Story ya kweli ya maisha yangu

holy holm

JF-Expert Member
May 6, 2017
3,110
2,000
Habarini Wapendwa,

Hope mko njema licha hili janga linalo tukumba Mungu ni mwema sana.

Leo naomba kushare story ya Maisha yangu Mimi holy holm. Wiki chache zimepita nilileta humu thread ya jinsi nilivyoanza mahusiano ya kimapenzi na jimama na nilihaidi kuwaletea story nyingne ya maisha yangu, basi kwa hiari yangu sina budi kuwaletea.

Hii story ita base Katika Mji wa Musoma maana ndo nimeishi sana huku. Baadhi ya majina ya watu sitayataja hii ni kuwalindia heshima lakini ikibidi nitawaja. Tuweni tu wavumilivu maana story ni ndefu kidogo na nitakua naitoa vipande ili iweze kueleweka vizuri.

Nimezaliwa Musoma mjini nilikua naishi Kata ya Iringo mimi na familia yangu,tuko watoto sita.Kwa wanaoijua mitaa ya musoma enzi hizo ilikua sio mitaa salama sana kwa usalama hii ni kutokana na wimbi la makundi ya kihuni yaliyokua yameshamiri nahisi ni kuanzia 2010 mpka 2014 au 2015 kama sikosei mwenye kumbukumbu nzuri ataliweka sawa hilo. Binafsi yangu mimi sikua kwenye hayo makundi ila nilkua na marafiki ndani ya hayo makundi.

Tumelelewa kwenye maadili mema tu mimi na familia yangu ila wazazi wetu walikua wako busy sana na shughuli zao Baba alikua mwalimu na Mama alikua anauza nguo za mitumba (Nyasho) so muda mwingi tulikua tunabaki home wenyewe tu mpk jioni wazazi wakirudi.

Mwaka 2004 nilianza darasa la pili shule ya Musoma ambapo niliamishwa kutokana na maendeleo hayakua mazuri nikaamia Mwisenge primary tena nikahama kuja iringo (B) primary. Kwenye hii shule nilkutana na marafiki ambao tulikua tunaishi nao mji mmoja walikua ni jirani zangu.Kama mnavyojua kwa mlio kaa mtaa wa iringo enzi hizo kulikua na wahuni sana tena hasa kule kastamu milimani ulikua ukijichanganya angazao imekula kwako. Mimi na hao rafiki zangu tuliokua tunasoma nao nakumbuka tulkua na mtindo wa kukaa na hao wahuni japo wazazi walikua hawataki kukaa nao lkn haikuwa rahisi kutuzuia maana mda mwingi walikua kwenye shuguli zao.

Mara nyingi hao wahuni walikua wanatutuma tukawaitie mademu ambao walikua wanawataka wao muda mwingine wanatutuma bangi kwa mapusha wao kipindi hicho sisi hatuvuti sigara wala bangi tena walikua wanatukataza wao wenyewe. Kipindi hicho tulikua tumepanga nyumba ya vyumba viwili na sebule, chumba kimoja walilala wazazi na kingne alilala sista na wadogo zangu wawili wa kiume mimi na bro wangu tulikua tunalala kwa jirani kila mtu sehemu tofauti. Mimi nilikua na lala kwa na rafiki yangu tulikua tunasoma nae darasa moja. Kiukweli huyu rafiki tabia zake hazikua nzuri alikua na tabia ya wizi ambayo aliniambukiza kimtindo nikajikuta na mimi nishakua kezi.

Nakumbuka siku ya kwanza mimi kuiba japo tulikamatwa siku, tulikua tunaenda shule (darasa la pili tulikua tunaenda saa nne) njia tuliyopita kuliku na Mmama mmoja anakibanda chake anauza vitu bidhaa za dukani pamoja na matunda.Sasa bna huyo rafiki angu akanambia twende tuchukue hela hapo kibandani, kulikua na utulivu yaani kulionekana hakuna mtu hapo maana tulivyofika tuliita kama mara tatu kibandani, kibandani....kibandani...tulivyoona hakuna mtu anae kuja jamaa angu alinambia niangalie usalama wakati yeye muda huo alipanda kwenye hicho kibanda na kupitia kwenye kale katundu ambako wanapitishia bidhaa, moja kwa moja kwenye kopo la hela akakomba zote ile anatoka tu anataka kushuka yule mama cjui alitokea wapi akaanza kupiga yowe la wezi.

Tukiwa na uniforms zetu za shule tulikimbia vibaya mno kuelekea shuleni bahati nzuri watu hawakua wengi sana ( hiyo ndo nature ya iringo asubuhi watu sio wengi sana mtaani) tulikimbia mpka tukampotea yule Mama hatukuenda shule moja kwa moja tulipitia yale maeneo ya Afilux hotel kujua tulikua na shingap alizochukua kucheki zilikua ni sh 18000 na vijisenti me nilipewa buku 6000 yeye nae akachukua buku 6000 iliyobaki tukaingia kwanza kwenyee ka mgahawa kupoteza mawazo, tulikula siku hyo donati za kutosha baada ya hapo tukaenda pale stendi kwa wamachinga me nilinunua saa zile disco zilikua ni jero pamoja vile vikamera ambavyo ukichungulia unaona wanyama mbalimbali, Rafiki angu yeye alinunua karedio na vile vigemu fulani hivi ndo vilkua vina trend kipindi hicho.Baada kufanya hiyo shopping tulielekea shuleni sasa tukiwa hatuna wazo kama huko nyuma tumefanya msala.

Nitarudi kuendelea maana story ni ndefu ndugu zangu.

Au nasema uwongo ndugu zangu
 

holy holm

JF-Expert Member
May 6, 2017
3,110
2,000
Chapter { II }

Baada kufanya shopping zetu basi tuliamua kulekea shuleni akili zenu zilisahau kuwa tuna msala tumeufanya huko nyuma ( labda sababu ya utoto pengine ) ile tunafika darasani tunaambiwa na monta tunahitajika osifi ya mwalimu mkuu ( mwalimu mkuu alikua anaitwa Meshack alikua ni mkali kingese R.I.P kwake) kwanza tuliambizana twende ama tutoroke maana tulikua tunajua kuwa ni kwa sababu tumechelewa kuja shule ilikua ni saa sita muda huo. Tulikubaliana kwenda ili hata kama ni kupigwa viboko tupigwe tu tumalize msala kabisa aisee ile tunaingia ofisini tunamkuta yule mama akiwa na vijana wawili mmoja alikua ni kijana wake.Mlango ulifungwa tumebaki hatujui tufanye nini wale vijana wakawatudaka kila mtu na mtu wake me nilishikwa na mtoto wa huyo Mama.Huyo kumbe baada ya sisi kukimbia alienda moja kwa moja shuleni akijua tu atatupata.

Mwalimu mkuu alitwambia tutoe hela tulizoiba jamaa angu akasema hatujaiba me muda huo nilkua nalia tu kitendo cha kusema hatujaiba kilikua ni kibaya tulipigwa bakora sio za nchii yule Mama akadai atupeleke polisi lakini yule ticha alikataa akisema tuyamalizie hapo hapo shuleni lakini alikataa maana jamaa alishikilia msimamo kuwa hatujaiba.Basi ticha big alikubaliana na yule mama tukafungwa mashati kwa pamoja ili tusikimbie akaitwa mwalimu wa nidhamu tukapelekwa kituo cha polisi Kitaji.

Tulivyofika kituoni (maana ilkua sio mbali sana na hyo shule tulienda kwa miguu tu ) Kwanza maafande walikua wanatushangaa labda hawakutegemea sana ujio wetu tulikua makid sana.kabla hatujaingia ndani ya kituo kuna afande alitulaki pale nje na maswali kibao kuwa tumefanya kosa gani yule mama alieleza kila kitu lakin yule afande alikataa kutupokea kisa sisi ni wanafunzi alicho kifanya alituoji kama kweli tumechukua hela me wakati huo ni kilio tu nikiwaza wazazi wangu wakipata taarifa itakuaje siku hyo.Yule afande alitusachi akatukuta na baadhi ya hela ko akamulu tufunguliwe yale mashati kisha viboko vikafuta tulipigwa viboko kumi kila mtu ukijumlisha na vile tulivyopigwa shule hayo maumivu yasikie tu.

Tulitoka pale kituoni kwenye midaa ya saa nane hivi wanafunzi walikua wameshatawanyika tukaamua twende moja kwa moja home ile tunakaribia na home tukakutana na Mama ake na huyo rafiki angu alicho kifanya alinivua ile saa nilikuwa nimenunua akachkua vile vitu vingine akatwambia tumfuate kufupisha habari ni kwamba tulichezea kichapo cha mbwa koko maana kumbe taarifa alikua ameshaipata tulinyimwa na chakula cha mchana siku hyo ilikua mbaya sana kwetu.

Mzee nae alivyokuja usiku alitugongesha kichapo kikali tena cha kikatili maana alitumwagia maji mwili mzima huku akitupiga na waya wa umeme siku hiyo sitohisahau kwa kweli. Mama angu yeye akutukugusa kabisa alikua ananihurumia tu kuona mwanae navyopigwa mpk alilia .Tulikaa nyumbani siku tatu tukiuguza vijeraha plus maumivu Baada ya hapo skuli ikaendelea ( yule mama alilipwa hela na Mzee wangu).

Baada ya kupata huo msala ndo kwanza tabia yetu haikukoma ndo kama vile waliichochea.maana tulikua tunaiba kwa akili sana hivi vitu vidogodogo kama viatu,hela,vyuma chakavu n.k.Nakumbuka pale stendi wale machinga tume wacheza sana bidhaa zao.

Kesho nitarudi kuendelea.
 

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
6,334
2,000
Mi story yako siitaki. Nataka story ya Mshua wako.

Yaani mwalimu anapanga nyumba ina vyumba viwili tu tena mkoani Mara. Huko Laki na Nusu si unapata nyumba nzima ata yenye vyumba vinne?

Hayo maisha ova mlikua Dar tu sasa.

Ila ninja umepitia mengi. Endelea kutiririka.
 

holy holm

JF-Expert Member
May 6, 2017
3,110
2,000
Mi story yako siitaki. Nataka story ya Mshua wako.

Yaani mwalimu anapanga nyumba ina vyumba viwili tu tena mkoani Mara. Huko Laki na Nusu si unapata nyumba nzima ata yenye vyumba vinne?
mkuu ngoja nikusaidie tu hapo iringo mzee wangu alipanga enzi hizo 1993 hata cjategemea kuzaliwa me nilikuta tu nipo hapo lakini baadae tulihama huo mtaa na kuchukua nyumba yenye vyumba vinne 2006 hyo sema umewai sana kuuliza na ilikua ni lazima nielezee huko mbele ya stori.

Cjui umenielewa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom