza Chanjo na Makampuni yanashindana kwenye kutengeneza Chanjo sisi tunamuwaza panya tu atusaidie kunusa watu wenye Corona.
Tuwekeze kwenye tafiti zitakazoleta faida na uvumbuzi wenye tija kwa Taifa na Dunia. Naona SUA wao kila kitu ni kuwaza Panya wao tu. Tumekuwa kama tumesimama mahali pamoja wenzetu wanakwenda mars na kurudi sisi tunalisha Panya Pumba tu hapo SUA. Na wameona hakuna Cha maana wanachofanya wameamua kuanzishwa course za Education. Jamani nafikiri hivi vyuo kila kimoja ki-save purpose yake.
Je kitu Wanachokiweza SUA ni Kutumia panya Kunusa Tu? Vyuo vikuu vingine wao kwani wanasemaje? Muhimbili pale kile kijumba Cha kujifukiza bado kipo?
Tunakwama wapi? Leo Tarehe 15/5/2021 asubuhi hii China imefanikiwa kurusha kifaa kwenda Sayari ya Mars na kimetua vizuri na kitakaa huko Miezi 3 kutafiti kama Kuna uwezekano wa maisha kwenye Sayari hiyo. Huko Sua Profesa anaamka na Box la Panya anaenda kuwachungulia na anatokea hadharani anasema amevumbua kitu.
Tubadilike... Dunia inakimbia sisi tumekaa kabisa na tumeanza kulala.
Ole Mushi.
0712702602