Style ya vyama vya siasa kufungua matawi yao uk na usa

T 2015 CDM

Member
Sep 6, 2012
39
10
Ndugu zangu nimekuwa nikishangazwa kidogo na siasa zinavoendelea nchini mwetu hasa kati ya vyama viwili vikubwa. Kitu hiki kidogo kimekuwa kikinitatiza. Ivi ni kwa nini vyama hivi vinafungua matawi US na UK tu tena kwa ushindani na kuonyeshana na hawafungui matawi yao kwenye nchi kama Rwanda, Burundi, Msumbiji, Sudani, Urusi, Italy, Iran, Saudi Arabia au Dubai? Na kwa nini zaidi Washington DC na si New York au state zingine tukichukulia mfano wa US?

Je haya matawi yana umuhimu upi kwa ustawi wa vyama vyenyewe na demokrasia nchini mwetu maana hata idadi ya wanachama wanofutwa huko ni kituko. Kuna nini jamani? Hebu tujuzane kwa mapana hapa.


Na je hayo matawi yaliyo UK na US wanashiriki vipi katika michakato ya kuchagua viongozi wa chama wa ngazi za kitaita kama NEC n.k

"Just food for thought"
:frusty:

LIWALO NA LIWE
:peace:
 
Asilimia kubwa ya sisi wakazi wa nchi hizo tajwa kwanza hata hatuhusiki na upuuzi huo...Wengi wanauza sura na soon fagio likipita mbona ukimya utatawala......HAINA TIJA KATIKA KUJENGA NCHI
 
Amini usiamini wanajua Future ya Tanzania ipo mikononi mwa Watanzania wa Diaspora. Hawa Watanzania hawajui rushwa, hawategemei serikali na wanasikilizwa zaidi na wathamini wa Tanzania kuliko hata viongozi wa serikali. Vilevile ndiyo wako mbele sana kwenye technologia mfano hapa JF hivyo wanajua hawa jamaa wakijiunga wanaweza kuwa na nguvu kuliko hapa Chama Cha Siasa.
 
hilo ni suala nyeti, tatizo sis malimbukeni sana na kujipendekeza kwanin nasema hiv nadhan kuna watanzania wengi south africa mbona hatuskii wakifungua matawi je huo si upendeleo? upande mwingine ni kweli wanadispola hao ni muhim sana kwa maendeleo ya nchi na si vema kuwaacha nyuma ktk kujenga taifa letu mana nyumbani ni nyumbani. huo ndio mtazamo wangu.
 
Back
Top Bottom