Street smartness, Career, Ujasiriamali, Mahusiano, Risk taking

shaurimbaya

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
1,915
2,329
habari wadau..


kuna dogo mmoja jirani ameniacha hoi sana style yake ya maisha..

ni mzuri darasan na hata kazini... ila hakai kazini zaidi ya 3 yrs hata iweje..

toka anaanza kazi 2011 kampuni moja kubwa alifanya vizuri tu na baada ya 3 yrs akaacha na kuhamia kwingine.. na ku draw nssf yake yote na kuinvest kwenye bajaj na kiwanja chanika. na akaendelea na kazi mpya.. ameendesha endesha biashara ya bajaj kwa changamoto na mafanikio kiasi..

ila mwenyewe hakuwa na stress as anakwambia hadaiwi na mtu anawekeza hela yake halali ya mafao uzeeni so hawez iacha nssf serikali waitumbue mwisho akizeeka wamsumbue kumlipa au wampe bila kuangalia inflation maana mtu aliyechangia nssf miaka ya 90 shilingi 100 hata leo akiacha kazi anapewa 100 ile ile..

kwa mwajiri wake mpya tena amekaa 2 yrs napo ameacha kazi na kwenda ku draw nssf yake na kuwekeza kwenye maji kule aliponunua kiwanja na kununua bajaj nyingine mpya ambayo anaiendesha mwenyewe wakati anatafuta kazi nyingine.. na hana wasi wasi anakwambia ataipata tu soon..

kuliko kuaicha hela yake nssf ni bora awe anaiwahi na hawezi kuiwah kama hajaacha kazi.maana nssf ni wajanja.

so mpaka sasa ana kiwanja, bajaj, kirikuu na mradi wa maji huku hadaiwi na bank hata shilingi 1.. so anasaka tena ajira mpya..

kwenye mahusiano ameoa banker mmoja ambaye anaponda sana maisha ya jamaa yake but ameshamzoea..

dogo tukimuuliza why ana risk ku loose his job bila kupata kazi nyingine..

anakwambia hii njia kwake inamsaidia sana kuwa free kutafuta kazi nzuri kwa uhuru, na pia anajiepusha na riba za ajabu ajabu za bank zetu ukikopa milion 10 unalipa milion 20... na pia mind inapata experience kubwa sana anaporudi mtaani tena jobless tofauti na akifanya kazi hadi astaafu bila kupata street experience.. na anawahi kuchukua chake mapema maana mifuko hii haitabiriki unaweza sikia imefirisika na hela zako kama wastaafu wazee wa east africa community

je anachofanya dogo ni sawa?
 
Back
Top Bottom