SUA badilikeni, achaneni na Panya imetosha

Mtoa maada hembu pitia hii page ya SUA, hzini baadhi ya Research zinazo fanywa na Professa mmoja kutoka SUA, nenda kaangalie Who is funding all researches the guy is doing. Ukimaliza njooo tuendelee kujadili kama taifa tunakwama wapi kukiwezesha chuo cha SUA kutupa its full potential.

Onyo : Msipende kuongea vitu msivo vijua

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Mbona hatujui kila siku panya tu haya waleteni hata kwenye zahanati wagundue hata iyo corona basi au wako kwa ajili ya corona za maprofesa
Hujui kwa sababu umechagua kuto kujua, pitia hyo website yao uome research zinazo fanyawa then njooo tujadili hapa.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Mtoa uzi usikalili maisha,huo utafiti kuhusu panya ni ka sehemu kadogo Sana kati ya tafiti nyingi zilizofanywa/zinazofanywa na SUA.
Hakijui hiki chuo!
Nafikiri ndiyo chuo kinachoheshimika zaidi Tanzania hata huko ulimwenguni kwa tafiti.
Wana maabara kubwa ya tafiti za mbegu na wanajenga maabara kubwa na BORA zaidi Africa.
SUA ukisikie tu mitaani ila ni chuo chenye tafiti nyingi zaidi ya panya.

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Na Thadei Ole Mushi.

SUA wamekuja na panya wa Kupima Corona... Mimi nshaanza kuchoka na hawa panya wa SUA.

Sayansi hii ya kufundisha wanyama kunusa (Sniffing) kwa wenzetu ilianza muda mrefu sana. Ni mojawapo ya Technolojia ya kizamani kabisa. Huko Cuba Panya wameanza kutumika toka 1954 kunusa maeneo yenye madini, mobomu nk. Kwa sasa haitumiki Sana kwa kuwa njia za kisasa zaidi zimeendelea kugundilika kila kukicha.

Ni wakati sasa wa kuwaambia SUA badala ya kutrain Panya zaidi ambao hatuwatumii popote wajikite kwenye kugundua mabomu ambayo tutayauza au wajikite kwenye kufanya tafiti tunawezaje kutumia uranium iliyopo kule Dodoma kuzalisha nguvu za Nyuklia. Au wajikite kutengeneza Chanjo ya Corona ambayo tutaiuza.

Waliwahi kuja na panya wa kutambua TB lakini hakuna Hospital hata Moja inayotumia Panya kunusa makohozi. Bado njia za kisasa za kupima TB ndizo zinazoendelea Kutumika mahospitalini.

Hata hii ya kutegua Mabomu kwa kunusa ni ya zamani Sana. Majeshi ya wenzetu hawatumii Tena sniffing technology Sana nadhani tunapaswa kuanza kufikiria kubadilika.

Sio kwamba wenzetu hawawezi ku train Panya kufanya sniffing. Wanaweza Sana Ila ni technolojia ya Zamani mno watu walishahama huko wanaitumia technolojia hii mara Chache Sana.

Yaani Maabara za Dunia zipo busy kutengeneza Chanjo na Makampuni yanashindana kwenye kutengeneza Chanjo sisi tunamuwaza panya tu atusaidie kunusa watu wenye Corona.

Tuwekeze kwenye tafiti zitakazoleta faida na uvumbuzi wenye tija kwa Taifa na Dunia. Naona SUA wao kila kitu ni kuwaza Panya wao tu. Tumekuwa kama tumesimama mahali pamoja wenzetu wanakwenda mars na kurudi sisi tunalisha Panya Pumba tu hapo SUA. Na wameona hakuna Cha maana wanachofanya wameamua kuanzishwa course za Education. Jamani nafikiri hivi vyuo kila kimoja ki-save purpose yake.

Je kitu Wanachokiweza SUA ni Kutumia panya Kunusa Tu? Vyuo vikuu vingine wao kwani wanasemaje? Muhimbili pale kile kijumba Cha kujifukiza bado kipo?

Tunakwama wapi? Leo Tarehe 15/5/2021 asubuhi hii China imefanikiwa kurusha kifaa kwenda Sayari ya Mars na kimetua vizuri na kitakaa huko Miezi 3 kutafiti kama Kuna uwezekano wa maisha kwenye Sayari hiyo. Huko Sua Profesa anaamka na Box la Panya anaenda kuwachungulia na anatokea hadharani anasema amevumbua kitu.

Tubadilike... Dunia inakimbia sisi tumekaa kabisa na tumeanza kulala.

Ole Mushi.
0712702602

View attachment 1785585
Mkuu nilikua nakuheshimu sana kutokana na nyuzi zako nyingi humu. Ila kwenye Uzi huu wa Leo nikiri kwamba umeji expose umbumbumbu wako
 
Hujui kwa sababu umechagua kuto kujua, pitia hyo website yao uome research zinazo fanyawa then njooo tujadili hapa.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
Hana anachokijua huyu, eti verified user....watu wanafanya tafiti na bado serikali haijatoa hata senti kugharamia. Halafu leo anataka watu wafanye tafiti za kwenda sayari ya mars, sijui mabomu ya nyuklia kwa pesa ipi? wajichangishe kutoka mifukoni mwao?
 
Hakijui hiki chuo!
Nafikiri ndiyo chuo kinachoheshimika zaidi Tanzania hata huko ulimwenguni kwa tafiti.
Wana maabara kubwa ya tafiti za mbegu na wanajenga maabara kubwa na BORA zaidi Africa.
SUA ukisikie tu mitaani ila ni chuo chenye tafiti nyingi zaidi ya panya.

Everyday is Saturday.............................. :cool:
SUA iko vizuri sema serikali haijataka kuwekeza kwenye elimu na tafiti. Madawati mpaka leo ni kitendawali eti leo mnataka muanze kuhoji tafiti.....

Nisawa na kutegemea lita 30 kwa siku kwa ng'ombe wa Mmasai anae shinda kutwa kuzurula kutafta chakula na maji.Its next to impossible.

Maabara zinazofanya kazi fresh apa SUA, 60% Zimejengwa kwa ufadhili wa watu kutoka nje. Na ni proposal za Ma professa wenyewe sio hata Wizara ya elimu.

Serikali yenu iko busy kupanga mipango ya miaka mitano ya uchaguzi.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
SUA ni Sokoine University of Agriculture sidhani kama wanextend mpaka kwenye Uranium uko good point mzee
 
Hao jamaa wanakela hatari,kila mara habari zao ni panya tu na unakuta wanalipwa mishaara kwa kazi zisizo na umuhimu wowote kwenye jamaii.
 
SUA iko vizuri sema serikali haijataka kuwekeza kwenye elimu na tafiti. Madawati mpaka leo ni kitendawali eti leo mnataka muanze kuhoji tafiti.....

Nisawa na kutegemea lita 30 kwa siku kwa ng'ombe wa Mmasai anae shinda kutwa kuzurula kutafta chakula na maji.Its next to impossible.

Maabara zinazofanya kazi fresh apa SUA, 60% Zimejengwa kwa ufadhili wa watu kutoka nje. Na ni proposal za Ma professa wenyewe sio hata Wizara ya elimu.

Serikali yenu iko busy kupanga mipango ya miaka mitano ya uchaguzi.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
Serikali ina pesa za kulipa wagonga meza, kama pesa za utafiti zipo wajuvi watwambie ni kiasi gani au ni asilimia ngapi ya GDP zimetengwa kupelekwa costech au kwenye vyuo kwa ajili ya kuwezesha tafiti, au tuendelee kutegemea wazungu waje na agenda zao za kitafiti. Naamini wazungu hawawezi kukuletea pesa ufanye utafiti wa kwenda sayari ya mars au utengeneze bomu la nyuklia, hayo wanafanya wenyewe.....wanasiasa wa hii nchi kufikiria kwamba nchi zilizopiga hatua kubwa kwenye maendeleo kiteknolojia zimewekeza sana kwenye elimu na tafiti, the type ya wanasiasa kama kibajaji na msukuma kuna kitu gani hapo unategemea.
 
Kama zipo tafiti nyingine mbona hazisikikii ?? Mimi uwa nasikia panya, panya tu
Pole.Jitahidi kusoma machapisho yao kwenye mitandao.SUA wametengeneza hadi chanjo za wanyama,wanazalisha mbegu za mazao ya aina mbalimbali ambazo zina ubora wa hali ya juu, Tafiti ktk uchakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo na mifugo,Wanyama pori,kilimobiashara,mazingira,n.k.Ishu zinazohusu Uranium nadhani mleta Uzi aliteleza kwasababu SUA ni chuo kikuu Cha Kilimo Sasa Uranium sijui itaingiaje.Aidha Mchango mdogo wa Serikali ktk kufanikisha Tafiti mbalimbali ndio kunasababisha juhudi za chuo hiki ktk tafiti za Kisayansi usionekane, maana tafiti nyingi ni ufadhili wa nje.
 
SUA hawataona huu ni ushauri,ni kweli kwa dunia ya leo kufanya utafiti wa panya sijui atambue nini,ni uzembe wa kiwango cha lami;
ningesikia wana-design sensors kwa ajili ya utambuzi wa magonjwa mbalimbali sawa,ila panya hapana;
Wewe umeshafanya utafiti kuhusu Nini??.Hivi vitu unaweza ukadhani ni vyepesi lkn si rahisi kihivyo,rasilimali pesa inahitajika Sana kufanikisha Tafiti,sasa bahati mbaya hata Serikali yenyewe haiwekezi vyakutosha ktk tafiti za Kisayansi.
 
Pole.Jitahidi kusoma machapisho yao kwenye mitandao.SUA wametengeneza hadi chanjo za wanyama,wanazalisha mbegu za mazao ya aina mbalimbali ambazo zina ubora wa hali ya juu, Tafiti ktk uchakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo na mifugo,Wanyama pori,kilimobiashara,mazingira,n.k.Ishu zinazohusu Uranium nadhani mleta Uzi aliteleza kwasababu SUA ni chuo kikuu Cha Kilimo Sasa Uranium sijui itaingiaje.Aidha Mchango mdogo wa Serikali ktk kufanikisha Tafiti mbalimbali ndio kunasababisha juhudi za chuo hiki ktk tafiti za Kisayansi usionekane, maana tafiti nyingi ni ufadhili wa nje.
Ni mwaka jana tu wametengeneza chanjo ya kuku inayokinga magonjwa matatu kwa mpigo. Ni ukombozi mkubwa kwa wafugaji wadogo.
 
Naunga mkono hoja. Ndiyo maana kina msukuma, kibajaji, kishimba, Gwajima na mamburula lukuki yamekamata podium kuongelea mambo mazito mazito ya kitalaamu wasiokuwa na uelewa nayo wao wapo tu na vipanya wao.

No wonder world ranking ya vyuo vyetu iko huko iliko kwenye maelfu kadhaa.

Mama Samia ana kazi kubwa ya kuturejesha mstarini.

Total overhaul ya system inaweza kuwa ndiyo njia ya kuchukua.
Vyote ru minashauri tukafugie wanyama wa kuliwa na ile ya dodoma rukaweke wabunge na wafanyakai wote wa umma mengine tubadilishe viwe kumbi za starehe.....list ni ndefu
 
SUA wanazingua wawatrain panya kugundua Kama wife katoka kwa mchepuko au Mr hii itakuwa biashara ya nguvu ingawa tutatembea na sumu za panya mfukoni ni kumuwahi Kama umetoka mahali.
 
Back
Top Bottom