SUA: 45% ya watanzania husaidiwa na tiba asili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
WAGANGA wa tiba Asili na Tiba Mbadala wana mchango mkubwa katika jitihada za Serikali na Wananchi katika kuendeleo kwa kaya na Taifa kwa kuhakikisha wanatoa tiba na kuboresha afya za watanzania na hivyo kuwezeesha jamii kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) upande wa Taalama Profesa. Samweli Kabote wakati akifunga maadhimisho na maonesho ya wiki ya tiba asili ya mwafrika Kanda ya Mashariki yaliyofanyika kwenye viwanja vya Soko Kuu la Chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro yaliyowakutanisha wadau wote kwenye mnyororo wa thamni ya mimea dawa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

’’Takwimu zinaonyesha kuwa tiba asili inachngia kwa kiasi cha silimia 45% katika kutoa huduma za afya kwa Watanzania na asilimia 55% ndio madawa mengine ya madukani kwahiyo asilimia hizo sio ndogo kama ambavyo watu wengi wanadhani maana naamini wengi zaidi wanaikimbilia tiba asili katika kutatua changamoto zao mbalimbali za kiafya na hivyo kupata afya ya kuwawezesha kufanya kazi za kiuchumi’´alisistiza Profesa. Kabote.

Aidha amewataka waganga wa tiba asili na tiba mbadala sasa kuendelea na juhudi za kuboresha dawa hizo kwa kushirikiana na watafiti wa SUA na Chuo cha Afya Muhimbili na taasisi zingine za kupima ubora na usajili ili zizidi kuaminika na jamii nzima bila kujali elimu ya mtu,kipato wala rangi yake na hivyo kuongeza soko na huduma zaidi kwa jamii na kujiongezea kipato.

Profesa. Kabote ametoa wito kwa waganga wa tiba asili kushirikiana na watafiti kote nchini katika kubaini miti dawa ambayo wanaona ina faida kubwa katika tiba ili ifanyiwe utafiti zaidi na kuongeza thamani ya mimea hiyo ili kupta dawa za kitanzania nzuri na zenye ubora wa hali ya juu kwa matumizi ya hapa nchini na nje ya nchi.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Shahada za juu utafiti, ushauri na uhawilishaji wa teknolojia Profesa. Hesron Karimuribo alisema Wizara ya Afya inatambua mchango mkubwa wa SUA katika jitihada za kusaidia tiba asili nchini na ndio maana wakapewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa m,aadhimisho hayo kwa kanda ya mashariki.

’’ Kama mkurugenzi mwenye dhamana ya utafiti SUA tumekuwa tukihakikisha tunafanya tafiti mbalimbali kupitia wataalamu na watfiti wa chuo chetu katika sekta ya tiba asili kwa kushirikiana na wadau hawa ili kuboresha na kuongeza thamani dawa zao na namna wanavyotoa huduma lakini pia kuhamasisha upandaji wa mimea dawa ili isiweze kutoweka kwakuwa inatumiwa sana na kuvunwa kwa wingi’’ alisema Profesa. Karimuribo.`

Ameongeza kuwa SUA imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanya tafiti za kupata dawa za kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO -19 ambapo umepata dawa mbalimbali ikiwemo dawa maarufu ya SYNADOL ambayo iantumiwa na watanzania wengi kwa sasa ndani nan je ya Mkoa wa Morogoro kutokana na ufanisi wake katika kusaidia wagonjwa hao.

Akieleza ushirikiano wa SUA na wadau wa tiba asili Mtafiti Mkuu wa Mradi wa GRILL Dkt. Faith Mabiki alisema kuwa uaizishwaji wa jukwaa la ubunifu la wadau wa bidhaa za tiba asili nchini GRILL ni moja kati ya mikakati mikubwa iliyozaa mafanikio makubwa katika kuwakutanisha wadau wote kwenye mnyororo wa thamani lakini pia kuwapa sauti ya pamoja na kubadilishana mawazo na uzoefu nchini.

’’Sisi kama watafiti wa SUA ambao tumekuwa tukifanya kazi karibu sana na wadau hawa wa tiba asili tunajivunia mabadiliko makubwa tunayoyaona sasa tunapofika kwa kila mganga wa tiba asili kwa kuona namna wanavyofungasha bidhaa zao na kutengenza dawa katika ubora wa hali ya juu tofauti na zamani mabpo walikuwa wakiwapatia wateja au wagonjwa wao magome ya miti,majani na kuweka kwenye mifuko isiyofaa kuweka dawa’’alifafanua Dkt. Mabiki.

Kwa upande wake Mratibu wa tiba asili na tiba mbadala mkoa wa Morogoro Dkt. Wille –Anne Ngalula alisema kuwa jukwaa la ubunifu la tiba asili Tanzania lililoanzishwa na SUA linaendeleza malengo na jitihada za Serikali katika swala zima la utoaji wa dawa na kuboresha afya nchini kupitia tiba asili.

’’Kwa sasa Mkoa wa Morogoro una waganga wa tiba asili waliosajiliwa na Baraza la Tiba Asili Tanzania wamefikia 1872 na tayari maduka 71 ya tiba asili yamesajili katika mkoa wa Morogoro, hii inaonyesha muamko mkubwa uliopo kwa wganga hawa katika kufuata sharia na kanuni za serikali katika utoaji wao wa huduma lakini pia muitikio wa wananchi katika kutafuta huduma zao ndio maana wanaongezeka siku hadi siku nah ii inatokana na kazi kubwa iliyofanywa na SUA pamoja na timu yetu ya mkoa na ’’´alieleza Dkt. Ngalula.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyamna vya Waganga wa Tiba Asili Tanzania Mkoa wa Morogoro (SHIVYATIATA) Ramadhani Sanze ameishukuru SUA kwa kuendelea kuwa mlezi wa waganga wa tiba asili nchini na kwa jitihada wanazifanya katika kuboresha utoaji wao wa huduma kwa wagonjwa kwani imeongeza thamani ya dawa zao lakini pia kuwajengea kuaminika na kujiamini katika utoaji wa huduma na hivyo kuwaongezea elimu na kipato.

Maadhimisho ya tiba ya wiki ya tiba asili ya Mwafrika Kanda ya Mashariki yamefanyika kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa huduma za ugani kwa waganga wa tiba asili kwenye maeneo yao ya kutolea huduma,kongamano la kisayansi la tiba asili kwa njia ya mtandao pamoja na maonesho makubwa ya kanda ya mashariki yaliyokutanisha waganga wa tiba asili na wadau wengine kwenye mnyororo wa thamani wa tiba asili kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania
 
Ni kweli kabisa.Kaka yangu kafanyiwa operation 2 za tumbo mwisho madoctor walimuambia wameshindwa.Kazi imeisha kwa kokwa la parachichi,mafuta ya kondoo na Asali.Sasa hivi Yuko Poa anadunda tu.Madoctor hawaamini.
 
Soko la dawa zetu lingekuwa juu ingekuwa hadi raha hakuna pesa ya kigeni kununua dawa ya mkoloni wa kizungu
Ilikuwaje akashindwa kujitibu na kupona kwa hizo dawa za asili mpaka akalazwa hospital zinazotumia madawa ya hao Wazungu Mabeberu?
 
Kabila wazungu kuja Africa mbona tulikuwa poa tu bila dawa zao na vita tulipigana nao tukiwa fit tu
 
Ilikuwaje akashindwa kujitibu na kupona kwa hizo dawa za asili mpaka akalazwa hospital zinazotumia madawa ya hao Wazungu Mabeberu?
Kifo kipo tu vinginevyo madaktari bingwa watumia dawa za Wazungu wangekuwa hawafi wangeishi milele
 
WAGANGA wa tiba Asili na Tiba Mbadala wana mchango mkubwa katika jitihada za Serikali na Wananchi katika kuendeleo kwa kaya na Taifa kwa kuhakikisha wanatoa tiba na kuboresha afya za watanzania na hivyo kuwezeesha jamii kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) upande wa Taalama Profesa. Samweli Kabote wakati akifunga maadhimisho na maonesho ya wiki ya tiba asili ya mwafrika Kanda ya Mashariki yaliyofanyika kwenye viwanja vya Soko Kuu la Chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro yaliyowakutanisha wadau wote kwenye mnyororo wa thamni ya mimea dawa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

’’Takwimu zinaonyesha kuwa tiba asili inachngia kwa kiasi cha silimia 45% katika kutoa huduma za afya kwa Watanzania na asilimia 55% ndio madawa mengine ya madukani kwahiyo asilimia hizo sio ndogo kama ambavyo watu wengi wanadhani maana naamini wengi zaidi wanaikimbilia tiba asili katika kutatua changamoto zao mbalimbali za kiafya na hivyo kupata afya ya kuwawezesha kufanya kazi za kiuchumi’´alisistiza Profesa. Kabote.

Aidha amewataka waganga wa tiba asili na tiba mbadala sasa kuendelea na juhudi za kuboresha dawa hizo kwa kushirikiana na watafiti wa SUA na Chuo cha Afya Muhimbili na taasisi zingine za kupima ubora na usajili ili zizidi kuaminika na jamii nzima bila kujali elimu ya mtu,kipato wala rangi yake na hivyo kuongeza soko na huduma zaidi kwa jamii na kujiongezea kipato.

Profesa. Kabote ametoa wito kwa waganga wa tiba asili kushirikiana na watafiti kote nchini katika kubaini miti dawa ambayo wanaona ina faida kubwa katika tiba ili ifanyiwe utafiti zaidi na kuongeza thamani ya mimea hiyo ili kupta dawa za kitanzania nzuri na zenye ubora wa hali ya juu kwa matumizi ya hapa nchini na nje ya nchi.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Shahada za juu utafiti, ushauri na uhawilishaji wa teknolojia Profesa. Hesron Karimuribo alisema Wizara ya Afya inatambua mchango mkubwa wa SUA katika jitihada za kusaidia tiba asili nchini na ndio maana wakapewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa m,aadhimisho hayo kwa kanda ya mashariki.

’’ Kama mkurugenzi mwenye dhamana ya utafiti SUA tumekuwa tukihakikisha tunafanya tafiti mbalimbali kupitia wataalamu na watfiti wa chuo chetu katika sekta ya tiba asili kwa kushirikiana na wadau hawa ili kuboresha na kuongeza thamani dawa zao na namna wanavyotoa huduma lakini pia kuhamasisha upandaji wa mimea dawa ili isiweze kutoweka kwakuwa inatumiwa sana na kuvunwa kwa wingi’’ alisema Profesa. Karimuribo.`

Ameongeza kuwa SUA imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanya tafiti za kupata dawa za kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO -19 ambapo umepata dawa mbalimbali ikiwemo dawa maarufu ya SYNADOL ambayo iantumiwa na watanzania wengi kwa sasa ndani nan je ya Mkoa wa Morogoro kutokana na ufanisi wake katika kusaidia wagonjwa hao.

Akieleza ushirikiano wa SUA na wadau wa tiba asili Mtafiti Mkuu wa Mradi wa GRILL Dkt. Faith Mabiki alisema kuwa uaizishwaji wa jukwaa la ubunifu la wadau wa bidhaa za tiba asili nchini GRILL ni moja kati ya mikakati mikubwa iliyozaa mafanikio makubwa katika kuwakutanisha wadau wote kwenye mnyororo wa thamani lakini pia kuwapa sauti ya pamoja na kubadilishana mawazo na uzoefu nchini.

’’Sisi kama watafiti wa SUA ambao tumekuwa tukifanya kazi karibu sana na wadau hawa wa tiba asili tunajivunia mabadiliko makubwa tunayoyaona sasa tunapofika kwa kila mganga wa tiba asili kwa kuona namna wanavyofungasha bidhaa zao na kutengenza dawa katika ubora wa hali ya juu tofauti na zamani mabpo walikuwa wakiwapatia wateja au wagonjwa wao magome ya miti,majani na kuweka kwenye mifuko isiyofaa kuweka dawa’’alifafanua Dkt. Mabiki.

Kwa upande wake Mratibu wa tiba asili na tiba mbadala mkoa wa Morogoro Dkt. Wille –Anne Ngalula alisema kuwa jukwaa la ubunifu la tiba asili Tanzania lililoanzishwa na SUA linaendeleza malengo na jitihada za Serikali katika swala zima la utoaji wa dawa na kuboresha afya nchini kupitia tiba asili.

’’Kwa sasa Mkoa wa Morogoro una waganga wa tiba asili waliosajiliwa na Baraza la Tiba Asili Tanzania wamefikia 1872 na tayari maduka 71 ya tiba asili yamesajili katika mkoa wa Morogoro, hii inaonyesha muamko mkubwa uliopo kwa wganga hawa katika kufuata sharia na kanuni za serikali katika utoaji wao wa huduma lakini pia muitikio wa wananchi katika kutafuta huduma zao ndio maana wanaongezeka siku hadi siku nah ii inatokana na kazi kubwa iliyofanywa na SUA pamoja na timu yetu ya mkoa na ’’´alieleza Dkt. Ngalula.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyamna vya Waganga wa Tiba Asili Tanzania Mkoa wa Morogoro (SHIVYATIATA) Ramadhani Sanze ameishukuru SUA kwa kuendelea kuwa mlezi wa waganga wa tiba asili nchini na kwa jitihada wanazifanya katika kuboresha utoaji wao wa huduma kwa wagonjwa kwani imeongeza thamani ya dawa zao lakini pia kuwajengea kuaminika na kujiamini katika utoaji wa huduma na hivyo kuwaongezea elimu na kipato.

Maadhimisho ya tiba ya wiki ya tiba asili ya Mwafrika Kanda ya Mashariki yamefanyika kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa huduma za ugani kwa waganga wa tiba asili kwenye maeneo yao ya kutolea huduma,kongamano la kisayansi la tiba asili kwa njia ya mtandao pamoja na maonesho makubwa ya kanda ya mashariki yaliyokutanisha waganga wa tiba asili na wadau wengine kwenye mnyororo wa thamani wa tiba asili kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania
Hilo ni kweli tupu....

Ila haliondoi UKWELI kuwa SAYANSI ni bora zaidi.....
 
Ni kwel kabisa watafika tumetoka kabisa kwenye utamadun wetu
 
Back
Top Bottom