Story gani katika kitabu cha dini yako unafikiri ni hadithi ya ngano tu?

Story ya Ester, bahati bukuku alitusimulia kupitia wimbo wake wa waraka,
Yaani kuanzia Wimbo unaanza unaweza kwenda sokoni kununua dagaa, unarudi unapika, unamalizia kusonga ugali ndio utasikia wimbo umefikia "ooh Ester aah kwa mahombi huku akisindikizwa na mioyo ya wayaudi" .

Du hapo tulipigwa.

Bora ww mimi nilishasikiliza ule wimbo toka bagamoyo mpka naipata njia panda ya moshi nilichoka
 
Kwamba Mungu aliumba dunia na kila kilichomo (sawa) kisha akaumba mwanaume na kuumba mwanamke kwa kumtoa ubavu mmoja mwanaume (sawa).

Kisha hao wawili (Adam na Eva/Hawa) wakazaa watoto wawili (Kaini na Abeli) - (sawa).

Kisha Abeli akawa mfugaji na Kaini akawa mkulima (sawa). Lakini Mungu alipendezwa zaidi na sadaka za Abeli kuliko za Kaini (sawa). Kaini akamuua kaka yake kwa wivu (sawa).

Mungu akampa adhabu Kaini kwa kumfukuza bustanini awe anatanga tanga huku na huko duniani (sawa).

Kaini akamwambia Mungu kuwa akitangatanga watu atakaokutana nao watamuua (shida inaanza kuja hapa). Mungu akamwekea alama usoni ili walimwengu wasimuue (shida inaendelea). Kaini akaenda huko nchi ya Nodi mashariki mwa Eden.

Kisha kaini akalala na mkewe akamzaa mtoto aitwae Henoki. (Sio sawa).

Reference: Soma kitabu cha Mwanzo 4:1-17.

Hii story haija balance kabisa hasa hapo mwishoni. Kama Mungu aliumba Adam na Hawa na wakazaa watoto wawili tu ina maana duniani palikuwa na watu wanne tu. Je hao watu aliokuwa akiwaogopa Kaini ni akina nani? Je huyo mwanamke alielala na Kaini na kuzaa nae mtoto alitoka wapi?

Wataalamu hebu naomba mtusaidie hapa.
Iko mambo unavurugwa kwenye page moja alafu nyingine inakurudisha kwenye mstari
 
Story ya Ester, bahati bukuku alitusimulia kupitia wimbo wake wa waraka,
Yaani kuanzia Wimbo unaanza unaweza kwenda sokoni kununua dagaa, unarudi unapika, unamalizia kusonga ugali ndio utasikia wimbo umefikia "ooh Ester aah kwa mahombi huku akisindikizwa na mioyo ya wayaudi" .

Du hapo tulipigwa.
Sasa ulipigwa na bukuku usimuliaje wake au kisa chenyewe
 
Story ya Ester, bahati bukuku alitusimulia kupitia wimbo wake wa waraka,
Yaani kuanzia Wimbo unaanza unaweza kwenda sokoni kununua dagaa, unarudi unapika, unamalizia kusonga ugali ndio utasikia wimbo umefikia "ooh Ester aah kwa mahombi huku akisindikizwa na mioyo ya wayaudi" .

Du hapo tulipigwa.
😂😂
 
Vitabu vya dini ukitumia logic, HUTOBOI. Maana kuna vingine havimake sense kabisa. Kufika mbinguni kazi sana.

Kuna muda unasoma unaona kabisa hii chai sasa, hasa yule mwamba aliyemezwa na samaki siku 3. Kwamba alikuwa tumboni amekaa tu. Sijui anapumuaje huko tumboni.

Mungu kama unatusikia tusamehe tu baadhi yetu
Kwenye katuni ya Tom na Jerry mtu anagongwa na Gari hafi,..sembuse huyo wa samaki😉😉
 
Vitabu vya dini ukitumia logic, HUTOBOI. Maana kuna vingine havimake sense kabisa. Kufika mbinguni kazi sana.

Kuna muda unasoma unaona kabisa hii chai sasa, hasa yule mwamba aliyemezwa na samaki siku 3. Kwamba alikuwa tumboni amekaa tu. Sijui anapumuaje huko tumboni.

Mungu kama unatusikia tusamehe tu baadhi yetu
Yaan alikata gogo humo humo
 
Hujathibitisha nililo kuuliza.

Nalusaidia kwa swali lako rahisi sana. Naizungumzia Qur'aan.

Mtume alikuwa ni katika Waarabu,na ndiyo maana Qur'aan imetermshwa kwa lugha ya Kiarabu.

Kisha ikawafikia wasio kuwa Waarabu sababu ni ujumbe kwa walimwengu wote.

Mola akajaalia ukijifunza jambo unalijua hata kama si la lugha yako. Watu wakafundishwa lugha ya Kiarabu na wakaelewa. Leo hii ukienda bara la arabu au ukisoma historia ya wajuzi wa kiarabu kiasili si Waarabu.

Sasa usiwe mjinga kukataa jambo usilo kuwa na elimu nalo.

Hakuna aliye zaliwa anajua,hata wewe bila kufindishwa leo hii usingejua kusoma wala kuandika,yaani ungebweteka.

Sasa nataka uthibitishe ya kuwa Qur'aan imeandikwa yaani imetungwa ba Mwanadamu.
Sasa mfano kwann ni kiarabu tu hata kwenye swala
 
Thibitisha.

Kwahiyo hekaya ina sifa hii ? Amekwambia nani hizi habari ?

Hapa chini nakuwekea aya zinazo mkosoa Mtume wa Allah.

1. Alikunja kipaji na akageuka,

2. Kwa sababu alimjia kipofu!

3. Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?

4. Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?

5. Ama ajionaye hana haja,

6. Wewe ndio unamshughulikia?

7. . Na si juu yako kama hakutakasika.

8. Ama anaye kujia kwa juhudi

9. Naye anaogopa,

10. Ndio wewe unampuuza?

11. Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.

12. . Basi anaye penda akumbuke. (Abbasa : 1-12)
Kukosoa
 
Sasa mfano kwann ni kiarabu tu hata kwenye swala
Wewe kabila gani? Lugha mama kwako ni ipi? Ukishajiuliza hayo na kupata majibu sasa jiulize hapa JF unawasiliana na watu wa makabila mangapi na kwanini isiwe kwa lugha ya kabila lako?

Ukijibu hayo utaelewa hekima ya Allah kuifanya Qur'an kwa Kiarabu na salat zote za Waislam dunia nzima kwa lugha moja tu. Ni muujiza tunaoishi nao.
 
Back
Top Bottom