Strategy wapinzani wanayotakiwa kuitumia..Tena sasa hivi yaani kuanzia sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Strategy wapinzani wanayotakiwa kuitumia..Tena sasa hivi yaani kuanzia sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KadaMpinzani, Oct 18, 2009.

 1. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  (1) Wasimu-attack Kikwete moja kwa moja ktk mashambulizi yao wanayoyafanya wakiwa katika majukwaa ya siasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi. Kwa nini ? Kumshambulia Kikwete moja kwa moja katika kushindwa kwake, kutasaidiwa na "sweeper" wake, hawa sana sana wanakuwaga wajumbe wa NEC wakiongozwa na Makamba, Chiligati, Msekwa and the team.

  (2) Wanachotakiwa kufanya sasa ni kuelezea failures za CCM, nini CCM imeshindwa kufanya, na iliahidi nini na kati ya hayo yaliyoahidiwa, yatajwe yale ambayo hayakuweza kufanywa. Baada ya hapo, wapinzani wasisitize kwamba CCM haina jipya litakalofanya na iwapo kuna jipya lingefanyika sasa hivi. Kile kinachoonekana katika serikali ya CCM sasa hivi ndicho hicho hicho kitakachofanyika katika awamu nyingine IWAPO serikali watachaguliwa, hili walisisitize kwa sana!

  Waendelee kuwapaka hawa wanaopaka rangi sera mbovu za ccm kwa kuwalaghai wanachi, na iwapo hii itafanya kazi basi kumuangusha Kikwete itakuwa rahisi, maana kwa mtazamo wangu ni kwamba hawa "sweepers" wanaomsafishia njia Kikwete wakati wa kampeni hufanya kazi kubwa kuliko afanyavyo Kikwete mwenyewe, maana njia inakuwa nyeupe baada ya hao jamaa kumsafishia njia. Kwa kifupi wakichafuliwa hawa tu, jamaa juu kazi anayo!

  Nyingine mtaongeza..................
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Can't blv ths is frm you......... wht happened?????
   
 3. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  oya, mm mchango wa kununua helicopter sina bana, sasa kama sina hata mawazo nikose ? hahaaa. Huyu ni yule yule ambaye hukudhani angeandika haya............................
  ........................
  .......................................................
  ..........................................................
  .................JADILI.................
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Haha haha haha!!!!!!!!!! poa mkuu bravo kwa mawazo mazuri!!!!!
   
 5. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Kuna mijitu ilikuwa mifisadi, kama Paulo wa kwenye Biblia, halafu ikamwongekea Mungu, na kuwa raia wema na wanaowajibika. Lakini hii haiwezi kutokea kwako, wala kwa mifisadi mingine iliyolundikana huko CCM.
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kada hapo nilipo highlight ndipo wanapotakiwa kutilia Mkazo, vile vile ni Muhimu wakatafuta Njia nzuri ya Kuwabana hao wanaojiita Wapiganaji kwani JK atawatumia 2010 mark my word. Sakata la Umeme ni Bonge la Opportunity
   
 7. A

  Audax JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kuongelea fact ni muhimu.vyama vingi wao hawana katiba,katiba inayotumika kwa sasa ni ya chama tawala japo ndo inatamkika kuwa ya nchi.naamini hata vyama vingi wakipewa madaraka wembe utakuwa uleule tu bila ufanisi wowote.kinachotakiwa kufanyika ni mabadiliko ya dhati kwa viongozi tulionao ili kuleta maendeleo.ukiwa kwenye nchi za ulaya,huwezi kukuta watu wanazurula,watu wanafanya kazi kwa bidii hata kamani ya mshahara mdogo.Maendeleo hayaji kwa kutegemea serikali tu,bali ni hata kwa kila mtu kuwajibika katika nafasi aliyonayo.
   
 8. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #8
  Oct 18, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Wakati serikali ya awamu ya 4 imeanza huu ndio ulikuwa mkakati. Kwa kuhakikisha kuwa tunadeal na Lowasa kwani tuliamini ndio nguzo ya utendaji wa Kikwete. Tukamaliza kazi baada ya miaka miwili na ushee hivi. Nadhani tuligubikwa na ushindi huo kiasi cha kusahau kwenda hatua ya pili - Ainisha failures na kwamba tatizo ni CCM na hawana jipya. Mbaya zaidi tumeacha ngoma inachezwa na wana CCM wenyewe tukiamini ni allies!

  Asante kwa kutukumbusha kaka!
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kila chama kina Katiba yake, CCM ina yake, CHADEMA ina yake, CUF halikadhalika, vile vile kuna katiba ya Nchi ambayo siyo hati miliki ya Chama chochote.

  Na hayo Mabadiliko unayoyazungumzia sijui ni yapi na Unataka yafanyike vipi, na nani afanye mabadiliko hayo.

  Halafu Mkubwa ni kosa kuvizungumzia Vyama vingi kama Kapu moja, hautakuwa Fair
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kuna siku kada alinieleza sirini kwamba yeye si mwana CCM ila ni muumini wa Mwalimu na mwaminifu kwa Katiba ya Tanzania na si ya CCM. Kada akasema huwa ana leta jokes hapa mie sikumwamini hadi leo alivyo onyesha ukweli wa maneno yale . Kada endelea bwana watu huwa wana ongoka na si kuokoka .So wacha tujadili . Mwisho wa siku point yao hii tangia nikujue maishani mwako na uandishi hapa kwa mara ya kwanza umesema kitu .
   
 11. M

  Msharika JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Zitto, braval, take it in action, hatua ya kwanza mlifanya vizuri sana, sasa hii ya pili hata miezi sita inatosha tu, wafungueni wananchi macho.
   
 12. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  I didnt know you also believe in kuchafua. Tanzania haiitaji kuchafua viongozi walioko madarakani ndipo ipate maendeleo, ili kuing'oa CCM win the people by impressing them through you excellent deeds, walking your talk, and presenting better arguements
   
 13. M

  Masatu JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Vipi Chopa ya mabua ishaanza kuruka?
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  strategy iwe kuonyesha failures hata kule walikofanyia kazi e.g ujenzi wa mashule (maana CCM watatumia hili sana tu kwenye kampeni zao..........tuwaonyeshe kuwa ujenzi ule wa mashule hauna tija......kwa mfano:

  1. bajeti ya elimu imekuwa ikishuka mwaka hadi mwaka....hivyo kuzorotesha mikakati endelevu ya elimu nchini i.e Uhaba wa Waalimu, uhaba wa vifaa vya elimu.........

  2. Mishahara/posho za walimu

  Mbali na elimu pia kuna suala la Afya......hapa CCM imefeli miserably

  Miundombinu (i.e barabara & associated features, reli, bandari)

  Sasa ni wakati wa Wapinzani kuwashawishi wananchi kuwa wao watafanya kwa hayo waliyoshindwa CCM.

  ....Nilifurahi niliposoma sehemu Mh Zitto akimjibu mwana JF mmoja kuwa Nyumba zote za serikali zitarudi serikalini (kama wao watapewa usukani) na infrastructure zoote ambazo CCM wamezipora toka mikononni mwa wananchi waliochangishwa............vitu/habari kama hizo inabidi ndio viwe vinatokea kwenye vyombo vya habari (TV, magazeti na Redioni)............
   
 15. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  He he heee! Kuishiwa ni kuishiwa tu.
   
 16. N

  Ngoshakugema New Member

  #16
  Oct 18, 2009
  Joined: Oct 17, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapinnzani mnatakiwa kutoa elimu ya uraia huko vijijini ili wananchi wajue haki zao na na namna ya kuzidai. Acheni kukimbilia mjini kwenye TV na Magazeti tu. Huku watu wengi wasomi na wenye kuelewa mambo hawapigi kura kwani ni kupoteza muda tu sanasana tutaenda kupiga kura mikoani kwetu. Mfano wabunge wengi wa Dar si halali na wamechaguliwa na watu wachache waliopewa pilau na kanga na wengine bia. Watu makini Dar hawapigi kura.
   
 17. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Ni lazima tukumbuke kwamba, hakuna kipindi ambacho upinzani katika historia ya Tanzania imeweza kutengeneza historia kama katika kipindi hiki. Haijawahi kutokea Tz'nia waziri mkuu akijiuzulu kwa sababu ya kashfa, mawaziri wakipelekwa mahakamani na kushtakiwa kwa tuhuma n.k. Kwa kifupi, wapinzani have a clear shot in winning the next election.

  Kwa sababu tunafahamu kwamba "wapinzani" wanadhani wanaweza kuingia ikulu uchaguzi ujao, kinachonishangaza ni kwamba KUDHANIA kwao huko kuko kwa wao wenyewe TU kama viongozi KWA MAANA KWAMBA wale wanaoweza kuwaingiza ikulu ( WAPIGA KURA ) wapo wapo tu, hawajawa energized enough kuweza kudhani KWELI wanaweza kuingiza mgombea wao ikulu ama kunaweza kuwa na mabadiriko makubwa.

  Pia ni lazima tufahamu kwamba, wapinzani kuingia ikulu itakuwa ni kitendo cha kihistoria, kwa sababu chama tawala kilitoa rais wa kwanza ambaye tunamchukulia kama baba wa taifa, na watu wakampenda, na chama chake kikatawala zaidi ya miaka 40, lakini ndani ya hiyo miaka 40, zaidi ya miaka 15 imetawaliwa na viongozi walioongoza taifa kwa kujinufaisha wao kwa njia zisizo sahihi. Kwa sababu hiyo, ndio kulipeleka wapinzani kuweza kumwondoa madarakani aliyekuwa waziri mkuu, na kama waliweza kufanya hivyo, kwa nini washindwe kumuondoa rais madarakani ? Kila sehemu wanayopita ccm, inasema imeshatekeleza ilani ya chama chake, na kwamba maendeleo yapo, sasa wapinzani na nyinyi kila kona mtakayopita, kila jukwaa mtakalopanda waambie kwamba mmesikia ccm imesema imewapelekea maendeleo, je madai hayo ni kweli ? na kama si kweli, waambie wananchi hao hawana haja ya kuwapigia kura ccm.

  Pia "wapinzani" msisahau kuwahimiza wananchi kuchagua viongozi WANAOWAJUA. Kwa maana kumekuwa na tabia ya viongozi kutoka pande moja na kwenda pande nyingine kugombea aidha ubunge, au uenyekiti n.k sehemu nyingine mbali na makazi yao ( wamekuwa kama mamiss, wanakaa dar wanaenda kugombea umiss shinyanga ). Watahadharini sana na hii tabia, maana kufanya hivyo ni kuchagua viongozi wasiowajua, na kuna uwezekano mkubwa kuchagua kiongozi fisadi iwapo humjui vizuri/kiundani huyo utakayempigia kura!

  Kupiga kura ni muhimu, na kila kura itahesabika, na kwa kura zao wanaweza kufanya mabadiriko makubwa, lakini hiyo haitakuwa rahisi hadi pale watakapobadiri mawazo yao hususan wakati wa kupiga kura, kwa hili lazima muwahimize!

  Narudia tena, hali ya Tanzania sio nzuri ( kwa wananchi wake ) na wao wenyewe ( wananchi ) wanalifahamu hilo, na ili kubadirisha na kuweza kuleta afadhali katika maisha yao, ni lazima waitumie nafasi hii ambayo katika historia ya Tanzania, wapinzani wapo karibu katika kushinda uchaguzi mkuu zaidi kulinganisha na wakati wowote! Na sababu hizo, ndizo zilizoweza kuwafikisha viongozi mbele ya sheria, kwa hiyo wahimizeni kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura!

  Pia lazima muwe creative wapinzani, maana mbali na "ufisadi", sioni kama kuna lingine ambalo kwa kweli linaweza kuwavutia wapiga kura. Ebu angalieni majukwaa yenu ya siasa, hayapendezi kabisa, yaani hata kidogo! Creativity inahitajika na sina haja ya kusema fanyeni hivi na vile, fikirieni wenyewe kwa hilo!

  Nina mengi, lkn kwa sasa acha niandike haya tu!
   
Loading...