STORY: Sitaki Tena

SEHEMU YA 45

~BAADA YA WIKI MOJA~



Nilikuwa mzima wa afya na safari ya kurudi kwetu Tanzania ilikuwa imeshafika sikuweza kuwaona wale watu tena pale wodini tayari Gervas wangu alikuwa pembeni yangu mzima tena tukicheka naye na kupiga stori kwenye gari huku tukielekea uwanja wa ndege wa zambia.
Hapakuwa mbali sana kwani ndani ya nusu saa tulikuwa tayari tunaingia ndani ya uwanja wa ndege huku tukielekea kupanda ndege ile ile iliyotuleta.
Furaha kwangu ilikuwa kubwa sana na hata Grvas naye alifurahi sana kwa upendo niliokuwa nimemuonesha wa kujitolea figo yangu ya upande mmoja na kumpatia.
‘’Levina huyu ni nani?’’
Ilikuwa ni sauti ya gervas akitaka kujua ni nani yule Mama tuliyeongozana naye mpaka Zambia.
‘’huyu ni mfanyakazi pale 'airport' dar na ametoa msaada mkubwa mpaka wewe kufika hapa...’’
‘’Ahsante sana Mama. Nakushukuru sana kwa msaada wako ulioutoa...!’’
‘’Hata nawewe nakushukuru mwanangu pole sana na naimani umeshapona kabisa’’
Nilipenda sana ukarimu wa yule Mama na hata tulipofika uwanja wa ndege Gervas alimuomba sana twende naye mpaka nyumbani kwetu.
Tuliingia Dar alfajiri sana kwenye saa kumi na mbili,
Siku hiyo hiyo tulipofika tuliandaa sherehe kubwa sana huku ‘Jammy’ akisaidiana na yule Mama kutengeneza vyakula tofauti tofauti,majirani walikuwa ni wengi sana pamoja na bosi wake Gervas wote walikuwapo katika kumpa pole Gervas.


~ BAADA YA MWEZI ~


Maisha ya pale nyumbani yaliendelea kuwa mazuri japo sio sana na tuliamua kuiuza ile nyumba ya kina Gervas tuliokuwa tumeipangisha hivyo pesa yote tukaiingiza katika miradi mbali mbali tuliokuwa nayo,yule Mama aliacha kazi ya usafi 'Airport' hivyo tukawanaye akisimamia baadhi ya miradi tuliokuwa nayo, Sikuamini hata siku moja kama yule Mama angebadilika kiasi kile labda ni kutokana na maisha, alikuwa mtu mtakatifu sana na alininyenyekea kwa kila kitu hivyo alitufanyia mengi mema.
Siku moja Gervas alivyorudi toka ofisini.
‘’Levina mke wangu’’
‘’surprise......!!!’’
‘’Otea ni kitu gani kizuri nataka kukwambia kimetokea ofisini leo...?’’
‘’Wewe niambie tu mimi siwezi kujua ni kitu gani mpenzi wangu’’
‘’Haya fumba macho nikupe kitu’’
Nikafumba macho kujua ni kitu gani ameniwekea mkononi mwangu. Haraka haraka nikafungua macho nakushuhudia bahasha ya kaki mikononi mwangu.
‘’Wewe niambie tu kunanini Gervas’’
‘’Haya nimekuruhusu ifungue mwenyewe uone ni kitu gani hicho’’
Nikafungua taratibu huku moyo ukinienda mbio akilini mwangu nilijua tu itakuwa kaongezewa labda cheo tena.
‘’Mungu wangu nini tena hiki?’’
Nilijikuta mwili unanyong'onyea kila nilipokuwa naendelea kusoma mpaka nikaamua kuacha kusoma.
‘’Kwahiyo Gervas ndicho unachofurahia hiki?.. Haya endelea kufurahia..! Endelea tu’’
Nilikuwa na hasira sana mpaka nikatoka zangu nje huku mishipa ya shingoni ikiwa imenitoka na mchozi ulikuwa ukinilenga lenga.
‘’Gervas sitaki unifuate nasema rudi ndani, rudi Gervas’’
Kiukweli nilimpenda sana mpenzi wangu Gervas na nilikuwa tayari kufunga naye ndoa kwani nimetoka naye mbali kwa shida na raha, na ile barua aliyonipa ilikuwa inamhusu yeye mwenyewe kuwa meneja Mkuu na siyo msaidizi tena na hata hivyo nusu ya wafanyakazi wa ofisi yao inahamia Mtwara na Gervas anatakiwa akasimamie tawi la Mtwara hivyo mshahara na cheo vimeongezeka mara mbili ya ilivyokuwa.
Amani ilinipotea kabisa mwilini mwangu huku nikiwa sijiamini kabisa kwani ni muda mrefu sijakaa na Gervas mbali.
Nikarudi ndani kuendelea na shughuli zangu za kawaida lakini Gervas alikuwa chumbani nikamfuata kumchungulia anafanyaje lakini nilipoingia chumbani nilimkuta kakaa tu kwenye Laptop yake anafanya kazini kasimama mlangoni nakumuangalia kwa huruma huku mchozi ukinitoka na kusisimka taratibu nikamfuata na kukaa pembeni yake kisha nikachukuwa mikono yangu na kupenyeza mabegani mwake huku nikimpapasa kwa kuitelezesha ile mikono yangu kwenye mabega yake,
‘’Gervas mme wangu.. Nakupenda sana...!’’
‘’Nalijua hilo na hata mimi nakupenda tena sana Levina’’
Nikamzunguka kwa nyuma na kumkumbatia kwa furaha huku nikijitahidi kujisahaulisha yaliyotokea lakini kabla sijamkumbatia mara nikajisikia vibaya nikakimbia moja kwa moja mpaka chooni huku Gervas akinifuata kwa spidi nyuma nyuma na nilipofika nikatazamana na sinki la pale karibu na choo nikaanza kutapika na nilitapika sana bila kujua ni kwanini, Kwani nilishikwa na kichefu chefu ghafla.
‘’Pole Levina, Nini tena lakini umekula?’’
‘’Sijui Gervas ila nahisi kama kizungungu zungu’’
Haraka haraka Gervas akanipakiza kwenye gari kutokea nyumbani kurasini mpaka hospitalini 'Ocean road' na tulipofika tu moja kwa moja akanipeleka kwa Dokta wake akanipokea na kuniingiza kwenye kachumba kisha.
‘’Wewe nisubiri hapo nje’’
Yule Dokta alimwambia Gervas kisha nikamwangalia akitoa vitu kama vichuma chuma vilivyounganishwa na waya kisha akaviweka tumboni mwangu huku akivisikilizia kisha akavitoa na kunishika shika tumboni, na baada ya hapo akachomoa kimrija kisha akanipa akaniambia nikidumbukize kwenyesehemu zangu za siri, Nikafanya hivyo baada ya muda nikampatia akakiweka kwa juu huku akikiangalia mara mbili tu na kuniambia.
‘’Hongera Levina..’’
Nilikuwa kama sijiamini amini huku nikidhani kama ni ndoto naota lakini ilikuwa ni ukweli mtupu.
‘’Embu niambie ukweli Dokta nini tena?’’
‘’Unamimba na ina wiki kama tatu mpaka sasa’’
Hapo hapo nikatoka spidi mpaka nje kwa Gervas na kwenda kwania ya kumwambia lakini nikiwa natoka Dokta akaniita
‘’Levina? Levina?’’
 
SEHEMU YA 46



********


‘’Umesahau chukuwa’’
Kugeuka hadi nilishikwa na aibu Mungu wangu kumbe nilikuwa nimeisahau nguo yangu ya ndani lakini ilinibidi kuichukuwa na kuingia chooni kuivaa, Kisha nikatoka nje kwa aibu kubwa.
‘’Levina vipi tena imekuwaje?’’
Gervas aliniwahi fasta akitaka kujua imekuwaje.
‘’Gervas..?’’
‘’Enhee! niambie mke wangu nini tena kimekusibu? Au ulikula mivyakula mibaya?’’
‘’Bora ningekula chakula kibaya’’
Dokta akawa ameshafika eneo tulilopo,
‘’Gervas... Naimani utakuwa na furaha ya hali ya juu!’’
‘’Kwani lipi Dokta mbona mnaniweka njia panda?’’
‘’Mkeo Levina anamimba na ina wiki kama tatu’’
Hapo hapo Gervas hakutaka kujua la zaidi akanivuta mkono nakuondoka mpaka anakamata breki ya kwanza tukiingia supermarket ya shorprite,
‘’Mimi nanunua tu kama wakiume atavaa na kama wakike naye atavaa tu’’
Gervas alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kwani mpaka tunaingia pale supermarket ilikuwa ni usiku wa saa mbili na alikuwa nafuraha ya kutarajia kupata mtoto hivyo akajikuta ananunua nguo zote zote bila kujali jinsia na vikoro koro vyote vya kuchezea mtoto ikiwa ni mpaka kitanda cha mtoto.
Baada ya lisaa tulikuwa nyumbani na hakuna hata mmoja wetu aliyekuwa na hamu ya kula kwani kila mmoja alikuwa na hamu ya kula zaidi ya kila mmoja kuwa na furaha ya kutarajiakupata mtoto baada ya miezi nane na nusu.
Sikuwa na hata lepe la usingizi zaidi ya kumsumbua Gervas usiku kutwa kitandani mpaka asubuhi, kero yangu ilikuwa ni kichefu chefu kwani ilinibidi niwe na kopo la kutapikia karibu yangu mpaka asubuhi.

******

Kesho yake sikwenda ofisini alikwenda Gervas na ilipofika mchana nilishangaa akirudi kabla hata ya muda wake nasafari hii alirudi na Jammy huku wakicheka kwa furaha.
‘’Gervas mmbeya?’’
Nilijikuta najisemea kimoyo moyo huku nikiwaangalia wakiwa wanaingia ndani.
‘’Waaooh Levina’’
Alikuwa ni Jammy akinikumbatia kwa furaha kwani ni kweli siku mbili tatu hatujaonana naye. Alinipa hongera kwani ni kweli Gervas alikuwa tayari ameshamwambia kuwa na mimba na pia aliniambia habari ya yeye kwenda kufanya kazi mtwara na kuwa hatakuwa akifanya kazi za usafi bali atakuwa kama mpishi mkuu wa ofisi hivyo wiki ijayo wataondoka wote na wiki hii ofisi za mtwara zinafanyiwa marekebisho kabla hawajahamia.
Nilizidi kuumia moyo si kwa kumkosa Gervas machoni mwangu la hasha bali ni hata kwa rafiki yangu kipenzi Jammy sitamwona mpaka labda apate kalikizo ndio nimuone.

~ BAADA YA WIKI ~



Hatimaye siku ya Gervas kuondoka ikatimia huku nikizidi sana kuumia moyo na kutamani Gervas abaki, Nilitamani sana kumsindikiza mpaka uwanja wa ndege lakini nilishindwa kwa hofu ya kipindi kilee nilichofanya mauaji pale.
Tulipanga mambo mengi sana kabla Gervas hajaondoka ikiwa ni pamoja na kuniachia miradi yote niiendeleze.



*********
 
SEHEMU YA 47


Ni siku ya pili sasa imekatika toka Gervas aondoke kuelekea mtwara kikazi zaidi, Mawasiliano aliyoyaonyesha ambapo kila baada ya masaa manne alikuwa akinipigia simu kunijulia hali, Nilizidi kumpenda mume wangu na pia aliniahidi kuwa nitakapojifungua tu ndipo mipango ya ndoa itaanza.
Nilijisikia faraja sana moyoni mwangu kila nikimfikiria mtoto nitakayempata,
Baada ya mwezi bado mawasiliano ya mimi na Gervas yanaendelea vizuri na safari hii Gervas alinitaka niende nikamsalimia na kuwa kuna kitu kizuri ameniandalia, Aliniingizia pesa nyingi kwenye akaunti yangu.
Hivyo nikafanya mipango ya kuondoka kuelekea Mtwara, Nilisindikizwa na yule mama mpaka uwanja wa ndege nikapanda ndege tena bila kumuogopa mtu yeyote na kumwachia pesa na nyumba yule mama mpaka nitakaporudi.
Ndani ya masaa matano nilikuwa tayari nipo Mtwara huku Gervas akiwa mtu wa kwanza kunipokea,
‘’yupo wapi Jammy?’’
‘’Kabanwa na kazi utamuona siku nyingine’’
Akanipeleka mpaka kwenye nyumba aliyopangishiwa na ofisi.
‘’Nzuri? Sasa jumba lote unaishi peke yako mme wangu!’’
Nilijisemea kiutani lakini hilo swali lilimkwaza sana Gervas. Kisha akatoka na kuingia jikoni na baada ya hapo akarudi na glasi mbili zilizojaa juisi ya maembe nikaichukuwa lakini kabla sijainywa akakatiza Paka pale sebuleni. Nikaitupa ile glasi chini kwa mshtuko.
‘’hivi wewe Levina, mbona unamakusudi hivyo..? Umeona juisi yangu haina thamani kwako eeenh...?’’
‘’Hapana Gervas si unajua mimi tangu zamani naogopa sana Paka na hata Mbwa?’’
Gervas alionesha kukasirishwa sana na kitendo cha mimi kuitupa glasi chini ikavunjika.
Nilikataa kuinywa tena ile juisi yake na hata usiku Gervas naye alionesha kuwa na hasira kwani hata muda wa kulala alinigeuzia mgongo mpaka asubuhi na ilipofika asubuhi alinitaka twende 'Beach' tukafurahie maisha, sikujali lakini tulipofika Gervas aliagiza Juisi za boksi tu kwani yeye hakuwa mlevi sana.
Lakini kabla hajanipatia nilihisi kunakitu amekiweka ndani yake lakini kwa kisirani nilichokuwa nacho nadhani labda ni mimba ndio ilikuwa ikinipelekesha sana.
Nijikuta nalichukuwa lile boksi la juisi na kulitupa kwenye swimming pool.
‘’hivi wewe Levina? Aibugani tena hiyo unayonipa? Enhe? Na utalipia mwenyewe hiyo juisi!’’
‘’Mume wangu Gervas! Yani juisi tu ndo unabadilika kiasi hicho, kwani juisi bei gani? Waiter embu chukua hii ela niletee juisi nyingine’’
Sikuelewa vizuri ni kwanini Gervas amebadilika kiasi kile.
Kesho yake nikafunga safari na kurudi 'Dar' lakini sikuweza kumuona Jammy zaidi ya kukwaruzana na Gervas hadi nikajuta kwanini nimekuja huku.

*************


Mawasiliano ya mimi na Gervas yalianza kubadilika kwani alikuwa akinipigia siku kwa siku hadi mara sita na sasa inapita siku bila hata ya mawasiliano yake mpaka nimpigie mimi,
Mimba ilikuwa tayari ina kama mwezi mmoja na wiki tatu nilizidi kuumia sana moyo lakini nikajikaza moyo wa kijasiri. Ilinibidi niwe mvumilivu tu kwani ilifika tena kipindi tukawa tunawasiliana mara tatu kwa wiki.



********
 
SEHEMU YA 48


‘’hallow Levina mke wangu’’
‘’Ndio Gervas wangu!’’
‘’Wiki hii nilikuwa bize sana jamani kwanza nisamehe kwa hilo, Vipi unaendeleaje na mimba’’
‘’Naendelea vizuri, ila Gervas umenitia wasiwasi sana mpenzi wangu’’
‘’Usijali mpenzi wangu vipi miradi inaendeleaje huko?’’
‘’Inaendelea vizuri tu mme wangu’’
‘’Kesho nitakuwa huko kwa ajili yako kwani nakupenda sana jamani’’
‘’Kweli Gervas wangu?’’
‘’Kweli Levina asubuhi nitakuwa hapo’’
Nilifurahi sana kumuona tena Gervas machoni mwangu kwa mara nyingine toka nimeachana naye nikivyoenda kule Mtwara anapofanyia kazi.
Usiku wote sikupata usingizi huku namfikiria mume wangu Gervas.
Ilipofika asubuhi nilimuamsha yule Mama na kusaidiana naye kila kitu lakimi ilipotimia saa tano za asubuhi tayari gari ilikuwa nje ikipiga honi, Haraka haraka nikatoka nje na kuwahi hadi kwenye lile gari na nilipolifikia lilifunguliwa mlango na kushuka Gervas ambapo kwa furaha zote nikimkumbatia na kuongozana naye mpaka ndani. Kila mmoja wetu alikuwa na furaha kwa mwenzake, tulishinda naye siku nzima tukiongea naye tu mambo yahusuyo maisha yetu.
‘’Vipi Jammy mbona sikuhizi simpati kwenye simu?’’
‘’Yupo ila sijuwi tatizo nini?’’
Nilimuulizia Gervas kwani kweli ni muda mrefu Jammy amekuwa kimya sana bila hata ya mawasiliano yoyote.
‘’Levina mke wangu si unajua mi napenda sana kwenda beach!’’
‘’Ndio mume wangu’’
‘’Hivyo jiandae kesho asubuhi tunaenda kushinda wote siku nzima 'sunrise beach resort'!’’
‘’kweli mume wamgu?’’
Nilifurahi sana na usiku huo tukalala kwa furaha tele huku tukifurahia maisha.

*********

Asubuhi na mapema nikajiandaa na kukuta yule Mama kashaandaa chai tukanywa na kumuacha kisha tukakodisha teksi mpaka 'Kigamboni' na kisha tukaingia 'Sunrise beach resort' Palikuwa ni pazuri kwani nilikuwa sijawahi kufika ilikuwa ni mara ya kwanza kufika pale.
‘’Pazuri hapa Gervas’’
‘’Ni kweli Levina hii yote nikukuonesha kuwa nakupenda sana’’
Tukaingia ndani na tulipofika breki ya kwanza Gervas akakodi vile viboti vidogo kisha tukaingia,
‘’’Mmesahau maboya ya kujikinga kifuani’’
‘’Hatuendi mbali sana achana nayo’’
Gervas alimjibu yule muhudumu wa pale kisha akawasha kile kiboti na kuongoza hadi karibu na kati kati palipokuwa patulivu, sehemu tuliyotoka ilikuwa ni mbali sana kiasi kwamba huwezi kumuoma hata mtu,
‘’Levina mke wangu…nataka kukufanyia surprise kabla hatujarudi kule’’
Aliniambia Gervas baada ya kufika eneo tulivu na kwa muda ule alikuwa ameizima ile boti katikati ya maji marefu kisha.
‘’embu fumba macho kisha lete mkono wako mmoja’’
‘’Gervas bwana acha utani wako huo’’
‘’Kweli lete mkono Levina’’
Nikafumba macho nakumpatia mkono mmoja kisha baada ya hapo.
‘’waooh Gervas wangu’’
Sikuamini macho yangu kwani ni kweli Gervas alikuwa kanivalisha pete ya uchumba ya dhahabu.
‘’Gervas mume wangu nakupenda sana nakupenda Gervas’’
Hapo hapo nikamkumbatia kisha akawasha boti tayari kwa safari ya kurudi.
‘’Gervas vipi! Endesha taratibu tutafika tu’’
Nilimwambia Gervas kwani alikuwa akiendesha vibaya.
‘’Mungu wangu Gervas niokoe, niokoe Gervas’’
Tayari miguu yangu ilikuwa nje ya ile boti ambapo nadhani ni bahati mbaya mawimbi yalitusomba lakini Gervas alikuwa bado kaing'ang'ania ile boti katika steringi huku anaendesha. Nikiwa bado mikono yangu imeng'ang'ania boti na miguu iko nje Gervas ndio kwanza akazidisha mwendo huku nikiburuzika kwenye maji,
‘’Gervas mume wangu nakufaaah!, Naumia tumbo Gervas Gervaaaaas..!’’
Alichukuwa kasia moja lililopo ndani ya ile boti nikadhani labda nimepata msaada lakini haukuwa msaada wowote kwangu kwani nilimshuhudia Gervas akipunguza mwendo kisha akachukuwa mkono wake mmoja na kuanza kunipiga vidoleni ili niweze kuachia ile boti, alinipiga piga kwa nguvu sana hadi nikaachia,
‘’Gervasss!, Gervasss! kwanini unanifanyia hivi?’’
Akawasha ile boti na kutoka kwa spidi huku akicheka kwa kitendo alichonifanyia. Nilibaki natapa tapa kwani sikujua kuogelea hivyo nikajikuta nazama kwenye kina kile kirefu zaidi huku nikiwa peke yangu.
 
SEHEMU YA 49



*********


Baridi kali nililokuwa nikilisikia na kelele kwa mbaali zilinifanya nifungue macho ili kujua,
‘’Mungu wangu’’
Nilikuwa uchi kabisa huku nikiwa mikononi mwa wavuvi wale wanaovua samaki usiku sana.
‘’Hapa ni wapi?’’
‘’Kigamboni’’
‘’Nani kanileta hapa?’’
‘’tulia Dada. Tumeukuta mwili wako umesogezwa na mawimbi ya maji mpaka huku na ikatubidi tuje kukuangalia, kwani vipi imekuwaje?"
Hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kugundua kuwa pale nilipokuwa ni Gervas ndiye aliefanya yote yale,
‘’Gervas? Gervas? Gervas?’’
Nilijikuta naongea mwenyewe huku wale wavuvi wakinishangaa.
‘’Gervas ndio nani?’’
Sikuwajibu zaidi ya kuitoa ile pete yake nakuitumbukiza kwenye maji kisha nikataka kunyanyuka lakini nikashindwa, Mungu wangu kumbe maji yalinipiga sana miguuni mpaka nikalegea nikashindwa hata kusimama,
‘’nipelekeni nyumbani’’
Walibaki wakinishangaa kwani kiukweli nilikuwa na nguo ya ndani tu hivyo ni kama niko uchi tu. Hapo hapo mmoja wa wale wavuvi akaingia kwenye boti yao na kunitolea suruali yake na shati la akiba nikavivaa na kupanda ile boti mpaka kivukoni.
‘’lete teksi’’
Nilichukuwa teksi
‘’nipeleke kurasini’’
Nikaenda mpaka nyumbani nikabebwa mpaka ndani nikamkuta yule Mama mwenyewe ndani,
‘’Gervas yuko wapi?’’
‘’Toka jana ulivyotoka naye sikumuona’’
Nilizidi kuchanganyikiwa zaidi hadi nakuona kama vyote ni ndoto tu.
‘’Embu nenda chumbani kwangu kwenye droo kachukue shilingi elfu kumi na tano uje umpe huyu dereva teksi na huyu mwingne mpe shilingi Elfu kumi kwa msaada walionionesha.
Nikachukua ile simu ya yule Mama na kumpigia Gervas simu ikawa haipatikani, nikampigia Jammy napo hivyo hivyo nikaacha, nitapiga tena baadaye.
Usiku wote yule Mama alinikanda miguu yangu na kulipokucha nilikuwa na nguvu zangu kama kawaida kwani niliweza kutembea vizuri tu.
Nikachukuwa tena simu na kumpigia Gervas lakini simu haikupatikana nikajaribu kwa Jammy napo hivyo hivyo.
Nikaingia chumbani na kuvalia pensi yangu kisha nikaingia uvunguni mwa kabati na kuichomoa bastola yangu ya kipindi kile nilikuwa nimeificha siku nyingi sana.
Nikaenda mpaka airport kupanda ndege, Nikapata ndege ya Mtwara inayopitia Mwanza nikachukuwa na kuelekea mpaka Mtwara.
Nilipofika nikaongoza moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Gervas lakini nilipofika sikumkuta kulikuwa kumefungwa hivyo nikaulizia jirani kwani nilikuwa sijui hata ofisi zao ziko wapi.
‘’Samahani mwenye hii nyumba yuko wapi?’’
‘’unamuulizia bosi Gervas?’’
‘’ndio huyo huyo’’
‘’yule mbona leo anafunga ndoa na mfanyakazi mwenzake anaitwa Jamila!’’
Moyo ukanilipuka ghafla na mwili kuninyong'onyea.
‘’Kanisa gani wapo?’’
‘’Hata sio mbali na hapa kule unapita kushoto kwa pale utaliona kanisa kubwa la 'ST. GASPER'!’’
Haraka haraka bila kupoteza muda nikatoka spidi na kuelekea, watu walikuwa wengi na nikweli Gervas alikuwa akifunga ndoa huku msimamizi wake akiwa Omari,
‘’Jammy!!!.. Jammy ndio wakunifanyia mie hivi, kumbe yote niliyofanyiwa ni kwasababu ya huyu shetani’’, Niliingia nakukaa siti ya nyuma kabisa huku nikiamini Gervas wala Jammy hawajaniona.
 
SEHEMU YA 50 .......... MWISHO


********



Ndani ya lisaa ndoa ilikuwa imekamilika huku wote Gervas na Jammy wakiwa wanavalishana pete zao, Niliumia sana moyo lakini ilikuwa haina jinsi, Tayari walikuwa wakitoka kwa mwendo wa taratibu tena wa maringo huku wakisindikizwa kwa matarumbeta, kelele za watu, vigelegele na vifijo vikiambatana na miruzi ndizo zilinikera sana katika fikra zangu nakujikuta nikisimama kwenye lango la kutokea huku wote wakishangaa,
Kama mjeshi vile pale pale nikawa nimeshaikoki ile bastola yangu na kuwalenga vichwani mwao risasi mbili tu kisha wote Gervas na Jammy wakadondoka chini na kufariki papo hapo, sikusikia tena mlio wa matarumbeta watu wote walibaki kimya na muda huu Omari alikuwa akinifuata lakini aliponikaribia nikamfyatua risasi ya usoni akadondoka, Watu wote wakatawanyika kwa uwoga huku wakiniacha pale, tayari mapolisi walikuwa karibu yangu nikaichukuwa ile bastola na kuielekeza kichwani mwangu ili nijiue lakini bahati mbaya ilikuwa imeshaisha risasi, hivyo nikanyong'onyea na kudondoka chini.



********


Watu takribani ishrini huku wengine wakitanda kwenye madirisha walikuwa wakinishangaa, nilizinduka nakujikuta nipo hospitali nisiyoifaiamu huku mkono wangu mmoja ukiwa na pingu iliyoshikana na kitanda na mkono mwingine ukiwa na dripu na upande wa mguu mmoja ulishikana na kitanda hivyo sikuweza kwenda popote mapolisi walikuwa wamenizingira, sauti ya yule Mama niliokuwa nakaa naye ndio ilikuwa inalia sana tena kwa nguvu.
‘’umefanyaje tena Levina.. Ona sasa Levina unaenda tena gerezani’’
‘’Mama yote ameyataka Gervas. Mama sitaki tena kuishi Duniani ni bora nife Mama’’
Nililia sana ghafla nikashangaa Polisi wanasogea pembeni kisha wakatokea watu kama watatu.
‘’Bosi nisamehe jamani, Happy na Mnama mnisamehe nakufa mie jamani’’
Sikuwa na jinsi tena kwani ni kweli bosi na Happy na dereva wao Mnama kutoka Zambia walikuwa tayari wapo Hospitalini na sijui hata ni nani aliyewapa taarifa.
‘’Huyu si wakumtibia hapa tunapoteza muda tu.. Apelekwe Gerezani tu moja kwa moja’’
‘’ngoja tusikie ushauri kutoka kwa Dokta kwani ana mimba ya miezi miwili’’
Walikuwa mapolisi wakisemezana kuhusu mimba yangu.
‘’Sirudi tena jamani, sitauwa tena, sitaki tena… Sitaki tena. Ni bora nife tu sasa hivi..’’
Nilikuwa na jazba sana mpaka nikachomoa ile dripu lakini sikuweza kufurukuta kutokana na zile pingu zilizoshikana na kitanda, nilishangaa napigwa vibao na maaskari huku Happy akiwa mmoja wapo kunirushia mateke.

MWISHO
 
SEHEMU YA 50 .......... MWISHO


********



Ndani ya lisaa ndoa ilikuwa imekamilika huku wote Gervas na Jammy wakiwa wanavalishana pete zao, Niliumia sana moyo lakini ilikuwa haina jinsi, Tayari walikuwa wakitoka kwa mwendo wa taratibu tena wa maringo huku wakisindikizwa kwa matarumbeta, kelele za watu, vigelegele na vifijo vikiambatana na miruzi ndizo zilinikera sana katika fikra zangu nakujikuta nikisimama kwenye lango la kutokea huku wote wakishangaa,
Kama mjeshi vile pale pale nikawa nimeshaikoki ile bastola yangu na kuwalenga vichwani mwao risasi mbili tu kisha wote Gervas na Jammy wakadondoka chini na kufariki papo hapo, sikusikia tena mlio wa matarumbeta watu wote walibaki kimya na muda huu Omari alikuwa akinifuata lakini aliponikaribia nikamfyatua risasi ya usoni akadondoka, Watu wote wakatawanyika kwa uwoga huku wakiniacha pale, tayari mapolisi walikuwa karibu yangu nikaichukuwa ile bastola na kuielekeza kichwani mwangu ili nijiue lakini bahati mbaya ilikuwa imeshaisha risasi, hivyo nikanyong'onyea na kudondoka chini.



********


Watu takribani ishrini huku wengine wakitanda kwenye madirisha walikuwa wakinishangaa, nilizinduka nakujikuta nipo hospitali nisiyoifaiamu huku mkono wangu mmoja ukiwa na pingu iliyoshikana na kitanda na mkono mwingine ukiwa na dripu na upande wa mguu mmoja ulishikana na kitanda hivyo sikuweza kwenda popote mapolisi walikuwa wamenizingira, sauti ya yule Mama niliokuwa nakaa naye ndio ilikuwa inalia sana tena kwa nguvu.
‘’umefanyaje tena Levina.. Ona sasa Levina unaenda tena gerezani’’
‘’Mama yote ameyataka Gervas. Mama sitaki tena kuishi Duniani ni bora nife Mama’’
Nililia sana ghafla nikashangaa Polisi wanasogea pembeni kisha wakatokea watu kama watatu.
‘’Bosi nisamehe jamani, Happy na Mnama mnisamehe nakufa mie jamani’’
Sikuwa na jinsi tena kwani ni kweli bosi na Happy na dereva wao Mnama kutoka Zambia walikuwa tayari wapo Hospitalini na sijui hata ni nani aliyewapa taarifa.
‘’Huyu si wakumtibia hapa tunapoteza muda tu.. Apelekwe Gerezani tu moja kwa moja’’
‘’ngoja tusikie ushauri kutoka kwa Dokta kwani ana mimba ya miezi miwili’’
Walikuwa mapolisi wakisemezana kuhusu mimba yangu.
‘’Sirudi tena jamani, sitauwa tena, sitaki tena… Sitaki tena. Ni bora nife tu sasa hivi..’’
Nilikuwa na jazba sana mpaka nikachomoa ile dripu lakini sikuweza kufurukuta kutokana na zile pingu zilizoshikana na kitanda, nilishangaa napigwa vibao na maaskari huku Happy akiwa mmoja wapo kunirushia mateke.

MWISHO

Bonge la story ... Safi sana...

Chapter Closed...



Cc: mahondaw
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom