Story yenye funzo: Tayari ameolewa

Ni jambo la kheri ikiwa ameolewa mwenye zimungu awajaalie kila lililo lenye kheri ili aepuke zinaa.

Nachoona hapa ni kuwa unajaribu kulaumu na una kinyongo kuolewa kwake bila kujuwa ulipwaya katika nafasi yako aliyokupa, umesema kuwa dada yake tu ndiyo alikuwa akijuwa akijuwa anakuja kwako.

Je? Unaona ni sawa kuwa na mchumba huku miaka miwili kwao hawakujuwi wewe, kwenu hawamjuwi yeye hapa nazungumzia wazazi sio marafiki.

Toka 2016,upo nae ikiwa yeye ni mwanamke wa kiislamu ulitaka afanye nini anapokuwa anapatwa hisia.... tena unalaumu eti miaka 22 bado mdogo?

Mwisho.... Nampongeza kwa uamuzi aliochukua wa kuolewa na kusitiriwa.
Hebu some tena uelewe. Wapi nimesema kuwa ni mdogo? Na wala sijamlaumu. Mimi nimeacha mambo yawe kamayalivyo kwa urahisi kabisa. Nimepitia mengi sana najua ninachokifanya. Unadhani hata ningemtambulisha home ndo ingekuwa solution?
Kuna mengi sikuyaweka hapo. No problem so far.
 
Kosa kubwa zaidi ulilofanya ni kutomtafuna.

Binti hana kosa, kosa liko kwako, huwezi kua na mwanamke kwenye mahusiano miaka 2 hujamtafuna, huo ni uzwazwa.

Kama mwenyekiti wa chama cha wanaume nakuwekea red color, naangalia mwenendo wako, hali hii ikiendelea unahamishiwa upande mwingine.
 
Ndo ujue kwamba Bongo kwetu Wanawake huwa hawa fall in love na Wanaume bali huwa na maslahi tu, kwa akifupi hakukupenda, chukua kama fundisho na ukumbuke hilo maisha yako yote jamii yetu hatulelewi na kufundishwa maana ya ku.fall in love hayo ni mambo ya kigeni tuliletewa tu,

Mwanamke ni swala la muda ukifika na Mwanaume gani yupo tayari kwa wakati huo na huyo ndiyo atakayeolewa naye, jifunze, hapo Mwanamke wa Kibongo ha fall in love hata siku moja bali ana maslahi tu!
Jamani Barbarosa, mbona mimi nilifall in love kwako na hakuna maslahi zaid niyapatayo. Burudani yangu ni mapenzi yangu kwako
 
Ndo ujue kwamba Bongo kwetu Wanawake huwa hawa fall in love na Wanaume bali huwa na maslahi tu, kwa akifupi hakukupenda, chukua kama fundisho na ukumbuke hilo maisha yako yote jamii yetu hatulelewi na kufundishwa maana ya ku.fall in love hayo ni mambo ya kigeni tuliletewa tu,

Mwanamke ni swala la muda ukifika na Mwanaume gani yupo tayari kwa wakati huo na huyo ndiyo atakayeolewa naye, jifunze, hapo Mwanamke wa Kibongo ha fall in love hata siku moja bali ana maslahi tu!
Ni kweli
 
Always mashukuru mungu kwa kila jambo kwa sababu atakukwamisha kwa kitu kimoja ili akupe kilicho bora zaidi
Glory to God
 
Habari za Jumapili wakuu.

Niende kwenye mada. Kama kichwa cha thread kinavyosema, ni kweli yule bint ameolewa. Let me take you to the story behind. Ni kisa kinachonihusu mimi mwenyewe. Mimi ni mwanaume, mwezi ujao wa May nitatimiza miaka 30.

Ilikua ni Jumamosi, 22 October, 2016; nilipomwona kwa mara ya kwanza huyu bint. Nilisafiri Ijumaa tarehe 21 lakini nilifika jioni sana jijini Tanga kumfuata huyu bint nikitokea Dar es Salaam. Mwenyeji wangu, rafiki wa kiume, classmate wangu wa chuo akanipokea na kunipeleka mahali ambapo nitalala. Sikuweza kulala kwake sababu ya uhaba wa mahali anapoishi. Akanipeleka lodge nikalipia hapo. Lengo la safari yangu lilikua kukutana na bint ambaye nilitambulishwa kwake na rafiki yangu mwingine kuwa anafaa kuwa mke. Tukiwasiliana kwa siku kadhaa kama marafiki wa kawaida tu. Makazi yangu yalikua jijini Mwanza ila nilikuja Dar likizo basi nikatumia muda huo kwenda Tanga kumuona mhusika ili tuweze kuongea japo mawili matatu tukiwa ana kwa ana nami ikiwa kama utalii kufika Tanga kwa mara ya kwanza.

Jumamosi ya tarehe 22 tukaonana na bint, mwenyeji wangu pamoja na yule bint wakashauri twende Raskazone. Tukaenda beach kule. Jamaa akatuacha kidogo tukizungumza mawili matatu. Alionekana mwoga na mwenye aibu sana yule bint. Naomba nimuite jina la Maryam ingawa si jina lake halisi. Mariam alikuwa anaongea na mimi huku amegeukia upande wa pili. Ilinichukua sekunde chache kugundua kuwa ni msichana asiye na mambo mengi na anaonekana ni mgeni wa vitu vingi sana. Nilishangaa kwa umri wake wa miaka 21 wakati huo na amesoma hadi chuo (certificate) na mji aliopo wa Pwani, ni kitu cha nadra sana. Nilihisi ana act. Nilifanya juhudi ya fasta fasta anizoee ili mambo yaende. She was very anxious. Tukatambulishana vizuri na kuelezana historia za maisha yetu kwa undani. Mwisho nikamuuliza, unataka kuolewa, ukiwa kama mke matarajio yako kwa mume au kwenye ndoa ni nini? Hakujibu hili swali. Baadaye tukarudi mjini, nikachukua bus nikarudi Dar na kesho yake nikapaa na Precision back to Mwanza nilikokuwa natakiwa kureport kazini Jumatatu ya tarehe 24.

Mawasiliano yaliendelea na Maryam alionekana kakolea kweli kweli. Kila mara alisisitiza nimuoe. Hii nioe ilizidi mno mpaka nikawa napata wasi wasi huyu anataka ndoa kweli au kuna kitu anatafuta. Mwaka 2016 ukaisha na 2017 ikaanza yeye ajenda yake ikiwa ni hiyo hiyo. Nilimueleza mpango wangu wote. Kwamba mwaka huo wa 2017 ninataka kuacha kazi nijiajiri. Nikishajiajiri I'll need atleast six months nikae sawa. Then naweza kuoa. Alikubaliana nami. Mwezi June 2017 niliacha kazi, nikarudi Dar, nikaanza michakato yangu. Dar ndipo nlipokulia na familia yangu yote ipo hapa. Nilikomaa mpaka mwaka ukaisha 2017. Hali yangu haikuwa nzuri sana. Alitoka Tanga akaja Dar na akawa anaishi hapa. Nilimtimizia mahitaji yake kwa kadri alivyotaka. Nilimpa muda wangu mwingi, mara nyingi mimi ndio nilikua nataka tuonane maana yeye mpaka ajipange kutunga safari na halijui jiji vizuri. Kwa hiyo tulikua tunaonana mara kwa mara. Sikuwahi kumgusa hata mara 1, nilifanya hivyo makusudi ili ajiongeze. Ikiwa kweli mi namtaka kwa ajili ya ndoa basi ataona matendo yangu.

Mwaka 2018 ukaanza bado hali haijabalance vizuri. Kwa sababu mwezangu alikua anapush mno nimuoe. Nikasema ikifika March mwishoni ntaanza mchakato afe kipa, afe beki.

Mungu si Athumani wala sio John. Mwisho wa March kama nilivyopanga mambo yakawa yanaenda vizuri. Lakini nilianza kuona mabadiliko ya mwendendo wake. Kuna siku akaja home kwangu, tukiwa tunaongea nikambana sana akafunguka huku analia. Nilimwambia nataka kupeleka kwao posa, akashtuka na kuniuliza nikipeleka posa ntakaa muda gani ndipo nioe.? Nikamwambia sitakawia. Machozi yanamtoka. Eti nimsamehe, amefanya uamuzi wa kijinga. Na anajutia.

Ndipo nikataka kujua undani wa kilio chake. Akafunguka kuwa, baada ya kuona mimi nakawia kumuoa alishauriwa na rafiki zake anipige chini atafute mtu amuoe. Na pressure ya mama zake (familia) nao huko kijijini kuwa yuko mjini huku muda mrefu kwa nini haolewi (maana tangu amemaliza chuo mwaka 2015 yuko tu home Tanga na hapa Dar kwa ndugu). Rafiki zake walimshauri kuna ustaadhi anafanya kuunganisha watu walio single waowane kupitia group ya whatsapp. Naye akajiunga huko. Ustaadhi alipomuona akata kumuoa mke wa pili (mathna) akakataa. Ndipo akapatiwa jamaa mwingine mwalimu wa sekondari. Wakakutanishwa....jamaa akamind mzigo. Ustaadhi akapeleka posa mwenyewe. Mahari ikalipwa. Na mpaka siku tunaongea nami harusi ilishapangwa tarehe 22 mwezi April. Haya yote yamefanyika ndani ya mwezi 1.

Nilisikitika. Nikanywa maji ya baridi kwanza. Nikamuangalia akijiliza. Nikamhoji mambo mawili matatu nikamwacha akaenda. Ila nikamwambia ntafanya kitu hiyo ndoa haitafungwa. Kesho yake hakupokea simu yangu akidai anaogopa nitambwatukia. Hivyo anataka tuchat tu.

Kesho yake hiyo akaniambia Meraki mahari imeanza kugawanywa hadi kijijini imetumwa. Na mama yake anakuja Dar tarh 15 mwezi April. Hajui afanye nini. Aanaogopa mi nikilianzisha atatia aibu kwa familia na ukoo wao sababu wale watu, ustaadh na muowaji aliwaambia mwenyewe wapeleke posa. Na siku hiyo ndo ustaadhi aliwaruhusu waanze kuwasiliana kwa simu. All the way long hawakuwahi kuwasiliana. I was in a shock. Nikakumbuka wimbo wa Kassim Mganga, harusi. Usijeitaka harusi kwa pupa. Yaani inaonekana alitaka tu kuolewa. Nikajiwazia, bint wa miaka 22 anaona anachelewa? Ila poa ndio maisha na kila mtu anayadefine atakavyo.

Niseme tu mimi ni sikuwahi kufahamika kwa nduguze hapa Dar japo yeye nilimtambulisha kwa baadhi ya watu wangu. Kiufupi sikufahamika kwao lakini dadake alikua anajua kuwa huwa anakuja kwangu.
Na pia mimi ni mtu wa imani kidogo. So nikamwamchia Mungu na kushukuru. Nikaswali rakaa 2 sunnati shukr kumshukuru Mungu kwa yote kisha nikafunga kitabu chake moyoni mwangu. Niseme ukweli hili suala halijaniumiza sana ila limeniongezea funzo kuwa usiwaamini sana wanawake hata yule usiyemdhania. Niliwahi kuumizwa na mapenzi huko nyuma nikaapa sitaki tena mapenzi yanitese namna ile. Nadhani hili limenisaidia kuvuka hiki kiunzi.

Nikashukuru Mungu nikasema Mungu amenipa muda wa kufocus na biashara zangu. Na mwezi wote huu wa April umekuwa busy mno na kama vile imekuwa take off yangu maana deal zimekuwa poa sana mpaka nakosa muda wa kufanya mambo mengine. I just move on. Ndio kwanza nina miaka 30 next month. Now I will marry when I want.

Story ni kama funzo kwa wengine. Sorry kwa uzi mrefu.

Jumapili njema.
Hakuna wa kulaumiwa,
Subiri subiri utakuta mwana si wako,
Na ww Mipango ya maisha hayakwenda vile ulipanga...
Muombee maisha mema ya ndoa, ww tafuta na kuza mwingine, this time na ww usirembe sana
 
Ungemtia mimba tu,hivyo angeenda na mimba yako! Ndoa ingevunjika ndani ya mwaka na angerudi kwako kiulaini!
Hapana, huu si utaratibu mzuri. Nafahamu sana hili lakini haukuwa mpango wangu
 
Mmmmmh
 
Similar Discussions

22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom