story ya kweli yenye uzuni na masikitiko ndani yake!..

dodoso33

Member
Oct 9, 2012
38
11
((((((STORY FUPI YENYE
MAFUNZO )))))))
Nilipoingia katika mahusiano naye
nilimuamini, nikampa kila kitu
nilichoweza. Nakumbuka enzi zile
nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na
kumpelekea kwao. Akanenepa!!
Penzi letu likawa huru alipoanza
maisha yake mwenyewe. Sikuwa
najua lolote kuhusu mapenzi.
Alinifundisha. Nikaegemeza maisha yangu yote kwake.
Akanifanya nikawa mtumwa wa
ngono kila nikienda chumbani
kwake.
Kama haikutosha sasa akaanza
kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume
wangu mtarajiwa, kwa nini
nikatae? Nilimkubalia kila kitu.
Alinilazimisha ngono hata
nilipokuwa katika siku zangu.
Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini
sikutaka kumuudhi huyo
niliyeamini kuwa ni mume wangu.
Nilipenda tututmie kinga lakini
aliipinga sana. Nikapata mimba ya
kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa
nyumbani nikafanya alivyotaka.
Kwa mara ya kwanza nikatyoa
mimba.
Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa
ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa tutaanza
kutumia kinga. Lakini hapana
haikuwa hivyo. Aliendelea
kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu
wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya
anavyojua.
Pombe kidogo na nyingine kidogo.
Nikazoea lakini nikawa nawahi
kulewa.
Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya
lililonifanya niandike haya kwako.
Akaniingilia kinyume na maumbile.
Alinilawiti!!
Nilishindwa kumshtaki popote.
Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume
asiyejulikana hata kwa wazazi.
Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea
eti hataki nipate mimba tena,
hivyo hiyo ni mbinu mbadala.
Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu.
Miaka ikapita, ule urembo wangu
niliozoea kuuona katika kioo
ukatoweka, simu za mara kwa
mara kutoka kwake zikatoweka,
akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati
huo nilikuwa nasoma chuo.
Pesa ya mkopo ikitoka
ananitafuta na tunakuwa marafiki
tena. Anasema ananipenda na
atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile.
Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha
nabaki mwenyewe katika msoto.
Sasa akaanza kubadilisha
wasichana waziwazi. Ningesema
nini mimi? Ninajua alishindwa kusema neno
moja tu. Tuachane!!
Nilijua tayari ameniacha!!!
Afya yangu ikadolola sana,
nikalazimika kwenda kupima
hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa
ushauri nikautumia.
Siku zikasonga nikampata
mwanaume mwingine. Huyu
alikuwa ananijali sana. Nikaanza
kumsahau yule aliyenitenda. Nilipomaliza chuo akajitambulisha
nyumbani na alitaka kunioa.
Akanio kweli. Maisha yakaanza.
Mwaka wa kwanza, mwaka wa
pili na hadi wa tatu. Sikuwa
nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu
sana, hakuwa hi kunilaumu. Lakini
niliumizwa na mawifi. Nikaamua
kwenda hospitali.
Nikaambiwa kizazi change
kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya
kinyume na maumbile
yamenivuruga kabisa.
Nililia sana huku nikimkumbuka
yule aliyeuleta uchungu huu
kwangu. Dunia haikuwa mahali pangu
sahihi.
Nimekuandikia barua hii mdogo
wangu. Uisome mwenyewe!!
Lakini uwasimulie wengi baada ya
kifo changu. Uwasimulie bila kuchoka
wasichana wa kileo
wanaodanganyika na kufanya
mambo magumu kuwaridhisha
wapenzi wao. Waambie watakufa
kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliz a usijisikie vibaya
maana hata mimi nilikuwa
siwasikilizi watu waliponambia
lolote kuhusu yule mume
mdanganyifu.
Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa u
mwandishi. Japo kwa sasa u
mtoto mdogo najua utaipata
nafasi siku moja ya kuwafikishia
wasichana hawa. Usilie kwa sababu nitakufa. Lia
kwasababu mwanaume
mwenzako AMENITENDA HIVI!!!
TAFADHARI TAFAKARI
 
Shairi linanikumbusha kundi la Talent pale Iringa (spw) walikua na igizo lao linaitwa ZULIA. Kwenye zulia kuna watakaoingia na viatu, kuna watakaovua viatu waingie na soksi pia kutakuwepo watakaovua viatu na soksi waingie peku na kuna watembea peku pia watakaoingia na kukanyaga zulia....zulia lilivumilia haya yote kuilinda sakafu ambayo mwisho wa siku haikua na shukrani. Zulia likaonekana halifai likaondolewa na sakafu ikabakia. Huyu dada katumiwa kama zulia kakanyagwa na wenye viatu, wenye soksi na watembea peku kuilinda sakafu (mume mtarajiwa) mwisho wa siku katupwa kwakua anachafua hadhi ya sakafu.
Lakini mie huwa nawalaumu sana dada zangu wanaokubali kutoa mimba tena ukubwani (wengine wakiwa vyuoni au kwenye ajira tayari) kisa eti analinda heshima yake...heshima gani unalinda huku ukiua kiumbe kisicho na hatia? Heshima gani unaitaka kwa kujiharibu kizazi kwa kutoa mimba kienyeji?
Pole sana na nahongera kwa hadithi yenye mafunzo...kwa ridhaa yako naomba kesho nikawasomee wanafunzi wangu wa kidato cha sita kwani haya uliyoyasema nimekua nikiyasisitiza sana darasani.
 
good work,nimeipenda kibavu,hiyo philosophy ya zulia nayo inavutia,nitaitumia siku moja kwa watoto,kuna watu hapa JF mnafaa sana kukaa pamoja mtengeneze kitabu cha hadithi mbalimbali,kitumiwe kwenye shule za msingi(class 6&7),na sekondari,vitasaidia sana hasa wewe dodoso33 Mtambuzi na Mzee Mwanakijiji,to help the young generation,seriously.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom