Stroke inaweza kumtokea mtu yeyote na ni hatari

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Tupo wanne tumetokea kuelewana na kuwa marafiki wakubwa. Rafiki yetu mmoja amefanikiwa kujenga nyumba nzuri tu ya ghorofa, anaishi na mume wake na mabinti zao wawili.

Weekend moja alitulika katika sherehe ya mtoto, hatukua wengi sana, kwakua sherehe ilikua ni ya watoto, yeye na mume wake waliamua kuwa na watu wao wa karibu. Tulikula na kucheka na kuagana.

Wiki iliyofuatia rafiki yetu aliymtupigia simu, mume wake amepata stroke! Ilimtokea akiwa anaoga asubuhi, alikimbizwa Hospital. Alilazwa kwa wiki mbili baada ya hapo alirudi nyumbani. Ilibidi awekewe kitanda sebuleni hakuweza kupanda ngazi za kwenda chumba kwake.

Aliendelea na mama cheza kwa mwezi mmoja. Baada ya hapo alitafuta mama cheza wa private. Alifanya mazoezi kwa miezi mitatu. Sasa hivi amerudi katika hali ya kawaida. Ila amebadili mfumo wake mzima wa maisha. Ana kimbia kila siku, hali nyama tena na pombe ameacha.
 
Huu Uzi umenishitua Sana aisee naogopa sana hii kitu ngoja nirudie kufanya mazoezi maana ilikuwa ni daily basis yangu kukimbia umbali wa km 25 ingawa Nina 49yrs now sijui nini kimenikumba nina miezi 6 sijafanya mazoezi ahsante sana dada yangu kwa Uzi huu

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
kuna ndugu yangu alipatwa na hilo tatizo...amepona kwa asilimia 89 tu...mkono wa kushoto sehemu ya vidole imegoma kuachia...nisaidie kama unajua chochote cha kufanya
Mazoezi ya mara kwa mara na vyakula hasa mbogamboga na matunda kwa wingi. Mara nyingi body weight ama umri mkubwa husababisha mifupa ya uti wa mgongo kukakamaa na kushikamana baada ya kupoteza ute na soft bones, ambapo husababisha kugandamiza na kubana neva za fahamu zinazopitia huko kutoka kwenye vidole hadi ubongoni.
 
Huu Uzi umenishitua Sana aisee naogopa sana hii kitu ngoja nirudie kufanya mazoezi maana ilikuwa ni daily basis yangu kukimbia umbali wa km 25 ingawa Nina 49yrs now sijui nini kimenikumba nina miezi 6 sijafanya mazoezi ahsante sana dada yangu kwa Uzi huu

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Mtigopesa tafadhali. Halafu usisahau ya kutumia na ya kutolea :)
 
Mazoezi ya mara kwa mara na vyakula hasa mbogamboga na matunda kwa wingi. Mara nyingi body weight ama umri mkubwa husababisha mifupa ya uti wa mgongo kukakamaa na kushikamana baada ya kupoteza ute na soft bones, ambapo husababisha kugandamiza na kubana neva za fahamu zinazopitia huko kutoka kwenye vidole hadi ubongoni.
mazoezi ya aina gani sasa kamanda
 
Kuna mama fulani alikuwa almost 96% out of shape!!! Aliugua sana kiasi cha kufa. Amesaidiwa na mazoezi ya kawaida tu ya kila siku: kutembea, kuinuka na kuketi, kufanya shughuli rahisi kama anazozimudu,, nk. Kifupi, kutokaa idle.
asante kwa ushauri...nae mgonjwa wangu ni mwanamke
 
Tupo wanne tumetokes kuelewana na kuwa marafiki wakubwa. Rafiki yetu mmoja amefanikiwa kujenga nyumba nzuri tu ya ghorofa, anaishi na mume wake na mabinti zao wawili...
Mazoezi na aina ya vyakula ndo jawabu.

Punguza nyama nyekundu.

Punguza pombe.

Pendelea kula punje za vitunguu swaumu mara lwa mara.

Fanya mazoezi(cardio) angalau 30mins kila siku.
 
Tupo wanne tumetokes kuelewana na kuwa marafiki wakubwa. Rafiki yetu mmoja amefanikiwa kujenga nyumba nzuri tu ya ghorofa, anaishi na mume wake na mabinti zao wawili...

Ana bahati sana huyo bwana. Angekuwa kwenye nchi za kina mfalme juha mbona nyungu, mikaratusi, michai chai, na hata kikombe cha babu Loliondo vingemhusu?

Bila shaka hata kwa mheshimiwa Mshana Jr kwa ajili ya kusafisha nyota angeshazuru.

Makwetu wa stroke kama hivyo huwa wametupiwa majini. Wa Corona hupelekwa kutibiwa Loliondo, kwa babu asiyekuwa na barakoa wala kuhitaji PPE. Yakimkuta tunasema Mungu alimpangia kufa hivyo.

Ujinga mzigo. Katika rundo la wajinga sote hatuwezi kufuata mkumbo kama misukule, hata kama "chief architect" ni jiwe mwenyewe mapumzikoni Chatto.

Ndiyo maana hachoki mtu hapa! Chanjo kwanza:

Mapambano yana maana pale tu tunapokuwa na afya zetu.

Aluta Continua!
 
Ndy umeandika ugoro gani huu??

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app

Kwani Mataga hukupiga chafya?

Na bado!
 
Tupo wanne tumetokes kuelewana na kuwa marafiki wakubwa. Rafiki yetu mmoja amefanikiwa kujenga nyumba nzuri tu ya ghorofa, anaishi na mume wake na mabinti zao wawili...
Ngoja niende mazoezi (jogging) nitarudi kucomment baadae.
 
Stroke mara nyingi usababishwa na high blood pressure so jitahidini kucontrol presha za miili yenu kupitia vyakula ,mazoezi na kupunguza mawazo.ikikupiga upande wa kulia ni mbaya sana unaeza jikuta pua huwezi kuzungumza
 
Back
Top Bottom