Stori ya kweli iliyonitokea kipindi nikiwa binti wa Miaka 18

Habari Zenu wana JF Poleni na Msiba wa Rais,

Tuendelee Sasa kipindi wakati nimemaliza Form four nikiwa Nyumbani tu Mama yangu Mzazi Aliniambia hataki nikae tu hivi hivi ni heli Anitafutie kazi ya muda wakati nasubili kwenda chuo...basi bana Akanitafutia kazi kwenye kiwanda kimoja hivi (jina kapuni) Mama yangu Alikuwa ni Mfanyakazi wa Serikalini kwahiyo Aliongea na Huyo Meneja wa Kiwanda kuhusu mimi Kupata kazi nakumbuka Siku hiyo ilikuwa Siku ya jumatatu Mama Aliandika kimemo tu Akanipa nipeleke kwa huyo Meneja ili Nianze kazi mnakumbuka zamani kimemo tu ndo unapata kazi basi bana nikaenda mpaka hapo kwenye hicho kiwanda kufika nikapokelewa na Secretary ni Mmama mchangamfu tu nakumbuka nolifika Saa mbili na Nusu Akaniambia Boss bado hajafika ila tu kwenye Saa tatu Atakuwa keshafika basi kweli ilivyofika Saa tatu boss huyo kaingia Ofisini kwakwe Mimi niko hap tu nasubili baada kama ya Dakika kumi yule Secretary wske Akaniita niingie Basi nikaingia nikamsalimia Akaitikia tu vizuli nikampa kile kimemo Akasoma Akajibu Ok....kumbe wewe ndo binti wa Fulani?

Yani Akataja jina la mama Basi hapo hapo Akapiga Simu kiwandani kumbuka hapo kiwanda mbele kuna Ofisi nyuma ndo kiwanda basi Akameambia Meneja Uzalishaji Aje ofisini kwake Akanitambulisha kwamba naitwa fulani nitaanza kaxi hapo kesho Asubuhi basi Meneja uzalishaji Akanipokea na kwenda sasa kiwandani kufika humo Akanitambulisha kwa Staff wenzangu Sasa kwamba kuanzua kesho tutakuwa pamoja Ukumbuke Mimi ndo nilikuwa mdogo kiwanda kizima nilikuwa nina Miaka 18.

Kasheshe Inaanza..

Basi bana siku ya jumanne nikaripoti kazini kama kawaida na tilikuwa tunalipwa kwa Wiki Sio kwa Mwezi mliofanya kazi kiwandani Mnajua basi bana kunbe mle kiwandani kuna Canteen yani mgahawa wa kunywa chai Sasa Sisi wafanyakazi tukawa tunapewa chai ya rangi kikombe kimoja na vipande viwili tu vya mkate tena mkavu bila Blue band.

Kiini sasa cha Stori hiii....
Basi bana wakati nimeingia mle canteen Akatokea kijana hivi ni Dreva wa Meneja Uzalishaji Akajitambulisha kwangu Nikamjibu pia mimi naitwa fulani Basi Akkanililiza mbona unakunywa chai ya rangi?

Nikamjibu Sina hela make mama Alikuwa Ananipa tu nauli basi Akaniambia Aaaa kuanzia leo Uwe unakula kila kitu unachotaka basi kuna mzee Aliekuwa Anaendesha hiyo canteen yani Tofauti na chai Aliyokuwa Anatupikia staff pia Alikuwa Anapoka chai ya maziwa, mayai, chapati, juice sambusa na kadhalika.

Basi yule Dreva Akanipeleka mpaka kwa yule baba Mwenye canteen akamwambia kuanzia leo naomba fulani Awe Anakula hapa Anachotaka then unaandika kwenye kitabu Mwisho wa Mwezi nitalipa Aisee nolifurahi Saaana nikasema Asante Sana kaka yangu Asante Akajibu Usijali bint mrembo kma Wewe hutakiwi kupata Shida kumbe yeye Ana Malengo yake.

Mtanisamehe kwa Mwandiko basi nikasnza Sasa kila Siku leo niasgiza mayau...chai ya maziwa labda na chapati yani kiulweli nilikuwa nakunywa chai ya nguvu mpaka Mwezi Ukaisha.

Kashehe Inaanza...
Basi kumbe yule Dreva Alilipa zile pesa Cantern lakini kipindi tukiwa tunakunywa chai Anakuja Anakaa na mimi uwezi Amini sijui nilikuwa na Akili za kitoto sana Sikuhisi hata kama ananitaka.

Basi nakumbuka Siku hiyo ndo natoka kazini Akanisubiria getini si Akaanza sasa kunitongoza Akaanza kuniambia Ananipenda Sana nikashtika nikamwambia Mimi Sitaki huo Ujinga kwana nitaenda kukusemea kwa Mama, mama yangu Aliniambia Nisijefanya kiti na Mwanaume nitapata Mimba hapi hapo ma kweli nikiwa Bikra kabisa na nilikuwa naogopa sana yale Maneno ya Mama Aliyokuwa Akiniambia basi yule Dereva Akachekaaa Akaniambia Tutafanya na Kondomu nikamwambia nimesema sitaki na Sjawahi fanya Matusi niache.

Nikaondoka Akakaa kimya siku ya pil Akaniambia ten nikakataa siku ya tatu tena nikakataa nakumbuka Silu ya Nne tulikuwa tunatoka Sasa kiwandani tuko Wengiii Akaja katikati ya kundi tuliokuwa tunatoka ghafra nasokia mtu Ananikaba Koo huku kashikilia nguo yani Sijui nielezeje ile mtu kukukaba hili utoe kiti chake Akaanza kupayuka NATAKA PESA ZANGU......NATAKA PESA ZANGU.

Basi nikaanza kulia sana Sasa Wale wenzangu wotee tuliokuwa tunafanya kazi wakamgeuzia kibao kwanini Umkabe? Nikawasilimulia yani ndo wachukia zaidi wakaanza kumtukana acha Ujinga wewe Ebu Muache binti wa watu mara tukasikia tunaitwana Meneja Uzalishaji tukaenda ofisini kufika Akauliza kwa nini Unamkaba tuite jina langu jane kwanini Unamkaba jane?

Akaanza kusema Ananidai pesa hapo hapo na Mimi nikaingilia nikamsimulia Meneja kila kitu nikamwambia halafu Eti Ananilazimisha tukafanye Matusi Basi meneja Alicheka sana yani Alicheka Akaniuliza Sasa Wewe Jane Wakati unakula hivi vitu Ulitegemea nini?

Basi akamuuliza yile Dereva Unamdai kiasi gani? Akamwambia Basi Akatoa waleti Akalipa ile pesa basi nikamshukuru nikamwambia Nikipata mshahara niktakuludishia meneja Akacheka Akasema sasa Mnalipwa kwa Wiki hiyo pesa huoni hata Haotatosha?

Maskini nasikia huyo Meneja Alfariki Alikuwa na roho nzuli sana pia Namshuru sana Mama yangu Alinijenga Saana nikawa sasa Ninajiamini hata hivi nilivyo ni matunda yake Aliyonijenga Rest in Peace My Lovely Mama na Story Imeisha.

WAZAZI TUONGEE NA WATOTO WETU KAMA RAFIKI UWA WANAWEKA KUMBU KUMBU KICHWANI AKITAKA KUFANYA KITI ANASIKIA SAUTI YAKO.
no free lunch
 
Unagoma kufanya matusi?😅Kwani ungekufa Kama ungemlipa kitandani😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom