STORY: Sitaki Tena

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
3,983
10,804
STORY: SITAKI TENA
MTUNZI: ANDREW CARLOS
IMELETWA KWENU NA: BURE SERIES

SEASON 1
SEHEMU YA 1


Nakumbuka Levina mimi nilikuwa na miaka 12,wazazi wangu walikuwa wakinipenda sana na walipenda kuniacha huru hata pale ninapokuwa nacheza na rafiki zangu michezo mbalimbali, nilikuwa napenda sana kucheza michezo tofauti na wenzangu c unajua tena utoto,na mchezo mkubwa niliokuwa naupenda ni huu wa rede (ule wa kukwepa mpira unaporushiwa).

Siku hiyo nikiwa mimi na rafiki zangu tunacheza,sikuamini macho yangu na ni vigumu kuamini mpaka sasa kwa kile nilichotenda kwani badala ya kuuokota mpira nirushe kwa ile haraka niliyokuwa nayo ndani ya ule mchezo nilijikuta naokota jiwe bila kujitambua nilichokuwa nimeokota huku nikidhani kuwa ni mpira na kumrushia Jeni na kwa bahati mbaya lilimpata Jeni kichwani na kuzimia palepale.

Juhudi zilifanywa haraka haraka na majirani huku mimi nikiwa pembeni cijui cha kufanya mchozi ukinitiririka huku kijasho chembamba kikipenyeza katika paji la uso wangu kupitia shingoni huku lile jasho likichochea mkojo ulioanza kunitoka taratibu palepale huku nikitazama kinachoendelea.

"Panda na wewe twende.. Nimesema panda huko usikii.?"
Aliongea na mimi mama mmoja kwa ukali huku akinitolea mijicho kana kwamba labda alikuwa ni mtoto wake lakini haikuwa hivyo kwani alikuwa ni mpita njia aliyekuwa shuhuda wa lile tukio.

Nilipanda taksi pamoja na wale majirani iliyokuwa imekodiwa haraka kwa ajili ya kumkimbiza Jeni hospitali.. kadri tulivyokuwa tunakaribia hospitali ndivyo mapigo yangu ya moyo yalinienda kasi mithili ya yule mwanariadha wa jamaika anayeitwa 'Bolt'... Huku nikiomba miujiza yeyote itokee ili Jeni apone turudi nyumbani, niliendelea kulia tena kwa sauti ya juu huku kamasi likinitoka.. Tulipokaribia kufika hospitali nilisikia mama mmoja aliyekuwa pembeni yangu akimshikilia Jeni..akitikisa kichwa huku akimwambia dereva apunguze mwendo kwani haina haja tena kuwahi huku akimsisitizia kuwa mtu waliyekuwa wakimuwaisha ameshapoteza maisha.

"Jeni amekufaaa.. Amekufaaa.. Hapana.. hapana.. Mama yangu weeee...mama..baaabaaa uko
wapi jamanii mama yangu weee..."
Nikazidisha kupaza sauti kwa kulia niliposikia yale maneno..
Sikuweza kuamini kama kweli Jeni amekufa mpaka nilipoona tunaelekea mochwari ndipo nilipoamini Jeni alikuwa tayari keshapoteza maisha kutokana na kupoteza damu nyingi zilizokuwa zikimtoka eneo la kichwani na puani.
"Umeshaua..? Ndio umeuwa naongea na wewe kinyago uliyefanya makusudi haya..!”
Aliongea yule mama..

"Sijau.. Kabla sijamalizia kujibu nikashangaa napigwa kofi kubwa la usoni mpaka nikajihisi
kizunguzungu, huku akiendelea kuniambia..
“tena ishia hapohapo mwanaidhaya mkubwa wewe na tunakupeleka polisi moja kwa moja mbwa we ukaozee huko huko ndio utanyoka...!"

Taarifa za mimi kufanya lile tukio tena kwa bahati mbaya lilitawanyika Mtaani kote na hakuna hata mmoja aliyeweza kuamini kwani taarifa hata zilipofikiwa wazazi wangu nao hawakuweza kuamini kilichonitokea walikuja pale kituoni japo kunitoa kwa dhamana lakini ilishindikana kwani huwa hakuna dhamana kwa kesi yoyote ya mauaji.. Nilishiwa nguvu,na kulegea viungo vyote na kusababisha kupoteza fahamu kutokana na kukataliwa dhamana..
BAADA YA SIKU (NNE).4

Sikuweza kupata hata lepe la usingizi takribani siku mbili kutokana na kulia sana,kichwa kiliniuma sana..nakumbuka ilikuwa asubuhi na mapema pale askari alipotuamrisha tupande gari la polisi kutoka pale kituo kidogo cha polisi kurasini na kuelekea kituo kikubwa cha polisi pale MSIMBAZI KARIAKOO.. Safari ilianzia kituo kidogo cha Kurasini nilipokuwa nimechanganywa na wenzangu niliowajua pale pale na wao waliletwa pale kwa makosa tofauti tofauti, huku tukikatiza Sheli ya BP mpaka raundi about ya Kamata,sehemu zote tulizopita bado machozi yalikuwa yakinitoka huku yakiandamana na mafua Makali yalionipata pale kurasini kituoni, kwikwi ilibana sana na haikuwa kwasababu ya kiu ya maji bali ilikuwa ni kwikwi ya kulia kwa mda mrefu.

"Embu nyamaza hukoo.. Haupo kwa baba yako wala mama yako..Tena unyamaze..??”
Aliongea kwa hasira askari mmoja alioonesha kukasirishwa na kitendo changu cha kulia mda
mrefu bila kunyamaza.

"Hivi we mtoto husikii..? Kwani sisi ndo tumekutumauue..?" aliendelea kunikalipia yule
askari. Mpaka tunaingia pale kituoni MSIMBAZI macho yalikuwa mekundu na yamenivimba sana huku sauti ikinikauka kutokana na kulia kwa mda mrefu..

* *

Tukiwa katika basi lenye namba PT 10319 ambalo lilikuwa likikatisha mitaa ya kariakoo likiwa linatokea kituo kikubwa MSIMBAZI huku nikiwa katika orodha ya mahabusu waliokuwa wamewekwa pale MSIMBAZI kituoni kuelekea mahakama kuu pale KISUTU kwa ajili ya kusikilizwa kesi yangu kwa mara ya kwanza. kila moja wetu akiwa amefungwa pingu mikononi.

nywele pamoja na nguo zangu zilikuwa chafu sana kutokana na uchafu wa pale kituo cha Kurasini na msimbazi. Huku basi la polisi likiwa linakata kona ya kuingia mahakamani, nikiangaza huku na huku labda naweza kumuona hata mama au baba,ghafla nikamuona mama kajifunika kanga upande mmoja wa paji la uso wake kuashiria kuwa alikuwa ameumia upande mmoja wa uso wake,nilijikuta nikipigwa na afande.

"Embu tembea hukoo... Unashangaa shangaa nini? Kwani hujui kama hapa ni mahakamani?"
Tukiwa mstari mmoja tulishuka na kuelekea kwenye vyumba ila mimi niliingizwa chumba maalumu kilichoandikwa maneno makubwa mlango wa kuingilia "CRIMINAL ONLY" kwa haraka haraka sikuweza kutambua lile neno linamaana gani kwakuwa ndo kwanza nilikuwa niko form one ila niliweza kuambulia neno moja tu lililoandikwa "ONLY" kwani nilipenda sana kuangalia ile tamthiliya ya kifilipino iliyokuwa inaitwa 'only you' nikijua inamaanisha 'Wewe Pekee..'sikuwa mbali na fikra zangu kwani kile chumba kilikuwa peke yake kwa ajili ya kesi za mauaji kama yangu ndo huwa zinasomwa hapa.

Nikiwa na mawakili wangu nisiowafahamu ila niliamini tu baba ndo aliwatafuta kwani alikuwa akiongea nao kabla sijaingia mule ndani. Chumba kilikuwa kidogo sana na watu walimiminika wakiwa ni pamoja na majirani,ndugu na marafiki huku kesi ikitaka kuanzwa kusomwa niligeuka nyuma nikajikuta nakutana jicho na mama mmoja..kwa hasira na jazba niliokuwa nayo nikajikuta Natoa fyonyo kali na la kupaza sauti ya juu..Wote mle ndani wakawa kimya ghafla wakinitazama, "xé@shh.. Mbea mkubwa we..!”
Kisha nikamtemea mate huku hasira zikinipanda kutokea miguuni kuelekea kichwani na mikononi, nilijikuta nataka kumpiga lakini mikono yangu ilikuwa na pingu hivyo hasira ikazidi mara mbili huku nikihema kwa kasi ikiambatana na makamasi yaliokuwa yakinichilizika mithili ya umande unapokutana na majimaji au konokona anapokuwa anaachia kofia yake..nikanyanyua Mguu wangu wa kulia tayari kwa kumtupia mateke yule mtu..nikawa tayari nimeshathibitiwa..

Hakuwa mwingine bali alikuwa ni yule mama tuliepanda naye taksi kumuwaisha Jeni hospitali yule aliyekuwa akinisema ovyo kwenye gari pia ndo alienipeleka Kunikabidhi polisi..nikiwa naendelea kumtolea macho huku nimekunja uso wangu kwa hasira mithili ya bi kidude akiwa jukwaani anaimba.. nilijikuta napokea vibao c kutoka kwa yule
mama bali alikuwa ni askari aliyekuwa akifuatilia tukio mule ndani., "Hata kesi haijaanza umeanza kuonyesha we nunda eenh... hatimaye hakimu aliingia Na lazima utaozea jela tu wewe.." Maneno yale yalivuta hisia nyingi sana ndani ya kichwa changu,mwili ulininyong'onyea ghafla,niakanza kutetemeka japo nilikuwa mdogo kiumri lakini nikawa tayari nimeshakomaa kifikra na pia jasiri ndani ya mda mfupi.

36498_255276594603677_879737111_n.jpg
 
SEHEMU YA 2

Usiku ule tangu nirudishwe tena rumande kwangu haukuwa mzuri,akili na viungo vya mwili wangu vilikuwa vimechoka sana, yote hiyo ni kutokana na kulia na kupigwa pigwa,sikuweza kupata hata chembe usingizi kila nilipofikiria kilichonikuta. . "Hivi kweki nimeua..? Mimi nimeua.? Miiiimi..? Hilo ndo swali nililojikuta najiuliza usiku kutwa bila kupata majibu,nilitamani nishuhudie Jeni akizikwa pengine labda ndo ningeshawishika na kuamini kama kweli nimeua lakini hiyo haikuwezekana, hakika usiku ulikuwa mrefu sana kwangu,mawazo mengi yalikuwa tayari yameshatawala kichwa changu pengine hata umri wangu haukuniruhusu kufikiri sana lakini tayar nikawa na fikra tena za kikubwa zaidi kwa mda mfupi tu tangu niwekwe rumande..

Sauti za bundi,popo na mbwa ndizo zilikuwa zinapaa sana kuzunguka huku na kule katika lile eneo la kituoni, wenzangu walikuwa wamelala fofo hawajielewi hiyo yote ni kutokana na shuruba shuruba za humu ndani, Mpaka ilipotimia saa 9 za usiku usingizi ukawa Tayari umeshanipitia lakini kimoja kilichokuja kunishtua ni kaubaridi kalikokuwa kakipenyeza ndani ya gauni nililokuwa nimevaa, huku miköno yangu miwili ndio ilikuwa mto,mwili wote ulikuwa ukinitetemeka mithili kifaranga cha kuku kikinyeshewa na mvua,kifupi palikuwa na baridi sana nadhani ni kwasababu sakafu ndo ilikuwa kitanda changu.. Taaratibu nilianza kujihisi kama kuna kitu kinanipapasa kupitia mapajani mwangu..lakini sikuwa na wasiwasi kwani nilijiamini sana kuwa tupo wanawake tu na kama askari ndo walikuwa mchanganyiko wakiume kwa wakike..kila mda ulivyokuwa unasogea ndivyo hisia zikawa zinabadilika ndani ya kichwa changu kwani niliweza kulifungua jicho langu La upande wa kushoto kuangaza huku na huku kujua kitu gani kinachonipapasa ghafla.. "Shhh... nyamaza...!

Na ole wako ufungua domo lako.?" ilikuwa ni sauti ya askari wa kike niliyekuwa nikimfahamu kwa sura,alikuwa kanishika mapaja yangu kwa nguvu huku akiwaambia askar wenzake ambao walikuwa wakiume wafanye haraka haraka., Moyo ulinipasuka,nguvu ziliniisha,hasira zilinikaa ghafla huku nikikosa pumzi kutokana na kuzibwa mdomo kwa mda mrefu.. hatimaye wale askari waliokuwa takribani watatu walifanikiwa kuniingilia tena kwa nguvu kwa takriban nusu saa pale huku wakiniacha damu nyingi zikinitiririka.. BAADA YA MWEZI Hatimaye upelelezi ukawa umeshakamilika na nilikuwa tayari niko kizimbani..nywele zilikuwa hazitamaniki,miguuni sikuwa hata nandala,mavazi nayo yakawa yameshachoka na kuchafuka kwani toka mwezi ule nibakwe Levina mimi ckuwa hata na nguo nyingine ya kubadilisha,nao mwili ulikuwa tayari umeshadhohofika kutokana na msosi mbaya tuliokuwa tunapewa hakika yalikuwa ni mateso makubwa na si jambo dogo akilini kwangu.. Kama kawaida ya kesi nyingine nadhani hii ni kutokana na shauku iliowataka watu wajue ni nini kitakachofuatia katika kesi yangu kwani umati mkubwa sana wa watu ulikuwepo ukishuhudia kiasi cha kunifanya moyo wangu ulipuke kwa huzuni.. Huku macho yangu yakiangaza huku na kule ghafla nilifanikiwa kumuona baba na safari hii hakuwa na mawakili kama ambavyo ningetegemea bali alikuwa kakalia kibaiskeli cha kupakia wagonjwa walemavu wa miguu huku akikokotwa na dada aliyekuwa amevalia mavazi meupe wazo lilinijie paleple na kugundua kuwa ni lazima atakuwa ni nesi.. "lakini kwanini amekuwa vile..? Au atakuwa amepooza nin?..."

nilijiuliza mengi kichwani bila kupata majibu.. Mda wa kuanza kusoma kesi yangu ulifika,pande zote mbili zilikutana ikiwa ni pamoja na mashahidi wa pande zote mbili.. "wewe ndio binti Levina..? Ndio mimi.. Unakumbuka mnamo tarehe 1 mwezi wa 2 mwaka 2009 ulifanya kosa... Nakumbuka.. Uliweza kuua tena kwa kukusudia..? Ndio.." hayo ndiyo maswali niliokuwa naulizwa na kuyajibu.. Hatimaye yalikusanywa maswali na majibu yote kuashiria kesi imeeleweka na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.., "Mwanangu...! mwanangu..! Kweli unafungwa mwananguu..?" hayo yalikuwa maneno ya mwisho kwa mama yaliyofanya na watu wengine waachie vilio pale pale huku nikibakiwa na roho ya kishujaa na kijasiri bila hata kutoka mchozi.. BAADA YA MIAKA 5 Vurugu zilizokuwa zinaendelea katika Gereza la kufungwa watoto watukutu lililopo mbeya, Ndizo zilizosababisha watoto wengi kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa maisha kutokana na mgomo waliokuwa wameuanzisha kutokana nakupewa chakula kidogo sana tena kichafu,milipuko ya magonjwa kama kipindupindu,msongamano wa wafungwa kiasi cha wengine kufariki kwa kukosa hewa wakati wa kulala usiku..

Namba CG.016/007369, ndiyo namba iliyokuwa inasomeka katika sare yangu ya Gerezani ., Tayari maisha nlikuwa nimeshayazoea mule gerezani,taarifa kutoka nyumbani nilikuwa nikiletewa na afande mmoja ambaye tayari nilimzoea na hata kuanzia siku ile nilipo hukumiwa pale mahakaman hali ya baba yangu kiafya haikuwa nzuri na hakukaa mda mrefu akawa amepoteza maisha, Mwenyezi mungu amlaze pahala pema peponi.. Na sasa mama ndio mzazi wangu pekee aliyebaki hata kama nitatoka gerezani... ucheshi, ufanyaji kazi kwa nguvu,bidii na kujituma zaidi ndicho kitu kilichokuwa kikiwavutia maaskari wengi pale kiasi kwamba nikapendwa sana na kuaminika.. "Levinaaa... Levinaaa.. ...Wewe Levina Christian?..

Aliniita askari wa zamu lakini sikuweza kumsikia vizuri kwa sababu ya makelele ya wenzangu waliokuwa wakipigana mule ndani.. "Abeee afande..nilimuitikia" "Embu fanya haraka kuna mgeni wako kaja kukutembelea fanya ukamuone.." "Sawa afande..." Mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio,lakini halmashauri ya kichwa changu iliweza kupambanua haraka haraka na kujua atakuwa ni mama tu... "Lakiiini...mbona afande hakuniambia kama ni mama au la! Maana mama yangu anamjua angeniambia tu?" ndio maswali niliokuwa najiuliza nikiwa njiani kuelekea chumba cha wageni.. Ghafla...
 
SEHEMU YA 3

BAADA YA MIAKA 5 Vurugu zilizokuwa zinaendelea katika Gereza la kufungwa watoto watukutu lililopo mbeya, Ndizo zilizosababisha watoto wengi kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa maisha kutokana na mgomo waliokuwa wameuanzisha kutokana nakupewa chakula kidogo sana tena kichafu,milipuko ya magonjwa kama kipindupindu,msongamano wa wafungwa kiasi cha wengine kufariki kwa kukosa hewa wakati wa kulala usiku.. Namba CG.016/007369, ndiyo namba iliyokuwa inasomeka katika sare yangu ya Gerezani .,

Tayari maisha nlikuwa nimeshayazoea mule gerezani,taarifa kutoka nyumbani nilikuwa nikiletewa na afande mmoja ambaye tayari nilimzoea na hata kuanzia siku ile nilipo hukumiwa pale mahakaman hali ya baba yangu kiafya haikuwa nzuri na hakukaa mda mrefu akawa amepoteza maisha, Mwenyezi mungu amlaze pahala pema peponi.. Na sasa mama ndio mzazi wangu pekee aliyebaki hata kama nitatoka gerezani... ucheshi, ufanyaji kazi kwa nguvu,bidii na kujituma zaidi ndicho kitu kilichokuwa kikiwavutia maaskari wengi pale kiasi kwamba nikapendwa sana na kuaminika.. "Levinaaa... Levinaaa.. ...Wewe Levina Christian?.. Aliniita askari wa zamu lakini sikuweza kumsikia vizuri kwa sababu ya makelele ya wenzangu waliokuwa wakipigana mule ndani.. "Abeee afande..nilimuitikia" "Embu fanya haraka kuna mgeni wako kaja kukutembelea fanya ukamuone.." "Sawa afande..." Mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio,lakini halmashauri ya kichwa changu iliweza kupambanua haraka haraka na kujua atakuwa ni mama tu... "Lakiiini...mbona afande hakuniambia kama ni mama au la! Maana mama yangu anamjua angeniambia tu?" ndio maswali niliokuwa najiuliza nikiwa njiani kuelekea chumba cha wageni.. Ghafla... "Sasa mbona simuoni mgeni wangu?.." nilijikuta namgeukia yule afande aliyekuja kuniita na kuniambia kuwa nina mgeni.. "Umeanza kisilani chako enhee..? Au unataka ukalime heka tatu peke yako sa hivi...?

" enhee..! Nikabaki kimya huku nikiendelea kumtolea macho ya ukali yule askari ambaye alikuwa anajulikana 'Jesca Tester' kutokana na kuwa mkorofi kwa wafungwa wabishi hata kipindi kingine huwa anakorofishana na maaskari wenzake.. "Si naongea na wewe kinyamkera...? Haya na huyu hapa ni mgeni wa nani sasa..?" Nikajinyamazia kimya huku nikikaa katika kajidirisha cha kuongea na wageni..nikimuacha yule askari akiendelea kubwabwaja pale.. "Na Nakupa dakika kumi tu uwe umeshamalizana naye na upotee hapa,sawa..?" "Sawa mkuu nimekuelewa..!" nilimjibu kwa heshima huku nikianza mazungumzo na yule mgeni wangu pale.. GERVAS; Sijui umeshanikumbuka..?" LEVINA; Hapana.. GERVAS; "Naitwa Gervas Phota..Tumeishi wote kurasini na kuchez..." kabla hajamalizia kuongea tayari akili yangu ilishaweza kuchambua fasta na kumjua.. LEVINA; we si mtoto wa mzee Phota pale jirani na nyumbani kwetu.? GERVAS; Haswaaa..! Ndiye mimi kumbuka tulikuwa wadogo sana lakini kwa bahati mbaya sikuweza kuwepo kuanzia siku ya tukio,kipindi cha kesi yako mpaka leo kwa sababu nilipelekwa shule mapema mno..

LEVINA; Usijali Gervas yote hayo nimaisha namshukuru mwenyez mungu mpaka nilipofikia hapa kwani nimebakiza miaka sita tu niwe huru.. "Mda umekwisha..haya we Levina inuke uwafate wenzako shambani..inuka" aliongea yule askari Jesca ambaye mda wote alikuwa akitusimamia.. Haraka haraka nilimuona Gervas akitoa kijimfuko kilichoashiria kina nguo.,kisha akatoa noti ya shilingi elfu kumi akanipatia kisha yule askari akampa shilingi elfu tatu kisha akaniaga na kuniahidi kuwa atakuwa akinitembelea mara kwa mara... Siku hiyo sikuweza kupata hata lepe la usingizi kwani nilijihisi tayari nipo nyumbani kwa zile nguo nilizoletewa na Gervas nilijikuta machozi yakinitoka japokuwa yalikuwa ni machozi ya furaha, Ikawa haipiti mwezi lazima Gervas aje kunitembelea na kuniachia japo chochote, hivyo nikaamini kuwa mtetezi wa maisha yangu ni Gervas na mama yangu pekee japo tangu nilipoletwa huku gerezan hajawah kuniona,moyo wa upendo taaratibu ulianza kunijia kwani hakukuwa na mtu aliyejionesha kunijali kama Gervas.. BAADA YA MIAKA 2 Nakumbuka siku hiyo Gervas alikuja kunitembelea lakini safari hii alionekana kuwa tofauti na siku nyingine kwani alikuja na furaha ambayo sikuitegemea na hakuweza kukaa sana ila akachukuwa mkono wake wakati ananiaga alipoachia nilihisi itakuwa kama kawaida yake ya kuniachia pesa lakini haikuwa pesa ila ilikuwa ni kijikaratasi kilichokuwa na ujumbe..

Niliagana na Gervas kisha nikaenda kutafuta eneo lililokuwa tulivu,taaratibu nikaanza kufungua ile karatasi ghafla moyo ukanilipuka, "Mpendwa Levina,natumai u mzima afya kwani mara nyingi huwa tunaonana., Nashukuru mwenyezi mungu mpaka hapa tulipofikia kwani umenifanya nijue mengi yanayotendeka humu ndani kwa kifupi nimejuana na kuzooena na maaskari wengi hapa, Levina mim na wew tumetoka mbali na sitapenda nikuache uendelee kuteseka hapo gerezani, Mwezi huu Rais atatoa msamaha ikiwa ni pamoja na gereza lenu lakini msamaha wenyewe utalenga wale wenye ulemavu nilichokifanya ni.. Kabla sijamalizia kusoma alitokea afande Jesca Tester na kunifokea.. "Hivi wewe Levina mda wote umekaa hapo umewakimbia wenzako kule,unafanya nini?" "Nika kaa kimya".. aliendelea kuongea afande kwa sauti ya ukali.. "Na kwanini umekuja kujitenga peke yako huku?" "Nisamehe afande sitarudia tena..wakati namjibu ghafla kile kikaratasi kikadondoka chini.. "Haya lete hicho ulichoangusha..Letee..!
 
SEHEMU YA 4
Nilijikuta nachukua kile kikaratasi na kumpatia afande Jesca nikiamini kuwa hajui kusoma kwani huwa mara nyingi akitumiwa ujumbe kwenye simu yake huwa ananitafuta nimsomee.. Alikichukuwa kile kikaratasi akakigeuza geuza kisha akanirudishia.. "Acha upuuzi wako nenda kwa wenzako sawa?" "Sawa" nilimuitikia lakini kishingo upande huku akili yangu ikinituma nielekee chooni nikakimalizie kukisoma,taratibu nikaongoza hadi chooni nikakifungua kwenye gauni kilipokuwa na kumalizia kukisoma, enhe ikawaje vilee., "lakini msamaha wenyewe utalenga wale wenye ulemavu nilichokifanya ni kutoa ada yangu yote niliyotumiwa shilingi laki mbili na kuwaonga polisi kisha wakalipitisha jina lako kwenye orodha ya watakao kuwa huru" Hapohapo nikakichukuwa Kile kijikaratasi na kukichana chana kisha nikakitupia katika tundu la choo,nikitoka na furaha ya hali ya juu huku nikijiona mshindi,

BAADA YA WIKI MOJA Ikiwa ni asubuhi na mapema tukiwa tumejipanga mstari halmashauri ya kichwa changu kikawa kimeshafanya kazi nakutambua ni kitu gani kilituleta katika eneo lile., Kama kawaida ya afande kimbele mbele afande Jesca alikuwa tayar akiwanyosha watu mistari huku akiwapiga na kuwafokea wale waliojifanya ni wabishi, Tayari maafande takribani nane walikuwa mbele yetu huku mkuu wa gereza akiwa kashikilia karatasi bila kuchelewesha mda akaongea kilichotuleta eneo lile na kuanza kutuita majina naweza kusema sikuamini kilichotokea kuwa kama ndoto kwani ni kweli na mimi nilikuwa katika ile orodha ya walioachwa huru, "nashndwa kujua nimfanyie nini huyu kaka 'Gervas'.. Gervas...! Gervas...! Nakupenda na Nitazidi kupenda daima" nilijisemea kimoyomoyo huku nikipiga ishara ya msalaba na kukusanyika na wenzangu huku tukitokea lango kuu, **** Gari aina ya Land Rover yenye namba T643 ABK iliyokuwa imebeba magunia ya mpunga kutoka Tunduma kuelekea Dar es salaam huku ikiwa imepakiza abiria wa nne tu,wawili wa kiume na wawili wa kike.. nikiwamo katika hilo gari kwa mwendo wa taratibu huku nikiwa na mawazo mengi yalionijaa akilini mwangu ikiwa ni pamoja na hofu juu ya safari kama tutafika salama, mda huo ilikuwa imeshatimia saa 2 usiku,tulikuwa tunakaribia kufika Iringa., mawazo gongana yaliniandama ndani ya kichwa changu hasa kwa kuzingatia kuwa bado nilikuwa sijajiamini kwa kile kilichonitokea kama kweli niko huru ama la.!

Huku nikiendelea kuwa katika dimbwi la mawazo usingizi ukanipitia. "Lete Jeki fasta...waambie na hao wadada washuke huko..!" sauti ya dereva wa ile gari akiongea na mwenzake ndiyo ilinishtua sana kwani gari lilikuwa limeharibika kilomita chache kabla hatujaingia Iringa.. Baridi lilikuwa kali sana,nilihisi kama mwili umeganda sikuwa na nguo yoyote ya kubadilisha,hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kujilaza pembeni ya lile gari huku nikitetemeka mdomo na meno yakiumana kama nimepigwa ganzi.. Nikiwa pale chini natafuta tena usingizi huku dereva akiendelea kutengeneza lile gari., kwa mbaaali niliona mwanga mkubwa ukitumulika huku unasogea taaratibu, akili yangu na wale wenzangu haikuwa mbali kwani lilikuwa ni gari lakini ilipofika karibu yetu dereva wetu akawa ameipungia mkono isimame kwa ajili ya kuomba spana.. ilisimama kisha wakashuka wanaume watano waliokuwa wamevalia makoti meusi huku mikononi wameshika panga na bunduki wakitufuata eneo tulilokuwa.. "Wote mikono juu" Na ole wake mtu asimame au aongee hata neno moja.." aliongea mmoja wa wale wanaume aliekuwa anasura ya kikomavu iliyojikunja kunja mithili ya mchekeshaji wanaomwita 'King'wendu', huku kavalia miwani meusi na mdomoni akivuta sigara na kutupulizia moshi..tukiwa bado tupo pale chini tukitetemeka na kuogopa pia tulikuwa kama tumeshajitolea kwa lolote litakalotupata..

Ghafla milio ya risasi ikaanza kurindima kuelekea kwenye matairi ya lile gari letu yakapasuka yote manne kisha wakamchukuwa dereva na wenzake wakawachinja mbele ya macho yangu kisha wakaondoka na kuniacha na mwenzangu niliyetokanaye gerezan, Roho ya Ujasiri,ukatili na ukakamavu niliokuwa nayo toka nipo kifungoni ilinisaidia sana kwani sikuogopa hata kidogo kilichonitokea mda mfupi uliopita nilimchukuwa mwenzangu na kutokomea naye msituni.. Nikiwa nimemshika mkono mwenzangu Pendo tulikuwa tayari tumeingia msitu wa Ruaha ambao kiukweli ulikuwa ni mkubwa sana na uliojaa na miti mirefu,hatukuweza kuogopa kitu kwani maisha ya gerezani yalikuwa tosha kwa mimi na Pendo kuwa wajasiri,wakatili na wakakamavu mda wote, "Nimechoka.,nimechoka siwezi kuendelea tena Pendo..tupumzike hapa.." Nilimwambia pendo huku nahema nikitokwa jasho usoni kwa mwendo tuliokuwa tunatembea haraka haraka hakika ulikuwa ni mwendo mrefu sana., "Sasa ukiendelea kudeka deka mi nakuacha, au unapenda kubakia hapa porini?" alisema Pendo kwa ukali kudhihirisha kuwa alikua amechoshwa na kitendo cha mimi kupumzika.,Nilijikaza na kuinuka tayari kwa kuendelea na safari lakini.. "Pendo.! Pendo.! Mama yangu wee mguu wangu..! Nilijikuta namuita Pendo asiondoke kwani mguu wangu kwa upande wa nyuma ulikuwa umeshachanika na damu nyingi zilikuwa zikinitiririka., Pendo hakuwa na jinsi kwani aliona kubaki na mimi katika ule msitu kungemchelewesha kufika kwao kwani safari yake ilikuwa inaishia Dodoma., "Pendo..! pendo..

! Usiniache pendo..! ntabaki na nani tena Pendo..!" aliniacha nikiwa katika hali mbaya huku machozi yakinitoka,na kukata tamaa,nakuona bora ningemsubiri Gervas aje kunichukuwa.,ulikuwa tayari ni usiku sana nahisi ilikuwa imetimia kwenye saa nane au tisa kwani giza tororo ndilo lilitawala sana, Nikiwa bado katika dimbwi la mawazo na hasira nyingi pale chini huku milio ya wanyama wakali ikipaza huku na kule, Ghafla nikaanza kusikia mshindo wa kitu kama kinakuja tena kwa kasi ya ajabu, kadri mlio ulivyokuwa unazidi kuwa mkubwa mapigo yangu ya moyo yalizidi kunipelekesha.nilihema mpaka nikajihisi nimeishiwa pumzi sikuwa na lakufanya zaidi ya kujitoa kwa lolote litakalonipata kutokana na mguu kuumia vibaya kutokana na kujiumiza na kipande cha bati kwenye gari wakati tunakimbia kujiepusha na yale majambazi waliotuteka kulee.. Hatimaye nikaanza kutambua kitu kilichokuwa kinakuja kwani mwanzoni nilijua labda atakuwa Pendo amerudi kuja kunichukuwa lakini haikuwa hivyo kwani alikuwa mnyama mkubwa mweusi aliyefanania na nyati ila alikuwa akija kwa mwendo wa taratibu huku akinifuata katika eneo nililokuwa nimekaa..mwili ulinitetemeka sana hofu kubwa ilitanda ndan ya kichwa changu,nilitetemeka sana huku mchozi ukiwa unanitoka ukiambatana na mkojo kwa kasi,maumivu ya ule mguu yakatoweka kutokana na kile kilichokuwa mbele yangu.. "jamani..! jamani..! jamani..! Nisaidieni nakufaa..! nakufaa..!" Nikiwa bado nalia pale ghafla..
 
SEHEMU YA 5
Ilipoishia., "jamani..! jamani..! jamani..! Nisaidieni nakufaa..! nakufaa..!" Nikiwa bado nalia pale ghafla.. Endelea., Ghafla nikamulikwa mwanga mkubwa nikaangaza huku na huku nikaweza kuwaona watu wakiwa wamenizunguka.. "Wewe ni nani.? Na unafanya nini hapa?" aliongea mmoja wa watu wale waliokuja pale nilipokuwa baada ya kupiga makelele kwa kuona mnyama akinifuata kumbe hakuwa mnyama wa kunidhulu bali alikuwa ni ng'ombe aliyechelewa kuingizwa bandani na katika lile eneo walikuwapo wanaishi watu.,

"Naitwa Levina nimetokea mbeya ila gari yetu ilipata ajali tukawa tumevamiwa na majambazi hivyo nikaamua nikimbilie huku msituni..kwani hapa ni wapi?" niliwajibu hapo hapo huku nikishusha pumzi na kuwauliza swali bila hata ya kuonyesha woga wa aina yoyote, "Hapa ni kijiji cha LIAMKENA tupo katikati na hili pori la msitu wa Ruaha., Haya mbebeni tumpeleke nyumbani na wewe John swaga huyo ng'ombe turudini nyumbani" aliamrisha mmoja wao kwa sauti ya juu., Safari ya kutoka katika ule msitu mpaka kuingia katika kijiji cha 'Liamkena' usiku wa manane ilifanikiwa kwani nilipofika tu wakaanza kunitibia kidonda changu kwa kutumia dawa za kienyeji huku wanakijiji wengine kutoka katika kijiji kile wakija kunishangaa si kwakuwa nilikuwa natisha bali walistaajabu kuokotwa usiku wa manane kwenye ule msitu ulioaminika kuwa na wanyama wakali tena wengi, Ndani ya siku mbili nikawa tayari nimeshazoea mazingira uku akili yangu nashauku kubwa nikiielekezea nyumbani na jinsi gani ntampata Gervas na kumshukuru kwa yote aliyonitendea.,

Hali ya kidonda changu haikuwa mbaya kwani kilianza kufunga taratibu, ila wanakijiji walipenda niendelee kubaki mpaka nipone kabisa jambo ambalo lilipingana na halmashauri ya kichwa changu, Ilipofika saa tano usiku huku kijiji chote kikiwa kimerindima kwa giza nene,sikuwa na hata chembe ya usingizi, jicho langu liliweza kupenyeza kupitia katundu kadogo kadirisha kalichokuwa kametengenezwa kwa kutumia miti, niliweza kujua mara moja sehemu ya kutokea hivyo nikachana kipande cha gauni langu na kukifunga katika eneo lakidonda changu kisha nikachukuwa mishale na upinde huku upande wa kulia kwangu nikashikilia panga tayari kwa kuingia tena msituni huku nikitafuta barabara ya kutokea,nilifanikiwa kutoroka na kuingia msituni,akili yangu na mwili wangu vikawa kama vimeshapigwa ganzi kwani sikuwa muoga hata kidogo,nilitembea taratibu lakini nikaona kama nachelewa hivyo nikaanza kukimbia wakati nakimbia niliweza kusikia kama kuna watu wananikimbiza nyuma yangu kama sivyo basi ntakuwa nimeingia katika ulimwengu wa wanyama pori tena wale wakali nikasimama na kujificha nyuma ya mti kisha taratibu nikachomoa mshale japo nilikuwa sijui kuutumia lakini niliweza kuuelekezea upande wa ile sehemu niliyotoka na kuhisi kile kitu kitakuwa kinatokea upande huo, Niliunyosha na kufanikiwa kuuachia,nikasikia sauti ya kike.. "Nakufaa mama niokoe.. Ooh.! Uuh.! Uuh.!" ghafla ikafuatia mshindo kuashiria kile kitu kimeanguka chini baada ya kuachia mshale wangu wenye sumu kali, bila kuwa na woga kwa kunyemelea nikaanza kufata lile eneo kumtambua yule mtu, huku nikikaribia pale nimeshika panga langu akatokea fisi maeneo ya karibu nikamfyeka akawa amekufa,nikaendelea na zoezi langu la kutambua ni kitu gani kitakuwa mbele yangu, sikuwa na tochi,ila nilipoukaribia ule mwili niliupapasa lakini bado haikusaidia kumjua ni nani lakini ulikuwa ni mwili wa mtu pale chini ambao kwa namna moja au nyingine sikuweza kuutambua mara moja, kwa ushupavu wa halmashauri ya kichwa changu ikanituma nichukuwe panga na ku

Nichukuwe panga na kuchana kipande cha nguo yake,nikafanya hvyo kisha kile kitambaa nikakificha katika pindo la nguo yangu ya ndani halafu safari ikaendelea,nilikatiza msituni bila kuogopa kitu chochote na wala kumuogopa yeyote hatimaye baada ya kukimbia mda refu nikahisi kama kitu kigumu nakanyaga chini,furaha na amani vikaanza kutawala ndani ya moyo wangu kwani nilikuwa tayari nipo katika barabara ya lami,akili ikawa katika kukisia ni upande gani ndo utakuwa unaelekea Dar na upande gani utakuwa unarudi Mbeya,nikiwa bado natafakari likapita basi la kwanza,nikashindwa kulisimamisha nikaamua kusubiri gari nyingine,kwani sikuwa hata na nauli hvyo nikaamua nijifiche niweze kudandia gari lolote litakalopita kwa mwendo mdogo., Baada ya kukaa pale takribani lisaa moja na nusu bila ya kuona gari lolote hatimaye nikaliona gari kubwa likiwa linakuja kwa kujikongoja., "Kama kufa wacha nife tu.,lakini hili gari siliachi.." nilijisemea kimoyomoyo huku nikijiweka tayari kwa kurukia lile gari aina ya roli,huku mikuki na mishale pamoja na lile panga nikilitupia msituni,kitendo cha lile gari kufika karibu yangu kikawa kosa kubwa sana kwangu kwani ndani ya mda mchache nikawa tayari nipo nyuma ya lile lori lililokuwa limebeba mbao., Kwa ujasiri niliokuwa nao nikaingia mpaka mule ndani ya lile lori kwa nyuma ambapo sikumuona mtu yeyote kisha nikarudishia mlango na kujilaza kwenye zile mbao huku nikiwa sina uhakika na ninapoenda, "Sijui ndo litaishia morogoro au ndo la Iringa hili gari?" hayo ni kati ya maswali yaliyokuwa yameandama ndani ya kichwa changu,huku safari ikiendelea taratibu baada ya mwendo mrefu kidogo, ghafla gari likasimama kwa mbali nikahisi sauti ya watu wanajibizana kwa nje., "Hapana mkubwa mzigo wetu hauwezi kuzidi kiasi hicho" hapohapo jibu likanijia kuwa tutakuwa tumefika maeneo ya mizani,

"Embu fungua nyuma tuhakikishe maana tani zimezidi na kama hutaki paki pale gari yako uandikiwe faini" Wakiwa bado wanabishana pale tayari kwenye gari nikawa natetemeka mwili mzima huku nywele zikinisimama na akili ikinituma nifungue mlango, nikisema nijifiche nyuma ya mbao siwezi kwani ni kweli kulikuwa na mbao nyingi kiasi kwamba nilipata kanafasi kadogo sana ka kujificha, "Mungu saidia.! Mungu saidia.! Saidia jamani.!" Ndio maneno niliyokuwa naomba nisiweze kukamatwa kwani nia yangu nikufika Dar, Mda si mrefu nikaskia mungurumo wa gari kuwashwa kuashiria safari inaendelea moyo wangu ukawa na furaha upya nikajihisi ni mtu tofauti sana duniani tena aliye na bahati mbaya kupelekwa gerezani lakini aliyejawa na bahati nzuri uraiani, Nikiwa sina hata lepe la usingizi huku safari ikiendelea niliweza kushuhudia tena kwa mara nyingine kuki kuchwa kwani mwanga ulikuwa umeshatoka kuashiria kuwa ni alfajiri,gari nalo likatembea ka mwendo kidogo kisha likasimama, sauti na makelele ya watu ndio yalichochea hisia zangu,niliweza kutoa jicho langu kupenyeza kwenye kauwazi ka mlango nikaweza kushuhudia watu mbali mbali,moja kwa moja nikapata wazo la kuangalia kile kipande cha nguo nilichokikata kule kwa yule mtu msituni alikuwa ni nani, Taaratibu mkono wangu ukaanza kupenyeza mpaka kwenye upindo wa nguo yangu ya ndani nikakichukuwa kile kitambaa na kukiangalia., "Mamaa..! mamaa..! nimeuwa tena mungu wangu..! Nisamehe Pendo..! Sijakusudia mimi..! Maaaaa aaaaaaah..!"

Kumbe kile kilikuwa nikipande cha nguo cha rafiki yangu niliotokanaye gerezani 'Pendo'.. wakati nikiendelea kutoa sauti kali nikahisi kunawatu wamezisikia kelele zangu hivyo nikasikia mlango unafungulia eneo nililokuwa.., "Sauti inatokea humu ndani bwana, tena ni sauti ya kike." aliongea mmoja ya watu waliokuwa wanazungumza nje ya lile lori nililokuamo ndani., "Mtoeni.!, mtoeni.! Tena anasema ameua,embu mkamateni tumpeleke polisi.." Nilibaki nimezubaa huku nikiwa sijitambui kipi cha kufanya,nikawa natetemeka sana huku nikiishiwa na pumzi,nahisi mapigo ya moyo yalizidiwa kasi kwani nilijihisi napata joto ghafla huku kijasho chembamba kikiambatana na mchozi uliokuwa unanitoka mithili ya maji yakifata mkondo wake, sikuwa na jinsi tena kwani niliamini ndoto zangu za kuwa uraiani zimekwisha na sijui ntawaambia nini Gervas na mama yangu endapo watasikia nipo tena gerezani, Huku kojo likiwa linanimwagika, ukakamavu na ujasiri wote ukinitoka nilijikuta natoa tena sauti ya ukali., "Sio mimi..! Sio mimi..! Jamani msinikamate.." Huku nikinyosha mikono yangu miwili kuelekea ile sehemu niliyoamini ni mlango,taratibu nikaanza kufungua ili nijisalimishe ile namalizia kufungua tu..
 
SEHEMU YA 6

Ilipoishia.., bado haikusaidia kumjua ni nani lakini ulikuwa ni mwili wa mtu pale chini ambao kwa namna moja au nyingine sikuweza kuutambua mara moja, kwa ushupavu wa halmashauri ya kichwa changu ikanituma nichukuwe panga na ku.. Endelea., Nichukuwe panga na kuchana kipande cha nguo yake,nikafanya hvyo kisha kile kitambaa nikakificha katika pindo la nguo yangu ya ndani halafu safari ikaendelea,nilikatiza msituni bila kuogopa kitu chochote na wala kumuogopa yeyote hatimaye baada ya kukimbia mda refu nikahisi kama kitu kigumu nakanyaga chini,furaha na amani vikaanza kutawala ndani ya moyo wangu kwani nilikuwa tayari nipo katika barabara ya lami,akili ikawa katika kukisia ni upande gani ndo utakuwa unaelekea Dar na upande gani utakuwa unarudi Mbeya,nikiwa bado natafakari likapita basi la kwanza,nikashindwa kulisimamisha nikaamua kusubiri gari nyingine,kwani sikuwa hata na nauli hvyo nikaamua nijifiche niweze kudandia gari lolote litakalopita kwa mwendo mdogo., Baada ya kukaa pale takribani lisaa moja na nusu bila ya kuona gari lolote hatimaye nikaliona gari kubwa likiwa linakuja kwa kujikongoja.,


"Kama kufa wacha nife tu.,lakini hili gari siliachi.." nilijisemea kimoyomoyo huku nikijiweka tayari kwa kurukia lile gari aina ya roli,huku mikuki na mishale pamoja na lile panga nikilitupia msituni,kitendo cha lile gari kufika karibu yangu kikawa kosa kubwa sana kwangu kwani ndani ya mda mchache nikawa tayari nipo nyuma ya lile lori lililokuwa limebeba mbao., Kwa ujasiri niliokuwa nao nikaingia mpaka mule ndani ya lile lori kwa nyuma ambapo sikumuona mtu yeyote kisha nikarudishia mlango na kujilaza kwenye zile mbao huku nikiwa sina uhakika na ninapoenda, "Sijui ndo litaishia morogoro au ndo la Iringa hili gari?" hayo ni kati ya maswali yaliyokuwa yameandama ndani ya kichwa changu,huku safari ikiendelea taratibu baada ya mwendo mrefu kidogo, ghafla gari likasimama kwa mbali nikahisi sauti ya watu wanajibizana kwa nje., "Hapana mkubwa mzigo wetu hauwezi kuzidi kiasi hicho" hapohapo jibu likanijia kuwa tutakuwa tumefika maeneo ya mizani, "Embu fungua nyuma tuhakikishe maana tani zimezidi na kama hutaki paki pale gari yako uandikiwe faini" Wakiwa bado wanabishana pale tayari kwenye gari nikawa natetemeka mwili mzima huku nywele zikinisimama na akili ikinituma nifungue mlango, nikisema nijifiche nyuma ya mbao siwezi kwani ni kweli kulikuwa na mbao nyingi kiasi kwamba nilipata kanafasi kadogo sana ka kujificha, "Mungu saidia.! Mungu saidia.! Saidia jamani.!" Ndio maneno niliyokuwa naomba nisiweze kukamatwa kwani nia yangu nikufika Dar, Mda si mrefu nikaskia mungurumo wa gari kuwashwa kuashiria safari inaendelea moyo wangu ukawa na furaha upya nikajihisi ni mtu tofauti sana duniani tena aliye na bahati mbaya kupelekwa gerezani lakini aliyejawa na bahati nzuri uraiani, Nikiwa sina hata lepe la usingizi huku safari ikiendelea niliweza kushuhudia tena kwa mara nyingine kuki kuchwa kwani mwanga ulikuwa umeshatoka kuashiria kuwa ni alfajiri,gari nalo likatembea ka mwendo kidogo kisha likasimama, sauti na makelele ya watu ndio yalichochea hisia zangu,niliweza kutoa jicho langu kupenyeza kwenye kauwazi ka mlango nikaweza kushuhudia watu mbali mbali,moja kwa moja nikapata wazo la kuangalia kile kipande cha nguo nilichokikata kule kwa yule mtu msituni alikuwa ni nani, Taaratibu mkono wangu ukaanza kupenyeza mpaka kwenye upindo wa nguo yangu ya ndani nikakichukuwa kile kitambaa na kukiangalia., "Mamaa..! mamaa..! nimeuwa tena mungu wangu..! Nisamehe Pendo..! Sijakusudia mimi..!


Maaaaa aaaaaaah..!" Kumbe kile kilikuwa nikipande cha nguo cha rafiki yangu niliotokanaye gerezani 'Pendo'.. wakati nikiendelea kutoa sauti kali nikahisi kunawatu wamezisikia kelele zangu hivyo nikasikia mlango unafungulia eneo nililokuwa.., "Sauti inatokea humu ndani bwana, tena ni sauti ya kike." aliongea mmoja ya watu waliokuwa wanazungumza nje ya lile lori nililokuamo ndani., "Mtoeni.!, mtoeni.! Tena anasema ameua,embu mkamateni tumpeleke polisi.." Nilibaki nimezubaa huku nikiwa sijitambui kipi cha kufanya,nikawa natetemeka sana huku nikiishiwa na pumzi,nahisi mapigo ya moyo yalizidiwa kasi kwani nilijihisi napata joto ghafla huku kijasho chembamba kikiambatana na mchozi uliokuwa unanitoka mithili ya maji yakifata mkondo wake, sikuwa na jinsi tena kwani niliamini ndoto zangu za kuwa uraiani zimekwisha na sijui ntawaambia nini Gervas na mama yangu endapo watasikia nipo tena gerezani, Huku kojo likiwa linanimwagika, ukakamavu na ujasiri wote ukinitoka nilijikuta natoa tena sauti ya ukali., "Sio mimi..! Sio mimi..! Jamani msinikamate.." Huku nikinyosha mikono yangu miwili kuelekea ile sehemu niliyoamini ni mlango,taratibu nikaanza kufungua ili nijisalimishe ile namalizia kufungua tu tu nikawa tayari nipo mikononi mwa raia nisiowafahamu lakini walikuwa ni wanaume wamevalia sare ambazo sikuweza kuzitambua mara moja huku juu wakiwa na mashati meupe na wengine masweta mekundu kutokana na hali ya baridi kali lililokuwa limezunguka maeneo haya, Ilikuwa ni mchana tulivu kwani jua lilikuwa si kali sana kutokana na kaubaridi katika huu mji,wale wenye hasira wakaanza kunishambulia kwa kunipiga makofi huku wengine wakinishambulia kwa matusi makubwa ya nguoni huku wakiniburuza mithili ya mzoga aliyeoza anayeenda kutupwa,nilipiga kelele lakini haikusaidia nilivutwa sana na wale vijana.. "Wauaji kama nyinyi ndo tunaowatafuta" aliongea mmoja wa wale watu huku wakiwa wamenichania vipande vya nguo yangu, nilikuwa sina tena ujanja na pia kulikuwa hakuna tena muujiza utakaotendeka kwangu ili niweze kujikomboa katika mikono ya wale watu nisiowafahamu walioonekana makatili wasio na huruma hata kidogo.,


Waliniburuta kwa mwendo mrefu sana,huku umati wa watu ukifurika kunishuhudia, walipokezana kunishika na kunivuta,huku nikiwa bado nalia na kung'ang'ania nisiweze kupelekwa kituoni, Nikiwa naendelea kulia huku nguvu zikiniishia na kuacha wafanye wanachokitaka,nikahisi pumzi zimeniisha kwani kwa sasa nilikuwa nahema juu juu huku damu zikinimwagika pembezoni mwa mdomo wangu, maji machafu pamoja na matope vilitawala mwilini mwangu huku sura ikiwa imenivimba sana, niliamini hata nikiendelea kulia haitasaidia chochote,na pale malengo yangu yalikuwa yamefikia tamati kwani nilikuwa nikipelekwa polisi, Tukiwa njiani mwa safari huku kipigo kikinizidia katika mwili wangu huku macho yangu yakiangaza huku na kule kupata japo msaada wowote ndipo yakakutana uso kwa uso na kibao kilichoandikwa, 'TOSAMAGANGA HIGH SCHOOL' Halmashauri ya kichwa changu ikafanya kazi fasta hapo hapo nakugundua kuwa wale si raia wakawaida kama nilivyodhani bali walikuwa ni wanafunzi katika kile kijiji tena katika shule anayosoma Gervas japokuwa sikumuona katika wale watu waliokuwa wakinipiga lakini niliamini lazima alikuwa akisoma katika shule ile kama alivyonielezea hapo awali kwamba anasoma shule ya wavulana tupu iliopo Iringa na inaitwa 'Tosamaganga' hayo yote aliniambia kipindi kile nipo gerezani, "kabla hamjanifikisha huko kituoni naomba mniitie Gervas Phota nimuage" Niliposema hivyo tu wale jamaa waliokuwa wamenishikilia wakaniacha ghafla kwa mshangao huku wengine wakiamini huenda nilikuwa nimejifanyisha nimeua ili niweze kuonana na Gervas na wengine wakijiuliza nimemjuaje Gervas? Wakanikazia macho, "Gervas.? Mbona sisi hatumjui" Walinijibu huku wengine wakinicheka na kunisonya kwa dharau, "We dada una mashetani au kichaa enhh..


Unamuitaji nani?" jibu alilonipa mmoja wa wale watu lilinifanya niingiwe na woga huku meno yakiumana nakuhisi labda Gervas alinidanganya anasoma shule hii lakini haiwezekani., Hasira zilizidi kunipanda kwani kipigo kiliongezeka mara mbili ya pale huku damu nyingi zikiendelea kunimwagika, ghafla nikasikia kama mlio wakengele ukipigwa pembeni ya shule huku watu waliokuwa wamevalia kofia wakiwa wako na virungu mikononi wakinifuata pale nilipokuwa nimeburuzwa na wale wanafunzi,hofu ilizidi kutanda kwenye ubongo wangu,mwili ulininyong'onyea kuona wale watu wamevalia sare kama polisi, kila walipokaribia lile eneo ndipo nilitamani nife hapohapo,nikiwa nagala gala pale chini huku wale wanafunzi wakianza kutawanyika kwa kuwaogopa wale watu huku wakiniacha peke yangu nilianza kujisogeza kwa mwendo wa taratibu huku nikitumia magoti na makalio yangu kujisogeza mpaka nikaona chupa ya soda,nikaivunja ili niweze kujiua kabla ya wale askari hawajanifikia, nikiwa nataka kuanza zoezi la kujiua mara yule askari akawa ameshanikaribia na kunipokonya ile chupa., "niache nife..,niacheni jamani..! Nikiwa nimeshakata tamaa tena ya kuishi,kwa haraka nikaweza kuyakodoa macho yangu na kumuangalia mtu aliyenipora ile chupa niliyokuwa nimeivunja vunja na kuacha ncha kali nikitaka kujiua,nikaangalia mara mbili mbili nikagundua kuwa yule hakuwa askari polisi kama nilivyodhani bali alikuwa ni mmoja kati ya wale walinzi wa ile shule waliokuja kutawanya na kuwakamata wanafunzi sugu waliokuwa nje ya shule mda wa masomo, "Pole sana binti angalia sana siku nyingine watakuja kukubaka wale wanafunzi wavuta bangi wale...!" nilishangaa sana yule mlinzi kunipora kisha akaniacha na kuendelea kuwafukuza wanafunzi wengine,nilijawa na nguvu na furaha ya ajabu nakujiona ni mtu wa bahati tena ya mtende, watu wengi walinishangaa sana hilo sikujali kwani maisha ya kupigwa kama yale nilishayazoea tangu kipindi kile nipo Gerezani. Huku nikiwa nimelowa damu na kuchanika karibu nguo yote nliokuwa nimeivaa, nliweza kujikokota chini chini mpaka eneo la nyuma na ile shule kisha nikaegemea chini ya mti mkubwa, kwa uchovu na maumivu niliyoyapata yalinifanya nianze kunyemelewa na kausingizi japokuwa kulikuwa na baridi kali sikuwa na jinsi yoyote yakukabiliana nalo, "Twende bwana au unapenda kubaki hapa porini..? Mi nakuacha...Hapana., Pendo usiniache..! Pendo usiniache...! Usiniache..! Usiniache...! Usiniache..! Peeeendooooooooo.......!"


Ghafla nikashtuka nakuanza kuhema kwa kasi huku nikitetemeka Levina mimi kumbe ilikuwa ni ndoto tena nilikuwa nikiota nipo na marehem pendo kule msituni,usingizi ukanikata nakuanza kuangaza kila upande nakuona giza limeanza kutanda lakini upande wa mbele yangu kulikuwa na taa kali zilizomulika ile shule, nikaanza kusogelea taratibu kwa kuzunguka yale majengo yaliokuwa yamewekewa uzio huku nikitafuta lango la kuingilia, hatimaye nikagundua geti lilipo,walinzi takriban watatu walikuwa wametanda pale lango la kuingilia hivyo nikatafuta eneo la choo kwani niliamini kukijua choo itakuwa ni njia nyepesi ya kuingia ndani ya ile shule, haraka haraka macho yangu yakaweza kuona wanafunzi wakiongozana wakiingia kwenye jengo lingine lililoonekana si kubwa sana kama majengo mengine huku wakiingia na kutoka, haraka haraka kwa ujasiri na kwa shauku niliokuwa nayo ya kutaka kupambana mpaka nimuone Gervas nikawa na nguvu ya ajabu yakuweza kuruka ukuta japokuwa haukuwa mrefu sana ndani ya dakika chache nilikuwa tayari nipo kwenye kale kajengo kalichokuwa na vyoo vingi vyote vikiwa na milango nikaingia choo kimojawapo na kujifungia huku nikishuhudia hamna mtu ndani, harufu kali ya kinyesi na mikojo katika vile vyoo nilipokuwamo ndani havikunizuia hata kidogo kuondoka mule ndani,niliweza kutulia kimya huku nikiombea aje kati ya Gervas au mwanafunzi yeyote nimuulizie Gervas, mpaka nikajishangaa kwa jinsi nilivyokuwa sina woga wowote, Ghafla nikasikia sauti ya kama mtu anakuja,nikazidi kukaa kimya ndani ya choo huku nikijiuliza ntaanzaje mara ile sauti ya mtu akiingia na kuanza kukojoa mlango wa pembeni yangu, nikafungua mlango wangu taratibu na kuanza kunyata kuelekea mlango aliokuwepo huku akili ikinituma nimuwahi na kumnyamazisha kabla hajashtuka na kuanza kupiga kelele, " Shhh..usiniogope wala usikimbie..Naitwa Levina natokea..." Kabla sijamaliza kujitambulisha yule mwanafunzi akawa ameshanitambua.. " We si yule dada ambaye nimetoka kuskia stori yako sa hivi kwa wenzangu kuwa umepigwa na kukuburuzwa mchana kutwa pale nje na umeokolewa na walinzi..?" "Ndio mimi ila nipo hapa kwa msaada mmoja tu, unamfahamu Gervas Phota..?" "Namfahamu na ninasoma naye lakini yupo Chumbani anaumwa leo siku ya pili yupo kitandani.."


"Tafadhali nisaidie kwa hili nenda kaniitie mwambie Levina, nipo hapa hapa chooni kwenye mlango huu nawasubiria mtanikuta.." Ndani ya mda mfupi nikawa tayari nimeshayazoea mazingira ya kile choo ikiwa ni pamoja na harufu kali ya mule ndani, niliweza kujifungia mlango mmojawapo kwa mda mrefu tangu nimefika bila ya hata mtu yoyote kujua, mara nikasikia sauti ya watu wanaongea kwa nje huku sauti kama niliyokuwa naifahamu nilianza kuingiwa na furaha na amani isiyokuwa na kifani kwani niliamini Gervas ndiye mkombozi wangu na anayepajua mpaka nyumbani kwetu kwani nilikuwa nimeshapasahau hadi jina la mtaa,sikutaka kujitokeza hvyo nikavuta subira huku nikiisikia ile sauti kwa umakini taaratibu nikaweza kuitambua kuwa haikuwa sauti ninayoifahamu hata kidogo na hata maongezi waliokuwa wanaongelea hayakuwa yakiunafunzi hivyo halmashauri ya kichwa changu ikapambanua fasta na kujua kuwa wale watakuwa ni walinzi kwani walikuwa wanaongelea mambo ya kifamilia na kikazi tena kazi ya ulinzi, moyo ulianza kuniripuka kwani walikaa mda mrefu huku wakipiga story na hata wanafunzi walipokuja nilisikia wakiwaamkia na kujisaidia na kuondoka zao,kwa ujumla nililegea sana na akili ilishaanza kuchoka,nikiwa bado nipo nao wale walinzi chooni huku wakinogewa na stori ila mlango nilikuwa nao tofauti bila ya wao kujua ghafla nikasikia sauti kali iliyotokea upande wa nje huku ikilitaja jina langu., "LEVINAAAA...! LEVINAAA...! LEVINAAA...! " YUPO MLANGU UPI UMESEMA..?" Nilitamani niweze kutoka lakini haikuwezekana kutokana na wale walinzi kukaa mda mrefu wakipiga stori, hakika ile sauti ilikuwa ni ya Gervas akiongea na mwenzake huku nikihisi ameshakaribia kuingia mule chooni,ghafla nikasikia ukimya umetanda halafu yakafuatia maswali kutoka kwa wale walinzi wakimuuliza Gervas, "Levina..! Levina ndo nani? Na mbona mwenzako amenyoosha kidole mlango huo ambao umefungwa..? Kuna nani...?" *************************
 
SEHEMU YA 7
Ilipoishia.. "Ni..mi..mi.. Ndo nimemu..uaaaaaaa Peeeeeendo... Endelea... Nilijikuta nimeropoka kila kitu huku kwa ghafla yule mzee akamuwahi kumshika mke wake kisha akanigeukia na kuniuliza tena., "Binti ulikuwa unasema?... Samahani sana sijakusikia vizuri nilikuwa namuwekea karibu na mdomo mama yako mfuko aweze kutapika..." Aliongea yule mzee bila ya kuonyesha wasi wasi wowote kama kuna neno baya ambalo Levina mimi nimeropoka, "Nilitaka kukupa mfuko huu hapa mkubwa nimeona huo mdogo hautatosha kwa maana mama anatapika sana.." Nilimjibu kwa kuzuga huku macho nimeyaelekezea chini kwa aibu kubwa niliokuwa nayo pale, nikajifanya kihere here kwa kumpa maji yakunywa yule mama aliyekuwa anatapika ambaye ni mama yake na Pendo, Mzee alinishukuru sana kwa wema wangu japokuwa ukweli nilibaki nao moyoni, "Umesema binti unaelekea wapi?" Aliniuliza yule mzee na kwa mda ule tulikuwa tukiendelea kupiga story za kawaida kuhusiana na maisha njia nzima japo ukweli kuhusu pendo nilikuwa nao moyoni., "Naelekea Dar es salaam kutafuta kazi" "Kazi gani binti yangu?" "Naenda kutafuta kazi za ndani"

Nilimdanganya sana kuhusu maisha yangu kwa ujumla na aliweza kuniamini kwa asilimia kubwa kuwa natokea Iringa naelekea Dar kutafuta kazi za ndani, Ile roho ya kikatili,ilikuwa imeshaanza kunikabili kwani sikuwa hata na huruma ya aina yoyote..huku tukiwa tumeshasafiri mwendo wa kama masaa manne hivyo nikamwambia mzee kwakua gari ilikuwa inapitia Morogoro halafu ndo inaenda Dodoma ilinibidi nimwambie mzee kuwa tukifika morogoro anishtue kwa sababu nimeshapasahau sitapakumbuka vizuri.. * * * * Ndani ya masaa kama sita huku kausingizi kakinipitia mzee alinishtua na kuniambia kuwa tulikuwa tayari tupo maeneo ya mzumbe tukikaribia kuingia morogoro,hivyo niwe tayari nisilale tena, nilianza kujawa na furaha isiyotabirika huku furaha yangu zaidi nikiielekeza katika mifuko ya ile traki suti niliyokuwa nimeivaa na kuchomoa zile karatasi za ramani kisha nikazing'ang'ania mikononi mwangu nikisubiri niingie Morogoro.. *** Hatimaye tukaingia ndani ya mkoa wa Morogoro,kisha nikamuaga mzee pale lakini nilishindwa kumuaga mama kwakua tayari alikuwa ameshapitiwa na usingizi., "Usijali binti utafanikiwa nakutakia maisha mema na ubarikiwe upate kazi na uishi kwa amani huko uendako.." Yale maneno hayakuniingia akilini hata kidogo kwani hayakuwa na ukweli wa aina yoyote pale ila nikaamua nimuitikie tu kwa kumridhisha yule mzee., "Ahsante sana mzee na poleni sana kwa msiba uliowakuta" Nilimwambia huku nikionesha tabasamu la huruma la uongo, nikampa mkono kisha nikamuaga kuelekea stendi ya upande wa pili huku yule mzee akiamini kabisa kuwa nlikuwa naelekea dar kumbe naweka kwanza kituo..

*** Mda ulikuwa umeshatimia kama saa nane mchana huku kukiwa na hali ya uvugu vugu iliyojawa na baridi lakini siyo kali sana kama la Iringa kwani manyunyu yalikuwa yakidondoka taaratibu kuashiria mvua inataka kunyesha,huku nikiwa nimejikunyata mikono yangu niking'ang'ania zile ramani ndani ya mifuko ya suruali,niliweza kutoa na kufungua mojawapo ya ramani iliyokuwa inaelekeza kwa 'Baba Ali' huku nikiiongoza inavyoelekeza.. "Sasa, hapa ndo nimeambiwa panaitwa 'Boma Road' na ramani inaelekeza kota hizi hizi... embu ngoja nimuulizie huyu mtu.." "Samahani kaka..Sijui unamfahamu 'Baba Ali'..?" Nilimuuliza mpita njia niliyeamini kuwa atanisaidia kumpata mtu ninayemhtaji., "Baba Ali..Baba Ali.. Yeeah, nimemkumbuka anaishi maeneo ya paleee juu tena mnene hivii alikuwa anaishi na mke wake na watoto lakini sasa hivi anaishi peke yake?.." "Ndo huyo huyo..",nilimuitikia tu huku nikiamini atakuwa ndo huyo huyo kutokana na maelezo aliyonipa Gervas., "Nyosha na hii barabara ukifika pale njia panda anza kuhesabu nyumba ya kwanza mpaka ya tatu ndo hapo hapo" "Ok., asante sana.." Furaha ilinizidia zaidi ya pale nilipokua naelekezwa sikutaka hata kugeuka nyuma akili yangu ikaelekea mpaka kwenye njia panda na nilipofika kwenye lile eneo nikaanza kuhesabu nyumba ya kwanza mpaka ya tatu, nikaingia ilikuwa ni nyumba kubwa iliyojaa wapangaji mbalimbali nilipofika nikapokelewa na majirani na kuwaulizia 'Baba Ali' kisha wakaninyoshea chumba anachoishi na kuanza kugonga hodi., "Karibu karibu.." ilisikika sauti yakiume niliyoamini ndo mwenyewe 'Baba Ali..'

"Wewe ndo baba Ali?" "Ndo mimi karibu binti" Niliingia ndani kwake japo alikuwa na chumba na sebule,ni kweli sikuona dalili yoyote ya mke wala watoto ,niliweza kumwelezea matatizo yangu yote kisa cha mimi kupelekwa gerezani na wema wote alionitendea mdogo wake ambaye ni Gervas,misukosuko yote hadi nilivyokwenda kwa Gervas akanipa ramani mpaka nimefika hapa, aliitikia kuwa ilikuwa ni kweli alikuwa akimfahamu Gervas kama ndugu na alikuwa akiishi na mkewe na watoto lakini wameshaachana na kuhusu kuelekea nyumbani kwetu nisijali kesho yake atanipeleka mpaka mlangoni kwetu, hivyo akanizidishia furaha na msisimko ndani ya mwili wangu zile ramani zikawa hazina tena maana kwangu nikampa akazichukuwa na kuzichanachana kisha akaenda kuzitupa nje. Ilikuwa imeshatimia saa tatu za usiku hivyo akaniandalia maji ya kuoga nikaenda kuoga niliporudi nikakuta kashanunua chakula (chipsi mayai) hivyo tukakaa mezani na kula,baada ya hapo akanielekeza chumba nitakacholala kisha taa zikazimwa nikamwacha akijilaza kwenye kochi pale sebuleni.. Ikiwa ni usiku wa manane huku nikiwa nimejifunika shuka sio zito sana huku nikiwa nimejikunja kwa kaubaridi kalichokuwa kakininyemelea nilianza kuhisi kama kuna mtu anahema mgongoni mwangu tena kwa pumzi ya hali ya juu,nilipaamini sana pale na pia nilivyomuheshimu 'Baba Ali' sikufikiria hata kidogo kama anaweza kunifanya chochote, kadri mda ulivyokuwa unaenda ndivyo nilihisi kama mikono inapenya katika makwapa yangu kisha inashika na kutekenya matiti yangu huku ikiteleza kwa kunipapasa pasasa ikihamia taratibu katika sehemu zangu za siri na kuanza kuzitekenya, nilishtuka lakini kwa ujasiri niliokuwa nao sikutaka kupiga kelele kwanza mpaka nimjue ni nani anayenifanyia vile, sasa nikawa napapaswa maeneo ya mapajani kwangu huku yule mtu akigeukia upande wa mbele yangu.. "Kohh..! kohh..! kohh..!" Nikakohoa kwa nguvu japo yule mtu ashtuke lakini hakutaka kuniachia, "Wewe nani? Naomba uniache..!" Niliamua kutoa sauti ya juu kidogo huku nikiwa na hasira kali na mishipa iliyonitanda usoni,lakini haikusaidia kwani kilichofuata nilihisi kama panga au kisu kikiumana na sakafu kisha haraka taa ikawashwa.. "Heee Baba Ali..?" Sikutaka kuamini hata kidogo kwani ni kweli alikuwa 'Baba Ali' juu ya kifua changu, aliyejitambulisha na kunipa hifadhi hapa kwake ndo alikuwa akitaka kunibaka..

"Shhh.. Nani Baba Ali..? Tena ukome siku nyingine kuniita hivyo,Gervas mie simjui na huyo 'Baba Ali' unayedhania ni mimi siyo na huko kwenu sikujui malaya mkubwa we..!" Yale maneno yalinichoma sana sikuwa na jinsi kwakuwa alinishikia panga na kunilazimisha kufanya atakavyo hivyo akaniingilia kinyume na maumbile usiku kuchwa huku akinisababishia maumivu makali na damu nyingi kunitoka mwilini mwangu.. Sikuweza kupata usingizi hata baada ya kunifanya atakavyo na kuniacha pale usiku ule Kitandani nikiwa sijiwezi, nilimshuhudia akichukuwa suruali yake na kutoa noti ya shilingi elfu moja na kunipatia.. "We malaya, chukuwa hii itakusaidia japo ukapate chai" Nilijikuta napandwa na hasira kali,huku nikihema haraka haraka pale bila hata kuongea chochote nikachukua ti sheti yangu na ile traki suti nyeupe aliyoniachia Gervas kisha nikamgeukia na kumwambia.. "Ahsante sana kwa wema wako ulionitendea" Kisha nikatoka nje,kupitia kwenye kakorido ambapo pembeni kulikuwa na beseni la vyombo vichafu vya majirani kwa bahati nzuri nikaona kisu katika vile vyombo hivyo halmashauri ya kichwa changu ikafanya kazi fasta, nikakichukuwa na kurudi ndani kwa kasi ya ajabu na kumkuta 'Baba Ali' akiwa kainama chini uku akifunga kamba za viatu,nikamuwahi kabla hajageuka na kuinuka na kumchoma kisu cha mgongoni kisha nikakichomoa haraka na kumuwahi tena kabla hajapiga kelele na kumchoma tena maeneo ya shingoni kisha nikachukuwa kitambaa na kumjaza mdomoni ,hivyo nikamshuhudia 'Baba Ali' akigala gala pale chini huku akitoa macho na mishipa ya shingoni ikimlegea. Zoezi lililofuata ni kuingia mpaka chumbani kwake na kutafuta hela zilipo, nilitumia kama dakika tano bila ya mafanikio huku nikishuhudia kuona madawa ya kulevya pamoja na vitambulisho mbalimbali vya watu tofauti feki hivyo nikagundua kuwa 'Baba Ali' alikuwa ni jambazi tena sugu lililoshindikana tena lilikuwa likitafutwa, baada ya kutafuta hela bila ya mafanikio hatimaye nikazipata pesa nyingi sana kwenye kisanduku alichokuwa amekificha chini ya kitanda, lakini mimi nilikuwa nahtaji kama shilingi elfu hamsini tu hivyo nikazichomoa, "Liwalo na liwe..!"

Nilijihisi kama yule stelingi wa muvi za kichina 'Jet Li', kwakuwa ilikuwa usiku sana kama mida ya saa kumi,niliweza kutoka pale bila hata ya kuonana na majirani wowote haraka haraka nikafuata ile njia niliokuja nayo na kuondoka kuelekea msamvu ambapo ndipo ilipo stendi ya mabasi ya mikoani., **** Nikiwa tayari nimeshakata tiketi katika basi la Abood, safari ya kutoka Morogoro kuelekea Dar ilianza na nilikuwapo ndani ya basi la kwanza kabisa lililotoka sa kumi na moja na nusu, na tangu nilipoingia katika basi sikuwa na wasiwasi wowote kwani moyo wa kishujaa na kijasiri ulikuwa umenitawala, lakini sasa takribani nusu ya watu kwenye lile basi walikuwa wakinishangaa huku wakiangaliana na kutikisa vichwa vyao, nilishindwa kujizuia nikajiangalia juu mpaka chini.. "Mmmh...! mmmh...!" Safari hii niliweza kuwah kujiziba mdomo ili nisiropoke jambo lolote baya kwani traki suti yangu yote ilikuwa imejaa damu huku na mikono yangu ikitapakaa damu mpaka sehemu za usoni kitendo kilichofanya njia nzima abiria wanishangae kwa kuwa vile.. Tukiwa tunakaribia kuingia chalinze, basi letu likasimamishwa na trafiki wawili mmojawapo akiwa ni askari polisi,kwa mara nyingine moyo ukawa kama unawaka,nywele zilinisisimka huku mdomo ukinitetemeka kisha nikalitega sikio langu kwa upande wa nje kusikia maneno ya kondakta wa basi letu akiwa na trafiki.,

"Umesema mmepakiza abiria wangapi?" "Sitini na mbili tu" "Hakuna waliosimama?" "Hakuna" "Usiniambie hakuna wacha nipande niingie nijionee mwenyewe ndo uniambie hakuna sawa?" Maneno hayo yalinifanya nizidi kulegea kwani aliyekuwa anaongea na kondakta alikuwa hajavalia mavasi meupe bali alivalia mavazi ya kaki yale yenyewe ya polisi huku akiwa kashikilia bunduki akapanda ndani ya basi huku akiangaza siti moja baada ya nyingine na alipofika kwangu.. "We vipi tena Mmepata ajali wapi?" "Hatujapata ajali yoyote huyo kapanda basi hivyo hivyo..!" Aliropoka dereva wa basi huku akisaidiana na kondakta wake kunimaliza.. "Haya shuka., shuka upesi chini.,we dereva endeleeni na safari yenu" Nilijikuta nipo mikononi mwa yule polisi haraka akiniwahi kwa kunifunga pingu baada kushushwa chini na kuacha basi likiendelea na safari.. "Mungu wangu...! Mungu wangu...! mbona umeniacha..? Mbona wanitenda hivi....!" Nilijikuta nikiandamwa na mikosi na kumshushia lawama Mwenyezi Mungu alieniumba na kujiona sifai kuishi katika dunia hii, huku nikiwa chini ya ulinzi pale barabarani,Yule askari polisi akaniangalia juu mpaka chini akawa anatingisha kichwa huku akicheka kuashiria kama mtu anayenifahamu sana.. "Levina..?" Sikuamini amini kama jina hilo atakuwa amelitaja yule askari au ameambiwa na mtu kuwa naitwa Levina,nilihisi kama moyo ukinipasuka ghafla,hivyo nikawa sina tena jinsi kwani nikawa nimeshapatikana, lakini swali lililoniumiza kichwa ni kwamba nipo pale kwa kosa lipi la mauaji? "maskini isikute baba yake 'Pendo ndo kamtuma huyu polisi..? ....Au., nilivyomuua 'Baba Ali taarifa zimemfikia huyu polisi..?" Nikiwa bado najiuma uma pale huku akili ikiwa haifanyi kazi kabisa,ghafla nikamuona yule polisi kabadilika zaidi ya pale kwani sura yake ilikunjamana ghafla huku akinifokea.. "Kwanini umeua Tena..?" Lile swali lilinifanya nilegee na kudondoka mpaka chini kwani nilikuwa sina nguvu tena ya kusimama huku nikishindwa kujua kipi cha kufanya pale chini...

"Au unapenda kwenda tena gerezani., naona safari yako nyingine sasa imefika..?" "Hapana nisamehe afande sijakusudia nii...l..ii...piii...ti...wa...,tu..na shetani..?" Kabla sijamalizia kujitetea nilishangaa kuinuliwa kwa kushikwa shati kwa nguvu kisha kilichofuata ni kupigwa vibao na mitama huku nikishindwa hata kujizuia kutokana na zile pingu nilizokuwa nimefungwa mikononi., "Kaka mkubwa, wacha nimpeleke kituoni Dar huyu mpumbavu ana kesi kubwa na nitampigia simu afande Geofrey aje msaidiane hapa.." Nilijihisi kama mtu asiye na bahati hapa duniani,maumivu aliyonisababishia 'Baba Ali wakati akiniingilia kinyume na maumbile ukiongezea maumivu aliyonisababishia huyu polisi vilinifanya niumie sana moyoni,huku mwili wangu ukiwa hautamaniki kwa majeraha.. ******* * * Levina amekamatwa kwa mauaji yapi, ya 'Pendo' au 'Baba Ali..?
 
SEHEMU YA 8

Ilipoishia.. ....uku mwili wangu ukiwa hautamaniki.. Endelea.. "...Ingia kwenye gari mpumbavu wee..!" Aliendelea kunikaripia yule polisi ambaye sikumfahamu kwa jina lakini lafudhi aliyokuwa akiongea ilinifanya niamini kabisa atakuwa ni muhaya tena yule wa kule Bukoba ndani ndani (Vijijini),Tukiwa ndani ya ile gari aina ya 'One Ten' huku nikiwa nyuma na askari mmoja na yule mwingine akiwa anaendesha gari, Ujasiri wangu feki niliuweka pembeni hivyo nikawa ni mtu wa kutoa machozi na kujiuguza sehemu zilizoonesha kuumizwa katika mwili wangu,njia nzima mpaka tunaingia Kibaha nilikuwa mtulivu bila kusemeshwa kitu chochote na yule polisi,Tulipofika maeneo 'Mbezi' yule polisi akafungua kinywa chake na kuniuliza, "Unasikia njaa..?" "Kimya..!" "Dereva embu pitia pale 'Mnama Restaurant' tupate chochote..." Maswali aliyoniuliza na maongezi aliyokuwa akiongea na dereva ndo kati ya vitu vilivyoanza kuuchanganya ubongo wangu.. "Mbona kabadilika tena huyu polisi..? Asije kuwa wananifanyia njama kama Baba Ali..? Kwanini wameniagizia chakula kama kweli nina hatia?..sijui nimuulize kosa langu ni lipi hapa hapa..?" Nikiwa bado nimekaa katika kiti cha mgawaha mmoja pale mbezi nikiwa mimi na polisi wawili mmojawapo ndo yule aliyekuwa akinishikia bunduki na ndo aliyenifunga pingu, "Wewe muuaji unakula nini? "Hapana...,

Sili chochot..." kabla sijamalizia kusema nilishtukia napigwa na kitako cha bunduki na yule yule polisi.. "Usitufanye siye wapumbavu, kuua uue..! Tunakuonea huruma japo na wewe upate chochote unatuletea 'usenge' au umeshazoea maharage ya Gerezani nini...?" Nilijikuta nanywea na kuwa mdogo na kukubali kula chakula kama walichoagizia wao ambapo walikuwa wakila wali nyama.. Ndani ya nusu saa nikarudishwa tena kwenye lile gari lakini safari hii nilishangaa hawakunifunga tena pingu mikononi hivyo nikabaki na maswali mengi sana kichwani.. * * * * Mawasiliano ya mimi na wale askari bado hayakuwa mazuri kwani hadi tunapita kimara hakuna hata mmoja aliyenisemesha zaidi ya yule mmoja kukaa karibu na mini nisiweze kutoroka huku mwingne akiwa dereva ndani ya ile gari... Mawazo yalitawala sana kichwa changu huku nikijiona si mtu tena wa kuonana na mama yangu wala Gervas..,nikiwa bado niko kwenye dimbwi la mawazo huku tukiingia kwenye foleni ya mataa pale ubungo ghafla macho yangu yakaamia kwenye gari la pembeni yetu aina ya 'suzuki' hasira nilizoshikwa nazo ghafla ziliwafanya hata abiria waliokuwa ndani ya daladala ambayo ilikuwa nyuma ya ile gari niliokuwa nimeikodolea macho waweze kunishangaa,hilo sikulijari kabisa maishani mwangu kwani Levina mi aibu ilishanitokaga siku nyingi ukianzia pale shuleni kwa kina Gervas waliponigalagaza wale wanafunzi,pia katika basi nililokuwa nimeshushwa hvyo ukinishangaa mi ntakuona mtu wa ajabu sana.,

Akili na mawazo yakiwa bado ndani ya kale ka suzuki ambapo macho yangu yalikutana uso kwa uso na mama ambaye sitakuja nimsahau hata nife, hakuwa mwingine bali ni yule mama aliyenipeleka polisi kwa mara ya kwanza na ndiyo aliyefanya maisha yangu yapo hivi mpaka sasa.., "lazima nife mimi au wewe" Nilijisemea kimoyomoyo huku nikimtolea macho yalioambatana na mchozi ulioanza kuniteremka kwa ghadhabu niliyokuwanayo, kilichofuata ni kuhema haraka haraka huku pua zangu zikianza kujaa makamasi kama mtu aliyepatwa na mafua ya ghafla..kama kawaida yangu sikutaka kuchelewesha mda.. "Bunduki kitu gani wacha anifyatue tu lakini kwa huyu adui yangu siwezi kamwe kumuacha.." Nikatoka spidi katika lile gari nililokuwa huku nikimwacha yule askari akinilenga huku akinikimbilia lakini hilo sikulijari ndani ya sekunde chache nikawa nshafungua na kuingia kwenye ile suzuki na ku loki milango yote tayari kwa kumvagaa yule mama aliyekuwa akiendesha peke yake ndani ya kale kagari.., Nilitumia kucha zangu na meno kama filamu zile za kutisha 'VAMPIRE' kuisambaratisha kwanza sura ya yule mama kisha nikachukuwa mtandio wake aliokuwa nao amejifunga mabegani na kuuvingirisha shingoni mwake tayari kwa kumnyonga,akiwa bado anakurupuka na kutapatapa pale gari zilikuwa tayari zimeruhusiwa na trafiki na wale polisi niliokuwa nao tayari niliweza kuwaona wakiwa nje wanataka kuingia ndani nilipokuamo,sikujua hata siku moja kuendesha gari lakini nilisikia kwa wenzangu tu kuwa kunakitu kinaitwa gia kipo kama rungu pia kingine kinaitwa krachi kipo miguuni, sikulielewa hilo lakini nilijikuta nimekanyaga chini bila kujua kama ndo breki au ndo hiyo krachi kisha nikalishikilia rungu na kulisogeza kisha nikashangaa kuona gari ikitoka tena kwa mwendo wa kasi pale,nikiwa huku nimekaza ule mtandio shingoni mwa yule mama huku upande mmoja nikishikilia msteringi nilijikuta nimevamia gari za watu wengine waliokuwa mbele yangu na kusababisha ajali mbaya pale huku umati wa watu ukifurika katika lile eneo kushuhudia ile ajari.,

Watu walikuwa ni wengi sana mpaka nikachanganyikiwa japokuwa nilijihisi mwili wote haufai kwa maumivu, ile gari niliokuwa nayo ilikuwa imeharibika vibaya baada ya mda mchache nilihisi kuna watu nje wanavunja vioo vya gari wanataka kuingia ndani katika kuangalia vizuri macho yakamwona yule polisi alionifikisha hapa nilipo.., "Levina...! Levina...!Jisalimishe mwenyewe unajitafutia matatizo" Yale maneno ya yule polisi aliyokuwa akiniambia, hayakuniingia akilini mwangu kabisa niliona kama anampigia mbuzi gitaa ili acheze.,yule mama sikujua kama alikuwa amekufa ila nilimwacha pale akiwa anahema kwa kasi ya juu huku akiwa hajitambui wala hajiwezi hata kunyanyuka,haraka haraka nikafungua mlango upande wa nyuma kisha nikatoka spidi huku nikiuacha umati wa watu ukiwa haujui nini kinaendelea kutokana na lile tukio.. Spidi niliyotoka nayo pale huku watu wachache wakinishangaa si kwasababu nimeponea chupuchupu kwenye ile ajali bali pia waliniona kama mtu aliyechanganyikiwa kwa jinsi nguo zangu zilivyokuwa hazitamaniki kwa uchafu tena ule uliokolea damu katika ile suruali aina ya trakisuti ilivyobadilika rangi nyekundu iliyokuwa imetapakaa damu na kuwa kama nyeusi nyeusi, Sikumuogopa hata mtu nilizidisha mbio huku nikielekea barabara ya kwenda mwenge, kelele za wapiga debe pale ubungo ziliongeza hisia zaidi ndani ya kichwa changu kwani kitendo cha kugeuka nyuma ilikuwa kosa kubwa sana kwangu kwani niliamini na kujua tu lazima umati mkubwa wa watu uwe unanikimbiza nyuma yangu huku, nikiwa nasonga mbele haijapita hata hatua ishirini mara kundi la watu wengine wakawa tayari wametanda mbele ya macho yangu...

* * * * Baada ya yule polisi kunishika ndani ya basi akanifunga pingu baada ya pale akatikisa kichwa chake kuashiria kuwa ananifahamu akaniita na jina "Levina...!" "kwanini umeua tena?" "Au unapenda kwenda gerezani tena" Hayo ni kati ya maneno ninayoweza kuyakumbuka kwani yalinifanya niishiwe nguvu na kudondoka mpaka nikapoteza fahamu,ninachokumbuka nilishtuka na kushuhudia nikipepelewa na yule polisi huku nikiwa kwenye gari ambayo sikuitambua vizuri kwa nje kwani alikuwa amenilaza ndani ya lile gari na mikononi mwangu bado nilikuwa na pingu hivyo nilipopata usingizi akaendesha gari mpaka nakuja kushtuka tumeshafika Dar na nilikuwa nikiota ndoto tena matukio ya ajabu ajabu kama lile la kumuua yule Mama na kuharibu vibaya lile gari lake pia kufukuzwa na umati mkubwa wa watu pale ubungo.. "Mungu wangu kumbe yote yale ilikuwa ni kama ndoto..!" Nilijikuta nausemea moyo huku nikishusha pumzi kubwa.. "Uuhh...! uuhh...!"

Taaratibu nikiendelea kuhema kwa nguvu na hasira kali., "Hapa ni wapi?" Nilijikuta nikimuuliza swali yule polisi aliyenitoa kule Chalinze na ndiye alikuwa amenipakia baada ya kuzimia pale Chalinze.. "Hupaswi kujua..unapaona pale?" "Nikakaa kimya.." Huku nikiona kibao kimeandikwa mbele yangu.., 'CENTRAL POLICE' Nilitamani kutoroka pale lakini nisingeweza kwani mda wote nilikuwa na pingu mikononi. "Levina...! Embu niambie ukweli hizo damu katika hyo suruali ilikuwaje?" Nikawa najiuma uma nashindwa nimpe jibu gani kwani ni kweli nimeua lakini nikisema ajue itanigharimu sana maishani mwangu.. "Afande hizi ni damu za kawaida tu ambazo nilipitia buchani kuchukuwa nyama na kupeleka nyumbani nilipokuwa kule Morogoro..!" Nilijikuta namdanganya lakini kiukweli alionesha kuchekeshwa na mimi sana mpaka nikamshangaa.. "Levina acha kunichekesha we mtoto...,

Mbona kule nilipokushusha kwenye basi nilikuuliza swali kama hili na ukaniambia kweli umeua ila kwa bahati mbaya..?" "Mi mi...? Labda utakuwa ulisikia vibaya afande...." Nilijitahidi sana kujikaza na kubadilika lakini yule askari hakuridhika na majibu yangu,na kwa safari hii hakuwa mkali wa kunipiga bali nilimshangaa pia kwa kuongea na mimi ndipo akataka kuniambia ukweli sababu kubwa ya kunichukuwa na kunileta mpaka maeneo haya kituo cha polisi endapo tu nitamjibu maswali yake kikamilifu, huku tukiwa tumeliangalia lango la kuingia polisi... "Sitapenda nikuingize tena pale polisi najua utateseka sana mpaka uje kutoka tena mdogo wangu..,Ila kitu kimoja ninachotaka kuongea na wewe ni unipe jibu moja tu ili niweze kukusaidia.. "Huko ulipotoka umeua?" "Sijaua na naogopa sana kuua maishani mwangu..!" Nilimjibu mara ya pili lakini kwa sasa nilianza kuonesha kauoga,kwani nilianza kuingiwa na hofu huku nikitoka jasho jembamba mwilini mwangu na niliamini kabisa ntakuwa nategwa.. "Mimi nataka kukusaidia Levina lakini unakuwa mbishi si ndio..?" Alianza kubadilika yule afande huku akinikodolea mijicho na kunionesha ufunguo wa zile pingu kuwa kama nitakuwa mkweli atanifungua pingu kisha nitakuwa huru na salama,kitendo kile kikanifanya uzalendo uanze kunishinda na kujikuta namjibu anavyotaka.. "Ni kweli nimeua lakini si kwa kukusudia.." "Umeua..? ..Nani uliyemuua Levina?" "B...aa..a..a..b..a.. A...l..i.." Nilitaja jina kwa kujiuma uma pale pale yule afande akabadilika ghafla na kugeuza ile gari kisha safari ikaanza lakini sikuweza kujua ni wapi nilipokuwa napelekwa zaidi ya kushuhudia akitoka kwa mwendo wa kasi huku nikiwemo ndani ya lile gari lake... ***************
 
SEHEMU YA 9

Mwendo wa kasi aliotoka nao yule afande haukuwa wa kawaida, kwani nilijikuta nabilingita ndani ya lile gari lake huku mikononi pingu zikinishika vilivyo.. Nilichoweza kuambulia kujua ni pale tulipokatisha maeneo yalionesha kuwa na maduka mengi huku daladala nyingi zikiwa na mstari mwekundu katikati na maandishi yaliosomeka 'ubungo - k/koo, hvyo halmashauri yangu ya kichwa ikanituma moja kwa moja na kujua tayari nimeingia maeneo ya kariakoo,nikiwa ndani ya gari huku yule afande akiliendesha gari mithili ya mtu aliyeliiba lile gari au kuna mtu anamfukuzia nilishangaa pia kulipita tena kwa kasi eneo lile ambalo nilishawahi kukaa rumande kipindi kile cha kesi yangu si kwingine bali ni kituo cha polisi cha 'MSIMBAZI' Safari ilizidi kusonga mbele kwani tulikuwa maeneo kidogo ninayoweza kuyatambua Kama vile tulikuwa kiprefti cha kamata lakini maswali mengi kichwani mwangu yalinizidia bila ya kuwa na jibu..

"Samahani afande.." "Samahani ya nini? Na unataka nini tena?" Majibu yake bado yakanifanya niishiwe nguvu., "Nahtaji kujua tunaelekea wapi?" "Nyamaaaazaa..!,Tena kimya nisikusikie tena ukiongea..!" Ilinibidi niwe mpole huku nikishindwa kujielewa na kujiona sina umuhimu tena hapa duniani,na sasa nilikuwa tayari kwa lolote litakalonikuta mbeleni., "Bora hata akaniue nijue moja kuliko kuendelea kuteseka namna hii" Niliusemea moyo maneno ya ajabu,mda wote moyo ulikuwa ukinienda tena kwa kasi ya ajabu huku kichwa kikiniuma sana nafikiri yote ni kwasababu ya kuwaza sana,Mara tukasimama eneo kama nilikuwa nalifahamu kisha yule afande akachukuwa funguo zake na kunifungua ile pingu, "Twende.." Mara nikashangaa kushuka naye huku kanishika mkono,lakini nikawa bado na wasi wasi kwani ile nyumba mbele yangu kama naifahamu japokuwa ilikuwa imepakwa rangi,niliendelea kumshangaa yule afande kunizungusha nyuma ya ile nyumba na kukutana na kaburi kubwa likiwa limeng'arishwa kwa kuezekwa marumaru nyeupe zilizong'aa mithili ya kioo,huku katikati kukiwa na picha kubwa.. "Uuuuwiii..! Uuuuwiii...! Uuuuwiii...!Baaaba umeniacha...! Najua mimi ndo chanzo..,Nisamehe baba yangu...! Baaaaaaaabaaaaaaa...!!


" Nililia sana na kwa sauti ya juu huku nikiamini ile picha ni ya baba yangu na pale tulikuwa eneo la nyumbani kwetu japokuwa hakukubadilika sana,sauti ya juu niliokuwa nikilia iliwafanya majirani kuja kushuhudia pale huku mlango wa nyuma ukifunguliwa.. "Maaaamaa..! Maaamaa...! Mnisamehe miiimi..." * * * * * Afande Deus ndo jina lililokuwa likitambulika sana kazini alipolitumikia jeshi la polisi, weusi na urefu ukichangia kuwa na mwili mkubwa ni kati ya vitu vilivyomfanya kuogopeka katika jamii haswa ukizingatia ukali aliokuwa nao akiwa kazini, hakuwa na cheo sana lakini uonekano wake ulimfanya aonekane kama mtu mwenye cheo kikubwa, Kazi yake kubwa ilikuwa ni kusindikiza watuhumiwa wa kesi mbalimbali mpaka mahakamani na kuwarudisha tena rumande huku akisaidiana na mapolisi wenzake, Alianza ukaribu na Baba yake Levina toka kipindi kile cha kesi ya Levina na hii yote ni kufanya levina anakuwa huru,alijitahidi sana mpaka kuwashawishi wakubwa wake ili Levina awe huru lakini ilishindikana na matokeo yake alisimamishwa kazi kwa mda mrefu wakamfanyia upelelezi ikaonekana hakuna ukweli ndani yake hivyo baada ya mda mrefu kidogo akarudishwa tena kazini lakini haikuwa mwisho wa kuwa karibu na Baba Levina kwani hata alipofunga ndoa msimamizi wake alikuwa ni Baba yake Levina na alizawadia gari ndogo ya kutembelea, Tayari walikuwa kama familia moja na hata Baba Levina alipofariki afande Deus aliumia kweli kwani alifanyiwa mengi sana ikiwa ni pamoja na kununuliwa kiwanja na kusaidiwa pesa kidogo za kujenga. Afande Deus aliahidi hata siku Levina akiwa huru atamsaidia kwani ilikuwa ni vigumu kumfatilia tena Levina Gerezani akiwa kama afande anayejulikana na aliyewahi kusimamishwa kazi kwa kesi ya huyo huyo Levina.. Akiwa bado kikazi na magwanda yake ya kipolisi na bunduki yake akitokea chalinze kuwasindikiza wazazi wake waliokuja kumtembelea Dar, alikutana na rafiki yake waliyewahi kusoma pamoja ambaye ni trafiki, kwa utani waliozoeana aliweza kukagua mabasi mawili ndipo akamgundua Levina alikuwepo kwenye basi moja wapo.,lakini ili kuua soo ilimbidi ajifanye mkali ili aondoke naye kiulaini...

~ BAADA YA MIEZI 9 ~ "Umesema kapanda basi lipi?" "Sijui vizuri lakini likizo zote huwa anapanda basi la 'HOOD'" Haraka haraka,nikatoka mbio kuelekea nyumbani nikampita mama sebuleni akinishangaa ndani ya dakika tatu nikatoka nikiwa nimevalia kiblauzi cha mikanda cha pinki chini nikipigilia kipedo changu cha jinsi huku chini kabisa nikiwa nimevalia viatu vyeupe aina ya 'makhirikhiri' usoni nikiwa na zile miwani kubwa za kuzuia jua na hivi kamwili kalikuwa kamesharudi,mtoto figa ninayo,makalio ndo usiseme, yaani daaah...!

Natamani kama ungeniona hivi? Kwani sikuwa tena Levina yule mliokuwa mnamjua zamani, Nilijipenda sana na hii yote ni kufanya Gervas na jamii kwa ujumla inione si Levina yule waliyekuwa wanamjua kipindi kilee cha matatizo., Nikiwa ndani ya daladala iliyoukuwa inatokea kariakoo na kuelekea ubungo kumpokea Gervas aliyekuwa amemaliza masomo yake ya kidato cha Nne huko Iringa., Nikiwa nimekaa siti ya pembeni na Mmama nisiyekuwa namfahamu nadhani ni kutokana na mavazi aliokuwa amevalia aina ya 'baibui'.. Tayari ilikuwa ni alasiri kwani hata saa yangu ya pinki aliyeninunulia afande Deus ilinionesha imeshatimia saa kumi na robo na Gervas alikuwa aingie mida ya saa kumi na mbili kwenye na nusu., nikiwa tayari nipo kwenye foleni maeneo ya manzese huku nikizubaa kwenye gari kutokana na kuwa na mawazo na shauku kubwa ya kumuona Gervas.., "Hapo dada, hapo mjomba..." Mama hapo... " Ilikuwa ni sauti ya kondakta akidai nauli za daladala.. "kaka si nimeshakupa? Unataka nini sasa?" Alilalamika kwa konda yule mama aliyekuwa pembeni yangu huku akioneshwa kuchukizwa na kitendo cha konda kumdai nauli mara mbili mbili, Tukiwa ndo tunaingia ubungo niliweza kumshuhudia yule mama akitoa baibui yake katika paji la uso huku akisogeza simu yake karibu na sikio aweze kuzungumza na simu.. "kumbe namfahamu..!Mshenzi mkubwa we unabahati sana...!" Alikuwa ndo yuleyule mama niliyowahi kumuota namnyonga na mtandio pia ndo yule aliyewahi kuniharibia maisha yangu enzi zile, Sikutaka tena ugomvi kabisaa kwani afande Deus alinisihi mambo mengi sana ya kujihadhari nayo ikiwemo ugomvi usiokuwa na maana.,Hasira na chuki zilinishika lakini sikuweza kukabiliana naye.., Saa yangu ilikuwa tayari inaonyesha ni saa kumi na mbili kama na dakika ishirini,Nikiwa tayari nimeshaingia mule ubungo ndani ya stendi ya mabasi. Hatimaye basi la 'HOOD' likaingia,watu ni wengi walioshuka,kila walipokuwa wanashuka ndivyo mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio,ghafla nikahisi kama kuna mtu ananigusa mgongoni nikajikuta nageuka bila kuangalia na kumkumbatia..

"Waaaooo Gervas...!" Maskini aibu kubwa ilinishika watu wakabaki wakinishangaa kumbe hakuwa Gervas.,bali alikuwa ni Mama aliyejitambulisha kwa jina la 'Mama Ali' huku akiwa na mtoto wake 'Ali' na vijana wawili wakiume waliovalia miwani meusi huku wakizunguka zunguka kuashiria wanakuja kumpokea ndugu yao., "Samahani binti mimi si Gervas.." "Nimeshajua hata mimi nimekosea ila naomba nisamehe" "Hamna neno kwani huyo Gervas ndo unamsubiria..?" "Ndio mama..ni ndugu na pia jirani yangu wa siku nyingi.." Nikiwa bado namjibu yule Mama aliyejitambulisha kama 'Mama Ali' mara nikamuona Gervas akishuka bila kuchelewa nikamuwahi na kumkumbatia,kisha wale vijana wakamuwahi na kuonesha vitambulisho vya kazi zao kilichofuata nikumshuhudia Gervas akifungwa pingu mbele ya macho yangu. "Kafanya nini tena..? Muacheni jamani..,muaaaaaaaaacheni...!" Nilihisi kama ndoto lakini ilikuwa kweli Gervas kafungwa pingu bila kujua kosa lake., "Geeervaaaaaas...!" * * * *

Taarifa za juu ya kifo cha 'Baba Ali' zilienea sana ikiwa ni kuanzia Kwa majirani Mpaka kwenye vyombo vya habari,siku ya Mazishi 'Mama Ali' alizimia mara mbili ikiwa ni pamoja na kupata pigo la kuachwa na mtoto ambaye ni Ali tena mdogo sana akiwa na miaka 4 tu, Upelelezi juu ya kifo cha Baba Ali ulifanyika kwa haraka zaidi na kuanzia usaidizi wa Majirani ambao walimshuhudia mtu wa mwisho aliyeingia ndani kwa Baba Ali hakuwa mwingine bali ni Levina japo majirani walimtambua kwa sura tu na si kwa jina., Uchunguzi uliofanywa kwa kina ulibainika kukutwa na karatasi mbili mifukoni kwa Baba Ali ambazo zilifinyangwa sana na zilionesha ramani ya anapoishi Baba Ali ambaye si huyu aliyeuliwa, Polisi walifanikiwa kumkamata Baba Ali mwenyewe na kumuweka hatiani kisha akafanikisha mpaka jinsi ya kumpata Gervas,hivyo polisi kwa kusaidiana na Mama Ali wakawa tayari stendi ya ubungo wakimsubiri Gervas,ambapo ilisemekana ameshapanda basi aina ya 'HOOD' hivyo kuanzia saa kumi na mbili atakuwa ameshafika Mama ali akisaidiwa na mapolisi wawili huku akishikilia picha ya Gervas aliyopewa na Baba Ali waliyemuweka hatiani kule Morogoro,wakafanikiwa kumpata Gervas., ************ * * * Je.,Nini hatma ya Gervas? * * * Na Levina atakamatwa kweli? Na itakuwaje akikamatwa?
 
SEHEMU YA 10

Nikajikuta navua viatu vyangu na kuvishika mikononi huku nikiitupa ile miwani kwani niliona haina umuhimu tena kwangu, Nilijitahidi sana nisiweze kupiga makelele eneo lile, nikabaki nafuta mchozi tu huku nikiwafatilia polisi kwa nyuma nijue watampeleka wapi,nikawaona wakiingia kituo cha polisi pale pale ubungo,nikashusha pumzi,kisha nikatazama ni jinsi gani naweza kuongea na Gervas,nikiwa bado najifikiria pale ghafla nikapigwa kikumbo na Mama Ali., "Na huyu hapa tumchukuwe aliniambia ni ndugu yake..!" "Nani..? Mimi...!,hapana...!, aah...! aah..!"

Nilijikuta namkana Kama Petro alivyomkana Yesu mara tatu,huku nikijifanya kama simjui Gervas kwakuwa nilikuwa tayari nilishalikoroga nilipomwambia mwanzoni kuwa Gervas ni ndugu na jirani yangu., "We binti.? Embu potea hapa haraka...!" Aliongea kwa sauti ya juu askari mmoja pale huku kanikazia macho. "Hapa leo siendi popote kama kurudishwa gerezani wacha nirudishwe mie na sio Gervas ambaye hana hata hatia.." Nilijisemea kimoyo moyo huku naongoza njia ya kutokea, " Lakini haiwezekani narudi, aah...! aah...!" Nilijikuta narudi tena huku nikiangalia saa yangu ikinionesha ni saa mbili kasoro usiku, hilo sikulijali kikubwa ni jinsi gani nitamtoa Gervas,Nikajikuta halmashauri yangu ya kichwa inafanya kazi fasta na kuchukuwa simu yangu tayari kwa kumpigia 'Afande Deus'.., "Haloo... Shikamoo Baba Deus..! Nipo hapa polisi "Wapi.? Na umefanya nini tena Levina...?" "Nipo hapa kituo cha polisi ubungo ndani ya stendi ya basi..." Nikiwa bado naendelea kumuelekeza Afande Deus nilipo,nikashangaa ananikatia simu.. Nilizidi kuumia moyoni kwani mi ndo nlikuwa mtu wa kumsaidia Gervas ili aweze kutoka pale., Ilimchukuwa lisaa tu kwa afande Deus kuweza kufika eneo lile,nikamshuhudia akipitiliza na kuingia ndani kituoni nadhani hakuniona vizuri nilipo hivyo nikamfuatilia kwa nyuma, "Jambo afande" "Habari, kuna binti yangu yupo humu ndani..?"

"Hakuna binti yeyote aliyeletwa leo humu....!" Wakiwa bado wanajibizana nikajitokeza kwa nyuma taaratibu huku nikinyata., "Mimi hapa Baba...!" "Twende nyumbani..!" Alinichukuwa kiaskari zaidi huku nikitetemeka na kuelekea upande aliokuwa amepaki gari yake,nikaingia na kupanda gari yake kabla hajaondoka nikamwambia ukweli, "Baba...!" "Unasemaje tena..?" "Aliyekuwa amewekwa ndani siyo mimi..?" "Nani sasa..?" "Ni Gervas..." "Naaaaaaaaaaaaaaaan.!" * * * * Nikiwa nimetulia kwenye gari peke yangu huku nikimwacha Afande Deus akirudi tena kituoni kumalizana na mapolisi wenzake kuhusu kutoka kwa Gervas, haikuchukuwa mda nikamwona anarudi peke yake huku akitingisha kichwa kuashiria kuwa kashindwa kumtoa Gervas, "Wamesemaje..?" Nilijikuta naropoka nikitaka kujua.. "Imeshindikana mpaka kesho kwani ni kesi kubwa sana..!" Miguu ilinilegea,mwili ukaingiwa na ganzi,kichwa kikawa kizito mda huohuo huku nisijue nini cha kufanya, gari ikawashwa tayari kwa kwenda nyumbani., Baada ya nusu saa tukawa tumeshaingia nyumbani kwani njiani hakukuwa na foleni kabisa,tuliweza kuingia nyumbani kwakuwa afande Deus alikuwa na haraka akaniacha nje na kuniaga kwa kuniambia kuwa kesho asubuhi atadamkia kwa Gervas,nikamuitikia na kuingia ndani, Nilipoingia ndani nikakuta hali si shwari kwani Mama alikuwa akilia sana bila kujua nini tatizo, "Au kwasababu nimechelewa kurudi..?"

Nilijikuta najipa maswali yasiyo na majibu, Nilijaribu kumnyamazisha lakini ilinichukuwa mda mpaka akanyamaza na kwikwi ikamuisha kisha akanipa barua aliyokuwa ameshikilia,nikaichukuwa na kuanza kuisoma huku presha ikinipanda na kushuka,nikiwa natetemeka.. Niliendelea kuisoma ile barua huku nikihisi kichwa changu kizito,huku ganzi ikinijaa mwilini,kadri nilivyokuwa naendelea kusoma ndipo kizunguzungu kikanizidia.., "LEVINA CHRISTIAN" Unahitajika Mahakama ya mwanzo mkoani Mbeya haraka upatapo barua hii.. Uchunguzi wa kina uliofanywa na jopo la Madaktari kutoka Iringa imebainika kuwa Marehemu Pendo amefariki kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mwili wake kuokotwa porini huko Iringa, Na siku alioachiwa huru gerezani alikuwa na wewe Levina Christian ambao wote mlikuwa wafungwa, hivyo ukiwa kama mtu ambaye uliongozana naye kutoka gerezani mara ya mwisho unahitajika na mahakama haraka iwezekanavyo kwa ushahidi juu ya kifo cha Pendo Abel..." Nilipomaliza tu kuisoma nikamgeukia Mama nakuanza kwani alikuwa bado anaendelea kulia tena kwa sauti ya chininini, kichwa na akili yangu vikiwa havifanyikazi, nilijihisi kujiharishia huku nikiwahi kulibana tumbo langu lililokuwa linaunguruma kwa kasi kisha nikamtazama mama yangu. "Nani ameileta hii barua..?" "Vijana wawili waliovalia nguo za kiraia wakiwa na gari..." Sikuhitaji kujua la zaidi,nilichofanya ni kumuhadithia Mama yote yaliyonikuta kuhusiana na Gervas, "Mama haiwezekani,inanibidi leo leo tena sasa hivi nifanye juu chini tena kabla hata afande Deus hajajua kitu chochote niwe nimeshaondoka na kwenda kulimaliza hili tatizo najua kesho asubuh Gervas atatolewa kwahiyo Mama nakuomba Gervas usimwambie lolote juu yangu" "Mama nakuomba sana.,sana tena sana.., Hii barua na hata hizi taarifa asizijue afande Deus,atashindwa kunisaidia kumtoa Gervas..!" "Mwanangu kwanini ni wewe tu jamani..? .......

Kwanini mikosi yote inakuja kwako tu..?" Aliongea kwa sauti ya kukwaruza kuonesha kwamba amelia sana na sauti inataka kumkauka.., "Mama Naumia na nitaendelea kuumia.,Najua na wewe unaumia lakini ninachokuomba uwe na moyo wa subira nitarudi salama tu wala usihofu? "Sawa mwanangu..,ila chunga sana mwanangu.." Haraka bila kupoteza mda nikaingia chumbani kwangu na kuvaa suruali yangu ya jinsi,nikajivika tsheti yangu ya kijani iliyokuwa na maandishi makubwa kwa mbele yaliyosomeka 'YOTE MAISHA' chini nikadondoka na raba za rangi ya kijivu,kisha nikachukuwa kijibegi changu cha mgongoni, nikatoka sebuleni na kumuaga mama, "Chukuwa hii itakusaidia huko ukipatwa na matatizo itakuepusha nayo" Alinivulia cheni yake ya dhahabu kisha akanivalisha, "na hii nauli itakusaidia uko uendako" Akafungua upindo wa kanga yake na kunipa kiasi cha shilingi elfu sabini, Haikuwa na jinsi ilinibidi nichukuwe hivyo vitu kisha nikafanya ishara ya msalaba na kuondoka zangu huku nikimsisitizia Mama afanye juu chini Afande Deus asijue chochote na amdanganye vyovyote, Sikuhtaji Mama anisindikize kwa usiku ule kwani nilijua kabisa inaweza kutokea Afande Deus akaja pale usiku kwa kushtukiza, Nikiwa nje natoka naelekea stendi ya mabasi japo nikaambulie gari lolote,nikashangaa mwanga mkali wa gari ukinimulika machoni,nikiwa najaribu kujizuia na kulikwepa mara nikashuhudia likisimama mbele yangu.. "Levina...! Levina...! Levina...! Unaenda wapi usiku huu., Hapa huwezi kututoroka hata mara moja,Na tupo hapa nje tangu ulipoletwa na Afande Deus..!" Moyo ulilia paaah..! Kisha nikahisi kama mlango unafunguliwa nyumbani nilipotoka, "Kwani nyie wakina nani?" "Huitaji kujua ila utajua ukifika mahakamani kule mbeya" Nikashuhudia afande mmoja akishuka kwenye gari kisha akanifuata na kunifunga pingu haraka akaniweka kwenye gari aina ya 'Toyota land Cruiser' nyeupe., Niliumia moyo,nguvu nilikuwa tena sina nilipojaribu kuangalia nyumbani macho yalikutana na Macho ya Mama yangu akiwa amesimama mlangoni huku macho yake yakionesha kuwa na simanzi tele,mara gari ikitoka pale kwa kasi ya ajabu.. "Mwanaangu....!" Ndio neno la mwisho nililoweza kuambulia kwa mama huku akiniliza na kunisisimua mwili wote kwani alinikumbusha aliniambia hivyo kipindi kile nahukumiwa mahakamani., * * * *

Safari ilianza kuanzia Dar lakini tulipofika Morogoro nilijikuta Nalia sana kutokana na mauaji niliyoyafanya ila nikajipa moyo na tulipofika Iringa haswaa tulipofika kijiji cha 'Liamkena' machozi mengi yalinitoka huku nikilia kwa sauti ya chini chini na kwikwi kwa mbali kila nikikumbuka mateso niliyopata pale kwa wale wanafunzi,pia nilipomua rafiki yangu Pendo bila kukusudia, Nilipigwa na baridi lakini sikuweza kulisikia nadhani hii ni kutokana na kuchanganyikiwa kwanza ni kuwaza itakuwaje kwa Gervas asubuh pili huko niendako kutoa ushahidi, Ilituchukuwa masaa kama kumi na moja mpaka kufika Mbeya, Tulifikia mahakamani moja kwa moja kwani kesho yake ndo kesi itasomwa ila nilishangaa kupelekwa pale mahakamani asubuhi asubuhi, wale askari wakanichukuwa hadi kwenye ofisi nisiyoifahamu pale pale mahakamani, nikiwa nashangaa shangaa huku na kule ghafla nikashangaa nasemesha kwa upande wa nyuma yangu.. "Hujambo binti..? Za masiku..?" Alikuwa ni baba yake na Pendo yule niliyomdanganya kipindi kile kuwa nafanya kazi za ndani na sasa alikuwa pale ofisini.. "Ba..a..a..a..a..b..a...Pe..ndo...Mi sijamuua mtoto wako.. ********************
 
SEASON 2
SEHEMU YA 11


"Niliendelea kuisoma ile barua huku nikihisi kichwa changu kizito,ganzi ikinijaa mwilini,kadri nilivyokuwa naendelea kusoma ndipo kizunguzungu kikanizidia.., Ndio maneno ya mwisho ninayoweza kuyakumbuka kwani nilivyoshikwa na kizunguzungu wakati naisoma ile barua iliyokuwa inaelezea kuvunjwa kwa nyumba za mtaani kwetu huku na nyumba yetu ikiwemo, ukijumuishwa na upande wa nyuma kulipokuwa na kaburi la marehemu Baba ukisisitiziwa utabomolewa upande wote wiki hii,ndicho kilichomuumiza na kumliza sana Mama,na ilinifanya mwili wangu ujae joto haraka,kuanza kutetemeka na hapo hapo niliitupa ile barua huku nikidondoka na kupoteza fahamu.., * * * * "

Yuko wapi Gervas..?" Ndio neno nililoweza kulitoa baada ya kuzinduka pale hospitali Juhuku nikishangaa nimetundikiwa dripu na kujua kuwa kumbe zile zote zilikuwa ni ndoto na hisia za ajabu eti mpaka napelekwa mahamakani,Nikakutana na 'Baba Pendo' na kuanza kumlilia kuwa sijaua, "Ooooohhh...! Uuuuuuuuhhh..! Mungu waaaaangu..! God forbid.....!" Nilijikuta nalitoa hilo neno la kiingereza japo sikuwa najua maana yake kwani nilimsikia mara nyingi Afande Deus analitumia anapokabiliwa na matatizo,huku kichomi kikinizidi kuniuma na kupumua haraka zaidi.. Kucheki pembeni yangu nikamshuhudia Mama akiwa amenishikilia dripu tena akiwa bado machozi yakimlengalenga kuonesha kuwa bado analia huku akinitazama.. "mwanangu...! nisamehe mimi...! mwanangu...! Najua mimi ndo chanzo cha yote hayo...! "Najuta kukuonesha ile barua....!" "Hapana Mama kwani mbona mimi mzima tu....!" Nilimjibu Mama bila ya kuwa na wasiwasi wowote huku nikijiamini mimi ni mzima tu, "Usilie mama...." "Hapana mwanangu.... Daktari amesema kuwa u..." * * * * * Juhudi za afande Deus kumtoa Gervas katika kituo cha Polisi pale ubungo zilifanikiwa kwani alikuwa akiheshimika na kufahamika hivyo alijitahdi kumtetea Gervas kwa kila njia mpaka akafanikiwa lakini ilikuwa kwa masharti kuwa Gervas hatakiwi kabisa kuönekana Dar es salam na Tanzania kwa ujumla kwani kuonekana kwake kutamletea matatizo makubwa Levina ikiwa ni pamoja na kuwekwa Gerezani tena kwa mara ya pili,hivyo Afande Deus alichokifanya ni kumchukuwa Gervas moja kwa moja mpaka kwa wazazi wake kisha kuwapa masharti aliyopewa baada ya kuafikiana wazazi wa Gervas wakahaidi kumtorosha Gervas na kwenda kuendelea masomo yake nje ya nchi, Mwanzoni Gervas hakuliafiki kabisa na yote hiyo ni kotakana na kumpenda sana Levina kutoka moyoni,lakini baada ya wazazi wake kumsema sana ikabidi wakubaliane tena kishingo upande kuwa ataondoka tu haina jinsi, Walienda nyumbani kwa kina Levina asubuhi asubuhi lakini waliwakosa hivyo Afande Deus akampigia simu Mama Levina na kuambiwa kuwa Levina kalazwa na wapo hospitali ya 'Ocean Road'.. * * * *

......Kabla Mama hajamalizia kuongea Mara akaingia Afande Deus akiwa na Gervas pamoja na Wazazi wa Gervas.. Nilijihisi nimepona pale kitandani lakini kila nikitaka kunyanyua mkono niinuke nilishindwa, "Nesi...! Nesi..! Nesi....!" Msaada hapa....!, Msaada Nesi...!" Ilikuwa ni sauti ya Mama iliyokuwa ikiomba msaada kwa Nesi aje kwangu kunisaidia.., Nikashuhudia Nesi akija haraka kunihudumia huku akiniinua mgongo.., Kisha akamwambia kitu afande Deus na Mama.. "Huyu mnyanyueni taratibu,kwani upande huu wote wa kushoto haufanyi kazi kabisa.., Hapo hapo Halmashauri yangu ya kichwa ikagundua moja kwa moja neno la mwisho alilokuwa anataka kuniambia Mama kabla afande Deus hajaingia ilikuwa ndo hilo kuwa nimepooza upande mmoja., Nilijikuta kama mtu asiye na bahati hapa duniani ikabidi nikabiliano nayo, "Pole Levina utapona usijali..." Sauti ya chinichini tulivu iliyopenyeza kwenye maskio yangu ikitokea kwa Gervas huku akionesha kuwa anahuzuni sana machoni, "Nakupenda Gervas....!" "Nakupenda pia Levina..!" Bila kuonesha woga wowote kutoka kwa wazazi wa Gervas na kwa kujiamini niliweza kuiona mikono ya Gervas ikinipapasa katika mkono wangu mmoja kwa kuteleza nikibaki namtolea jicho la aibu kisha akashika ile dripu huku akiugusa kwa kuupapasa ule mrija wa kupitishia damu na kuanza kutoa mchozi huku akiniangalia kwa huruma,Haraka pale nikashtuka kwa msisimko uliokuwa unaendelea kisha Nikabadilisha mada kwani afande Deus alikuwa akinitolea macho sana... "Vipi mmeshayamaliza huko Polisi..,

Kabla hajanijibu Gervas nikamwona Nesi ameshawasili kwenye wodi niliyolazwa na kuwafukuza watu lakini sura ya huyu Nesi haikuwa ngeni machoni mwangu ila sikuweza kuwa na kumbukumbu vizuri kutokana na fahamu kutonirudia vizuri na kwa haraka... "Jamani wapendwa mda wa kuona wagonjwa umeisha..., Tunawaomba muondoke sasa ni zamu ya daktari kuja kumtibia mgonjwa wenu.." Iliongea kwa ukali tena mara mbili mbili ile sauti ya Nesi wa zamu aliokuwa amevalia mavazi rangi ya machungwa., "Levina..,Ugua pole, Jioni tutakuja tena kukutembelea na kukuletea chakula..." "Haya...,Ahsanteni" Nikawajibu wazazi wa Gervas na afande Deus kwa sauti ya upole kwani hata na sauti yangu ilishindwa kabisa kutoka.. kisha hao wakaondoka huku Mama akiwatoa nje na kuniahidi kuwa kesho asubuhi watakuja tena kunitembelea.. * * * * Mpaka kufika saa Kumi na Mbili jioni hakuna mtu yoyote aliyekuja kututembelea hivyo Mama alinilazimisha kula chakula (mtori) kile cha mchana nilichokuwa nimewekewa katika hotpoti nikala na kupumzika, Sikuweza kupata usingizi kabisa,sauti tulivu za ndege kwa mbaaali na mlio wa maji ya bahari niliyokuwa naiskia kutoka nje ya hii hospitali ya 'Ocean Road' ndo kati ya vitu vilivyochochea hisia zangu za mimi kuanza kupata usingizi taaaaratibu, Hata hivyo ilipotimia saa saba za usiku usingizi ulikuwa tayari umeshaanza kunipitia huku Mama yangu akiwa amejiegesha upande wa pembeni yangu akiniangalia kwa msaada, Kitanda cha pembeni yangu kulikuwa na mgonjwa aliyekuwa analia sana huku akihitaji msaada wa Nesi,Punde yule Nesi aliwasili na ni yule niliyemwona mchana na ndiye aliyewaondoa kwa mara mwisho wakina Gervas hapa hospitalini, "Nimeshamkumbuka huyu mshenzi...! Nilishaweka ahadi na kuapa lazima nimteketeze huyu mtu...!" Hasira zilinijaa sana kwani sikuamini kuwa huyu Mama atakuwa Nesi? "Ina maana siku zote ni Nesi..? Mungu wangu nani aliyempa kazi...?"

Ni kati ya maswali yaliyonishtua baada ya fahamu kunirudia vizur na kugundua kuwa huyu alikuwa ni yule Mama aliyenifanya mpaka nimekuwa hivi,yule ambaye nilikuwa namuota ovyo kwenye matukio mojawapo lile la kumnyonga na mtandio,na hata juzi nilivyoenda kumpokea Gervas tulipanda naye dalalada japo sikumgundua vizuri mpaka alipovua baibui yake tena kwa mbali ndo nikawa nimemgundua.. Kila nikimwangalia pembeni yangu ndivyo hasira ilinizidi kuninyemelea akilini mwangu kwakuwa nilikuwa sina nguvu tena upande mmoja kwa kupooza nilijikuta naropoka kwa sauti ya chinichini bila yeye kusikia.. "Unabahati sana nimepooza...kwani ilikuwa ni safari yako sa hivi..." Kisha nikajiegemeza taratibu kutafuta tena usingizi, Baada kama ya nusu saa usingizi ukawa umenipitia na kilichokuja kunishtua ni Mkojo uliokuwa umenibana ukiambatana na haja kubwa pia nilikuwa najisikia kizungu zungu sana huku kichefuchefu kikinishika niliweza kumwamsha Mama na kumuelezea ikabidi amuite Nesi...., Alitoka na kwenda mbio na kumuita Nesi, Punde akarudi naye, "Hata kama naumwa....,lazima nikumalize..., Mmbeya mkubwa wee...!" Niliongea taratibu na kuachia fyonyo kali huku nikimwacha yule Nesi pamoja na Mama wakishtuka na kushangaa wasielewe imekuwaje pale, kilichofuatwa yule Nesi alichukuwa kibaiskeli cha kupakizia wagonjwa na kunichukuwa tukatoka wote kwa pamoja na Mama lakini tulipofika mlango wa chooni nilimsikia yule Nesi akimwambia kitu Mama... "Mama...! Mama....! wewe usisumbuke huyu wacha niingie naye nimhudumie mimi tu..!" "Hapana Mama twende wote...!" "Levina acha ubishi..! Hata huyo atakusaidia tu kama mimi..!" Nilimbishia Mama kwani niliamini kabisa yule Nesi tayari alikuwa ni adui yangu na anaweza kunidhuru... Basi tukaingia chooni kisha yule Nesi akafunga mlango kwa ndani kwa kutumia ufunguo huku tukimuacha Mama nje akitusubiria.. "We muuaji upo..? !...Umetoka gerezani lini..?" Alianza kuongea kwa dharau huku akinibenulia mdomo wake lakini mimi Nilikaa kimya huku nikimwangalia yule Nesi akichomoa dripu ili aweze kuniinamisha choöni niweze kujisaidia.. ".....Kama uko gerezani walikuacha leo mi sikuachi......!"

"....kwani nimefanyaje...?" "..Ssshhhh...! We si Levina yule muuaji aliyewekwa gerezani miaka kama sita au saba iliyopita...?" "Aaaahhh....! Aaaaaahh....! Si...o..o..o.. mi..m..i.." Nilimjibu kwa kujiuma uma kisha nikashangaa kitendo kilichofanyika pale kwani alichukuwa kichwa changu akaniinamisha kwenye tundu la choo tena kile choo cha kuflashi kwa mda mrefu.., Nilishindwa kuongea chochote kwani sura yote ilikuwa imeinama kwenye tundu la choo, sikuwa na nguvu kwani upande wangu mmoja ulikuwa umeshapooza,kwa lile tukio nilijikuta natoa haja kubwa na ndogo papo hapo... "Nyoooooo...! Ushajinyea enhh..? Maana harufu ya kinyesi chako kishaanza kunuka tena sanaaaaaa.." Aliongea kwa sauti ya chini chini ambayo mtu yeyote hawezi kuisikia kisha akanivua nguo yangu ya ndani ambayo ilikuwa tayari na kinyesi na kuitupia kwenye tundu la chooni likawa limetapakaa kile kinyesi changu kisha kabla hajaflashi akinikamata shingo tena kwa nguvu na kuniinamisha tena kwa mara ya pili chooni, maskini Levina mimi nilijikuta nakutana na kinyesi changu,huku nikikosa pumzi nilijikuta naachia mdomo wazi hivyo mdomo wangu ukakutana na kinyesi changu mwenyewe,nilikuwa sina jinsi zaidi ya kujikuta nikikimeza, Alinifanya atakavyo kisha akaflashi kile choo huku kichwa changu kikiwa bado mule ndani ya choo,nilitapika sana,maskio yaliziba kwa mda na macho yakawa kama kipofu kwani sikuweza tena kuona mbele kwa mda ule zaidi ya kuhisi bado nimekabwa shingoni.., ".....Bado hujafa tu....!" "Utakufa wewe......! sio mimi....!" Nilimjibu kwa hasira ya hali ya juu huku nikizidi kumchochea na kumjaza hasira tena yule Nesi akiendelea kunitolea mimacho.. "..Unajifanya mbishi enh...? ...Hapa nakutoa maiti tu nampa Mama yako akakuzike muuaji mkubwa wee..." Ghafla nikamshuhudia yule Nesi akiingiza mkono kwenye mfuko wa gauni lake na kuchomoa vile Visu vidogo vikali vya kufanyia operesheni na kuanza kukata kata mirija ya ile dripu ikaanza kuvuja kisha akaniangalia usoni.... "Embu niambie wewe Muuaji nikuanze wapi...? Halafu uanze kusali sala zako za mwisho hapahapa...!" "Tuuuhhh.....!

Tuuuuhh...! Nikamtemea mate usoni mwake kwani nilikuwa sina nguvu za kumpiga, akakasiria na kunitoa kwenye kile kigari.. "Haya simama tupigane sasa...! Simama wewee..!" Alinitoa kwenye kigari akinitaka nisimame,sikuweza kusimama kwakuwa nilipooza upande mmoja hivyo nikadondoka moja kwa moja mpaka chini huku nikiwa uchi wa mnyama.. Alichoanza kukifanya ni kuchukuwa miguu yangu miwili na kuitanua,kisha akiwa kashikilia viwembe vyake tayari alikuwa amenishika matiti yangu na kutaka kuyakatakata.., Akiwa anataka kunikatakata na vile viwembe mara Mama akaanza kugongo hodi kwa nje.. "Nesi...! Nesi...! Nesi...!Bado hamjamaliza tu..! Levina....! Levina...! Levina....! Mwanangu...!" Nilitamani niitike lakini tayari vile viwembe vilikuwa mdomoni mwangu., "Ole wako uitike...! Nakuchana chana sasa hivi..!" "..Namvalisha Mama tunatoka sasa hivi...!" Aliongea kinafki yule Nesi huku akinivalisha haraka haraka kisha vile viwembe akavitupa kwenye tundu la choo naku flashi.. Alinitoa pale nikiwa sijielewi ila ninachoweza ni kutoa macho na kusikia sauti kwa mbaaali sana, huku yule Nesi akinikokota na Mama mpaka wodi yangu wakanilaza, Baada ya mda kidogo nikaanza kusikia sauti kwa mbali ya minong'ono nilihisi tu atakuwa ni Mama na Nesi wakizungumza.. "Yani Mama..Mtoto wako alinisumbua sana kule chooni..!, haswa pale alipohtaji kujisaidia kwani ilikuwa ndo mara yake ya kwanza ndo mana tukawa tumechelewa kutoka..!" "Usijali mwanangu...asante kwa msaada wako Mungu atakubariki...kaendelee na kazi tu...!" Nilitamani niropoke pale pale lakini sikuweza kumuonesha wazi Mama kama namchukia sana huyu Nesi pia kwa vitendo alivyonifanyia.. Sikuweza kupata usingizi kabisa zaidi ya kutoa macho mpaka alfajiri kulipopambazuka na kumshuhudia Gervas akiwa mtu wa kwanza akiingia pale wodini.. "Shikamoo Mama..!"

"Marahaba mwanangu Mama na Baba umewaacha wazima..?" "Wazima tu Mama" Taratibu Gervas akaweka ule mfuko aliokuja nao ukiwa na chupa ya chai na ki hotpoti kidogo japo sikujua ndani yake kunanini..,kisha Gervas akanisogelea kitandani na kuongea na mimi huku akitokwa na machozi.. "vipi unajiskiaje Levina toka tulipokuacha...!" Sikuweza kumjibu kwani sauti ilikauka nikabaki machozi yakinichururuzika mithili ya maji ya sabuni yakiteleza mwilini, "Levina...! Levina....! Naomba japo nisikie sauti yako jamani...!" Nilipenda sana nimuitikie Gervas nakuongea naye lakini ilishindikana kwani kitendo alichokuwa amenifanyia yule nesi kilinifanya nishindwe kufanya lolote., * * * * ~ NYUMBANI KWA KINA GERVAS ~ Wazazi wa Gervas hawakulala walifanya juu chini kuhakikisha Gervas anaondoka, mchana wa jana yake uleule waliotoka hospitalini walianza kufanya mipango na watu wa uhamiaji kwa ajili ya kumhangaikia pasipoti yeye Gervas na Baba yake,kwahiyo leo watachukuwa pasipoti zao na ndani ya siku mbili watakuwa wameshapata Viza ya kuingia Marekani.. Gervas alijitahidi sana kufanya kila liwezekanalo awe amemuweka Levina wazi lakini haikuwezekana kutokana na hali aliyomkuta nayo Levina.. ~ HOSPITALI ~ Kweli hujafa hujaumbika mpaka leo siku ya pili na sasa hivi jua linaelekea kuzama hakuna hata ndugu yeyote aliyekuja kunitembelea zaidi ya Gervas na Mke wa Afande Deus kuja kuniletea chakula,Nilijiona tangu matatizo yangu ya jela ukiongezea na haya yamenifanya nitengwe na ndugu mpaka baadhi ya Majirani.. "Kwanini ni mimi na mama yangu tu....! Kwanini wanatunyanyapaa kama wagonjwa wa ukimwi....?" Hayo maswali niliojiuliza yalinifanya hata nishindwe kupata chakula kwani hasira iliniongezeka maradufu na kubaki namuangalia Mama huku mchozi ukinidondoka taratibu.. "Kula basi mwanangu upate nguvu....!" Niliitikia kwa kutikisa kichwa nikimaanisha siwezi kula kwa mda ule lakini alinielewa... "Kunywa basi angalau uji wa ulezi umechanganywa na maziwa ni mtamu sana mwanangu....!" Nilikubali aninyweshe ule uji,nilikunywa japo taratibu sana..,mara nikatapika uji wote..,niliumia sana kwani Nilimuona yule Nesi mbaya wangu na ndio aliyenifanya nitapike,haraka haraka akaja... "Ooohh...!

Pole mgonjwa enhh...! Mama embu lete huo uji nimmnyweshe mwenyewe...!" "Chukuwa mwanangu labda wewe kwakuwa Nesi atakubali kunywa bila hata kutapika....!" Kila nilipotingisha kichwa nikionesha kukataa Mama hakunielewa,akamkabidhi yule Nesi kibakuli cha uji kikiwa na kijiko aninyweshe... "Nesi...! Nesi...! Ngoja niende uwani nikajisaidie,nakuomba uendelee kumlisha huyu... "....Usijali Mama....! Haya Levina kunywa uji basi...!" Nilijikuta nakunywa ghafla nikamtapikia yule Nesi kwa makusudi huku akibaki kakunja sura yake.... "Unajifanya mjanja siyo....?" Akaingia kwenye mfuko wa gauni lake na kuchomoa sindano kisha nikamuona akiichanganya kwenye kichupa kidogo... Nilikuwa niko tayari kwa lolote,sikuweza kufanya chochote huku nikibaki nguvu zikizidi kuniishia... "Haya chagua sasa nikuchome wapi wewe muuaji...!" Nilibaki kimya,mara nikasikia sauti... "Nichome mimi tafadhali..!" Alidakia yule mgonjwa aliyekuwa amelazwa pembeni yangu na yeye hakuwa na msaidizi nadhani alikuwa katoka au hayupo kabisa, lakini sikujua kwanini amesema vile... "Huyo hana hatia...njoo kwangu unichome nife...! Njoo...! Njoo...!" Kabla hajamalizia kusema nilishuhudia yule Nesi akimrukia yule mgonjwa na kumchoma sindano ya shingoni halafu akamfunika mpaka usoni... * * * * * Haikuchukuwa mda mrefu Mama akawa amerejea pale huku akimkuta yule Nesi anajiandaa kwa ajili ya kuondoka, "Mgonjwa wako mwenyewe kagoma kunywa uji...!" Akiwa anageuza na kuondoka zake yule Nesi mara... "Nesi...! Nesi..! Nesi...! ...Samahani msaada pale kwenye kile kitanda yule mgonjwa pale anaonekana anatapatapa pliz kamsaidie Nesi....!"

Haraka haraka yule Nesi akamfata na kumshika kifuani kisha akafunika mwili wote.. "Hatunaye tena...! Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amina...!" Aliongea yule Nesi huku akikimbia eneo lakutokea na baada ya mda nikamwona akirejea na wenzake huku wakibeba kitanda cha kubebea maiti wakaichukuwa ile maiti na kuondoka nayo... "Maskini mimi Levina...ilikuwa mimi ndo nife..!" Nilijisemea kimoyomoyo huku nikimwangalia mama yangu akimwaga mchozi kwa kumlilia yule mtu aliyekufa... Niliogopa sana ilipofika usiku tena kila nikijifikiria kuhusiana na yule Nesi kwa jinsi alivyomkatili, Hatimaye usiku ukawa,kwa kuhisi ingeweza kuwa imeshafika kwenye saa Nne kwani mama alianza kujikunyata kuashiria ananisubiria nilale naye apate japo kausingizi... Nikiwa na mawazo tele huku nikimuangalia Mama akiwa kachoka sana nami nilijikuta napitiwa na usingizi.,kitu kilichokuja tena kunishtua usiku ule ni kama mtu niliyemhisi kama ananyata,niliogopa sana na kila nilipojitahidi kuvuta mkono wangu wa kulia japo Mama ashtuke haikuwa hivyo kwani Mama alikuwa amelala fofofo,yule mtu alipofika karibu yangu akaninong'oneza karibu na sikio langu la kulia... "Nimekuja kukuua wewe...!" "Hivi nimekufanya nini we Mwanamke...?" Kwa mara nyingine nilijikuta sauti yangu imeweza kutoka.. Mara yule Nesi akavuta mto niliokuwa nimejiegemeza nao na kuuchukuwa kisha akanifunika usoni kwa nguvu akaniziba usoni huku akinibana kwa nguvu zake zote... Nilijihisi vichomi mwili mzima vilivyoambatana na mafua ya ghafla kutokana na kukosa pumzi...Nilitapatapa japo upande mmoja ndo ulikuwa mzima,nilitumia upande wa kulia ambao ulikuwa haujapooza,mpaka nikafanikiwa kudondosha dripu ndipo Mama akashtuka.., "Vipi tena Nesi...!" "Hapana Mama namsaidia kumwekea dripu sawa kwani iliachia hivyo ikawa haitembei...!" "...Ooohh Mungu wangu...! Ahsante sana Nesi kwani nilipitiwa na kausingizi kabisa,nisamehe kwa hilo...!" "...Usijali Mama na wala usiwe na wasiwasi nipo kwa ajili ya kazi hiyo...!" Maneno waliokuwa wanaongea kati ya Mama na yule Nesi hayakuniingia akilini hata kidogo kwani baada ya Nesi tu kuondoka... "Mama pliz...! Iwe isiwe..! Utake usitake...! Nakuomba asubuhi nirudi nyumbani hapa hakunifai Mama...! Nitakufa Mama si kuzuri hapa kabisaa Mama...!"

~ SAFARI YA NYUMBANI ~ Alfajiri na Mapema Mama hakutaka kupoteza mda akafanya njia zote nikakubaliwa kutoka pale hospitali lakini ilinibidi nitoke na kigari cha wagonjwa na kwenda kumalizia kutibiwa nyumbani kwa kuwa nilikuwa nimepooza tu pia kuwa na gharama kubwa ambazo Mama asingeziweza nazo zilichangia mimi kutoka pale hospitali haraka... Mama alikodi taxi yakutupeleka nyumbani na kabla hatujaingia maeneo ya nyumbani hofu ilianza kunitanda na kila nikimwangalia Mama naye alikuwa anatetemeka huku akifungua pochi na kumlipa dereva teksi shilingi elfu kumi.., "Mungu wangu nini tena hiki..." "Kwani ni nini Mama..?" "Levina....! Tumekwisha Levina....! Tumekwisha mwanangu...! Na hatuna mtetezi kwa hili tena...! .....Levina Mwananguuuuuuuuuu....!" ************************ * * * Je.,Levina na Mama yake wamekutana na nini? * * * Levina anajua juu ya Mauaji yaliyofanywa na Nesi, nini hatma yake yule Nesi...?
 
SEHEMU YA 12

Ilipoishia.... "...Mungu wangu nini tena hiki..." "Kwani ni nini Mama..?" "Levina....! Tumekwisha Levina....! Tumekwisha mwanangu...! Na hatuna mtetezi kwa hili tena...! .....Levina Mwananguuuuuuuuuu....!" Endelea... "Kwani ni nini Mama..?" "Nyumba yetu imebomolewa mwanangu...! Ona sasa yani sisi ni watu wa mikosi tu kila siku...! Uuuuwii..! Uuuuuuwiii..!Levina tutaishi wapi tena Mwanangu..! Tutakuwa wageni wanani sisi...! Uchungu aliokuwa nao Mama ulinifanya na mimi niweze kutoa sauti lakini Dereva wa ile teksi alikuwa ameshatufikisha nyumbani hivyo kazi kubwa ilikuwa ni kunipakiza kwenye kibaiskeli cha wagonjwa alichopewa Mama pale hospitalini.., Ndani ya sekunde chache nikawa tayari mimeshashuswa na Mama ndio alikuwa akinikokota kuelekea nyumbani ambapo kulikuwa kumebomolewa vibaya... Kadri tulivyojuwa tunapasogelea nyumbani ndivyo akili na nguvu nikawa sina...

tulipofika tu Mama aliniacha ghafla kisha akakimbilia ile sehemu kulipokuwa na kaburi la Baba ile marumaru iliyonakshiwa ikawa hamna tena,vumbi tupu ndo lilitawala eneo lile, Mara Mama akajilaza pale na kuanza kutapatapa pale... "Ni nani aliyefanya hiivi....! Mamaaa.....! mamaaaa....! jamani nakufaaaaa....! aiiyaaaa...! uuuuuh....! Nilijikuta nadondoka pale kutoka kwenye kibaiskeli na kuanza na mimi kutapata tapa tena kwa upande ule uliokuwa umepooza,sikujihisi maumivu kwa mda ule... Nililia sana huku nywele zikinivurugika kwa kuchafuka na vumbi la pale chini..,Majirani walijitahidi japo kutuzuia lakini ilishindikana.., Mama akanivuta mkono kwa kuniburuza huku tukielekea sehemu kulipokuwa na kile kibaiskeli lakini kabla hatujafika pale ghafla nilishangaa Mama akiniacha na kukimbia ndani kwenye ile nyumba yetu iliyokuwa haitamaniki kwa matofali yaliobaki bila kuwa na mpangilio,nyufa tu ndo zilikuwa zikionekana huku paa likiwa kama linataka kupepea..Akili na macho yangu yalikuwa kwa Mama nimuone amekimbilia nini mule.,nilijitahdi japo nitambae upande upande lakini haikuwezekana hivyo nikabaki natoa macho,nikamuona mama alipofika kwenye mlango akafungua pindo ya kanga yake haraka haraka na kuchomoa ufunguo kisha akafungua mlango mara nikashangaa akinikimbilia eneo nililopo... "Pole mwanangu kwa kukuacha Mwenyewe....!" "Usijali Mama nipo pamoja nawe...!"

"Nimechanganyikiwa mwanangu usinione hivi...!" Akanipakiza kwenye kibaiskeli tayari kwa kuingia ndani.,nilisikitika hatukuwa na sebule tena zaidi ya vyumba viwili vilivyokuwa vimesalia,sikuweza kuona hata kijiko wala sahani mule ndani kwani hata upande wa jikoni sikuweza kuutambua vizuri wala upande wa kutokea na kuingilia.. * * * * Kumbe Kipindi chote ambacho afande Deus hakuonekana hospitali alikuwa akitetea nyumba yetu isiweze kubomolewa, alijitahidi sana lakini ramani ndo ilikuwa lazima ibomolewe hivyo wakabomoa vyumba viwili,choo,jiko na sebule nakutuachia vyumba viwili tu..usiku wa siku ile tuliowasili nyumbani ndiyo Afande Deus alikuja kutupa taarifa juu ya bomoa bomoa na ilikuwa tena kilio kwangu na mama., Ilipotimia asubuh nayo sikuweza kumuona tena Gervas zaidi ya kuja kuletewa taarifa na Mama yake kuwa ameshasafiri kama ilivyopangwa ili kulinda usalama wangu.. Nikawa kama mtu aliyepigwa ganzi nakusubiria iishe mwilini apate maumivu.. "Kwanini nateseka hivi..?nani wa kulaumiwa...?" Levina mimi mkosaji nisiye na hatia ndo nilikuwa nimeketi kwenye kibaiskeli cha wagonjwa chumbani huku nikiwa na mawazo yaliochanganyikana na maswali yasiyo na majibu., "Lakiiiini...! Kwanini Gervas hakuniaga.....?" Niliumia moyo sana lakini haikuwa na jinsi zaidi ya kuwa na subira na kuamini iko siku nitamwona tena japokuwa sikupata kabisa nafasi ya kukaa na Gervas.

. ~ BAADA YA MIEZI 4 ~ Maisha kwetu yakawa ni ya kimaskini sana huku msaada mkubwa kwetu tukiuelekeza kwa Afande Deus,na mara moja moja tulikuwa tukipata msaada kwa wazazi wa Gervas kwani Mama hakuwa na kazi yeyote yakumuingizia kipato,Mazoezi ya kusimama peke yangu ambayo nilikuwa napewa na Mama yalionesha matumaini makubwa kwangu kwani niliamini mda si mrefu nami nitaanza kutembea kama wengine..,nilipungua sana hata na Mama pia. "Levina mwanangu..!" "Abee Mama..!" "Leo nimechoka embu jaribu kutembea na kibaiskeli mwenyewe..., Utaweza tu mwanangu.....!" Ni kweli ilifika kipindi Mama akawa anachoka lakini kwa sasa nilikuwa ninauwezo wa kusimama peke yangu huku nikitembea kwa mtindo wa kukikokota kile kibaiskeli taratibu huku nikitembea kwa mwendo mrefu kidogo na kurudi nyumbani., Ilipofika usiku wa kama saa tano nikiwa na kauchovu kidogo kwa kuzunguka mda mrefu,Mama alikuwa ameshalala ghafla nikasikia sauti za watu nje zikipiga kelele,mwanzoni nilipuuzia lakini kadri nilivyotulia bado ile sauti ilizidi kupaza kwenye masikio yangu ikitokea kule nje.., Nikafungua pazia na kutoa jicho taaratibu kujua ni kitu gani..,sikuweza kuambulia kitu zaidi ya kuona watu wa mtaani wakiwa wake kwa waume wakimshambulia mtu kwa matusi na wengine wakimpiga kwa mawe na fimbo..,nilipuuzia kwani sikuwa nawafahamu pale mtaani zaidi ya jirani yetu tu ambaye ni wazazi wa Gervas.. Nikiwa bado naangaza vizuri mara nikaliona gari la Afande deus lakini nilishangaa kuliona limepaki pale.. "Mmmhh.....! Atakuwa ni yeye kweli..?" Nilijikuta naguna mwenyewe na kujiuliza bila ya majibu., haraka haraka bila hata ya kumwamsha Mama nikafungua mlango taaratibu huku nikiwa na kibaiskeli changu nikajikokota mpaka nje kushuhudia ni nini.. "Samahani anti...!" "bila samahani..!" "Eti pale kuna nini usiku huu...!" "kuna kijiaskari kimoja huwa kinajifanya kimbeya na pia huwa kinatabia za kuchukuwa wake za watu..,sasa leo wamekikomesha na lazima kife pale...!" "samahani tena...!

......unaweza labda ukawa unamjua jina lake....?" "Heee....! We dada vipi au na we alikuwa mpenzi wako....? Haya gari yake anayoendeshaga ile palee wanaiponda ponda...! Nenda kamsaidie..!" Alinijibu kwa nyodo mpaka nikajuta kwanini nilimuuliza... Nikaondoka na kumwacha pale akiendelea kubwatuka.., "Looo..! Kamezidi sana kwa wake za watu leo atakoma lazima aisome namba...! Sikuwa na hamu tena ya kumsikiliza yule dada niliyomuuliza,hapohapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta na kugundua lile ni gari la Afande Deus lakini nani atakuwa alikuwa anaendesha..? Nikaanza kukaribia lile eneo latukio huku nikiendesha kibaiskeli changu kwa kutumia mkono mmoja ule wa kulia uliokuwa mzima..,kadri nilivyokaribia moyo ulizidi kunipasuka na kwenda mbio.,kila nikilitazama gari lililokuwa likipondwa linafanana kabisa na la Afande Deus.., "Nilipolisogelea lile gari kweli lilikuwa la Afande Deus nilianza kuhisi ugonjwa unaanza tena kwani kwa sasa mwili wote ulikuwa haufanyi kazi.. "Mamaaa...mama uko wapi mamaa....! Afande Deus wanamuua huku..! Nililia kwa uchungu na kwa sauti kali iliyowafanya wale watu waache kumpiga yule mtu na kuniangalia..kuangalia nyuma yangu mama alikuwa anakuja kwa kunikimbilia nikatumia mwanya huohuo wa mimi na kibaiskeli changu kuudondokea ule mwili wa yule mtu aliyekuwa akipigwa pale chini.. "Niueni mimi..! Kwanini mnampiga...? Kawafanya nini..?" Yale maneno yalichochea hisia za wale watu waliokuwa na hasira kali, wakaendeleza kipigo kwangu bila ya kujali naumwa.. "nakufaaa....! nakufaaa..! uuuhh...! uuuh...! niueni..! niueni...!

Nimalizieni nife..!" ~HOSPITALI TENA~ Mwili wangu ulikuwa tayari umeshajaa plasta kwa kipigo nilichokipata, ni wazazi wa Gervas ndo walionileta wakisaidiana na Mama, nilivimba sana haswaa maeneo ya usoni, sasa idadi ya dawa za kumeza zilizokuwa zinatuliza maumivu zilizidi mara tatu yake.., "Mama kwani Afande Deus alikufa..?" "....Mwanangu...!ntakuelezea tukifika nyumbani..!" Japokuwa niliumia siyo sana,wazazi wa Gervas wakishilikiana na Mama walipendekeza niendelee kutibiwa nyumbani tu.. Akili na hofu kubwa ilikuwa ni kwa afande Deus., "Jamani hivi ninamikosi gani..? .....Isikute naenda kushuhudia kaburi..?" Nilijiuliza kimoyo moyo huku nikiwa sijui nini kinachoendelea kuhusiana na Afande Deus, * * * * Ndani ya lisaa nikiwa mimi na wazazi wa Gervas tayari tulikuwa nyumbani kwetu wakitushusha na kuelekea kwao huku nikiona Mama wakimpatia pesa kidogo.. "Levina..! Ugua pole na kuwa mwangalifu mama eenh....!" "Haya..!,Ahsanteni sana..!" Niliwaitikia tu ilimradi waondoke kwani alichoongea kilipitia upande huu nakutokea upande ule..,hao tukaingia ndani huku nikikokotwa kwenye kibaiskeli cha wagonjwa nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kilichotokea jana yake.. "Enhee Mama niambie basi imekuwaje..? Au..nayeye Afande Deus mlimkimbiza hospitali..?" "Hapana mwanangu yule hakuwa Afande Deusi tunayemjua...?" "...Niiiini..? Alikuwa nani sasa...? Mama acha kunificha mi namjua Afande Deus ni yeye mwenyewe alikuwa...?" "Hapana Levina.....!" "Ni yeye Mama....!" "Hapaaaaaaaaaana....!" Kwa mara ya kwanza nilimshuhudia Mama akikasirika na kunijia juu kwani baadaye alikuja kuniweka wazi nikaamini., Aliniambia kuwa lile gari la usiku lililokuwa likipondwa pondwa ni kweli la Afande Deus na kwa usiku ule Afande Deus alikuwa amekamatwa na kutekwa na majambazi na hajulikani aliko mpaka sasa na inasemekana kuwa hata wakati Mama alipompigia simu Afande Deus jana usiku hakuipokea yeye bali walipokea polisi wa zamu waliofanikiwa kumkamata Mama mmoja akiwa na mtoto mmoja aliyetambulika kama 'Mama Ali' pamoja na simu ya Afande Deus..,na uchunguzi unaendelea juu ya kumpata Afande Deus aliko.., "Umesikia Mwanangu..? Hata kama unajifanyia vijizoezi vyako vya kutembea uwe makini sana....!"

"........Sawa Mama nimekuelewa..!" Nilimwitikia tu Mama huku nikiamini kabisa kuwa akili yangu haikuwa pale kwani nilijiuliza sana huyo Mama Ali lazima atakuwa amenitaja tu.,halafu wakinipata na sina cha shahidi wala mtetezi itakuwaje..? Kila nikimfikiria Afande Deus kwa jinsi anavyotusaidia hapa nyumbani ndo kwanza nachanganyikiwa kabisaa.., * * * * Taarifa juu ya kuokotwa Kwa maiti kwenye daraja la sarenda ziliwafikia polisi haraka wakaenda kulithibitisha hilo na kuliwakilisha panapohusika, maiti iliweza kutambulika kirahisi kutokana na kufahamika kwake kwa mapolisi wenzake.. Vilio vingi vilitawala nyumbani kwa Afande Deus.,Tukiwa kama watu wakaribu na marehemu kwa kushirikiana na Mama Deus tulikuwa tayari tumetinga mavazi yetu meusi na sasa ilikuwa mda wa kutupia mchanga...Nikiwa kwenye kibaiskeli changu huku nikishikwa na watu niliweza kuvumilia kwa mda kidogo tu... "Baaaaba...! Kweli umeniacha...? Ntaenda tena wapi Baaaba....?" Nikachotewa mchanga tayari kwa kuuchukua kidogo na kuutupia kwenye kaburi... "Baaaaba..! Kweli umekwendaaaa....?

Baba Deus....! kwanini....? Nani aliyekuuuua....?" ~ BAADA YA MIEZI 3 ~ Siku zilizidi kukatika nilianza kumsahau Afande Deus maishani mwangu, ila kitu ambacho kinaniuma mpaka leo hii ni Gervas.,Hakuna hata siku niliyoambiwa na Mama yake kama amepiga simu au amenisalimia...! "Yani kweli miezi saba yote hiyo hata barua..? Au alikuwa hanipendi kuniona na sasa yuko mbali na mimi ndo kanyamaza kabisaaa...? Laaaaaakini asije akawa na demu mwingine anayemchanganya..?" Nilikuwa najiuliza peke yangu na kujijibu huku nikimpikia Mama chakula kwani Levina mimi si Levina yule uliokuwa ukimjua tena.., Mazoezi yalinisaidia saana japokuwa sikuwa nimepooza upande mkubwa, Tofauti n kipindi kile sasa nikawa levina mpya asiyetembea na kibaiskeli cha wagonjwa.., Kupitia vyama vyao vya kusaidiana sasa Mama akapata kamkopo kalichomfanya afungue kagenge kadogo kwa ajili ya mimi na yeye kujikimu na maisha kwani hakukuwa na msaada mwingine tena maishan..,
 
SEHEMU YA 13
Sikuwahi kutembea na mwanaume yoyote maishani mwangu zaidi ya kuambulia kubakwa mara mbili,Moja nikiwa kule gerezani na mara nyingine nikiwa Morogoro nyumbani kwa marehemu 'Baba Ali'.. Nilipenda sana siku moja Gervas aje kuwa Mme wangu wa ndoa kutokana na yeye kuwa kimya nikawa tayari nimeshakata tamaa.. Kunakipindi Mama aliugua sana kwani alikuwa akisumbuliwa na kisukari nilipata shida sana kumuuguza kwani hela ya kumtibia ilikuwa shida na sikuwa na elimu yoyote zaidi ya kuishia kidato cha kwanza tena Mwanzoni kabisa na ndicho kipindi nilichowekwa gerezani, kutokana na ugumu wa maisha na kuugua sana kwa Mama, genge likafilisika kutokana na kutokuwa na sehemu nyingine ya kutuingizia kipato, Tangu Mama alipoanza kuugua wazazi wa Gervas wakatutenga hakuna cha msaada tena.. * * * * "....Sema kaka....?" "....Unaniambiaje sasa...?"

"...wewe tu...,Kulala elfu kumi cha fasta fasta buku tano...!" Ndiyo ilikuwa lugha yangu ya kazini, kwani ukinikuta mawindoni mida ya usiku huwezi amini., Kwanza kabisa jina la Levina nilikuwa nikilitumia mchana tu,na usiku naitwa 'Vina', Mwili ulikuwa umenirudi japo si sana,ila makalio yangu bado yalikuwa ni makubwa na chuchu zilikuwa ndogo sana.. "...Sikulazimishi kakaaa kama umeshindwa hapa...! Nenda kwa wengine wasiojua kukatikia sawa....?" Ni kati ya maneno yaliokuwa yakiwachanganya sana wanaume..,na kujikuta wakining'ang'ania, kutokana na kuanza kuishi kwa uafadhali kulimfanya Mama asifanye jambo lolote na kutokana na kuniunga mkono juu ya kujiuza mwili kulinifanya nitembee na wanaume huku wengine waume za watu haijalishi ni mchana au usiku we twende tu.. Ndani ya Mwezi tu mtaa mzima ukawa umeshajua kazi yangu,kutembea na wanaume sita hadi nane kwa siku lilikuwa ni jambo dogo sana kwangu.. Siku moja nikiwa mawindoni usiku.. "...Oyaaa...Sista vipi kinaeleweka..?" "Vipi fasta fasta au kulala..?" "Aaaah Vina..... Leo unataka kunibania enhh...? Mi wa kulala bhanaa vipi..!" Aliongea kijana Mmoja mnene hivi japo sikumtambua kwani nina wateja wengi ila nilijikuta namkubalia kwenda kulala kwa tamaa ya pesa... "Tulipane kabisaa.., nipe changu mapemaaaaa....!" Hakuwa mtata hata kidogo yule jamaa akatoa burungutu la pesa na kuchomoa noti ya shilingi elfu kumi na kunipatia.. "Jammy...Nishkie kesho ntakuja kuchukuwa kwako.." Kwa kawaida huwa nikipata wateja wa kulala nao sipendi kutembea na hela hivyo Jamila alikuwa rafiki yangu anayenichukulia pesa na mara nyingi... Nikiwa nimevalia kimini kifupi kilichoachia mapaja yangu wazi huku ndani nikiwa mtupu kabisa kutokana na biashara zetu zinavyoruhusu..Tayari tukawa tumeshaelewana na yule Jamaa,nikawa ndani ya gari lake kuelekea hotelini au gesti yeyote kwa ajili ya kumpatia anachotaka huku akiendesha gari pia simu yake ikiita mara kwa mara naye akikata.. Hapakuwa mbali sana kwani ndani ya mda mfupi tayari alikuwa akiipaki gari kwenye hotel niliyokuwa sihifahamu vizuri..akacheki simu yake pale.. Kama kawaida yangu huwa sipendi kuchelewesha mda tulipoingia chumbani tu..

"....Chooni wapi....?" "Ingia humo....!" Nikachukuwa taulo la pale hotelini, nikachukuwa na pochi kisha nikaingia bafuni., Nilijisafisha vizuri kwani tayari mteja nilimuona ana hela ya kutosha tangu alipochomoa burungutu la hela na kunipa elfu kumi kwahiyo ni kumpa mavitu mpaka mwenyewe aniongezee hela zaidi.. Nikajifungia mule chooni na kuchomoa sabuni yangu ya 'DETTOIL' nikachanganya na cream ya 'SPOT' ni kati ya vitu vinavyonifanya maumbile yangu ya ndani yanakuwa madogo (samahani sana msomaji kama utakerwa na mimi,nisameheni sana kwa hapa.) Nikatoka huku sina hata lile taulo na kujitupa kitandani.. "Vipi unaenda kuoga au.." "....Hapana nipe kwanza cha fasta nikaoge....!" Tukaingia pale kitandani na kumpatia anachokihitaji,nilimchanganya sana kwa viuno nilivyomkatikia "....Inaatoshaa....! Inaatoshaaa....! Wacha nikaoge kwanza..." Akatoka spidi na kwenda kujimwagia maji huku akiniacha nimeduwaa pale kitandani...Nikainuka kwenda kuzima taa lakini kabla sijaifikia kibonyezeo cha kuzimia taa suruali ya yule mtu ikadondoka kutoka pale karibu na kakabati spesho kwa kuweka nguo, ikanibidi niikote nakuirudishia ndipo nizime taa.. Ile nainua tu suruali nakutana na picha imedondoka ikimuonesha Afande Deus akiwa enzi zake akiwa hai., Hofu ikanitanda nikaona ntakuwa nimemfananisha wazo likanijia kutafuta mifukoni,kwa haraka zaidi kabla hajatoka nikakutana na nyingine Nne zikiwa zinamuonesha Afande Deus akiwa ametekwa na kufungwa mdomo kwa plasta huku macho yakiwa yamejaa damu nilihisi watakuwa walimtoboa macho.., "Mungu wangu...! Kumbe niko na muuaji..?" Kwa haraka zaidi nikazichukuwa zile picha na kuzifungasha pamoja na nguo yangu ya ndani niliokuwa nimeibadilisha mda ule.. Nikiwa namalizia kuweka zile picha mara simu ya yule mtu ikaingia ujumbe mfupi (meseji) ,haraka haraka kabla hajatoka bafuni nikaichukuwa na kuisoma.. "UMESEMA JINA LAKE ANAITWA LEVINA? NAKUAMINIA FANYA JUU CHINI TUMUWEKE HATIANI,SI UNAJUA NI MDA MREFU TUMEMSAKA?" Ile namalizia kusoma nikaiweka ile simu haraka haraka na yule jamaa akawa ndo anatoka bafuni hivyo nikabaki sina tena ujanja wowote wa kukimbia zaidi ya kukubali kulala, Nikawa namtaimu apate usingizi tu nisepe,haijapita mda akawa amepitiwa na usingizi japo sidhani kama ulikuwa ni usingizi sana kwani alinikumbatia huku akikohoa mara kwa mara kuashiria yuko macho na hata simu yake inapoingia meseji alikuwa fasta kuipokea na kurudisha majibu kisha kujilaza tena., "Nimekwisha Levina mimi..?

....lazima nijikatae mbele yake kwanza mi siitwi Levina naitwa 'Vina'.. Hata kina jammy wanalijua hilo...!" Nilijipa moyo huku nikiamini asilimia kubwa sitaweza kushikwa pale., Taaratibu bila kupoteza mda nikamnyemelea akiwa kashapitiwa na usingizi nikamsogeza mikono yake aliokuwa amenikumbatia,nikavuta simu yake na funguo za gari,na lile burungutu lote ile simu nikaizima na kuitumbukiza kwenye pochi yangu kisha nikavaa nguo zangu fasta fasta tayari kwa kuondoka.,ile nafungua kitasa tu nikamsikia akikohoa kuashiria kama mtu aliyeshtuka... Sikutaka kuchelewesha mda kabisa nikatoka spidi mpaka kwenye gari yake na kuingia,sikuwa najua kuendesha gari na nakubali hilo ni kosa kubwa sana kwangu, kwani nia kubwa ya kuchukuwa huu ufunguo ilikuwa ni kutafuta undani wa huyu mtu hivyo nikawa ndani gari yake nikipekua makaratasi yake.,ndani ya sekunde chache nikawa nimeshayapata baadhi pamoja na pingu alizokuwa kaweka kwenye gari,nikazichukuwa na kutaka kugeuza kwenda kumfunga pingu.., "Aaaaah..,lakini acha tu niende nyumbani..!" Nilijikuta naghairi kurudi,hivyo nikazichukuwa zile pingu na makaratasi na funguo niliziacha palepale kwenye gari lake nikaondoka zangu na kuelekea nje huku nikitafuta taksi niweze kwenda nyumbani usiku ule.., Pale getini hapakuwa na wakunizuia kwa jinsi nilivyokuwa nimevaa dhahiri walishajua tu mi ni malaya hivyo mda wowote natoka na kuingia.. * * * * * Nikiwa nyumbani nimejipumzikia nyumbani huku nikipekuwa zile karatasi, "Aaah...! Sasa nimeshaanza kuzielewa kumbe yule alikuwa ni askari mpelelezi...! Lakiini kwanini alikuwa ananitafuta mimi..?" Ni kati ya maswali yaliyokuwa yananichanganya juu ya yule mtu niliyomtoroka hotelini, ikanibidi nimkabidhi Mama zile picha pia nimuelezee kilichonikuta..,Mama hakuwa na la zaidi ya kuniambia niachane na hiyo biashara kwa mda wa usiku... Sasa nikawa Levina kamili na siyo Vina tena kutokana na Biashara yangu kuifanya mchana Na siyo usiku tena., Mawindo yangu ni kwa waume za watu kwani niliamini ndo walikuwa wakinilipa vizuri..Nilitokea kuchukiwa na kila mtu hapa mtaani lakini hilo sikulijali.., * * * * Hali ya Mama ikazidi kubadilika kwani hakuwa anaumwa kisukari peke yake pia alikuwa na presha ya kupanda jambo lililoniwia vigumu maishani mwangu kwani msaada mkubwa ulijuwa ukitoka kwangu.. "...Niongeze elfu kumi tena nikupe na nyuma kabisa...!" Ilinibidi wakati mwingine nikubali tu kuingiliwa kinyume na maumbile hii yote ni kuhakikisha Mama yangu anapona., Ilifika kipindi Mama alishikwa na kisukari mpaka miguu ikamvimba na vidonda vikamtoka miguuni sana,hali hiyo ililichanganya sana lakini sikukata tamaa ya maisha nilichokifanya kwangu nikuendelea kufanya kazi yangu ya kujiuza mwili mpaka hapo Mama yangu atakapopona, kuna mda mwingine nilikuwa nikidhulumiwa na wanaume niliokuwa nikitembea nao,kipindi kingine nawakubali kufanya nao mapenzi hadi wanaume wawili mpaka watatu kwa mara moja,Nilijihisi kama mtu aliyechanganyikiwa na maisha.. "..Leo twende tukalale kwangu..! Ntakuongeza pesa..!" "..Sawa tu..!" Nilikuwa radhi nikalale na mwanaume kisha mama nimuache akijiuguza nyumbani peke yake... * * * * "..Leo nakuongeza dau..! Kamata kwanza elfu ishirini kisha ukimaliza kazi nakupa na ishirini.." "...Levina.. levina.. levina...,nasikitika kuwa bado naipenda kazi yangu..,na kila mara nilikuwa nikikutoa mimba hata kwa buku kumi na tano nakukubalia..." "..Ndio Dokta..,ni kweli..?" "...sasa basi.! leo nasema NO..!" "...Dokta pliz.. Dokta.. nitoe Dokta...Ntakupa chochote Dokta nitoe...!"

"...Nimesema NOOOOO..!" "Endapo nitakutoa hii mimba lazima uhatarishe maisha yako,kwani nitaharibu kizazi chako pengine usiweze kuzaa tena Maishani mwako...! ...umeshawahi kuskia wanawake wagumba Levina..?" "..Ndio.." "...kwahiyo unapenda kuwa mgumba..?" "Hapana...!" "...Haya potea fasta..." Nilinywea nakujihisi nimekuwa mdogo kama kidonge cha piliton.,Nikabaki nalia huku Nisielewe mimba ni ya nani.., "..Nitamlea hata kama atakuwa hana Baba.." Nilijisemea kwa sauti ya chini chini huku nikitafuta njia ya kutokea pale zahanati.. * * * * Umati wa watu uliokuwa umefurika pale nyumbani kwetu ndo ulikuwa umenishtua asubuh asubuh nikiwa nimetoka kwenye biashara zangu.. "..mbona kunanitisha hivi... kweli kutakuwa na Msiba pale..?" Nilijikuta nikijiuliza mwenyewe huku nimejibanza kwenye kona,nguo nilizokuwa nimevaa zilikuwa fupi sana na nilikuwa nimechelewa kurudi nyumbani kwani kawaida yangu nikurudi alfajiri kwenye mida ya saa kumi usiku.. "..Daah leo Levina mi nimeumbuka...? Lakini mbona kumetundikwa maturubai na Mapolisi wanazunguka zunguka..?" Nilishindwa kujitambua kabisa mpaka alipopita mpita njia.. "Samahani kaka..! Pale kuna nini..?" "..kuna Msiba..!" "Maaamaa siamini...Mama yangu amekufaa..!" "..dada kwani vipi.?" "...Hapana.. hapana.. Mama yangu ndo nimeshampotezaaa..!" "..lakini Dada..!" "...Hakuna chanini...Embu niache..Nenda zako tu kaka...oooh Mama..! mama..! mama..! mamaaa..!" "...Sista Msiba haupo nyumba ile pale..!" "..uko wapi sasa..? "Uko nyumba ya tatu kutoka pale,kwani yule mzee alikuwa mtu Maarufu sana na watu wanazidi kumiminika ndo Mana wameweka turubai refu kiasi kile..!" "...Inamaana aliyekufa ni Baba Gervas..?" "...yeah...! ndo huyo huyo na mi niko njia moja kuelekea pale... ***************
 
SEHEMU YA 14

Ilipoishia... "...Inamaana aliyekufa ni Baba Gervas..?" "...yeah...! ndo huyo huyo na mi niko njia moja kuelekea pale... Endelea... Kila nikipiga akili ni jinsi gani nitaingia nyumbani sipati jibu..,haraka haraka halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta., "...'enewei' hii pesa niliyotaka kumpa yule Dokta wacha niinunulie kanga nivae..!" Njia hii niliyotumia ndo ilikuwa sahihi kwani niliweza kuvaa kanga na kujifunika mpaka eneo la usoni na kuacha kijisehemu kidogo tu cha kutolea macho, Watu walikuwa ni wengi sana eneo lile nilijipenyeza mpaka kwenye mlango wetu nakuingia ndani.,nikamkuta Mama akiwa hoi pale kitandani., "...Mama vipi bado tu umelala..!" "...Ndio mwanangu ntaenda wapi na hali yangu kama unavyoniona..!" "...Unajua Nje kuna Msiba.....?"

".....Ntajulia wapi tena mwanangu kama unavyoniona miguu imenijaa vidonda na ndo inavimba kila mda...kwani msiba wa nani...?" "Mama..!,Baba Gervas hatunaye tena..!" "...Levina unasemaaa...?" Maskini sikujua kama ile taarifa niliyompa juu ya msiba itamletea madhara kwani nilishangaa Mama akianza kujiuma uma meno kisha akatapa tapa nakutoa mapovu mdomoni kana kwamba anaugua kifafa,baada ya mda tena nikamwona akinyong'onyea huku anavuta pumzi kwa tabu pale pale nikamuwahi na kuukutanisha mdomo wake na wangu kisha nikaanza kumpuliza ili naye apate pumzi kidogo. Baada ya mda akarudi katika hali yake kisha.., "...Levina nipe maji..?" " pumzika kwanza Mama.!" "...Naskia kiu Mwanangu nipe hayo Maji..?" Nikawa mbishi kumpa maji kwani daktari alishaniambia Ninapomuona Mama katika hali ile nisithubutu kumpa kitu chochote mpaka baada ya masaa. ~ BAADA YA MIEZI 4 ~ Tayari tulikuwa tumeshasahau habari za msiba wa Baba Gervas,kwani mpaka msiba unaisha sikuweza kuiona hata sura ya Gervas,.. "Au pengine alibanwa na shule au... aliogopa kuja kwasababu anatafutwa na Mapolisi...?" Ila kwa upande wa Mama yangu, hali yake bado ilikuwa ikibadilika siku baada ya siku, Mpaka mimba inamiezi minne bado niliendelea na biashara yangu ya kujiuza mwili kwani sikupata njia nyingine mbadala wa kujikimu na maisha, mtaa wote kila mtu alikuwa akikerwa na tabia yangu ya kutembea na waume za watu na hata Mama yake na Gervas alikuwa mmojawapo aliyenichukia sana na hata baada ya mumewe kufariki., Ndipo nikapata wazo la kumrudia Mungu. "...Bwana Yesu asifiwe..!"

"..Amina karibu binti..!" "...Mchungaji..! nipo hapa mbele yako kutubu zambi zangu zote..!" "...Unaitwa nani Binti..?" "Levina...!" "...Sogeza kichwa chako karibu..,Fumba macho...!" "...Baba katika jina la Yesu..! Weza kumfungulia binti huyu njia..,muachanishe na nguvu zote za ajabu zitakazompinga..,Baba Mwenye majina Mengi..Yehova Baba.., Masiha...kwa nguvu na utukufu wako nakemea Mapepo wote wanaomzunguka...kwa jina la Yesu..!" "...AMINA.....!" Baada ya hapo mwili wote ukasisimka na sikuamini maishani mwangu kama ipo siku ntakuwa vile..,Nikawa mlokole safi asiyemjua mwanaume,mara kwa mara Mchungaji alikuwa akija nyumbani kumuombea Mama,mpaka ikafika kipindi akapata nafuu kidogo naye akawa anaweza kutembea japo kidogo.. "...Oya unamnyaka yule Malaya wa pale..?" "Si yule aliyekuwa anatembea na waume za watu..?" "...aaahaa unasemea Levina..?" "...Exactly..!" "Enhee kwani amefanya nini..?" "...Si kameokoka eti..!" "....Oya kausha...! kausha..! Acha kunivunja mbavu mwana..!" Nilidharauliwa kila kona niliyopita,kwani ni kweli nilikuwa nime'change' kuanzia Mavazi,Nilikuwa Levina mimi wa kutembea na Biblia mda wote kuhubiri neno la Mungu mtaa kwa mtaa., "...Ushindwe katika jina la Yesu...!" Nilikuwa mkali kukemea mapepo pale wanaume walipokuwa wakinitaka kimapenzi., * * * * "..Hodi...! Hodi..!" "Karibu... Levina embu nenda kafungue mlango naskia kama mtu anabisha hodi..!" Ile nafungua tu mlango nakutana uso kwa uso na sura niliyokuwa nikiifahamu.,kwani alikuwa amevalia kisasa, suruali ya jeans inayong'aa, tisheti nyeupe iliyoandikwa kwa herufi kubwa 'BACK FROM US'..huku mwili wake uking'aa kwa cheni alizojizungushia kuanzia mikononi,shingoni mpaka pembeni mwa mifuko ya kwenye suruali yake,hakika alipendeza., "...Oooh..! Gervas...!" "..Levinaaa...! c'om n hug em'..!" Sikumuelewa vizuri alichoongea ila kwa vitendo alivyoonesha viliingia kwenye hisia zangu nakutambua kuwa anahtaji nimkumbatie., "Ooh...baby..! baby..! baby..! R u aukey..! Haw abau ua Mama..!" Niliambulia kusikia neno Mama lakini nikamwelewa anamzungumzia Mama., "...Mmmh yule pale sebuleni mzima tu..! Pole kwa msiba..!" "...Naaah Naaah usijali Levy.., t was da past...!" "...Unasema.?" Nilimuuliza kwani sikuwa namuelewa kabisa anachozungumza kwani alikuwa akichanganya lugha, nikamwacha pale akiongea na Mama kisha nikakimbia chumbani kwenda kubadilisha nguo "..Shikamoo Mama..!" "Marahaba Mwanangu Gervas mzima wewe.?" "Mimi mzima tu..sijui nyie mnaendeleaje..!" "Tunamshukuru Mungu..!" "..kumebadilika sana hapa hata na kwetu pia kidogo nilishapasahau...Mama nilishindwa kuja kwenye Msiba kwani nilikatazwa na ndugu kutokana na ilee kesi ya levina...

" "Aaaaahhh ok, ok, ni kweli..!" "....Hata hivyo hakuna kilichoharibika nimekuja kuangalia kaburi la Baba pia nimeomba misa kesho asubuhi tutasali pale nyumbani...!" Nilivyorudi nikamkuta bado Gervas anaongea na Mama..., Baada ya mda Mama akaelekea chumbani na kuniacha pale na Gervas., "Enhee...! Niambie Gervas za kutususa tangu ulivyoondoka...?" ".....Hapana Levina mimi sijawasusa ila tangu nilivyoondoka na mzee kipindi kilee sikuweza kupata njia yoyote ya mawasiliano na wewe, Niliumia sana moyo japo hutaniamini kwa hilo..!" "....enhee nakusikiliza....!" "....Baba akaniacha na kurudi huku bongo, nilikaa miezi mitano bila ya kuwa na mawasiliano yoyote na nyumbani, sikuweza kuwa na mchumba yeyote kwani niliamini wewe ndo wangu wa ndoa.," "...Ya kweli hayo Gervas.?" "...Kweli Levy.,ilifika kipindi nikapata kazi katika kampuni moja huko ya kutengeneza pombe kali aina ya 'HAMMIER WHISKY' nikawa nafanyakazi huku najisomesha,kila siku nilijitahidi sana angalau nipate kusikia sauti yako lakini ilishindikana..!" "..Kwanini ilishindikana..?" "...Levy ...kila nikiwapigia simu wazazi wangu japo nipate kuongea na wewe wananiambia nikuache haunifai na nisiwe na wewe tena kwani umebadilika sana na unatembea na kila mtu hapa mtaani..!" Nikashusha pumzi huku machozi yakinilengalenga kwa huruma nikaendelea kumsikiliza Gervas., "...enhee ikawaje...?" "...Mimi na wewe Levy tumetoka mbali na elewa kuwa nakupenda na nitazidi kukupenda milele, sijataka kuwasikia wazazi wangu hata pale waliponiambia kuwa umebadilika, Baba yangu alifariki akiwa bado anakuchukia, Mama yangu pia mpaka sasa anakuchukia kwani nilivyomwambia kuwa nahtaji kukuona leo alinijia juu na kuchukia sana...! Levy..., Embu niambie kweli unanipenda....?" Nilikaa kimya huku naitazama mimba yangu na mwili kunisisimka na ulokole wangu kuuweka pembeni kwa mda...., ".....Levy hata kama mimba si yangu mi niko tayari kwenda kuishi na wewe huko Marekani, hiyo mimba mi nitalea....Elewa kuwa bado nakupenda..." "...S...a..a..a..wa..! Na Mama je? "..Kwani Hamna ndugu wa kumuacha na Mama yako...?" "...kama unavyoniona Mimi ndo kila kitu kwa Mama..!" ".,Kwahiyo hutaki kwenda kuishi na mimi au hunipendi..?" Alianza kuzungumza kwa sauti ya ukali Gervas akanifanya nitetemeke na kujikuta nikitoa jibu haraka haraka... "

...Sawa Gervas nimekuelewa na nitajitahidi tutakuwa pamoja..!" Hakuna mwanaume ambaye amekaa moyoni mwangu kama Gervas na hata kama angekaa miaka Mia ndo akarudi bado tu ningempenda kwa dhati, Juhudi nyingi alizonionesha toka kipindi niko Gerezani mpaka nilipo ni jambo la kumshukuru Mungu kwakweli..Nilimalizana na Gervas kisha alichoniambia kuwa kesho yake atakuja kuniaga kwani Ofisi ilimpa ruhusa ya siku tano tu za kukaa hapa. * * * * Asubuhi na Mapema nikiwa nafanya usafi wa hapa na pale huku Mama nikimwacha sebuleni akizubaa mwenyewe,Nilifanya usafi fasta fasta kisha nikaingia ndani kumuogesha Mama yangu na baada ya hapo nikaingia bafuni,na kutoka nikiwa safi kisha nikavalia gauni langu refu huku pembeni nikiwa na Biblia na kalamu nikilichambua Neno la Mungu.Nikiwa bado naendelea kusoma Biblia Mara nikasikia hodi inapigwa mlangoni., "Karibu...! aaaah..! Gervas karibu mpaka ndani...!" "..Hata siyo mkaaji kwani nina mda mchache na hapa Naelekea Mjini kidogo nikamfanyie 'Shopping' Mama kisha nitarudi jioni sana..!" "...Kwani safari ni lini..?" "...Yani hapa unaponiona Tiketi nilishakata zamani ya 'go an return' kwahiyo usiku kwenye saa 8 leo hii ndio nitaondoka..!" "...aaah sas..." Kabla sijamaliza kumuuliza akadakia na kuendelea kuzungumza., "...Wacha nimuage Mama then utanisindikiza ndio utajua kila kitu..!" Akaingia mpaka sebuleni akakaa kisha nikaenda chumbani kumuitia Mama aje amuage.., ".....Mama kwaheri mi usiku wa leo narudi Marekani..!" "...Mbona haraka haraka Mwanangu...,Mi nikajua upo hapa hata kamwezi kamoja ndio urudi..!" "Hapana Mama natakiwa haraka sana Shuleni pia Kazini ninapofanya kazi wananihtaji sana..!" "......Haya Baba safari Njema huko uendako pia usitusahau Mwanangu uwe unatukumbuka..." "...Sawa Mama usijali ntaendelea kuwakumbuka huko niendake Mama...!" Najua Gervas aliongea kwa makusudi ili Mama asiweze kujua mpango wetu wa mimi na Gervas.Tulitoka pale moja kwa tukawa tunaekea nyumbani kwao..., "...Hapana Gervas mi sifiki kwenu Mama yako namuogopa sana...!" ".....Niiiiiiiiiini..?" "....Gervas nielewe kwa hilo pia usijali Mama yako niko naye pamoja..!" ".....Levy ninachotaka ni twende nikakukabidhi kwa Mama sababu leo hii natangulia Mimi then nitawaachia Mipango yote ya kuja we na Mama yangu si ndio?" "....Sawa Gerva lakiini..!" "Hakuna cha Lakini..., si umeshajua Mama yako mtu wa kumwacha naye?" "...Ndio nimeshajua....!" Nikamuitikia kwa woga huku nikiwa sijitambui nitamwacha vipi Mama yangu. * * * * Ni Wiki moja imeshapita tangu Gervas aondoke na kuniacha,Nilijutia kumdanganya hata Mama yake Gervas kuwa sipo na Mama yangu naishi peke yangu,Mpaka sasa Mama Gervas anajua kuwa Mama yangu aliugua sana nikamsafirisha Moshi nyumbani na kwa bahati mbaya akafia hukohuko hivyo sasa hivi naishi peke yangu., Siku aliyoondoka Gervas alinipatia Dola thelathini pamoja na simu huku akinisisitizia tufanye haraka mi na Mama yake tuwe tumeshaondoka. Namkubali Mungu na nipo naye Daima lakini kila nikimfikiria Gervas nakuwa katika wakati mgumu,kwani Mama yake Gervas hanipendi kabisa na mimi niko tayari hata nimuache Mama niondoke na Mama Gervas nikaishi na Mpenzi wangu Gervas.,Siku moja tukiwa katika pilika pilika za kuhangaikia Viza ya kusafiria pale ubalozi wa Marekani., "...Hivi wewe Levina na tumbo lako na umalaya wako unaenda kwa nani...?" "...Mama.,siku hizi nimeokoka na nimemrudia Bwana Yesu hivyo mi si Levina yule wa zamani..!" "

...eti Si Levina wazamani nyooooooooooooooo...Na huko tuendako..? Walahi nitahakikisha unarudi huku huku Malaya mkubwa wee 'x@sh@hhzzzzzshhh'..." Aliachia sonyo kali mpaka kila mtu aliyekuwepo pale alishangaa,Sikuweza kumrudishia zaidi ya kumwachia Mungu na kuendelea kuvumilia kwani ndoto yangu ni kuishi na Gervas maishani mwangu. ~ BAADA YA WIKI MOJA ~ Furaha ilinitawala moyoni kwani tayari tulikuwa tumeshapata Viza na tiketi tukawa tumeshaweka booking, Ndege ya shirika la 'EMIRATES' ndo tuliotarajia kwenda nayo ikianzia safari yake hapa kisha kupitia 'Kenya' na kituo cha pili kitakuwa 'Dubai' kwa ajili ya kubadilisha ndege itakayotupeleka mpaka 'Stockhom' halafu itaelekea uwanja wa 'Amsterdam' pale Uholanzi kubadilisha tena ndege ya kuelekea moja kwa moja mpaka 'Maryland' ikipitia kusini mwa 'Canada' na huko ndo tutajua ni jinsi gani tutafika kwa Gervas ambaye anaishi jimbo la 'Detroit..' Si furaha tu niliyokuwa nayo bali pia na huzuni huku nikiwa sijitambui Mama yangu nitamwacha na nani.....? Gervas alikuwa akinipigia simu karibu kila siku huku akinisisitizia kuwa nikienda huko sirudi kwani ndo tunaanza Maisha..Sikuweza kuihofia mimba niliyokuwanayo kwani alishaniahidi kumlea mtoto ntakayemzaa.. Safari hii halmashauri yangu ya kichwa ilinituma vibaya kwani nilijikuta nikitupa ulokole wangu pembeni na kuanza kufanya mambo kinyume na yale ambayo yasiyompendeza Mwenyezi Mungu.. * * * * Siku zilizidi kupungua hadi ikafikia siku Nne zimebaki huku nikiwa sijielewi kama safari kweli ipo au la !,nikawa kama mtu aliyechanganyikiwa kwani hali ya Mama yangu ilikuwa inabadilika badilika sana haipiti siku bila miguu yake kumvimba na ndio hapo hapo presha inamuanza na kuzidia lakini roho ya kikatili ikanitawala kuna kipindi Nilithubutu hata kumshindisha Mama yangu njaa karibu kila siku hiyo yote ni kuhangaikia safari...,Mama yake Gervas bado aliendelea kunichukia lakini hilo sikulijali zaidi ya kumvumilia nakuona ipo siku atabadilika huko tuendako. Roho ya kikatili iliendelea kunirudia tena kila mda na kila siku tena nilikuwa na roho mbaya kama ile ya kule msituni nilipomuua 'Pendo' na ile ya Morogoro pale Nilipomuua 'Baba Ali' Mama yangu nikawa simpikii chakula zaidi ya kumnunulia vijichipsi vikavu siku nyingine nampa chai iliyokorogewa chumvi na hamna wala kitafunwa cha aina yoyote ili mradi tu ajaze tumbo siku ipite., Mara zikasalia siku mbili ikabidi nijipendekeze kwenda kwa Mama Gervas kujua safari itakuwaje hiyo keshokutwa ikifika, "....Shikamoo....!" ".....Sihitaji shikamoo yako kama chakula ile.., Enh upo tayari we malaya usio na hata chembe ya aibu..?" ".....Nipo tayari ila..." "....ila nini......?" "......Safari si keshokutwa mchana Mama..?" Nilijikuta nambadilishia mada bila ya yeye kujitambua kisha nikamuaga akiwa amefura kwa hasira,huku akinisindikiza kwa fyonyo kali kuonesha kuwa hanipendi kabisaa.,

".....Na hapa usije.., Tutakutana 'Airport' hiyo keshokutwa we malaya.!" Akaniaga huku Moyoni nikiwa sina raha ya vitu vitatu,kwanza nitawezaje kuishi naye huyu Mama Gervas huko niendako? Pili itakuwaje hii mimba kwani ndio kwanza ina miezi Minne na Nusu, Tatu nitamwacha mwacha vipi Mama yangu na hali yake ile? "....aah liwalo na liwe....." Nikajisemea kimoyo moyo huku nikijongea nyumbani kwetu, safari hii nilimuonea huruma kidogo Mama kwani ilipofika usiku tu nilimtengenezea uji tena ule wa ulezi hadi akanishangaa, alipomaliza kunywa tu, "......Ahsante sana Mwanangu uji mtamu, umenikumbusha mbali mno...!" ".....Usijali Mama nakupenda.." Nilimjibu kinafki huku nikilitambua kuwa sasa simpendi Mama hata kidogo na hii yote ni kwasababu ya safari.., Ulipofika mda wa kulala Nilimwacha Mama akiwa amejiegemeza kwenye kochi tena akiwa amepitiwa na usingizi, nilishangilia ushindi kimoyo moyo huku nikiamini mpaka kesho itakuwa imesalia siku moja tu. Nikaingia chumbani kwangu tena kwa kunyata nikafungua Biblia yangu na kuanza kuomba, "....Eeeh Mwenyezi Mungu nakuomba unisamehe sana kwa kitendo nitakachofanya hivi punde...! Kisha nikamaliza kwa kufanya ishara ya msalaba." Nikafunika ile Biblia,kilichofuata nikachukua panga na kamba nene ndefu na kurudi tena sebuleni kwa kunyata lakini nilipofika tu sebuleni sikumkuta Mama pale nilipomuacha,hofu ikaanza kunitanda,nikahisi moyo wangu umepasuka huku na kule nikitoa macho kumtafuta Mara nikaona karatasi pale Mezani imefunikwa kwa hofu niliyokuwa nayo nikaiwahi haraka haraka kwenda kuichukua lakini kabla sijafika pale ndo nakaribia tu mara.. * * * Ni kitu gani kitatokea? * * * Je., Mama yake Levina atakuwa wapi?
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom