Stori ya kweli: Jinsi kujifukiza kulivyookoa maisha yangu mwaka 2006 na 2009

baiser

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
1,456
2,179
Habarini za kwenu ndugu wana JF, poleni sana na mihangaiko katika kipindi hiki kigumu cha Corona ambapo biashara zimekuwa ngumu na maduka mengi yamefungwa ila ni imani yangu hali itarejea shwari na mambo yatasonga kama zamani.

Lengo la uzi huu ni kutoa shuhuda ya kweli jinsi kujifukiza kulivyookoa maisha yangu mwaka 2006 na mwaka 2009
Nakumbukua ilikuwa mda wa sa tano na nusu hivi usiku nikiwa kidato cha nne, mimi, rafiki angu ambae tulikuwa tunasoma darasa moja na kukaa nyumba moja pamoja na mdogo wangu ambae pia tulikuwa tunakaa pamoja yeye akiwa kidato cha kwanza.

Tulikuwa tunatoka shule kujisomea kwani tulikuwa tunasoma kutwa ingawa shule ilikuwa na bweni pia hivyo ilikuwa ni kawaida wanafunzi wa kutwa kwenda kujisomea shule kwani kule ndo kulikuwa na umeme wa jenereta.

Wakati tunarudi nyumbani usiku huo wa sa tano tulikuwa tunakatiza kwenye msitu mnene wa milingoti kama mnavyofahamu Shule nyingi hupanda miti kuzunguka eneo lake na kwa mikoa ya kusini hupandwa kama mradi wa miti wa Shule

Basi tukiwa njiani nilipigwa na kitu usoni kama panzi hivi au mdudu anayepita kwa kasi. Kesho yake nikaamka macho yangu hayawezi kufumba na pia mdomo hauwezi kula, yaani taya hazina nguvu.

Hivyo hali hii ilifanya rafiki angu kuripoti hali yangu shule kwa uongozi, na kupelekwa hospitali moja ya misheni
Kama ulivyoutaratibu nilipokelewa na kwenda moja kwa moja chumba cha mahojiano na daktari ili niweze kumpa historia ya tatizo ili imsaidie kutambua ugonjwa.

Nakumbuka daktari alikuwa mzee wa makamo mwenye mvi nyingi kichwani, alichonambia kwa miaka 30 ya udaktari wangu sijawahi kukutana na tatizo kama lako, ila nakushauri nenda nyumbani wewe umerogwa watajua namna ya kukusaidia kiufupi alitaka kunambia niende kwa mganga wa kienyeji.

Ila alinishauri ninunue banzoka niwe najaribu kutafuna masaa yote kufanya misuli ya taya isipoteze ufanisi wake.

Basi bhanaa safari ya kwenda nyumbani ikaanza, nilipokelewa na mamangu kwani baba alikuwa kashafariki toka nikiwa kidato cha kwanza.

Mama akataka kunipeleka kwa mganga wa kienyeji ilaa niligoma kwani nilikuwa naogopa sanaa ,usiku nikiwa nimelala nilitokewa na mzimu wa babangu ukanambia usipomsikiliza mamako pumbavu utakufa,basi nilistuka usingizini nikaenda chumbani kwa mama nikamweleza ndoto niliyo ota.

Asubuhi safari ya kwa mganga wa kienyeji ilianza majira ya sa tatu tukawasili tukapokelewa na uongozi wa pale kwa mganga .

Ndugu mganga akapiga ramli pale akasema nimetupiwa vitu na nilikuwa naenda kuwa kichaa kisa wivu sababu ndugu walijua ntakuja kufika mbali kielimu ikumbukwa sijawahi shika nafasi ya pili toka darasa la tatu mpaka kidato cha nne na cha sita pia na chuo kikuu pia sikua mbaya .

Basi ndugu mganga akaamua nifukizwe kwa vyungu kumi tofauti hapo ndo niliamliwa nivue nguo zote nibaki na nguo ya ndani nikawa nainamishwa kwenye kila chungu chenye mvuke wa hali ya juu huku nimefunikwa shuka mvuke usipotee na mdomo niachie wazi huku macho nimefumba ,nilipofika chungu cha kumi niliona mwili mwepesi macho yangu yakaanza kufumba na kufumbua mdomo ukaanza kuwa na nguvu .

Baada ya kuchuja maji ya mwisho ya chungu kidogo ulipatikana mfupa na kioo kidogo. Basi mwisho nilipigwa chale mwili mzima nikapewa Dawa ya kunywa pale pale nikawa nimepona na kurudi shule kuendelea na masomo nikiwa mzima wa afya.

NINI KILITOKEA KATIKA AWAMU YA PILI YA KUFUKIZWA MWAKA 2009

Itaendelea...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Tukawasili tukapokelewa na uongozi wa pale Kwa mganga."

Uongozi = Management.

# Tukawasili tukapokelewa na management ya pale Kwa mganga.
 
😷
 

Attachments

  • IMG_20200427_081522.jpg
    IMG_20200427_081522.jpg
    65.1 KB · Views: 3
Mbona umeifanya ya siri sana, ilitokea wapi? Unasema ulikuwa unatoka shule halafu sehemu nyingine unasema chuo kikuu ulikuwa mkali, wakati huo ulikuwa shule au chuo kikuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichojifunza siku zote ni kuwa wabaya mara zote ni watu,ndugu wa karibu,tujifunze baadhi ya maendeleo au mambo mema ya ndani mwetu yabaki kuwa ya ndani tu,haya mambo unamwambia shangazi wa mtoto kuwa mwanao ye ni namba moja tu,anakuangalia baadae ndo mambo kama hayo.

Unanunua gari unaenda nalo kijijini ukirudi njiani wanakuletea zengwe,tuwe wenye kiasi katika taarifa zetu,unaowaambia wanaweza kuzichukulia kama tambo basi wakaanza kuwasumbua.Mbaya hatoki mbali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom