Straika Mpya Simba Aanza Makeke Aifungia Simba Ikishinda 3-1

vyankende

New Member
Dec 6, 2017
1
0
d463242a7a89046dfff0cf0fed6c32e9.jpg

Straika Mpya Kutoka Zambia, Jonas Sehukawa ameifungia klabu ya Simba goli la Pili katika ushindi wa goli 3-1 ilioupata Simba dhidi ya klabu ya KMC jioni ya leo.

Sehukawa ameweza kuifungia timu hiyo goli ambalo huenda likampatia tiketi ya moja kwa moja kusaini mkataba wa kuitumikia simba wakati dirisha la usajili likielekea kufungwa.
 
Yaani kufunga goli moja ndio kigezo cha kusaini Simba sc, tena na timu dhaifu kama hiyo aliyocheza nayo.

Lamsingi inabidi kujua historia yake ya Soka, Ligi ya VPL ni ngumu, Ilimshinda Blagnoni ambaye alikuwa anafunga ktk kila mechi ya majaribio.

Kama pesa ipo Simba isajiri wachezaji wenye uwezo hasa kama anatoka nje ya nchi.

Acheni mambo ya ubabaishaji
 
d463242a7a89046dfff0cf0fed6c32e9.jpg

Straika Mpya Kutoka Zambia, Jonas Sehukawa ameifungia klabu ya Simba goli la Pili katika ushindi wa goli 3-1 ilioupata Simba dhidi ya klabu ya KMC jioni ya leo.

Sehukawa ameweza kuifungia timu hiyo goli ambalo huenda likampatia tiketi ya moja kwa moja kusaini mkataba wa kuitumikia simba wakati dirisha la usajili likielekea kufungwa.
Kwa taarifa tu Huyo bwana jonas sakuwaha ni mchezaji mzee na alishawahi kuja hapa bongo kucheza akiwa na club ya el marreikh ya sudan katika kagame cup ya 2011 na inaonesha ana miaka 34 sa hv sasa kiafrika mchezaji kusema umri wake halali kama mnavyojua wito wangu simba iachane na mchezaji huyu kwani kwa hatua simba inapoelekea kuwa ya kisasa kusajili wachezaji wanotafuta pension si wakati wake huu hata kama tunataka wanaotafuta pension tujitahidi kuleta wale waliovuma katika soka ili tuweze kuvutia wachezaji toka mataifa mablimbali kuja kucheza ligi ya bongo mfano si mbaya kumleta emmanuel adeabayor,ariside bance, na si hawa waliocheza katika low profile na sasa wanatafuta pension
 
Hivi Pape Ndaw mechi za majaribio hakufunga??
Nimemkumbuka sana huyu foward matata toka mitaa ya msimbazi nasikia mnataka kumrudisha tena
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom