Strategy ya Corona ya Rais Samia ni ipi?

Mzee2000

JF-Expert Member
Aug 7, 2009
527
221
Wakati tukiona wimbi la tatu likianza nchi za jirani, Raisi wetu ana mpango gani kuhusu korona?

Mbona bado takwimu hazijaanza kutolewa? Je, huko mikoani kuna vipimo?

Je, hospitali zote hasa mikoani zimetayarishwa pamoja na vitendea kazi?

Je, vyama vya madaktari vinasemaje?

Sent from my SM-A505FN using JamiiForums mobile app
 
Kwa wale mnaoipenda na kuiwaza/kuiogopa sana Corona nawashauri muhamie Uganda mkakae Lockdown, au mjifungie majumbani. Hizo wave zitaenda mpaka wave ya 9 au 10, solution ni kuendelea na shughuli zako tu. Kama afya yako mgogoro kaa kwako jifungie Ila msitake kila mtu awe muoga wa mafua aina ya Corona.
 
Mbna mmeng'ang'ana na Korona Sana aisee, kila sku Korona Korona , e bhana eeh hatuna Korona Sisi , na hatuna hela ya kununua chanjo full stop ...!! Misaada tunachukua kama kawa
Yani hawa jamaa wanaboa sana. Sisi hatuna Corona, lakini wao wameng'ang'ana kila siku Corona, Corona, sijui wanaombea na sisi tupate Corona?! Mambo mengine yanatia mpaka kichefuchefu, usipokuwa na kiasi unaweza kujikuta umemtukana mtu.
 
mlidai mtu anayeitambua corona.

mama akawapa kucha mkune upele,
mnataka roho yake sasa naona.
 
Yani hawa jamaa wanaboa sana. Sisi hatuna Corona, lakini wao wameng'ang'ana kila siku Corona, Corona, sijui wanaombea na sisi tupate Corona?! Mambo mengine yanatia mpaka kichefuchefu, usipokuwa na kiasi unaweza kujikuta umemtukana mtu.
Wewe umeenea nchi nzima kujua hatuna Uviko 19?
 
Mi ninachoshukuru ni approach ya kutoujali sana huu ugonjwa. Maana ulileta hofu kubwa. Na hofu ikasambaa kila mahali. Matokeo ya hofu huwa ni mabaya, kwani inaleta upungufu wa kinga mwilini, na hivyo kuugua magonjwa kirahisi, na hatimaye kupoteza maisha. Ushauri ni kuendelea na maisha binafsi ya kujilinda.
  • Epuka misongamano
  • La sivyo tumia barakoa
  • Penda kunawa, ama la tembea na "sanitaiza" unapotoka nyumbani
Hayo matatu yanatosha kabisa kukukinga
 
huu ugonjwa hadi sasa haueleweki hata hizo Pfizer na modema wamesema zinaaribu figo na mapafu . kwa hiyo ni kizungumkuti
Data za leo hizi. Chanjo ni salama kabisa 🤭

3d04f956ba6c8c2a.png
 
Vaa barakoa, jifungie ndani, pata chanjo.

Strategy gani unaitaka ulimwengu wa utandawazi? Unataka atufungie wote ndani? Au unataka aamrishe kila mtu avae barakoa?

We anza usiulize....
 
Kupima usd 100 kapime hujakatazwa. Mbona mnapenda kila kitu kufanyiwa?

Kama vipi nenda Uganda.

Wenzako EURO2020 wako wamejaa uwanjani hata barakoa hawana.

Hujazuiwa kujifungia, kuvaa Barakoa unataka Rais nayo akuambie.

Dogoyangikulu
 
Back
Top Bottom