Stuck in the middle dont know what to -mawazo yako vitasaidia dada huyu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stuck in the middle dont know what to -mawazo yako vitasaidia dada huyu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by noella, Jan 28, 2012.

 1. n

  noella Senior Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Habari ya weekend wakuu,natumai mu wazima.

  Ni matukio ya maisha yake ya mapenzi. Yanaenda namna hii. Tutahitaji mawazo yenu yenye hekima na busara ukishaisoma.
  Ni shosti tumeshibana sana,ana boyfriend wa muda mrefu kidogo wako pamoja kwenye shida na raha, ingawa mahusiano kawaida sio straight line ila ya kwao maugomvi yanachukua 90 percent katika maisha yao ya kila siku. Shosti ana wivu na jamaa ana wivu.

  Jamaa anadiriki kuingia kwenye simu ya shosti na kujibishana na wanaomtokea bi dada. Shosti nae kutwa kutafuta kesi kuhusu jamaa ili mradi shughuli. Kuachana kwa wiki mbili na kurudiana kwao ni kitu cha kawaida. Mara ya mwisho ni wiki iliyopita lakini after two days wakarudiana,jamaa aligoma kwenda kazini na kuanza kunywa pombe na kuvuta bangi kisa bi dada kamuacha.

  Ni watu wazima wawili mwanaume yuko kwenye late thirties na bi dada early thirties. Wameahidiana kuoana mwaka huu ingawa hakujatolewa posa mahari wala pete hakuna. Mdada anatokewa na watu kedekede now more than ever nas wote wanaclaim kumpenda na wanataka awe mke. By the way sikusema kuwa wawili hawa wana mtoto mmoja.

  Na hawa wanaomtokea wanadai kumpenda mtoto na kumtunza. Mdada ndo muda wake umefika anataka kuolewa ila amechanganyikiwa kwa kuwa hajui aendelee na jamaa yake waendelee maugomvi forever amen au achague anayemeet vigezo kati ya wanaojileta.ingawa anasema anampenda jamaa ila kachoshwa na malumbano ya kila siku yasiyo na kichwa wala mguu. Je ungekuwa wewe ungefanyaje?
   
 2. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Pole kwa yaliyomkuta huyo mwenzio. Mtazamo wangu, ndoa haihitaji kuikimbilia kwa sababu ya umri wa kuolewa kufika. Ni hatari sana kuingia kwenye ndoa kwa kutumia kigezo cha namna hii.
  Mahusiano mengi na ndoa nyingi huvunjika kwa sababu ya watu wanaoingia kwenye ndoa kwa sababu kama umri kufika, tamaa ya pesa, msukumo wa ndugu, msukumo wa marafiki nk.

  Ulikuingia kwenye ndoa yakupasa kuhakikisha kuwa yule unayefunga naye ndoa ni mtu ambaye umependa kwa dhati na siyo vinginevyo. Migogoro mingine huwa inavumilika na kutatulika.

  Ushauri wangu, aolewe na mtu anayempenda kutoka ndani ya moyo wake kuepuka baadaye kuja kutoka nje ya ndoa na kuwa na migogoro isiyo na lazima.

  HorsePower
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama kweli amechoka maisha anayoishi na huyo jamaa basi amuache. Na sio amuache na kukimbilia kwa mwingine bali amuache, apumzike, kisha aangalie ustaarabu mwingine. Asije akakurupuka na kuolewa out of desperation alafu akajikuta kwenye mambo yale yale aliyoyakimbia.

  Alafu huyo jamaa nae needs to grow up. Late thirties anaenda kulewa na kuvuta bangi kisa kaachwa? What is he. . . A teen? Hiyo ndio ile style ya kutaka huruma iokoe mahusiano. .huyo dada akomae tu aachane nae kama yamemshinda. Huyo mzee will get over it. . . EVENTUALLY.
   
 4. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Huwezi kufanya kitu kilekile kila mara halafu ukategemea matokeo tofauti.Msaada kwa wote ni kuachana ama kumshauri huyo rafikiyo avunje uhusiano halafu atulie atapata muda wa kutafakari ili aone kama jamaa ata-change or not na asikimbilie mahusiano mapya,wakati mwingine ni vizuri kuyatizama matatizo yako mwenyewe ili ufanye maamuzi sahihi na ujifunze.
  Ushauri kidogo the rest unatumia kichwa na ubongo ulopewa bure.
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  ni mabangi yao yanawasumbua.
  Unachezea nyasi, zinafanya maamuzi magumu hata ambapo haitakiwi.

  Labda amshauri aanza kula majani yake, hutumika kama mchicha vinginevyo aachane naye fasta hakuna kitu hapo.
   
 6. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Duh!Hao wanahitaji ushauri mkubwa,hawataweza kuishi na yoyote hata kama wakiachana,hawajiamini kwa kiwango kikubwa sana!
   
Loading...