BOMBAY
JF-Expert Member
- Apr 16, 2014
- 4,682
- 3,392
Habari wana JF,
Natumai mko poa, na mishemishe za kulikimbiza tonge la kila siku zinaendelea vizuri.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,
Nikiwa ninamaanisha kuwa suala la kuchelewa kuolewa si la wanawake tu bali hata kwa wanaume tunaojitambua pia tunalo janga la kuchelewa kuoa, suala ambalo wengi wetu tunapofikia umri flani huwa linatuumiza vichwa kila kukicha.
Kumekuwa na mijadala mingi humu ihusuyo kuchelewa kufunga ndoa ambayo kwa namna moja au nyingine ni wanawake pekee ndio wamekuwa wakihusishwa na kadhia hii hatimae wanaonekana kuwa na stress za hitaji la ndoa bila mafanikio.
Binafsi napingana na dhana hii kwa kusema kuwa suala hili la stress za ndoa si kwa KE pekee bali hata kwa ME licha ya kutofautiana kwa namna moja au nyingine kati yetu.
Sitaki kuamini kuwa kama kuna asiependa kuitwa "Mume wangu"katika uhalisia wenyewe na yule ampendae kwa dhati wakiwa ndani ya ndoa.
Nina mifano mingi ya wanaume wengi nami nikiwemo ambao wameshachoshwa na maisha ya ubachelor, yaani ni wahitaji wa kweli wa ndoa lakini mpaka sasa bado hawajafanikiwa kuingia katika taasisi hii nyeti kutokana na sababu mbalimbali ambazo zimekuwa ni kikwazo katika kufanikisha jambo hili.
Sababu kuu ambayo kwakiasi kikubwa nimeisikia ikilalamikiwa sana na vijana wengi wa kiume ni UGUMU WA MAISHA ikifuatiwa na HOFU YA MAUMIVU YA MAPENZI ambavyo chimbuko lake ni USALITI, KERO NA CHANGAMOTO MBALIMBALI zinazojitokeza katika ndoa ambavyo vimekuwa ni gumzo kwa wanandoa kila kukicha.
Ugumu wa maisha ndio sababu kubwa inayochangia vijana wengi kujiweka mbali na suala la ndoa na, wengi tunajifariji tu lakini ukweli utabaki palepale.
Nina rafiki yangu hivi juzi kati amepatwa na kijihoma cha siku nne akiwa kitanda hajiwezi, anasema umuhimu wa kuwa na mke ndo ameuona kwa jinsi alivyokuwa mpweke, nia ya kuoa anayo lakini kipato ndo kinachompa stress.
Bila kuwachosha ningependa kuwasilisha mada hii kwenu wana Bodi ili kama mtakubaliana na mtazamo wangu kwa pa1 tuungane kuipinga dhana hii yakuhusisha wanawake pekee katika suala hili ijapokuwa wao ni wahanga zaidi kuliko sisi.
Naomba kuwasilisha.
AHSANTENI