Story za kwenye DALADALA Special Thread.

Yo Yo

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,217
1,702
Na mahsusi kwa story mbali mbali tunazokutana nazo kwenye dala dala.Naanza na hii.

Oya, Shika Mchuma!

Kondakta: Kaa mkao wa pesa.
Abiria: Si tumetosha? Twende basi!
Kondakta: Tunafanya kazi kwa hesabu mama mdogo.
Abiria: Hebu twendeni. Kuna watu huko mbele.
Kondakta: Kama una haraka ungeenda toka juzi. Tuko kazini hapa.
Mpiga debe: Wenye haraka wanaonyesha. Wenye haraka huchukua teksi.
Abiria: Tukichukua teksi mtakula wapi. Hebu acheni dharau. Twendeni, gari si imejaa?
Mpiga debe: Jamani, mchuma haujai. Inayojaa ni ndoo ya maji. Haya, Kariakoo, Kariakoo... gari nyeupe hii.

Kondakta: Manzese wapo?
Abiria: Tupooooo...
Kondakta (akijifanya kuwa hakusikia): Manzese hakuna sio?
Abiria (kwa hamaki): Shushaaaaa...Tupo!
Kondakta (huku akijizuia kucheka): Babu endesha, Manzese hakuna.
Abiria: He, we konda vipi? Tumesema tupo!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom