Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Inaendelea


Siku zilivyokua sinasonga nilianza kuzoea mazingira ya Arusha, kama kawaida yangu kupiga misele ndo ilikua jadi yangu nahisi mitaa ya Arusha ambayo cjafika ni michache mpk loliondo nilitimba huko ndani ndani Arashi kote huko nilifika.


Pale nilipokua nimepanga tulikua wapangaji kumi, mmoja tu ndo alikua anaishi na familia yake, tuliyobaki sisi ni ma Bachelor...kuna mpangaj mmoja alikua ni binti wa kinyaturu cku moja alimpokea rafiki ake wakike ni Muiraq ( ndo hao hao wambulu tu )..huyo rafiki ake alikua ni mrembo kweli mweupe alafu mwembamba.


Huyo muiraq nilijikuta tu nimeanza nae mahusiano ( cjui hata yalianzaje hayo mahusiano )....kuna siku alinambia niende nae kwao ( karatu ) akawasalimie ndugu zake alafu turud cku hyo hyo.


Sijui kwanini nilikubali kilahisi vile....kazini niliomba ka likizo ka siku 4 ( kwa mwaka likizo jumla ziko 28 )....basi nilipewa kishingo upande hyo likizo na karani.Jumapili mapema tu tulikua kisongo tukapanda gari ( hice ) mpk karatu...tulipokelewa vizur na mzee wake, Mama yake alikwisha fariki tokw zamani ko alikua anaish na Mzee wake na ndugu zake wengine.


Siku nilikula vizur sana ( kwenye kupika nawa appreciate sana ) tulivyomaliza kula tukapiga story na hyo familia waliniuliza me mwenyej wap nikawaambia natokea Mara Tarime ( nilidanganya wilaya )...jioni ilifika tukashindwa kurud Matevesi gar zilikosa ko ilibid nilale pale ( ukweni ).

Kesho yake mapema tu tuliamua kusepa zetu,.....huyo Manzi niliona amechukua mabegi yake ya nguo me nikajua labda ameamua kuchukua tu kwenda nayo kwa huyo mnyaturu.Sikumuuliza kwanini achukue yale mabeg yake maana niliona hayanihusu.

Ile tumefika pale tunapoishi badala aingize yale mabegi chumba anachokaa.Yeye akayaingiza mageton kwangu....nilimuuliza "kwani loyce hayupo"....alijibu yupo nikamwambia mbn mabeg tena kwangu akasema kwanzia muda ule yeye ni mke wangu maana mpaka kwao nilishaenda na wananijua.

Pozi liliniisha kwa kweli mke tena usawa ule jamani,nilimwambia mbn hakunambia na mbona ni mapema hvyo asee me kuwa mume wake.Alijibu ndo ishakua tena alianza kupiga na usafi kabisa.


Hii ndoa nayo ilkua ni ya kibabe sana nilifikiria huyu mtu nitamtorokaje maana hizo pigo za kuishi na mwanamke nilikua ctaki kabisa...yani cku hyo nililala nae bila kumgusa kabisa.

Kwa vile likizo yangu ilibakisha siku mbili niliamua kwenda kwa wale washkaji zangu walionipokea kuwaambia hilo tukio...Walicheka sana wakanambia kuwa nilifanya makosa makubwa kwenda kwao na huyo manzi walinambia ni kawaida ya wasichana wa kule kujilengesha kwa wanaume ili waolewe hata bila mahari.


Niliamua kuishi nae hivyo hivyo nilikubaliana na hari.Uzur wake alkua hakai home alkua anafanya kazi mgahawa mmoja hivi uko kisongo karibu na sokoni kwa hyo alikua akitoka asubui anarud saa moja usiku.

Ila huyu manzi nilimuona ana msaada sana, me hua ni mvivu kwenye vikaz vya home ko alikua akivifanya yeye.


Nilikua nikipata mchepuko nilikua nampeleka kwa wale jamaa walio nipokea maana funguo za mlango wao nilkua najua wanapozitunzia.


Huyu mke nilikuona naona yupo serious na mimi alikua ana nambia kuwa anataka niombe likizo hata ya wiki mbili ili twende nae musoma akawaone Wazazi wangu.Nilimwambia labda mwezi December ndo nitachukua lkizo ili niende nae musoma.Lakin yeye alikataa akataka nimuongezee nauli alafu ni mdairekti ( direct ) aende mwenyewe.

Mwez September katikati Mama angu alikua anarud kwake yeye mwenyew lakin wagonjwa mmoja alienda dodoma na mwingine alienda Mwanza ( wa kike ndo yupo dodoma )...Mama nilimwambia kuwa nimepata mchumba, kabla hajarud musoma nili mwambie huyo wife aende morombo akawasalimie.

Mama anamkubali sana huyo mwanamke cjui kisa ni mweupe na kipindi cha nyuma ndo nimepewa taarifa za kuja Arusha Mama alinambia kuwa nikiona sana nimeshindwa kujizuia na wanawake nitafute mmoja niweke ndani kama mke.Ko nadhan alifurahi kwa hilo.


Mama aliondoka nae kwenda musoma yupo mpaka leo hii.Kipindi hayupo nilijinafas kuna msajili laini ( sim card's ) wa voda na yeye ni pisi kali ya kimbulu niliitafuna kimasihara tu, ila sio mageton kwangu ni kwa washkaji.

Kiwandani nilifanya kazi kwanzia mwez wa 07 mwez wa 11...


Bado na kama visa viwili au vitatu ni hitimishe Uzi wangu



Nitarejea
Kwahyo huyo manzi wa karatu, yuko msoma hadi Leo mkuu??
 
Inaendelea


Nikiwa bado nipo Arusha sema huku ckufanya matukio sana, ila ndo sehemu ambayo nilijifunza kupiga keyboard kikweli kweli.

Nilikua nawadanganya washkaji zangu me ndo mpiga kinanda kanisan kwetu ( na walivyokua wakiniona napiga kwenye simu ) walikua wana niamini kingese, sasa cku hyo jumamosi kwa vile me nilikua off nilikuwa nipo magetoni nimelala kufidia usingizi niliokua naukosa.

Mlango uligongwa kufungua nilimkuta ni mshkaji wangu mmoja hv yupo na mkaka mmoja na wadada wawili.

Tulisalimiana kisha yule mshikaj wangu akanambia kuwa kawaleta wale watu kuwa wanashida na mimi.mmoja wa wale wageni alijitambulisha kuwani fulani wametoka kanisa la wasabato ( silitaji ) walikua wanaomba niwe mwalimu wao wa kwaya, nilivyosikia hvyo nikawauliza wamejuaje kuwa mimi ni msabato....yule mshikaji wangu ndo akanambia kuwa kawambia ( maana c me nilimdanganya kumbe alichukulia ni ukweli ). Niliwaambia hilo sio shida alafu nikawaambia kuwa niko busy na kazi za kiwanda ko nahisi itakua ngumu.

Walisema sio shida me ni kupanga tu rratiba yangu fresh. Bora hata wangesema niwe mwalimu tu walitaka niwapigie beats nyimbo zao walikua nazo kama tatu niliwaambia kinanda sina huyo jamaa akasema kitapatikana ( duh....) aisee nilikuibali tu kuwa nitawapigia bure kabisa beats na ilikua beat nianze kupiga cku ya jumanne nikiwa off ( Off yangu ilikua jumamosi na jumanne ).


Walivyosepa nilimlaumu mshkaji wangu kwanini kawaleta wale watu, niliamua kumwambia ukweli me cjui kupiga kinanda nilikua nawadanganya....sikua na namna maji niliyavulia nguo mwenyewe.


Siku hyo niliweka bundle la kutosha nikawa YouTube tu naangalia zile tutorials how to play piano for the beginner, how to create beat yani cku hyo nili such mambo mengi mpk nikaanza kujua chord za f# ( sharp ) niliona ndo rahisi kwangu alafu nikabahatisha na namna ya kutengeneza beat ko nilijifunza kwa bidii sana kwa hizo cku sana nilikua nakomalia nijue chord kwanza uzur idea nilikua nayo ko haikua shida sana kuielewa.


Kesho yake jumapili nilienda kanisa moja la walokole nia yangu tu nipate kinanda.Ila ckufanikiwa kupata maana napo cku hyo nilikua naingia shift ya usiku ko kipindi natoka kiwandani jumatatu asubui nilipita kwenye kanisa moja nikamuona jamaa mmoja anapiga kinanda ( kanisa lile ni la nje )....nilimfuata pale alipo nikamwomba samahan kuwa anielekeze jinsi wanavyo creat beat nae akasema hajui anajifunza.

Kinanda kilikua ni Yamaha psr 2100 vile ambavyo vinatumia diskette ( sio flash ) ko nilichofanya nilichukua simu nikaingia YouTube faster.

YouTube inasaidia sana tena sana kila kitu inacho yani hadi raha.Nilianza kujarbu mdogo mdogo mpk nikajikuta naanza kuweza weza, nilikomaa cku hyo mpk ikafika midaa ya saa 7 mchana ndo nikaenda magetoni kujiandaa tena na shift ya usiku ili kesho ndo niwe off.

Jumanne ilifika na nilitoka cku hyo saa mbili asubui maana tulicheleweshwa kupewa kadi ( bila kadi na barakoa huingii kiwandani ) nilivyofika tu magetoni nakutana na yule msabato ananisubir nje ya geto langu....niliona huyi jamaa vipi ni mwambie tu ukweli kuwa me cjui kitu aah...niliacha nilisema ngoja tu nikaaibike tu kihivyo hivyo.

Nilimkaribisha ndani akasema hakai me nijiandae tu ili niondoke nae akanipeleke kwenye kinanda nianze kazi.Mimi hata kama kitu cjui nitakwambia najua na ninasimamia huo ukweli kuwa najua kumbe cjui.

Tuliondoka nae mpk sehemu moja hivi Ngara ya chini ( ilikua sio mbali sana na pale napoishi ) tulifika kwenye nyumba flani hivi nzur tu tukaingia mpk ndani sebuleni nikakutana kinanda kipo mbele yangu kinanisubir .

Nilitaman umeme ukatike lile zoez lisifanyike lakin wapi...ilibidi tu nikakae kwenye kinanda tu ckua na ujanja.Uzur ni kwamba yule jamaa alinambia niwasubir wale wadada waje ili wame wanaimba alafu me napiga beat.

Nilitumia muda huo kuingia tena YouTube kukumbushia niliyojifunza cku zilizopita.

Nilianza kukipiga kinanda kwa uwoga hapo bado wale wadada walikua hawajaja na kinanda kilikua ni Yamaha psr 650 kilikua kinatumia flash na MID cable, styles zake nilizipenda drums,jazz, rap na kadhalka.

Walipofika wadada niliwaambia kabla hatujanza kazi tuombe kwanza tena me ndo niliomba na niliomba ombi la huruma sana.Nadhan Mungu alisikia ombi langu.

Nyimbo ya kwanza ilkua haina kona kona nyingi ( Minor ) ko ilikua nyepesi kidogo nilivyojua tu hatua zake kwenye chord ya f# ( sharp ) basi nilienda kwenye function kuanza kutengeneza beat

Kazi ilkua ni kupiga intro na zile lead zake duh..mwanzo mgumu ila hyo beat niliibahatisha mpk wao waliipenda niliweka break za kutosha ( me hua napenda sana beat zangu kuwa na break ).Wimbo uliofuata nilishindwa maana ulikua una minor za kutosha mpk nikawashaur tubadili uwe na format nyingine, walikubali ko cku hyo beat nilipiga moja.

Nilifurahi maana kalee ka beat ninako mpk leo hua nikikasikiliza hua nakumbuka mengi.

Ila cku hyo ndo nilijua sasa kinanda vizur yan mpk nimerud musoma hua napigia kwaya beat japo saiv nipo mbali na kinanda lakin kwenye simu yangu hakikosi hua napiga beats ili ujuz usiondoke.

nitarejea tena.
mkuu ni app gani unatumia kutengeneza beats
 
inaendelea


Hatimaye cku zangu za kuishi na kupiga kazi zilifika tamati mwez wa 11 mwanzoni kabisa yani nilikua nasubir tarehe ya mshahara tarh 08 nichukue mshara wangu.

Siku hyo ilikua jumapili niliwai kiwandani mpk idarani kwangu nikakabidhiwa machine na operator ( alikua mdada bonge ) sasa nilianza kufuma vitambaa vya mifuko kama kawaida mpk kwenye saa tatu asubui wakaja ma in charge wawili pamoja na mwalimu wetu alie tufundisha.

Sijui walkua wanakagua nini ila alivyofika kwangu wakanambia kuwa kama nimesoma ratiba vizur nikasema ndio....wakanambia kaisome tena.Niliisoma duh nikakuta kumbe cku hyo nilikua naingia shift ya usiku ( ratiba ilibadilishwa maana ilikua ni mwanzo wa mwezi )...walinambia niache mashine nirud home kujiandaa na shift ya usiku.

Niliacha nikarud home kulala, saa kumi na 11 jioni nilijiandaa fresh tu afu nikaelelekea kiwandani.Kwa vile nilikua nimewai niliamua kusikilizia kwanza nje ya get kusubir saa kumi na mbili ili niingie idarani.

Hatimaye niliingia idarani lakini siku hyo kwenye line yangu machine zilikua zimejaa, yaani nilikosa machine cku hyo, nikamfuata fundi wa hyo line nikamwambia kuwa sina machine akanambia niende kwenye line namba 4 ( me nilikua line namba 5 ).....kwenda huko line no 4 nako kulikua kumejaa ko nikarudi tena kwenye line yangu nikawa napiga story na operator mmoja hivi nilikua nimepanga nae sehem moja.

Alikuja meneja wa sections yetu akaniona napiga story akaniita kuniuliza mbn sifanyi kazi nikamwambia nimekosa machine.

Kila operators lazima aendeshe machine tatu kama tu amemaliza mwezi mmoja toka aajiriwe, machine mbili ukiwa umemaliza zile siku kumi za kufundishwa na machine moja ndani ya zile siku kumi.

Manager alinambia nimfuate ko tulienda kutafuta nae line ambayo machine zipo tu tukakosa akanambia iki nisikae bure aliniomba niwe dereva boy ( delivery boy ) niwe nasambaza zile cone ( Nyuzi ) kwa ma operator...nilkubali nikaanza kusambaza hizo cone me najamaa mmoja ni Bubu tokea saa 1 jioni nilikua nasambaza hizo koni mpk saa nne ambapo in charge aliiniita akanambia kwanini nafanya kaz isiyo nihusu..nilimwambia akataka niache alafu akanipeleka kwenye machine line namba 1 nikapewa machine tatu.

Hizo machine zilikua ni mbovu hatari alafu cone zake ni clearly ( yaani ile mifuko ambayo rangi yake ni kama silver hivi ).. hizo cone za clear usiku zinasumbua hatar kutokana na hyo rangi yake, pale unapochomeka uxi kwenye matundu ya mikanda ya machine usipokua makini unaweza ukatoa Reject ( mfuko kuwa hauna ubora ).

Machine hzo nilizopewa zilikua zina speed ndogo ko ili niweze kutoboa lengo langu zilitakiwa ziwake bila kuzima mpk asubui, lakin kutona na kuwa mbovu yaani niliteseka nazo sana nikawa namuita fundi anatengeneza lakin wapi zikawa bado ni mbovu tu.

Kama nilivyowaambia kwenye section yetu kulikua na machine za aina nne na kila machine ilikua na speed yake na lengo lake.Ile line namba tano niliyowekwa ilikua machine zske ni nzur mpk raha kuziendesha speed nzuri sana.

Sasa hizi nilizopewa cku hyo 😂😂 kwanza speed ilikua ndogo lengo kubwa.nilipambana siku hyo ( Mungu na ma operator waliokuepo ni mashahidi )

Ilifika saa nane za usiku machine bado zilikua zinasumbua ssna.nikiona wenzangu wana mita za vitambaa karbia 900 eti me ndo machine iliyokua na mita nyingi ni moja ilikus na mita 205....niliamua kuziacha hizo machine bila kutoa taarifa ( nilikua cjui kama ni kosa ) basi kulikua na machine zilikua hazitumiki kwenye hyo hyo line nikaziwasha nikaanza kupiga kazi.

Hizo machine zilikua nzur mpk nikawa nasema kwann nilipoteza muda bure kuhangaika na yale machine mabovu.

Nilipiga kazi sana na huyo fund alkua anakuja kwenye hizo machine ana cheka huku anasema umeamua kuchukua machine nyingine huku anssema piga kaz kijana pambana sanaa.

Asubui ilifika saa kumi na mbili nilikabidhi machine kwa operator aliyekuja kunipokea alafu me nikaenda zangu chooni kunawa ili nisubir kad yangu nisepe.

Wakat nasubir kadi nilishangaa naitwa na madamu mmoja hivi kuwa niende kwa in charge nahitajika.Sikuia na wasiwasi wowote nilienda mpk kwenye kiofisi cha in charge.

In charge aliniuliza kama me ndo niliendesha machine fulan nikasemas ndio ila niliziacha kutokana ubovu wake nikaamua kuendesha nyingine.

Kumbe yule fundi alikua ni mnafki mkubwa, yeye ndo alimwambia in charge kuwa niliacha machine nikaenda kulala 😂😂😂😂😂 ...sasa pale idaran ungelala wap na huku makelele ya machine ni 24/7...nilijieleza kuwa niliona machine ni mbovu nikaamua kuchukua nyingine ili lengo langu litimie, lakin in charge alinambia hataki kuniona tena pale ( akawa kanifukuza kazi ) nilimwambia fresh tu nikawa naondoka kutoka idaran.

Lakin kuna madam mmoja hivi alinifuata akanambia nikaombe msamaha hata kama sina kosa.nilimsikiliza yule madamu nikarud tena kwa in charge ili nimuombe msamaha lakin wapi alinitolea lugha chafu sana mbele za watu mok akawa anamuita KK aje anitoe kwa nguvu..

Kwa vile kulikua na makele sana Kk alikua mbali na hakusikia saut ya in charge kwa huo muda.

Nilivyoona in charge hana hata dalili za kunielewa niliamua kwenda tena choon kunawa sasa kipind narud ili nitoke nje in charge aliniona akanambia kwa ukali ngoja ni mnukuu "wee **** c nimekwambia utoke nje huelewei nini wewe nimesema toka nje sitaki kukuona hapa"....nilimwambia dharau aache kusema hivyo napo ikawa ni kosa, alinitukana sana nikaona huyu boya anijui.

Kulikua kuna ndoo ilikua karbu na machine line namba 4 ilikua ni ya rangi zile za machine ya printers...ilikua ni nzito nzito niliichukua nikampiga nayo huyo in charge shavuni mwake, mpk alidondoka chini, ashukuru sana mafund ndo waliwai kunishika.

Nilipelekwa stoo mimi na huyo in charge ( kueleza mashitaka )...tulivyofika huko sikua na mtetez zaid ya yule madamu mpole.in charge alitaka niondoke na nisirud tena pale idaran nikasema poa tu hakuna shida ila nilimwambia dharau me sipendi.

KK alikuja kunitoa nje, kadi yangu huyo in charge aliichana chana ko tulitoka nje na yule KK akawa anasema ndo maisha hayo dogo pia akanambia niende kwa ma HR ilinipatee msaada zaidi.

Kazi kweli nilikua naipenda sana maana nilikua nshaizoea ila ckua na namba niliona niiache tu pengine ckupangiwa kuifanya na Mwenyezi Mungu.

Niliumia sana nikaenda geto nilifika nikamjulisha kwanza sister kuwa nimefukuzwa kaz kisha pia wengine wafuata.

Mzee alinambia nirud musoma haraka nikaish na yule manzi wa karatu.Manz mwenyew nilimwambia kuwa nimefukuzwa kazi itabid arud kwao tu lakin aliktaa alisema hawez kurud kwao.

Sikuondoka mwez huo nilikaa kwanza nikawa na muwinda yule in charge ili nimpige alafu ndo nisepe zangu na ana bahati sana sikumpata kabisa.Nilikua namuwinda pale nje ya geti sema tu ndo walikua wanachelewa kutoka ila ningemshika nilikua namchana na wembe usoni.

Niliamua kuuza baadh ya vitu kwa washkaj zangu vingine niligawa bure na hata kodi ya nyumba ilikua bado haijaisha ko nilimpa jamaa mmoja aimalizie me ilivyofika mwez wa kumi na mbili niliamua kurud musoma.

nitarejea tena.
 
Hongera kwa kupata mke, nakumbuka mke wangu naye nilimpata kwa staili inayofanana.... Demu alileta bag akakomaa haondoki huku alisisitiza yeye ndio mke Mungu kanipa, nikawa mkali nikampa mateso yote aliyashinda

Kaka bora uishi ndan na mwanamke anaekupenda kuliko asiekupenda alaf ww unampenda ni zaid ya mateso,komaa nae huyo ndio chaguo lako mzee
 
Hongera kwa kupata mke, nakumbuka mke wangu naye nilimpata kwa staili inayofanana.... Demu alileta bag akakomaa haondoki huku alisisitiza yeye ndio mke Mungu kanipa😅, nikawa mkali nikampa mateso yote aliyashinda🙌
hongera pia mkuu...huyu mwanamke wangu nacho mpendea ni heshima aliyonayo kwangu na kwa wazazi.Tayar na ndoto nae ni yeye ndo aje azingue
 
hongera pia mkuu...huyu mwanamke wangu nacho mpendea ni heshima aliyonayo kwangu na kwa wazazi.Tayar na ndoto nae ni yeye ndo aje azingue
Ila maisha ni safar ndefu sana yan wakati uko musoma pamoja na kua na mademu wengi hukubahatisha kumpata wa kukufaa mpaka ulipotimba arusha utakutana na mkaratu

Mpenzi sahihi anakuja kwenye maisha yako pasivo ww kutegemea wala hakuna sababu ya kulazimisha vitu

Hii story ina vitu vingi sana vya kujifunza
 
Back
Top Bottom