'Street codes' za kukusaidia uishi vizuri na watu mtaani kwako katika mji wowote Tanzania

Namba moja naitumia sana kitaa kwa vile mimi ni mtu wa salamu na utani wa hapa na pale, ila kuna nyumba jirani na ninapoishi ina watu wa ajabu (mostly wanawake)
Nilianza kuwasalimia kila ninapopita hapo asubuhi ila wakawa wanaitikia kwa taabu sana yaani kinyonge kama hawataki vile... nikaendelea kuwasoma pasipo kujua tatizo ni nini!
Mara ya mwisho nikasalimia (walikuwa wanawake watatu) kibarazani, wote wakakaa kimya kama vile hawajasikia salamu yangu.
Kuanzia siku hiyo nikajiapiza kutowasalimia tena.. yaani mpaka kesho napita kama siwaoni vile.
Hujawakomoa, salimia mara 1, akiitikia kwa unyonge acha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Vipi kuhusu kwenda kujitambulisha kwa wale wapenda shiriki yaan wabobezi katika kada ya uchawi ,wanga na ulozi waliopo mtaani kwangu maana hayo yote nimekwisha kuyafanya lakini walozi na wachaw Bado wanaendelea kuniletea sintofaham kubwa sana hapa mtaani kwangu kwa mtogole.
hili la kwenda kujitambulisha kwa wazee magwiji wa mtaani kwako nalo lina umuhimu wake.
 
Kujenga mazoea na mhuni uko sawa japo utegemee yote ,

Niliibiwa kiti mmoja akasaidia tukakipata bila kuumizana nikasema hapa fresh, mwisho wa siku huyuhuyu akaiba kuku akanaimbia mshkaji wangu nipoze chochote kuku wetu mzee kasema niuze nipate nauli ya kwenda kijijin kusalimia
chupuchupu nile pingu uzuri busara za mwenye kuku zilisaidia
ni muhimu kuchukua tahadhari zote wakati unaanzisha urafiki na vijana wahuni wa mtaa. uwe ni urafiki wa kimaslahi.
 
Kujenga mazoea na mhuni uko sawa japo utegemee yote ,

Niliibiwa kiti mmoja akasaidia tukakipata bila kuumizana nikasema hapa fresh, mwisho wa siku huyuhuyu akaiba kuku akanaimbia mshkaji wangu nipoze chochote kuku wetu mzee kasema niuze nipate nauli ya kwenda kijijin kusalimia
chupuchupu nile pingu uzuri busara za mwenye kuku zilisaidia
pole sana ugobha.
 
Ukikaa Uswahilini, ili uwe salama, ni lazima uji-attach na vibaka wa mtaani, kamwe hautaibiwa. Mfano, ukiwapita kijiweni unawapa salaam, unawachia hata fegi, siku moja moja.
 
Back
Top Bottom